Thursday 7 October 2021

USIJISAHAU KWENYE MAZINGIRA HAYA

 USIJISAHAU KWENYE  MAZINGIRA HAYA. 

Habari ndugu msomaji wa makala zetu za fikia ndoto zako ikiwa ni muda kidogo umepita bila kukuandikia makala kupitia blogu leo tena ni siku ya bahati ya pekee kukuandikia makala hii maalum, ni makala maalum kutokana na ujumbe wake kuwa mchungu kuumeza lakini muhimu na wenye manufaa ikiwa utakubali kuumeza, karibu sana tuambatane. 

Kama ilivyo kichwa tajwa hapo juu somo linahusu kutojisahau katika mazingira upitiayo na kabla sijaendelea  sote kwa pamoja tujibu maswali haya kimya kimya;

#Umewahi kujutia kwa kutamani siku zirudi nyuma utumie mazingira fulani kufanya jambo zuri la maisha yako? 

# Umewahi kuwa na nafasi ambayo ilikuruhusu ufanye jambo fulani na sasa huwezi tena kulifanya kutokana na wewe kuwa nje ya nafasi hiyo kwa sasa? 

#Umewahi kuona watu wakiwa maarufu na sasa tena unawaona wakiwa katika hali ambayo hakuna anayetamani kufahamu habari zao ?

Bila shaka kuna majibu yanakujia akilini kuwa kuna nyakati na jambo ndani ya nyakati hizo ambalo ukilifanya hutojutia ( hapa nazungumzia jambo lenye matokeo chanya), ugumu ni utatambuaje nyakati hizo zimebeba jambo lipi? 

Kila nyakati kuna kusudi la wewe kupitia humo hilo ndio jambo kuu ambalo unatakiwa kulifanya kwa juhudi zote ikiwezekana kwa kipaumbile kikubwa zaidi kwa mfano ukienda shule kuna mambo mengi ya kufanya lakini kuu ni kusoma kwa bidii ili baadaye usitamani tena kurudia shule ili usome kwa bidii wakati huo utakuwa haiwezekani tena pengine. 

Unapopitia mazingira fulani penda sana kutafuta lengo kuu la wewe kuwa hapo na jitahidi kulifanya kwa juhudi zote, karibu kila mtu ana wakati wake wa kuwa bora katika eneo fulani hapo ndipo hupaswi kulewa mazingira bali kusimama kweli kwenye nafasi yako kwa sababu ubora huo unakuandaa kuwa mtu fulani kesho.

Maisha ni makusanyo wa nyakati mbali mbali unazopitia leo mpaka kufikia kesho utakuwa mtu mwingine tofauti kutokana na alama ulizojikusanyia kwenye nyakati hizo ulizopitia  hivyo sio wakati wa kubeza na kujisahau kwa nyakati unazopitia tafuta ubora wako uko wapi na uishi ubora huo kwa juhudi zako zote. 

Makala hii imeandikwa na  Saul Kalivubha 

Mwanasayansi tiba 

+255652134707