KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo la leo ni kuendelea na sehemu ya tano ya siri ya Urafiki. ..ni vyema ukajifunza sehemu ya nne SIRI YA NNE kisha uendelee na siri ya tano( SIRI YA NNE)..... lengo la kufundisha urafiki ni kutaka tufahamu jinsi ya kuishi na marafiki kwa lengo la kufikia ndoto zetu ...maana mafanikio yako yapo kwa rafiki yako. ...karibu.
SIRI YA TANO YA URAFIKI.
Siri ya tano ya urafiki ni mawasiliano .Kwenye mawasiliano tuangalie kwenye upande mmoja tu. jinsi mawasiliano yanavyoweza kuvunja urafiki. ....nafikiri utakuwa tayari umeshuhudia urafiki ukivunjika kwa sababu ya mawasiliano. ....au inaweza kuwa umekutwa na tatizo hili la kupoteza marafiki kwa kigezo cha mawasiliano. ....
Mawasiliano yanaweza kavunja urafiki kupitia sehemu hizi.
- Mawasiliano mabovu, ..hapa nina maanisha kiwango cha chini cha mawasiliano au mawasiliano ambayo hayana hisia za Upendo. ....kila mazingira yana aina yake ya mawasiliano na kiwango chake, ukiwa kwenye mazingira yenye kuhitaji mawasiliano kwa wingi ila wewe ukafanya chini ya kiwango , urafiki utakuwa unaelekea kwenye hatari ya kuvunjika. ....jitahidiutambue aina ya urafiki uliyonayo, mazingira mliyopo. .ili ufanye mawasiliano yanayostahili.
- Mawasiliano hupoteza thamani ya habari, ...utafiti wa kisaikolojia unaonyesha kwamba habari inavyozidi kupita mikononi kwa watu wengi ndio inavyozidi kupungua uhalisia wake, ila kuna watu bila kufanya utafiti wa kina wamekuwa wakifanya maamuzi ya kudumu kwa kupitia taarifa imeyopitia mikononi kwa watu wengi. ..hali hii imefanya watu wengi kupoteza marafiki .....fanya tasmini kabla ya maamuzi, unavyozidi kuwa mbali na chanzo cha habari ndivyo ukweli wa taarifa unavyozidi kupungua. .....
Seeyou at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652 134 707)
Thanks for your good work
ReplyDeletewelcome back
ReplyDelete