Wednesday 4 April 2018

PANDE MBILI MUHIMU ZA UWEKEZAJI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani upo mzima kiafya,pia nikupe pole kwa wewe ambaye afya yako haipo sawa,Mungu akuponye.....karibu.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze pande mbili za uwekezaji,ambazo ni muhimu sana,nimejifunza kwangu ,pia nimejifunza kutoka kwa wawekezaji mbali mbali..............pande hizo ni zipi?,karibu tujifunze.


 PANDE MBILI ZA UWEKEZAJI.

Kabla hujaanza uwekezaji ,kuna sehemu mbili muhimu ambazo lazima ujipange,kuingia kwenye uwekezaji bila kuwa vizuri kwenye sehemu hizi,nakuhakikishia,uwekezaji wako utakuwa wa mashaka sana.......tuziangalie sehemu hizo;

1.PESA ZA KUENDESHA MRADI...Kitu amacho wengi tunakosea ni kwenye kupanga bajeti za kuendesha uwekezaji,wengi tunadhani ukisha fungua uwekezaji wako tu basi inatosha......hapana,kuna pesa ya kufungulia mradi na kuna pesa ya kuendeshea mradi wako,ni vitu viwili tofauti,wengi huwa tunaazisha biashara /uwekezaji tukiwa na pesa ya kufungulia mradi.......je mradi wako utajiendeshaje?.Bora uanze na mradi wa gharama ndogo ili ubakize kiasi cha kuendesha mradi wako,na sio uanzishe mradi wenye gharama kubwa ,halafu  ukose fungu la kuendeshea mradi wako,hutofika popote,utaishia njiani.


2.USIMAMIZI....Kabla ya kuanzisha mradi wako,jifanyie tathimini,una muda wa kutosha wa kusimamia mradi wako?....kama asilimia za kusimamia mradi wako ni chini ya 60,bora usianzishe huo mradi wako.Mafanikio ya uwekezaji hayapo kwenye kuanzisha uwekezaji huo tu,yapo kwenye jinsi ya kusimamia aina ya uwekezaji huo.Usimamizi mzuri una faida nyingi sana,ila kubwa na muhumu ni kuzalisha matunda bora,ukisimamia vizuri,mazao yatakuwa mazuri pia,maana usitegemee kuwa kuna watu watajituma kwa juhudi kusimamia mradi wako zaidi ya juhudi zako,wewe ndio unapaswa uwe na usimamizi mzuri ili wafanyakazi wako wafate ubora wako.



Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
        
        0652 134 707.