Saturday 14 January 2023

 HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA UWE MTU WA KUJUTIA MAAMUZI YAKO

 HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA UWE MTU WA KUJUTIA MAAMUZI YAKO 


Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 


Ulijawa na furaha siku hiyo na hata kama angetokea mtu wa kukwambia kuwa unachotaka kufanya ni hatari pengine ungemuona ni adui asiyependa mafanikio yako lakini furaha yako leo haipo tena 😞 Unajutia  maamuzi yale .Kwa nini umekuwa mtu wa kujutia maamuzi yako ? Na ilihali jana ulijiona upo sahihi kwa maamuzi hayo? Twende darasani. 

Maamuzi ni eneo muhimu sana kwenye maisha yetu kwa sababu maamuzi ndio miguu yetu ya kutembelea , upo hapo ulipo leo  kwa sababu kuna maamuzi uliyafanya jana na hata hao unaowashangaa leo wapo hivyo kwa sababu kuna maamuzi waliyafanya jana .

Kujutia sio kitu kigeni kwa sababu karibu kila mtu ana siku moja au zaidi za kujutia maamuzi yake, hakuna ambaye hajawahi kujutia katika maisha yake lakini wapo watu ambao kwao ni zaidi yaani kwenye maamuzi kumi waliyofanya basi   zaidi ya maamuzi matano kwao sio sahihi ni lazima wayajutie.

Kwa nini leo ujione umekosea na wakati jana ulijiona sahihi kwa maamuzi yale yale?  Yapo mambo mengi ambayo yanachangia hali hiyo kutokea  na vizuri uyafahamu mambo hayo ili ujue namna ya kupunguza majuto , na kama unakuwa mwingi wa majuto kuna uwezekano mkubwa ukawa ni mtu ambaye huna furaha kwenye maisha yako kwa sababu unakuwa unafikiria  yaliyopita tu .

Ufahamu wako wakati wa maamuzi ni sababu kubwa sana ya majuto kwa wengi, wajua ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu kinachofanya uamue ni Ufahamu wako wa muda huo hivyo kama ufahahamu wako ni mdogo sana basi hata maamuzi yako kwa asilimia kubwa  yatakuwa sio bora pia na siku ufahahamu wako ukikua ni lazima utaona kuwa ulikosea maamuzi . Tunajutia maamuzi yetu ya jana kwa sababu tuliyafanya tukiwa na ufahahamu mdogo tofauti na leo tulivyo kwa mfano  kama jana ulifanya maamuzi ya kuacha shule kwa ufahahamu kuwa shule inakupotezea muda  ni bora ufanye biashara lakini ulipoanza biashara ukakutana na changamoto zikakumbusha kuwa kuna kiwango cha elimu kinatakiwa ili uweze kuimudu hiyo biashara na hapo ndipo utaaanza kujiona ulikurupuka kwenye maamuzi. 

Matokeo ya maamuzi yetu tuliyoyafanya jana ndio yanasema na sisi leo kutu onyesha ni jinsi gani tulikosea/kupatia  kwenye maamuzi yetu hayo , kuna kanuni moja ya kimaamuzi inasema kuwa kila maamuzi uliofanya ni lazima matokeo yake yaje kusema na wewe siku moja na hapo ndipo utagundua ni jinsi gani ulikuwa sahihi. Matokeo hufanya watu tujifahamu vizuri tukoje na kama utakuwa mtu chanya basi utatumia matokeo hayo kujifunza. 

Mihemko pia ni sababu nyingine inayofanya tukosee maamuzi kwa sababu maamuzi yako yatakuwa ni matokeo ya hisia za muda mfupi tu zisizo na fikra ndani yake ndio maana unashauriwa kuwa na utulivu kabla ya maamuzi japo kuna maamuzi mengine ni lazima tuyafanye kwa haraka kulingana na uhitaji wake lakini hayo ni kama dharura  tu ila maamuzi mengi lazima kuna muda utapata wa kufikiria hivyo kabla hujaamua jitahidi huna mihemko . Mihemko mara nyingi chanzo chake ni kukosa utulivu na muda mwingine kuchochewa na mazingira ya nje ikiwemo kuishi kwa kujilinganisha sana. Ukiishi kwa kujilinganisha utakuwa mtu wa kujiona umechelewa kwenye maisha na mwishowe utaanza kufanya vitu bila utulivu .

Kushindwa kuitawala shauku yako pia ni sababu inayoweza kukufanya ukosee maamuzi kwa sababu utakuwa mtu wa kukurupukia mambo kabla ya wakati wake ili tu ukidhi shauku yako Maamuzi yako Hayawezi kuwa sahihi kama unayafanya kwa shauku ambayo haikudhibitiwa .

