Thursday 30 March 2017

HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni siku nyingine Mungu amefanya tukutane kwa lengo la kufundishana jinsi ya kufikia ndoto zetu
.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu hatua ya awali katika safari ya maisha yenye ushindi, bado kuna watu ambao wamejaribu kila namna ya kupiga hatua ili kufikia malengo yao ila badala ya kusogea mbele wao wanarudi nyuma. ........Kibaya zaidi watu hao wameshindwa kufanya tasmini ya matokeo yao ambayo hayaridhishi. ..
Tatizo nini? .....zinaweza kuwa zipo sababu nyingi ila sababu kubwa inaweza kuwa ni kosa la awali. ...ni lipi hilo? .....karibu tujifunze.

 HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.
Unapoweka malengo ya safari yako lazima ujue mambo muhimu ya kukufanya upige hatua, bila hivyo unaweza kuwa na malengo mazuri yasiyo tembea, zipo njia nyingi ambazo watu tofauti tofauti wanaweza kuzieleza, ila kwa upande wangu taeleza njia tatu za kufanya uweze kupiga hatua, njia ambazo hutengeneza hatua ya awali na muhimu kwenye mafanikio yako. .....njia hizo ni hizi ;

1.Kuwa na marafiki sahihi.ni usemi wa kila siku kuwa mafanikio yako yapo kwa rafiki yako, ila wengi huwa hatujui hilo, bora utumie muda mrefu kuishi bila rafiki kuliko kuwa na rafiki asiyetambua umuhimu wa kusudi lako,Watu wengi wameshindwa kufika waendapo kwa kuwa karibu na marafiki hasi, ....lazima uwe na rafiki sahihi ili uweze kupiga hatua
.
2.Matumizi ya muda. Kwenye matumizi ya muda ndipo kuna mafanikio yote  (tembelea Google search uandike muda wa ziada kalivubha blog ujifunze matumizi sahihi ya muda).Ni ngumu kupiga hatua yoyote ya mafanikio ikiwa bado una matumizi mabovu ya muda,  kuna mambo ambayo lazima uyafanye ili yakupe kibali cha kuendelea, mambo hayo yanahitaji uwe na matumizi mazuri ya muda wako, hatua ya awali ni pamoja na kuwa na ratiba zinazofata muda wako vizuri.

3.Kutambua madhaifu yako. ..wanafalsafa wamewahi kuzungumza kuwa, .."mtu anaekushinda mafanikio kuna mambo anayofanya ambayo wewe hufanyi "..nini maana yake?.ni muhimu kufanya tasmini ya madhaifu ambayo yanaweza kuwa sababu ya kuzuia hatua zako, hiyo itakusaidia kujifunza namna ya kupiga hatua kwa kutumia njia tofauti tofauti zenye kuziba madhaifu yako, ..kujifunza kwa kupitia watu waliofanikiwa sio vibaya, lazima ujue nini ambacho wao wanakushinda .

Ni hatua chache sana za kukufanya upige hatua kwenye malengo yako, ila ni watu wachache sana wamekamilika katika hatua zote hizo tatu, ...fanya tasmini ya maisha yako.

          See you at the top.
          scientist Saul kalivubha.
              (0652134707 )

Wednesday 22 March 2017

MUDA WA ZIADA -2

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha kila jumatano
jumatano ya wiki, nashukuru Mungu
kwa kuendelea kunisamamia....karibu.
tujifunze.

KUSUDILA SOMO.

Kabla ya kuendelea na kusudi la somo letu hili, nikukumbushe kuwa somo letu lina sehemu mbili. 1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.........

ili tuwe sambamba pitia somo la sehemu ya kwanza, tembelea Google search na kuandika kalivubha blog muda wa ziada au Tembelea page ya FIKIA NDOTO ZAKO Facebook.
Leo tunaendelea na sehemu yetu ya pili.
kumbuka kuwa muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja, huu ni ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi. .....karibu tuendelee.

2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.....

