Saturday 15 December 2018

MBINU ZA KUTOKA NJE YA DUARA LA UMASKINI.

Karibu sana kwenye blog hii ambayo inatoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu ,ni tumaini langu kuwa u mzima wa afya na unaendelea vyema na harakati za kukuwezesha kufikia ndoto zako....Leo nataka tujifunze mbinu kuu tatu za kutoka nje ya duara la umaskini.Somo hili limekuja maalumu kwa sababu ni wazi kwamba ,wengi wetu tunazaliwa na kulelewa katika familia zenye kipato kidogo,sasa tunapoanza kupiga hatua,tunajikuta tuna mzigo mkubwa nyuma yetu,mzigo ambao tuna wajibu wa kuubeba lakini usiathiri hatua zetu za mafanikio....Karibu tujifunze.

DUARA la umaskini ni mzunguko amabao unaanzia kwa maskini na kuishia kwa maskini ,DUARA hili mara nyingi hutokea kwa watu ambao wamezaliwa katika familia za kimaskini,mimi pia ni mmoja wapo,....inakuwa hivi;

Wazazi/ndugu(MASKINI)  >MTOTO(ambaye analelewa katika hali ya kimaskini,ya wazazi wake).

Katika hali hiyo,matatizo ya  waliokutangulia yataendelea kukufuata mpaka pale utakapo amua kutengeneza  mfumo ambao utawafanya wawe na utegemezi wao binafsi(wajitegemee),kinyume na hivyo,kidogo chako kitakuwa kinategemewa na wengi ambao sio wazalishaji.......Hebu tuangalie hizo mbinu tatu ambazo mimi pia ninazitumia,wewe pia zinaweza kukusaidia.

1.Tambua kuwa wewe ndio daraja la kupitisha wengine,hivyo lazima uwe imara zaidi ya hao unaotaka kuwavusha ,uimara ninao uzungumzia hapa ni wa kiuchumi na mawazo,kiuchumi simaanishi uwe na milioni za pesa,la hasha,namaanisha uwe na mfumo unaoeleweka.

2.Tengeneza mfumo ambao chanzo kitakuwa ni wewe lakini waendelezaji watakuwa ni hao umeokusudia kuwasaidia(maana huwezi kusaidia kila mtu),hapa nimaanisha kwamba wewe yafaa uwe mtaji wa mawazo na pesa kwa huyo uliyekusudia kumsaidia kwa lengo la kumfanya awe na mfumo wa kujitegemea.

3. Kumbuka, kutoa pesa kila wanapohitaji sio msaada wa ukombozi,ni bora uwe bahili kwa muda ili kile kiasi ambacho ungekuwa unawapa ukitunze kisha uje ukitumie kutengeneza mfumo ambao utakuwa unajiendesha wenyewe kwa lengo tu la kuwasaidia wao(hapa nazungumzia wale ambao wanategemewa na watu  ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kusimamia wala kufanya biashara zao,....tengeneza wewe biashara alafu faida ndo itumike kuwasaidia pale wanapohitaji na sehemu nyingine ya faida itumike kuendeshea hiyo biashara) 

Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa FIKIA NDOTO ZAKO.
 

Saturday 11 August 2018

FUNGU LA PESA,UNALOPOTEZA.

Karibu tena ndugu msomaji wa makala zetu za FIKIA NDOTO ZAKO  ,ni tumaini langu kuwa afya yako ni njema na unaendelea vyema na mapambano ya kila siku ya ushindi,maana kushindwa ni hatua ya kushinda......karibu tuendelee.


FUNGU LA PESA,UNAYOPOTEZA.
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        Leo nataka kukushirikisha  somo hili juu ya pesa inayopotea, pesa ambayo unaitumia kufanyia manunuzi lakini unaitoa kwenye fungo lisilo stahili,je ni pesa gani unaitumia kufanyia manunuzi? na ni aina gani ya manunuzi unayafanya?.........Hapa nataka tuzungumzie manunuzi ya vitu ambavyo havizalishi pesa,mfano radio,tv,kabati ya nguo nk.....je huwa unanua vitu hivyo kwa kutumia pesa  ya aina gani?