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

Mitandaoni tunapatikana kwa jina la fikiandotozako. 

Pia kitabu cha namna ya kudhibiti mwili kinapatikana kwa soft copy Tsh 3000 

+255652134707

Sunday 8 January 2023

JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI

 JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI KWENYE MAHUSIANO 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Wivu kwa maana rahisi ni kutojiamini , unahisi kuna watu wenye sifa zaidi yako watakuibia mpenzi wako 😔 Wivu hukoleza mapenzi 😊 

Kutojiamini ni wivu uliopitiliza kiasi , muda wote unahisi umpendaye ana njama mbaya dhidi yako kiasi cha kila siku kuwa na migogoro isiyoisha 

Kutojiamini ni sumu ya mahusiano.Wafikiri sababu zake ni nini? Na utajijuaje ikiwa una tatizo hili ?  Karibu darasani 

DALLI ZA KUTOJIAMINI 

Asipojibu meseji kwa wakati tayari unahisi kafanya makusudi 😔 

Asipoitikia simu yako wewe unajua yupo anafanya kitu kibaya 😔 

Ukimpigia simu akiwa anaongea na mtu mwingine tayari unahisi yupo anakusaliti 😢

Siku haiishi bila kumuwazia mabaya yaani unahisi kama vile hakupendi au anakudharau 😔 

Muda wote unahisi kama anakudanganya tu hakuna siku unamuamini 😔 

Unakuwa mwepesi kukasirika kwa vitu vidogo vidogo tu

Hujui bahati mbaya kila kitu kwako unaona ni njama mbaya aliyoipanga kukufanyia 😔 

Akiwa na marafiki zake tayari unahisi anakusaliti au wanamshaurii mabaya kukuhusu wewe 😔


Weka alama ya tick kwenye dalili inayokusumbua ikiwa kila migogoro ya mahusiano yako chanzo ni dalili zaidi ya nusu kati ya hizo kuna uwezekano mkubwa kati yenu kuna tatizo la Kutojiamini .Kutojiamini kuna leta migogoro na ni ngumu kuwa na mahusiano yenye afya nzuri ikiwa kati yenu kuna migogoro ambayo chanzo chake  kikubwa ni Kutojiamini .

Mbona hata dalili za wivu ni kama zinafanana na za Kutojiamini?  Swali zuri sana hilo ni kweli kabisa dalili pia za wivu ni kama hizo hizo sema kama nilivyokwiaha kusema juu kwenye utangulizi kuwa wivu ni Kutojiamini kuliko na kiasi na huwa hakuna migogoro kwenye wivu wa mapenzi bali hukuza mahusiano yenu ya mapenzi , bila wivu wa kiasi mahusiano huwa hayana raha. 


Kwenye wivu kuna upendo lakini kwenye kutojiamini  kuna upendo wa mashaka ndio maana kutojiamini ni chanzo kingine cha kuvunja mahusiano au kufanya watu wakuogope kwa sababu tu ya migogoro kila siku, hakuna anayependa migogoro ya kila siku .

Kutojiamini chanzo chake ni nini?  Kuna vyanzo vingi vya tatizo hilo yawezekana ikawa ni sababu za kimazingira au za kuzaliwa nazo( kurithi). Tuone sababu chache zifuatazo:

Kuwa na historia ya kusalitiwa : Mara nyingi tatizo la Kutojiamini linaonekana kwa watu ambao wana historia ya kusalitiwa na wenzi waliowapenda sana hivyo wanakuwa hawana imani tena watu , na mara nyingi tatizo linakuwa kubwa kama muhusika ataamua kuingia kwenye mahusiano mapya bila kupona kwa jeraha lake la kwanza hivyo matokeo yake anakuwa anaishi na mtu wa pili kama vile ni mtu yule wa kwanza.Tiba ya  tatizo hilo ikiwa chanzo ni hiki basi tiba yake ni kujiponya majeraha kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya. 

Chanzo kingine ni tabia yako ya kutafuta ukamilifu wa 100%; Tatizo hili ndio chanzo cha kutoamini kuwa kuna bahati mbaya ndio maana mwenzio akifanya vitu bahati mbaya tayari unajua ni makusudi kakufanyia na tayari ni mgogoro huo , hutaki kumuona kama na yeye ni binadamu bali unamuona kama ni malaika ambaye hakosei hata kidogo.  Tiba yake hapa  ni kujifunza kupuuzia baadhi ya vitu vinavyotokea kwenye mahusiano yako muhimu tu visiwe vina madhara makubwa kwenye safari yenu , kuna mambo unaweza kuyapuuzia na yasilete madhara kwenye mahusiano yenu lakini ukikata kufuatilia kila kitu lazima mtakuwa na migogoro mingi sana kwenye mahusiano yenu .

