Sunday 10 December 2017

DAFTARI LA MALENGO

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya,kwa wale wagonjwa,Mungu yupo kwa ajili yetu,atatuponya,tusichoke kuzungumza naye.......Karibu tujifunze.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze kuhusu daftari la malengo,somo letu litakuwa katika sehemu kubwa mbili,maana ya daftari la malengo na umuhimu wa daftari la malengo.......karibu tuendelee.

MAANA YA DAFTARI LA MALENGO.
Daftari la malengo nafikiri ni neno maarufu ila lenye kutumika mara chache sana kwa watu,daftari la malengo ni daftari ambalo linatumika kuandikia malengo na jinsi ya kuyafanikisha hasa kwa kuzingatia mipango inayoonyesha namna ya kukamilisha malengo hayo..................kabla ya kuhamia sehemu ya pili,tujifunze sehemu muhimu zinazotakiwa uwe nazo kwenye daftari lako la malengo.

  • Anza na kurasa chache kwa kuandika malengo yako na kikomo cha malengo hayo(deadline)
  • Kurasa zinazofata andika mipango ambayo unatakiwa kuifanya ili uweze kufikia malengo yako,mipamgo ni sehemu ambazo zinatakiwa kukamilishwa ili zisaidie kutimiza malengo hayo....mfano,una lengo la kununua gari,lazima uwe na mipango ya kufanya ili uweze kupata pesa inayotakiwa.
  • Kurasa baada ya mipango,andika bajeti ,,,,,bajeti itakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa na yenye uhusiano mzuri wa malengo yako.....

UMUHIMU WA KUWA NA DAFTARI LA MALENGO.
Zipo faida nyingi za kuwa na daftari la malengo,ila faida kubwa sana ni kutimiza malengo yako.....daftari la malengo linasaidia kukupa kifungo ,kifungo ambacho muda mwingi kitakufanya uwazie malengo yako,na kitakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa,maana utakuwa na hofu ya kutumia pesa iliyo nje ya bajeti yako.

       Makala hii imeandikwa na mkurugenzi wa label ya fikia ndoto zako.....Saul Kalivubha.
             0652 134707.