AKIBA ,hii ni pesa ambayo inatakiwa itumike kununulia vitu ambayo vinazalisha pesa nyingine,ukitumia pesa ya akiba kununulia kitu kisicho ingiza pesa ,unakuwa umeipoteza pesa hiyo.....Kwa nini unakuwa umeipoteza hiyo pesa?........kwa sababu ulitumia muda mwingi kuiweka hiyo pesa kidogokidogo,alafu unakuja kununua kitu ambacho badala kikuingizie pesa ,kinahitaji uendelee kutoa pesa ili ukihudumie,mfano ,unaweka pesa kama akiba ,alafu unakuja kununua radio,ambalo litahitaji uendelee kulihudumia kama vile kununulia CD nk, .....pesa umeyolimbikiza kwa muda mrefu,unaipoteza kwa siku moja,kimahesabu,hapo unakuwa unarudi nyuma,huendi mbele.........Unatakiwa ufa
nye nini?  ....iwekeze akiba yako,ikuzalishie faida kwanza.


                                                                                                             FAIDA,Hii ndio pesa inayotakiwa itumike katika matumizi ya aina mbili,ambayo ni  ;

  • Kununulia vitu visivyoingiza,mfano ,kama radio linauzwa Tsh 100000,ni bra uiwekeze hiyo  pesa ikuletee faida ambapo  hiyo faida ndio uitumie kununulia radio........hapo utakuwa hujapoteza.
  • Faida inatumika kupanulia uwekezaji wako.......                                                                                                                                                                                                                                                        Kabla ya manunuzi ,hakikisha unatambua hicho unachataka kukinunua kina ongezeko la aina  gani kwenye uhuru wako wa kifedha, hiin itakusaidia kufahamu aina ipi ya pesa itumike katikamanunuzi. 

  •    Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha.

  •                                        0652 134707              

Wednesday 4 April 2018

PANDE MBILI MUHIMU ZA UWEKEZAJI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani upo mzima kiafya,pia nikupe pole kwa wewe ambaye afya yako haipo sawa,Mungu akuponye.....karibu.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze pande mbili za uwekezaji,ambazo ni muhimu sana,nimejifunza kwangu ,pia nimejifunza kutoka kwa wawekezaji mbali mbali..............pande hizo ni zipi?,karibu tujifunze.


 PANDE MBILI ZA UWEKEZAJI.

Kabla hujaanza uwekezaji ,kuna sehemu mbili muhimu ambazo lazima ujipange,kuingia kwenye uwekezaji bila kuwa vizuri kwenye sehemu hizi,nakuhakikishia,uwekezaji wako utakuwa wa mashaka sana.......tuziangalie sehemu hizo;

1.PESA ZA KUENDESHA MRADI...Kitu amacho wengi tunakosea ni kwenye kupanga bajeti za kuendesha uwekezaji,wengi tunadhani ukisha fungua uwekezaji wako tu basi inatosha......hapana,kuna pesa ya kufungulia mradi na kuna pesa ya kuendeshea mradi wako,ni vitu viwili tofauti,wengi huwa tunaazisha biashara /uwekezaji tukiwa na pesa ya kufungulia mradi.......je mradi wako utajiendeshaje?.Bora uanze na mradi wa gharama ndogo ili ubakize kiasi cha kuendesha mradi wako,na sio uanzishe mradi wenye gharama kubwa ,halafu  ukose fungu la kuendeshea mradi wako,hutofika popote,utaishia njiani.