Chanzo kingine ni kuathiriwa na huyo umpendaye yaani unayempenda anakuwa na historia ya kukusaliti hivyo tayari kumuamini tena inakuwa ngumu hivyo anakujengea tabia ya Kutojiamini tena na matokeo yake ni kuwa na mashaka dhidi ya matendo yake. Tiba ya hapa inachukua muda wa kutosha na lazima yeye ndiye akutibu kwa kukuaminisha kuwa kaacha tabia zake za awali .

Chanzo kingine ni urithi; Tayari umezaliwa upo hivyo tu yaani una tatizo la Kutojiamini la kuzaliwa nalo , hapa kuna tiba kutoka pande mbili ambazo ni kutoka kwako na anayekupenda. Lazima ujikubali kuwa una tatizo na kujidhibiti pale uwezapo  na huyo akupendaye inabidi ajue kuwa una kasoro hiyo Hivyo lazima ajifunze kuishi na wewe. 

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

Mafunzo yetu yapo mitandaoni kote kwa jina la fikiandotozako 

Pia kitabu cha siri za urafiki kinapatikana soft copy ( nakala tete) kwa Tsh4000 tu , ukilipa utatumiwa muda huo huo 


+255652 134707

Friday 6 January 2023

KILA MTU ANA MTU WA HADHI YAKE  😊 MATESO YAPO PALE UTAPOWANG'ANG'ANIA WASIO WA HADHI YAKO 😢 

 KILA MTU ANA MTU WA HADHI YAKE  😊 MATESO YAPO PALE UTAPOWANG'ANG'ANIA WASIO WA HADHI YAKO 😢 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Bila shaka kichwa cha andiko kimekusisimua 😄 kama ni kweli basi nawe tayari upo kwenye kundi la watu ambao wanasumbuliwa na watu 😔 Mwanasayansi kakuvuruga? 😔  haya twende darasani ✍

Kuna watu hata kwa nini hamuwezi kukaa kiti kimoja mkaelewana kwa sababu tu mna hadhi tofauti  mpaka mmoja apande/ashuke kwenye hadhi ya mwingine ndio mtakaa pamoja na kuelewana, wewe una hadhi gani? watu gani unawakumbatia? Ndugu yangu ukitaka mahusiano yakutese wakumbatie watu mnaopishana hadhi 😔

Kwa mfano wewe kwa sasa hadhi yako ni kuhudumia shilingi elfu kumi kwa mwezi wafikiri utaweza kukaa na mtu mwenye hadhi ya kuhudumiwa milioni moja kwa mwezi?  kwa namna yoyote hapo haiwezekani tu kabisa mpaka ajishushe kwenye hadhi yako au wewe upande kwenye hadhi yake tofauti na hivyo utatumia nguvu kubwa mpaka kukopa au kuuza rasilimali zako ili tu uendane naye lakini ukweli ni kuwa unaweza kufanikiwa mwanzoni tu lakini baadaye utashindwa na utabaki hovyo sana  

Huo ni mfano tu mmoja lakini ipo mifano mingi kwenye maisha ya kila siku ambapo watu hujikuta kwenye mateso kwa sababu tu ya kuwakumbatia watu wenye hadhi tofauti.  Ukiona hudumu sana na watu kwenye mahusiano yoyote yale kaa chini jitafakari sio ukimbilie kusema wewe una mkosi la hasha yawezekana una kasoro hii ya kuwakumbatia watu mnaopishana hadhi na mwisho wa siku unakuwa mtu wa kulaumu tu na wakati mchawi ni tabia yako hiyo.

Utajuaje hadhi yako? Swali nzuri sana hili , ni kweli ni lazima kwanza ujitambue hadhi yako kwa sasa ni ipi na sio kazi ngumu hata muhimu ni kujiangalia kwenye maeneo haya matatu WEWE NI NANI, UNATAKA NINI NA UNA MUDU KIPI.   Kama unajitambua kwenye hayo na bado matokeo ni yale yale basi yawezekana pia wewe ni mbishi hutaki kujikubali kuwa wewe ni nani ndio maana unalazimisha wasio na hadhi yako.

