Friday, 15 September 2017

SAIKOLOJIA YA PESA.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha ,nashukuru Mungu kwa kunipigania kwake kila siku, furaha yangu kubwa ni sababu  na wewe ni mzima.,kama ni mgonjwa pia ondoa hofu,yupo mponyaji mkuu kwa  ajili yako ambaye ni Mungu.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze saikolojia ya pesa katika sehemu kuu tatu ;BAJETI,AKIBA NA UWEKEZAJI....Kabla ya kuanza somo letu hili ni vizuri ukaelewa kwanza  maana ya Saikolojia kwa ufupi.
SAIKOLOJIA sio neno geni sana,ila kwa ufupi lina maana ya elimu ya tabia ,sababu zinazofanya utokeaji wa tabia na madhara ya tabia......kwa leo tujifunze tabia ambazo pesa inahitaji ili iweze kukaa mikononi kwako.......karibu tujifunze.



 BAJETI.
Bajeti ni muongozo ambao unahusisha mapato na matumizi ya pesa,ni watu wachache sana ambao wanatumia pesa kwa kufata bajeti,maana rahisi ni kwamba watu wengi hawana malemgo kwenye maisha yao ya kesho,haijalishi kipato chako ni cha ukubwa gani,lazima utengeneze bajeti ya kuonyesha pesa unayoingiza,matumizi unayotumia na akiba unayoweka.......Mambo muhimu sana ya kuzingatia kabla ya kupanga bajeti ni haya; Ukubwa wa pesa unayoingiza,  malengo yako yanayohitaji pesa ,  mazimgira yako(familia yako) na ufahamu matumizi ya lazima na yale yasiyo ya lazima....Mambo hayo machache yatakusaidia uishi maisha yanayo endana na bajeti yako ila yenye mchango mkubwa kwenye malengo yako ya kesho.



AKIBA.
Akiba ni pesa ambayo unahifdhi kabla ya kuanza matumizi yoyote ya pesa na kwa lengo maalumu,lazima uwe na malengo kisha ndio uanze kuweka akiba,Ukiona unashindwa kuweka akiba jitahidi upitie bajeti yako vizuri na kisha uanze kupunguza matumizi yasiyo ya lazima au kununua  vitu vyenye bei ya kawaida .....kiufupi lazima uishi maisha ya kawaida kwa sasa ili kesho uishi maisha ya tofauti,.....Kuna watu wanajidanganya kwmba kuweka akiba lazima uwe na kpato kikubwa,jibu ni hapana.....nakumbuka kuna kipindi nilikuwa naingiza laki moja kwa mwezi ila nilifanikiwa kupanga bajeti hadi kuweka akiba ya laki sita kwa mwaka,hivyo nikawa na jeuri ya kufanya kitu bora zaidiya kile cha kuingiza laki moja kwa mwezi.



UWEKEZAJI.
Ukiwa na bajeti nzuri utakuwa na uwezo wa kuweka akiba,usiweke akiba kama huna kitu cha kufanya kesho,utaitumia pesa yako ovyo,weka akiba kwa lengo flani,ili ile akiba ianze kukuzalishia pesa,......njia nzuri ya kutumia akiba ni kuwekeza au kufanyia biashara.....kwa hiyo ni vizuri kuwa na elimu ya pesa,elimu ya kile unachotaka kuwekeza na ukubali kuishi maisha ya kawida kwa muda flani.


            See you at the top
               Saul kalivubha
                  0652 134707

13 comments:

  1. Ahsante.Ila naomba kuuliza hiyo akiba naweka kutokana Na FAIDA niliyopata kwa siku husika au pato la siku hiyo kwa ujumla?.msaada Tafadhari.

    ReplyDelete
  2. Ahsante.Ila naomba kuuliza hiyo akiba naweka kutokana Na FAIDA niliyopata kwa siku husika au pato la siku hiyo kwa ujumla?.msaada Tafadhari.

    ReplyDelete
  3. Asante Sana kwa elimu hii, barikiwa Sana.

    ReplyDelete
  4. 🤝 nimekuelewa vizuri sana

    ReplyDelete