2.USIMAMIZI....Kabla ya kuanzisha mradi wako,jifanyie tathimini,una muda wa kutosha wa kusimamia mradi wako?....kama asilimia za kusimamia mradi wako ni chini ya 60,bora usianzishe huo mradi wako.Mafanikio ya uwekezaji hayapo kwenye kuanzisha uwekezaji huo tu,yapo kwenye jinsi ya kusimamia aina ya uwekezaji huo.Usimamizi mzuri una faida nyingi sana,ila kubwa na muhumu ni kuzalisha matunda bora,ukisimamia vizuri,mazao yatakuwa mazuri pia,maana usitegemee kuwa kuna watu watajituma kwa juhudi kusimamia mradi wako zaidi ya juhudi zako,wewe ndio unapaswa uwe na usimamizi mzuri ili wafanyakazi wako wafate ubora wako.



Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
        
        0652 134 707.

Monday 12 March 2018

JINSI YA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIDHAA YAKO.

Karibu sana kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,hongera kwa hali uliyo nayo,ipo sababu ya wewe kuwa ivyo.


KUSUDI LA SOMO.
Somo hili ni majibu ya watu ambao kila siku wanaogopa kufanya biashara au kuwekeza kwenye kitu ambacho tayari kinafanywa na wengine,kwa hofu ya kupata soko la kutosha.....karibu upate majibu. Kabla hujaendelea mbele,jifunze( JINSI YA KUTENGENEZA SOKO)........Karibu tuendelee.


JINSI YA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIDHAA YAKO.

Mwaka 2016 nilifanya utafiti wenye lengo la kugundua sababu zinazofanya wanakijiji wengi waendelee kulima bila kupata mafanikio ya kutosha,utafiti huu niliufanya kwenye kijiji kimoja mkoani Morogoro,,,,,pamoja na mengi niliyoyapata,yapo mambo mambo muhimu matatu ambayo wengi wetu tunakosea hadi kufanya soko liwe changamoto kubwa.


Jitahidi uongeze thamani ya pili kwenye bidhaa yako.mfano,kama una unaona kila mtu ana duka la mbolea,wewe fanya kinyume toa ushauri wa jinsi ya kutumia hiyo mbolea......watu watakuja kupata ushauri huo,wakiridhika ,ni ngumu wakanunue mbolea sehemu nyingine tofauti na kwako.


Usiingize bidhaa yako sokoni ukiwa na shida inayohitaji utatuzi wa haraka.....utajikuta unatumia mbinu ya kuishusha thamani ya bidhaa yako kwa kuiuza kwa bei ya chini,....wanakijiji wengi huingia kwenye kilimo ili watatue matatizo yao kwa haraka,mwisho wa siku wanajikuta wanauza mazoa yao kwa bei yoyote ile,tena wanauza haraka baada tu ya kuvuna......!


Ifanye bidhaa yako kuwa adimu,unaifanya vipi?......hapa unafanya bidhaa yako iwe inapatikana kwa utaratibu ambao wengi hawaufanyi,fatilia wateja wnapata usumbufu gani hadi kuja kuipata bidhaa yako......wapunguzie usumbufu huo....mfano badala ya kuwauzia sabuni kwenye gazeti,wauzie kwenye mfuko mweusi.


Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya fikia ndoto zako.

0652 134707

Friday 2 March 2018

MAPATO ,MATUMIZI YENYE KURUHUSU UWEKEZAJI.



Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo na jinsi ya kufikia ndoto zetu....nina imani kwa namna yoyote ile ,unaendelea vyema.....mshukuru Mungu kwa hali hiyo uliyonayo.ipo sababu ya wewe kuwa kwenye hali hiyo.......karibu sana.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu mapato na matumizi...hili ni somo pana sana na karibia kila mtu ana nidhamu yake kwenye elimu hii....ila nina kitu pia cha kukuongezea kwenye ufahamu wako.......ila hapa nataka wale wenye mawazo ya kutaka kutumia kidogo walichonacho ili waje wawekeze.....karibu sana.

MAPATO.
 Mapato ni kile kiasi unachoingiza,unaweza kukigawa kwa mwezi au kwa siku ...au hata kwa mwaka,je unaingiza shilling ngapi?...hapa ndipo kuna shida sasa.

