Sunday 16 July 2017

SIRI YA KUMI YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani wewe hapo ni mzima wa afya,kama ni mgonjwa usijali,Mungu yupo kwa ajili yetu wote.


  KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya kumi ya urafiki ambayo ni UKWELI ,ila kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukapitia na kujifunza kwanza siri ya tisa ya urafiki(SIRI YA TISA YA URAFIKI).


           SIRI YA KUMI  YA URAFIKI   (UKWELI).
Kwenye urafiki kuna kuwekana wazi mambo,ila kabla ya kuweka wazi mambo yako kwa rafiki yako lazima kwanza uwe umejihakikishia uaminifu wa kutosha ,ila wakati mwingine kuna watu wapo kwenye urafiki kwa kuficha ukweli,wanatumia uongo kutengeneza ukaribu wao....je hii ni sahihi?


Wanasaikolojia wa mambo ya mahusiano wanazungumza kwamba ...Watu wanatafuta wasiyoyafahamu,hawana shida na wanayoyafahamu,,,hii tafasiri yake ni kwamba rafiki yako anatafuta mambo ambayo hayafahamu kutoka kwako,inaweza kuwa umemdanganya jambo fulani,siku akilifahamu lazima sura ya urafiki wenu ubadilike,...jifunze kuwa mkweli.


Ni bora kumficha mtu jambo kuliko kumdanganya,sababu za kumficha mtu jambo zinaweza kuwa zina maana kubwa kuliko sababu za kumdanganya mtu,,,,,kumdanganya maana yake umemwambia ukweli wenye hila ndani yake,umetafuta kuaminiwa kwa njia isiyosahihi.



Ukiona rafiki yako amekukwepa kwa sababu umemwambia ukweli,jua huyo sio mtu mzuri kwako,maana ukweli una thamani kubwa sana kwenye urafiki wa kweli,urafiki ambao una lengo la kufikia mafanikio makubwa.


Tatuzo ukisha anza na uongo tu kwenye urafiki wako,itakufanya kila siku uendelee kutengeneza uongo wa kudumisha uomgo wa mwanzo....urafiki wa aina hiyo una umuhimu gani?, ukijiona mjanja wa kudanganya ,tambua thamani yako inashuka,pia unapoteza muda wako kudanganya na kuendeleza uongo wako.



Kitabu cha SIRI ZA URAFIKI kinaelekea kuwa tayari,utakipata kwa mawakala wa fikia ndoto zako....


                           See you at the top.
                    Scientist Saul kalivubha.
                              0652 134707

Monday 10 July 2017

SIRI YA TISA YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa uzimab wake kwangu ,pia ni imani yangu kuwa wewe ni mzima........karibu.



   KUSUDI LA SOMO.

Tunaendelea na somo letu la siri za urafiki,leo ni siri ya tisa ambayo ni mipaka ya ufahamu,...kabla yakuendelea na somo letu hili,ni vyema ukajifunza kwanza siri ya nane ya urafiki(SIRI YA NANE).,karibu tuendelee.



SIRI YA TISA YA URAFIKI(MIPAKA YA UFAHAMU).

Katika urafiki ni jambo la kawaida sana kufahamu habari za rafiki yako,swala hili ni zuri sana ikiwa unataka kufahamu habari hizo kwa lengo la kudumisha urafiki,ila kuna habari zingine za rafiki yako zinaumiza,kama hauna ujasiri,badala ya urafiki kuimarika,utavunjika......kabla ya kuanza kuzifatilia habari za rafiki yako jitahidi kufahamu haya.

  • Weka mipaka,hakikisha unafahamu mambo yenye fada tu katika ujenzi wa urafiki.
  • Kuwa makini na chanzo cha habari, sio kila chanzo cha taarifa za rafiki yako ni chanzo sahihi.
  • usifatilie habari za rafiki kama kumpeleleza,akijua urafiki wenu utapoteza uaminifu,kuwa mpole na taratibu tu utafahamu mengi kuhusu yeye.
  • Fanyia kazi mambo utayo yafahamu kwa rafiki yako kwa lengo la ujenzi na sio kwa leng la kumuhukumu rafiki yako.


Mwamdishi mmoja wa mambo ya saikolojia aliwahi kuandika kanuni moja muhimu sana ,kanuni hiyo ni hii   "Msongo wa mawazo(Stress) unaongezeka,kila ufahamu unapoongezeka"
Kanuni hii inasaidia kupunguza kufahamu mambo yasiyokuhusu,watu wengi kwenye urafiki wanaishi kwa mawazo kwa sababu tu walifatilia mambo yasiyo wahusu ya rafiki zao.


Kuna mambo sio lazima uyafahamu kutoka kwa rafiki yako,utaumiza kichwa bure tu,tena kibaya zaidi hakuna uwezo wa kuyabadilisha mambo hayo,tena kuyafahamu kwako hakuna faida yoyote kwenye uraki wako .....


                        See you at the top.
                            Saul kalivubha
                               0652 134707.

Sunday 2 July 2017

SIRI YA NANE YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. ......Karibu sana kwenye muendelezo wa somo letu la urafiki, nina imani kuna kitu unajifunza. ..karibu.

LENGO LA SOMO. 
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nane ya urafiki kulingana na mpangilio wangu, siri hiyo ni  Jichunguze tabia yako. ... .Unaweza pitia kwanza SIRI YA SABA, kisha uje tuwe wote. .....karibu tuendelee.

SIRI YA NANE  (JICHUNGUZE TABIA YAKO ).

Urafiki unapitia mazingira mengi sana, kila mazingira huwa yanahitaji style  (mfumo ) wa kuishi ili kuhakikisha urafiki unaendelea na thamani yake.Ila kuna kipindi mtu anaona rafiki yake kabadilika tabia, amekuwa na tabia mpya ambayo hapo nyuma hakuwa nayo.

  • Je umewahi kukutwa na hali hiyo? 
  • Urafiki wako ulikuwa na sura gani baada ya hali hiyo? 
  • Unafikiri chanzo chake ni nini? 
Ni hali ya kawaida sana kusikia mtu akilaumu kuhusu kubadilika kwa tabia ya rafiki yake, tena kwa sababu nyingi za kujiona yeye mshindi na kumfanya rafiki yake kuwa mwenye hatia. ..
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.

Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.

            See you at the top.
           scientist Saul kalivubha.
               0652 134 707.
0