KUWA NA MAMBO MENGI;Kuwa na mambo ambayo yana positive effect (matokeo chanya)kwenye ndoto yako sio tatizo, tatizo ni pale mtu anapokosa utaratibu katika kupanga mambo yanayostahili kwanza yawe mbele. ..ukianza kutumia muda wako wa ziada leo  kufanya mambo ya kesho hata kama ni mazuri, utakuwa unapoteza muda, ....lazima uwe na utaratibu katika kufanya mambo yako ili upate muda wa kutosha kufanya yanayostahili kwanza.

STAREHE; hapa ndipo kundi kubwa la watu lipo, maana wengi wanajua starehe lazima itumie pesa  .........hata
ukitumia muda wa ziada kwa mambo yaliyo nje ya ndoto zako tunasema upo
kwenye starehe.
Hili tatizo wanalo watu wengi ambao hawana malengo, ambao hawaumii kutumia sentensi hiii. ."NIPO NAPOTEZA MUDA ".....kila muda unaopoteza lazima utaulipa , je utaulipaje? .....utaulipa kwa majuto.

KULIPA NAFASI JAMBO MOJA. ...hapa tuelewane vizuri , kuna watu ambao wapo addicted na jambo flani, muda wote wa ziada anakuwa busy na jambo hilo tu. .....sio tatizo ikiwa ndio maisha yako yapo kwenye jambo hilo, ..ila kama kuna mambo mengine yamebeba maisha yako ,utakuwa unapoteza muda kwa kufanya jambo hilo moja. ....toa nafasi kwa mambo mengine pia. ...

NB....Kila muda unaopoteza, lazima utaulipa kwa majuto yasiyo na tiba,wengi wetu huwa tunapuuzia usemi huo sababu madhara ya kulipa muda huo huwa yanachelewa. .ila
muda ukifika wa kulipa muda huo lazima mtu akumbuke mambo yaliyo poteza muda wake. .....
Tumia muda wako vizuri leo, ndoto zako zipo kwenye matumizi mazuri ya muda wako wa leo. .........
Unatumiaje muda wako wa ziada?

Karibu kwenye somo mpya muda kama huu. ....

                   See you at the top.
            scientist Saul kalivubha.
                    0652 134707.


Wednesday 15 March 2017

MUDA WA ZIADA -1

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa wema wake kwangu, ni jambo jema kama na wewe una utaratibu wa kumshukuru Mungu kwa makuu yake kwako.
Leo ni siku nyingine tena ambayo nimeona vyema tujifunze jinsi ya kutumia muda wetu vizuri ili tufikie malengo yetu.

KUSUDI LA SOMO .
Lengo la somo letu hili ni kujifunza mambo makubwa mawili ambayo ni.
1. SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA. 2.MATUMIZI MABOVU YA MUDA
WA ZIADA.

Kabla ya kuanza na sehemu ya kwanza ya somo letu, tuangalie maana ya muda wa ziada.
Muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja , huu ni ule ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi.

      1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.

Utofauti uliopo kati ya watu wenye majukumu sawa ila mafanikio tofauti upo kwenye jinsi ya kutumia muda wao wa ziada, zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha utofauti huo,
ila matumizi ya muda wa ziada yana nafasi kubwa kwenye kufanya utofauti huo. siri zilizopo kwenye muda wa ziada ni hizi hapa.


Kwenye muda wa ziada ndio sehemu pekee ambayo mtu unaweza tulia na kufanya tasmini ya safari yako, umefikia wapi, na nini ufanye ili kufika uendapo.
Watu wengi huendelea kuishi maisha yasiyo badilika sababu hawafanyi tasmini ya maisha yao.....huwezi kufanya maamuzi ya kubadilisha aina ya maisha unayoishi ikiwa kwenye muda wako wa ziada unautumia kuboresha mazingira ya maisha yenye matokeo hasi.


Kwenye maisha tunapitia mazingira mengi sana hadi kufikia ndoto zetu, kila mazingira yamebeba mchango mkubwa wa ndoto zetu......kuna uwezekano wa kutofikia uendapo ikiwa  utafanya uzembe katika mazingira yako unayopitia.......ili uweze kujua mazingira uliyopo yamebeba nini kwa ajili yako, lazima uwe na muda mzuri wa kuchambua mazingira hayo. .....!

Wana falsafa huwa wanasema kwamba. ....   "usipo charge akili yako huwezi kuwa na uelewa
Nini maana yake?   walimaanisha ili  tuweze kuwa watu wapya lazima tuwe na muda wa
wa kuingiza mambo mapya na yenye  kubeba malengo yetu.....lazima upate muda wa
kuongeza maarifa,utaongeza vipi?  ...fatilia somo la njia za kuongeza maarifa, litafata baada
ya somo hili.

Kuna watu ambao ni wazee sasa, ila hawajui utofauti wao ni upi, kila mtu ana kitu cha
tofauti ambacho ni zawadi kutoka kwa Mungu, ila kuigundua inahitaji muda wa ziada.
utofauti wako ndio umebeba mafanikio yako, kama una matumizi mabovu ya muda wako,
unaweza usijue utofauti ulionao  (labda ije neema ya Mungu tu ).....

Jiulize, unatumia vipi muda wako wa ziada? ...zipo gharama za kulipa kila muda unaopoteza,
unazifahamu? .......................Tukutane wiki ijayo.


                           see you at the top.
                             scientist Saul kalivubha.
                              (0652 134 707 )









Wednesday 8 March 2017

HOFU YA KUSHINDWA -3

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, upande wangu nashukuru Mungu anazidi kuonekana katika maisha yangu,ni jambo la kushukuru Mungu ikiwa na wewe ni mzima wa afya.
Karibu tena katika sehemu ya tatu na ya mwisho wa somo letu la HOFU YA KUSHINDWA.
NB. unaweza fatilia sehemu ya 1 na 2 ya somo hili kwa kuingia Google na kuandika. ...hofu ya kushindwa kalivubha blog  , ni vyema ufanye ivyo ili twende sambamba na sehemu yetu hii ya tatu. 

KUSUDI LA SOMO. 
Leo tuna jifunza sehemu ya tatu ya somo letu,kumbuka somo letu lina sehemu tatu ambazo ni  1.CHANZO CHA HOFU YA KUSHINDWA 2.MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA NA 3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA. 
NB. Kumbuka tu huwezi kufanikiwa kufanya maamuzi sahihi ikiwa upo kwenye hali ya hofu. 


                3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA .
Leo tuangalie njia za kuishinda hofu ya kushindwa ambayo ni ugonjwa hatari sana katika mafanikio yetu, na mbaya zaidi, watu wengi ni wagonjwa wa ugonjwa wa HOFU. ......
Kuna sehemu nyingi ambazo mafanikio yake yanahitaji uishinde kwanza hofu, siwezi kuelezea kila sehemu ,ila nimechagua sehemu tatu ambazo taeleza jinsi ya kukabiliana na hofu kwenye sehemu hizo, ukiweza vizuri itakusaidia kwenye sehemu zingine. 
Sehemu hizo ni BIASHARA, MAHUSIANO NA MAFANIKIO KWA UJUMLA. 
NB. Kumbuka hofu ni tatizo ambalo linahitaji muda ili kulimaliza, na lazima muhusika mwenyewe ajitambue kwanza. 

BIASHARA; watu wengi tumeishia kuwa na malengo ya bila vitendo katika kuanzisha biashara kulingana na HOFU YA KUSHINDWA, nini kifanyike? .....kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unatambua kuwa changamoto zipo, usianze ukitegemea faida tu, kwa kutambua hilo itakusaidia kupunguza hofu ya kushindwa, maana tayari umetambua changamoto kabla ya kutokea. ........ila utaendelea kuwa imara kupitia changamoto hizo 
Wanasikolojia wanasema.." Changamoto ambayo umesha itambua kabla haiumizi sana "