Usidharau kiasi unachoingiza,hata kiwe kidogo namna gani,kiandike kwenye daftari,na kwa ushauri wangu ni vizuri ugawe kipato chako kwa sikiu.....mfano kama unaingiza elfu 30 kwa mwezi ,basi kwa siku utakuwa unaingiza 1000 kwa siku....nini umuhimu wake?.....tutajifunza kwenye matumizi.

Kama unaingiza chochote ,lazima uwe na uwezo wa kutoa chochote pia,hivyo heshimu sana unachokiingiza,na hakikisha unakuwa mbunifu kwa kidogo hicho unachokipata ili ukitumie kuongeza vyanzo vya mapato.

Ili uwe na uwezo wa kuongeza chanzo cha mapato ,lazima uwe vizuri kwenye kutambua unachoingiza ili ujibane kwenye matumizi kwa lengo la kubaki na kidogo utakachozalisha.

MATUMIZI

Hapa ndipo kuna matatizo sasa,.....nilisema ugawe mapato yako kwa siku ili ujipime matumizi yako kwa siku yapo juu/chini ya unachoingiza kwa siku?.......je kiasi kinachozidi unakipeleka wapi?....

  1. Tengeneza bajeti ya siku moja,kisha tafuta jumla kwa mwezi unatumia kiasi gani,,,,ila jitahidi unachotumia kwa siku kisizidi kile unachoingiza .
  2. Kwenye maisha kuna dharura ,kutenga kiasi cha dharura sio vibaya,ila lazima uangalizie na dharura ambazo unaweza kuleta matokeo,nyingine ziache zipite.
  3. Namba moja nafikiri inakufundisha kutumia kwa nidhamu,usitumie kilicho nje ya uwezo wako.....je bajeti yako inaruhusu ubaki na chochote?
  4. Tunashariwa kuweka akiba kabla ya matumizi ,ila ni vizuri ukafahamu kwanza mapato yako yakoje kisha ndio uanze kuweka akiba.
  5. Akiba ipe thamani ya kipato kingine,akiba ndio mtaji wako sasa,kama unatafuta mtaji kila siku na huna nidhamu ya kuweka akiba utasumbuka sana.....kama una akiba basi tayari una mtaji mmojawapo.....
NB. Kuwekeza au biashara ni elimu nyingine tofauti na elimu ya kuweka akiba,ingawa unatakiwa uweke akiba ukiwa unafahamu nini unatakiwa kufanya kesho......!!!


Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa label ya FIKIA NDOTO ZAKO.

0652 134707



Wednesday 28 February 2018

MAMBO YANAYO PUNGUZA UWEZO WA KUFIKIRI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu....nikupongeze kwa maamuzi yako ya kuamua kuwa mtembeleaji wa blog hii,nina amini hutobaki kama ulivyo....lazima mafunzo haya yatasogeza hatua zako mbele ....karibu.

KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza sababu zinazopunguza uwezo wa kufikiri,.....na hili somo limekuja maalumu kwa sababu huwezi kufanikiwa nje ya fikra zako,pale ulipo ni matokeo ya kile unachokifikria....mambo gani yanapunguza uwezo wa kufikiria?...jifunze kwa nini rafiki yako hakuamini(urafiki)......


MAMBO YANAYOPUNGUZA UWEZO WA KUFIKIRI.

1.Mahusiano mabovu,..Hapa nazungumzia mahusiano ambayo yamekufanya kuwa mtumwa,haya ni yale mahusiano ambayo yanakufanya muda wote uyafikirie,...kufikiria mahusiano sio vibaya ,ila ubaya huja pale ambapo uliye naye kwenye urafiki amekutengenezea mazingira ya kutojiamini,..muda mwingi utakuwa unafikiria ufanye nini ili asiondoke na matokeo yake utajikuta unakwamisha mipamgo yako mizuri kwa sababu hutoipa nafasi kuifikiria mipango hiyo.

2.Marafiki,Jaribu kuchunguza kile unachokiwaza sana,kisha jiulize ,kwa nini unakiwaza sana?......fatilia marafiki zako wa karibu,wana mtizamo gani kwa kile unachokiwaza sana?.....kama unazungukwa na marafiki wenye uwezo mdogo wa kufikiri,usitegemee kuwa na fikra zaidi yao,.....

