Hii kauli imefanya watu washindwe kujitafajari pale wanapopoteza kwa kujifariji kuwa HAIKUWA RIDHIKI .
Inaweza kuwa ni ridhiki yako ndio lakini ukaipoteza kwa ujinga au tabia zako na kwa sababu ya hiyo faraja unayoijipa unabaki kuamini tu kama ni chako kitakuwa na kama sivyo kitaondoka lakini swali ni je hata kama ni CHAKO KITAKAA KWENYE TABIA ZISIZO RAFIKI?
Wengi hutafasiri kuwa kwa sababu tu ulipangiwa basi wewe huna mambo ya kufanya ili kufanya hayo mambo yaje na kudumu kwako badala yake unabweteka ukisubiri tu sasa kwa namna hiyo UTASUBIRI SANA BILA MAFANIKIO.
Ukisoma ajira hazikutafuti bali wewe ndio unatakiwa uzitafute .
Mchumba sahihi atakaa kwako ikiwa tu umeweka mazingira rafiki kwake la sivyo watakuja na kuondoka nawe utabakia tu kujifariji kuwa KISICHORIDHIKI HAKIKAI
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako