LENGO LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nane ya urafiki kulingana na mpangilio wangu, siri hiyo ni Jichunguze tabia yako. ... .Unaweza pitia kwanza SIRI YA SABA, kisha uje tuwe wote. .....karibu tuendelee.
SIRI YA NANE (JICHUNGUZE TABIA YAKO ).
Urafiki unapitia mazingira mengi sana, kila mazingira huwa yanahitaji style (mfumo ) wa kuishi ili kuhakikisha urafiki unaendelea na thamani yake.Ila kuna kipindi mtu anaona rafiki yake kabadilika tabia, amekuwa na tabia mpya ambayo hapo nyuma hakuwa nayo.
- Je umewahi kukutwa na hali hiyo?
- Urafiki wako ulikuwa na sura gani baada ya hali hiyo?
- Unafikiri chanzo chake ni nini?
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.
Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134 707.
0
No comments:
Post a Comment