3.Ukosefu wa maarifa,Watu wasio na malengo hawpati shida katika kufikria kwa sababu hakuna wanachokitafuta,na mara nyingi watu ambao hawana malengo hupungukiwa pia na  maarifa,....ukipata maarifa,lazima utaongeza uwezo wako wa fikra ili uyahamishe malengo hayo kuwa vitu kamili......kwa hiyo kadri unavyokosa maarifa ya kutosha kuhusu jambo flani ndivyo uwezo wako wa kurifikria jambo hilo unapungua.

4.Historia ya maisha yako,Changamoto ni kinu cha mafunzo ila kwa wasiofahamu hilo mara nyingi hujikuta kwenye falsafa hasi...watu hawa mara nyingi huamini kuwa waliyoptia yaliwapunguzia vigezo vya mafanikio,hivyo hawaoni sababu ya kufikiria mambo  makubwa zaidi,muda mwingi hufikria waliyopitia.....

Hapo ulipo ni matokeo ya uwezo wako wa kufikiri,je upo sehemu sahihi?,kama sio hakikisha unapunguza mambo unayoyapokea kutoka kwenye mazingira yanayokuzunguka,.......jitengenezee uwezo mkubwa wa kufikri ili ubadilishe hivyo ulivyo.


 Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha ,mmiliki wa label ya FIKIA NDOTO zako,

      0652 134707.


Friday 16 February 2018

KWA NINI RAFIKI YAKO HAKUAMINI?

Tarehe 22 FEBRUARY ni siku ambayo nasherehekea siku ya kuzaliwa kwangu......pamoja na furaha yote ya siku hiyo,huwa ni siku pia ambayo nimejiwekea utaratibu wa kukumbuka mambo ambayo yalitokea kwenye safari yangu ya maisha......kiufupi safari yangu kwa asilimia kubwa ilikuwa ya maumivu......hapo ndipo nakumbuka nafasi ya rafiki katika maisha yangu........karibu.

KUSUDI LA SOMO.

Lengo la somo hili ni kutaka kutoa majibu ya kwa nini huna imani na rafiki yako?.....au kwa nini yeye hakuamini?.....hii ni vita kubwa sana ambayo inayumbisha urafiki wa watu wengi na kusababisha kifo cha urafiki..........karibu.

KWA NINI HUNA IMANI NARAFIKI YAKO?.......Sabubu za kwa nini humuanini rafiki yako zipo sawa na kwa nini yeye hakuamini.........hivyo ngoja nielezee sababu zinazo fanya ukose imani na rafikiyako.....kisha utazigeuzia upande wa pili.

1.HISTORIA YAKE.......kufahamu historia ya rafiki yako sio vibaya.na inaweza isiwe hatari kabisa kwa yeye kuptia historia hiyo...tatizo liko wapi?.........hadi wewe kukubali kuwa na urafiki na mtu unayejua historia yake,ni wazi uliamini kuwa kabadilika....lakini kubadilika kwake haina maana kuwa attaishi bila madhaifu yoyote yale........kosa lipo pale ambapo utaanza  kuunganisha madhaifu yake ya kawaida na maisha aliyopitia.....ukiruhusu hali hiyo,nakuhakakishia,hutomuamini hata kidogo,utakuwa mtu wa wasiwasi tu muda wote......ukiona huna busara ya kubeba historia ya nyuma ya rafiki yako,au umejiaminisha kuwa bado hajabadilika......kuwa mbali.

2.HISTORIA YAKO,.....Usipokuwa mwenye hekima na busara,kile unachokitenda au umechotendewa au kuona wengine wakitendewa,kitakufanya uamini watu wote duniani wapo hivyo.....hali hii ukiiruhusu,itakufanya ujihami.....unajua madhara ya kujihami?.......KWANZA wewe mwenyewe utakuwa sio muaminifu,pili, rafiki yako utampa uhusika wako ....hutomuamini pia........kuna kipindi inabidi uishi bila hamasa za nje,hamasa ambazo ni za mawazo hasi.,,,zitakufanya uingiwe na ugonjwa wa kutoamini watu wasio na hatia............

 Hapa nakumbuka utafiti wangu ambao niliufanya ili kugundua ni kwa namna gani watu hawana imani na marafiki zao sababu zilizosababisha hivyo........nilitumia marafiki wa jinsia tofauti,,,,wavulana kumi ambao nilwaulizwa wanajisikiaje ikitokea simu ya rafiki wake wa kike  haitapokelewa au itakuwa busy(kutumika)  pindi wakiwatafuta.......maatokeo yalikuwa hivi:

SITA walisema ,wakikuta hali hiyo,watahisi kusalitiwa,wawili walisema watajisikia vibaya tu.....wengine wawili wa mwisho walisema hiyo ni hali ya kawaida tu......kwa ufupi utafiti huo unaonyesha ni namna gani uaminifu umepungua ......nilivyofatilia zaidi kwa marafiki hao sita ndipo nikapata somo hili la leo......ndani ya sababu hizo mbili kuna sababu ndogo ndogo nyingi.....


Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.....Mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO ZAKO.

                                  06552 134707.


Friday 9 February 2018

MAMBO MATANO MUHIMU KABLA YA BIASHARA.

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,nikupe pongezi tu kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutembelea blog hi,hutobaki kama ulivyo....karibu tujifunze.


KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo hili nataka tujifunze mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukusaidia katika kuanzisha biashara yako.........mambo haya nimejifunza kupitia uzoefu wangu niliojifunza kwenye biashara ambayo nimeahi kuifanya na kwenye uwekezaji ambao tayari nipo naufanyasasa, ,pia mengine nimefanya utafiti kutoka kwa  watu wengine........Karibu tujifunze.


Nafikiri kama wewe sio mfanya biashara ,basi utakuwa umewahi kuwaza kuwa mfanya biashara......na kwa sababu umeamua kusoma makala hii,kuna mambo mawili....moja,utakuwa umewahi kufanya biashara lakini haikukulipa,pili utakuwa una shauku kubwa ya kuanzisha biashara ......ni mahali sahihi,.......karibu tujifunze mambo hayo matano.


1.Kuwa makini na biashara zinazofika mtaani kuwa zinaingiza pesa haraka,......inaweza kuwa ni kweli ndio,ila mvuto huo usiwe ndio hamasa namba moja ya kukufanya uifanye bishara hiyo.....biashara inayosifika sana huwa haikawii kuchoka kwa sababu hufanywa na wengi,......kwa hiyo ifatilie kwa kina upate taarifa kamili za wakati huo kuhusu soko lake.....mfano wa biashara zilizosifika ni kilimo cha matikiti,mpunga,bodaboda na bajaji.......bodaboda na matikiti soko lake sio lile ambalo lilisifika miaka michache iliyopita,..limeshuka.....usiingie kwenye biashara bila kuwa na taarifa za wakati huo.

2.Jitahidi uiandike biashara kwenye daftari kabla ya kuanza kuifanya,........andika kuanzia mtaji ,soko lake na malengo ya wewe kuamua kuifanya biashara hiyo.....jipe kikomo cha kukamilisha malengo hayo........weka mikakati itayokufanya uyafikie malengo hayo kwa kupitia biashara hiyo......mfano mimi ni mkulima ambapo malengo yangu ni kumiliki ekari zaidi kumi hadi mwaka kesho kutoka kwenye chache nilizonazo.

3.Weka fungu la pesa,au anzakutafuta pesa ili ukamilishe biashara hiyo sasa uliyoiandika kwenye daftari,...jitahidi tu usitumie pesa yako yote kuanzia biashara,.....tumia akiba kuanzishia biashara.