Siku utakokubali kuwa kuna watu tu sio hadhi yako ndipo utayaona mahusiano ni mazuri kwa sehemu 😊 na utaona ukipendwa na kuheshimiwa 😊 lakini huyaoni hayo kwa sababu upo na watu ambao sio hadhi yako unaumia tu kila siku na kucheleweshwa na usipokuwa makini utakumbuka shuka tayari ni asubuhi 😔  Fanya tu maamuzi magumu ya kuwaacha watu wa ambao sio hadhi yako ili upatane na wenye hadhi yako au tulia kwanza ukuze hadhi yako ndio upate wenye hadhi sawa.

Kuna watu huwapati na hutowapata kwa sababu tu sio hadhi yako na unapoteza muda kwenye hilo. Kuna msemo unasema kuwa embe halianguki mbali na mti wake , huu ni msemo wenye hekima na wahenga waliifikiria mbali kwenye hilo maana sio kazi rahisi ukute embe chini kusiko na mti wake labda tu liwe limetupwa 😄  na kwa nini litupwe ? Ila ukiona embe chini kikawaida kuna mti wake pembeni ndio sawa na maisha yetu ukiona wawili wanaendana kuna uwezekano mkubwa wakawa na hadhi moja tofauti na hivyo basi kuna mmoja amekubali kuwa mtumwa wa mwingine 😔 Sasa kwa nini ukubali kuwa mtumwa? na wakati wa hadhi yako yupo tu na mngefurahia maisha tu

Tafuta mtu wa hadhi yako ndio sasa taratibu muanze kupanda hadhi pamoja na kama utapata mtu asio wa hadhi yako mkaendana basi pia shukuru Mungu na hii huwa inatokea lakini ni mara chache sana 


Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

+255652134707


Madarasa yetu yapo Instagram  kwa jina la  fikiandotozako 

Sunday 1 January 2023

KUNA TOFAUTI KATI YA MTU MASKINI NA MTU AMBAYE HANA PESA 

 KUNA TOFAUTI KATI YA MTU MASKINI NA MTU AMBAYE HANA PESA 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Mtu anaweza kuwa hana kabisa pesa hata shilingi mia lakini asiwe MASKINI na mtu anaweza kuwa anakula tu vizuri na kila kitu cha ndani lakini akawa MASKINI 😔  Mwanasayansi kakuchanganya? 😄 🤣 

Hapana nipo sahihi ✍ 

Umaskini ni IMANI lakini kukosa pesa ni MAPITO , Unaweza pitia kipindi cha kukosa pesa lakini imani yako ni ya KITAJIRI 

Umaskini ni imani kama zilivyo imani nyingine tu za kiroho mfano uislam na Ukristo ulivyo na waumini ndivyo ilivyo hata kwenye Umaskini kuna waumini wake wamo humo ndio maana sio kazi rahisi kuaga Umaskini, narudia tena sio kazi rahisi kuaga Umaskini kama ilivyo ngumu kumbadilisha muislamu kuwa mkristo  au kinyume chake, unajua sababu? Ni kwa sababu tu kila muumini ameshika mizizi ya dini yake hivyo sio rahisi kuiachia kirahisi. 

Umaskini huanzia kwenye akili ya mtu ndio maana watu maskini huwa wana viashiria vya kufanana kwa sababu tu wapo imani moja, je wajua viashiria? ( Dalili za umaskini)


#Ni watu wa visingizio

#Ni watu wa kuridhika na maisha ya kujaza tumbo tu

#Huamini kuwa wanaoshindwa wametoa rushwa au ni wenye imani za kishirikina 

#Kila jambo wanasema ni mpango wa Mungu hata ambalo  ni matokeo ya uzembe wao

Hizo ni dalili chache kati ya nyingi za muumini wa UMASKINI yawezekana unazo chache au zote kati ya hizo basi jijue wewe ni muumini wa UMASKINI tayari 😔 

Unaweza kutoka humo? Ndio inawezekana kutoka humo japo sio rahisi kama nilivyokwisha kusema kuwa sio rahisi kubadili imani 😔 nguvu kubwa inatakiwa 

Lazima kwanza ukubali kuwa wewe ni maskini upo kwenye imani hiyo sasa unatakiwa kuanza taratibu kuzikana imani hizo za kimaskini ili uhame kutoka imani hiyo uende kwenye imani ya UTAJIRI 

UTAJIRI ni imani pia yenye waumini wachache lakini na misingi ya imani yao ipo kinyume na misingi ya umaskini hivyo ni rahisi tu kuwa humo kama tu utaikana misingi ya umaskini 


Nikutakie mwaka mpya mwema ndugu yangu 


+255652 134707