Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,maana nina imani kuwa na wewe ni mzima,.....karibu tujifunze.
Kusudi la somo.
Leo ni muendelezo wa siri za urafiki,tunaendelea na siri ya sita ya urafiki ambayo ni utatuzi wa migogoro,kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukajifunza kwanza SIRI YA TANO ,Karibu tujifunze.
UTATUZI WA MIGOGORO YA URAFIKI.
Jambo la kufahamu kwenye urafiki ni kwamba ,unakutana na mtu ambaye hujazaliwa naye,ana madhaifu yake na pengine ana historia yake ya maisha tofauti na yako.......lazima kuna migogoro itatokea tu ndani ya urafiki,,,,,jaribu kujibu maswali haya kabla ya kuendelea mbele......je umewahi kuingia kwenye mgogoro na rafiki zako?,ulifanya maamuzi gani ?.baada ya maamuzi hayo urafiki wenu ulipata sura gani?
Migogoro kwenye urafiki ni muhimu sana kwani ni dalili ya kuonyeha hali ya kutokuwa sawa sehemu flani,ila inaweza kuwa na madhara ya kudumu kwa wahusika endapo watashindwa kutambua sababu za utokeaji wa migogo hiyo,
Uwezo wa utatuzi wa migogoro ya urafiki bila kuharibu thamani ya muhusika ndio kipimo kizuri cha uwezo wa uendeshaji wa urafiki.
Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye utatuzi wa migogoro.
- Kabla ya maamuzi yoyote hakikisha unajua chanzo cha tatizo .
- Usipende kuonekana mshindi,ili kumudu hili hakikisha unatawala hisia zako za hasira ili usifanye maamuzi yenye msingi wa hasira.
- Kama kosa lipo kwa rafiki yako,vaa uhusika ili upime yeye angefanya maamuzi gani juu yako.
- Usipende kutumia ushauri wa watu wengine katika kutatua mgogoro unaokuhusu wewe.
- Hakikisha unajua tafasiri ya kila changamoto kwenye urafiki wako,ili ufanye maamuzi ambayo hayana majuto.
Kumbuka tu ili uweze kufikia ndoto zako ni muhimu uwe kwenye system ya marafiki waliobeba kusudi lako,ila kuwa na rafiki ambaye kabeba kusudi lako sio tafasiri ya kutokuwa na migogoro.
See you at the top.
scientist SAUL KALIVUBHA.
0652 134 707.
No comments:
Post a Comment