4.Fanya maamuzi magumu,ishinde hofu ya kushindwa....ukimaliza maandalizi ,mara moja anza biashara.......ila hakikisha umetengeneza soko kabla ya biashara.....tambua ni watu wa aina gani umekusudia waipate bidhaa yako.

5.Fanya biashara kwa juhudi zako zote,kwa ubunifu ,hakikisha unafanya ambayo wengine hawayafanyi kwenye biashara iliyo sawa na wewe.....kuwa mvumilivu na mwenye subira,...biashara mara nyingi hainzi sawa na ulivyotarajia ...utasumbuka kidogo mwanzoni hadi kuja kufikia matarjio.



     Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa label ya fikia ndoto zako.


                             See you at the top.
                                  0652 134707

Friday 12 January 2018

WAZO LA UJASIRIAMALI.

Karibu sana kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,....kwanza nikupongeze kwa kuanza mwaka mpya vizuri,nafahamu kuna mapito mengi,mengine yalikuumiza,mengine yalikupa raha,ila yote na yote kila ulipopita,kuna kitu ulijifunza.........kwa kuanza na mwaka huu ,nimeona vyema nikushirikishe somo letu zuri ambalo kwa sehemu nina amini litakufanya uwe wa tofauti.


KUSUDI LA SOMO.
Somo letu la leo ni wazo la ujasiriamali,somo hili litatupa hatua za kufanya wazo letu lizae matunda,inawezekana kwa muda mrefu umekuwa ukiweka mawazo kuhusu biashara /uwekezaji flani.ila mwisho wa siku unaishia kuwaza tu,wazo lisilotekelezeka ,huwa ni wazo sisilo la kijasiriamali,.....wazo la kijasriamali ni nini?.....karibu tujifunze.



WAZO LA KIJASIRIAMALI.
Hili ni wazo ambalo mwisho wa siku ,linatekelezwa,...wazo la kijasriamali huwa lina hatua zake ili liwe na sifa ya kutekelezeka,..wazo linapotekelezwa ,lazima lilete matokeo,matokeo sio lazima yawe na faida tu,yanaweza kuwa na hasara pia......ila faida ya kuwa na wazo la kijasiriamali ni mafunzo tunayoyapata(iwe ni faida au hasara).............jiulize wazo lako ni lipi?, umelipa hatua zipi?


HATUA ZA WAZO LA KIJASIRIAMALI.
Wazo la kijasriamali,lina lina hatua zake tatu,ambazo ni kama zifatazo;

1.WAZO,hii ni hatua ya kwanza,lazima uwe na wazo,wazo una amini litakufikisha uendapo,wazo hilo inatakiwa litanguliwe na kujitambua........ukijitambue wapi unataka kwenda,temgeneza wazo la kuongoza safari yako,.....mfano wazo la kilimo,ufugaji ,biashra flani,elimu nk.....wazo lipi litakufikisha uendapo?......hapa namaanisha nini ufanye ili ufikie unapotaka kwenda?

2,MAANDALIZI: Ukisha kuwa na wazo tayari,anza maandalizi.....maandalizi ni pamoja na kuweka mikakati itayosaidia kuliwezesha wazo lako,.....fanya tafiti za kutosha,jitahidi utambue uhusiano uliopo kati ya wazo lako na mazingira,,,,hii itakusaidia kutambua kama wazo lako hilo litasaidia kutatua chngamoto za watu?...... wazo lako hilo litakupa uhuru wa kujitegemea kuliko kutegemea?

3.UTEKELEZAJI.
Huu ni muda ambao ni wa utekelezaji tu,.....kosa ambalo wengi tunafanya ni kuchangamya vipindi,....kipindi cha utekelezaji ndio tunafanya maandalizi......mara nyingi watu wanao changanya vipindi,huwa wanaishia kupanga tu...........MUHIMU TU....kumbuka kila hatua lazma utakutana na hofu ,jitahidi tu kupunguza mazingira yenye kukupa hofu,.....hofu ndio chanzo kinachofanya watu waishie kwenye hatua ya kwanza.



     Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa fikia ndoto zako label.
                             mawasiliano: 0652 134707.