MAHUSIANO; Vijana wengi huwa na hofu ya kuambiwa wamechelewa kuingia kwenye mahusiano hadi ndoa, hii imefanya vijana hao kuchukua maamuzi ya haraka na yenye kuipendezesha jamii bila kuwa na manufaa kwao. ....ipo pia hofu inayozuka pale mtu anapoachana na mchumba wake  (hofu ya kutopta tena ).....nini kifanyike? ..hakuna kanuni
ya moja kwa moja ila zipo njia ambazo kwa aslimia nyingi zinaweza punguza HOFU. 
(i).KUJIAMINI, lazima mtu ujiamini kuwa una thamani kwa mwenye kuijua thamani yako, kutambua hilo litakusaidia kufanya mambo yako binafsi huku ukisubiria mtu sahihi kwenye wakati sahihi. 
(ii) kuhakikisha unafahamu uendapo , ni ngumu kupoteza muda na mtu asiye wa kwako. ...ikiwa wako unamjua. ...kwanin usiwe mvumilivu kumsubiri? ....huwezi kuwa na hofu ya kuchelewa ikiwa  unamjua wako yupo njiani. .......yapo mengi ila hayo ni machache ambayo ukiyafahamu unaweza punguza hofu ya kushindwa. 
MAISHA KWA UJUMLA; maisha hayataki haraka  (kama wasemavyo waswahili),yanahitaji 
uvumilivu wa kutosha, ila mtu mwenye hofu sio mvumilivu. ......wataalam wa saikolojia wanasema mtu mwenye hofu hutamani kujisaidia kwa kukimbia  (haraka ) hivyo mambo yake huwa ya haraka haraka. .......nini kifanyike? lazima utambue kuwa mambo unaweza kufikia ndoto zako endapo tu ukiwa na subira, ila iwe subira yenye juhudi. 
Hivyo hata upitie changamoto nyingi sio njia ya wewe kutengeneza hofu. ..ila jifunze na ukiweza badilli mfumo wa utafutaji ili kuendelea na safari ya kuelekea mafanikio yako. 

Nina imani kuna kitu umejifunza kuhusu jinsi ya kuipunguza hofu kwa njia sahihi, somo la hofu ni pana sana, na hofu ndio adui mkubwa wa mafanikio yetu,Shetani pia hupenda mazingira yenye hofu. 
Kwa wale wanao amini, njia nzuri ni kuweka imani na Mungu, ukiweka hofu maana yake huna imani na Mungu. 
ulicho jifunza kitumie katika sehemu zote za maisha, ....ishinde HOFU YA KUSHINDWA. 

Karibu tena kwenye somo mpya muda kama huu, somo hilo ni MUDA WA ZIADA.......
ukitumia muda wa ziada vibaya utajuta milele. ...unatumiaje muda wako wa ziada? 

                                    see you at the top. 
                          scientist Saul kalivubha. 
                           ( 0652 134 707 )

Wednesday 1 March 2017

HOFU YA KUSHINDWA -2

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa hali yako ki afya ni nzuri, ila kwa wale ambao hawapo vizuri ki afya, Mungu asimamie harakati zote za kuirudisha afya yenu. Tupo kwenye kumalizia robo ya kwanza ya mwaka huu, nakusihi rejea kwenye daftari lako la malengo ujitasmini umefikia wapi.

Karibu kwenye somo letu la HOFU YA KUSHINDWA, nikukumbushe tu kuwa somo letu lina sehemu tatu ambazo ni. 1.CHANZO CHA HOFU. 2 . MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA. 3 . JINSI YA KUSHINDA HOFU YA KUSHINDWA.

KUSUDI LA SOMO.
Leo tunaangalia sehemu ya pili , MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA, nakusihi upitie somo la kwanza, unaweza fata link hii  (http://kalivubha.blogspot.com/2017/02/hofu-ya-kushindwa-1.html?m=1) au ingia Google search,andika kalivubha blog hofu ya kushindwa, utapata somo hilo.
NB.Lengo la somo hili ni kujifunza jinsi HOFU inavyoweza kuzuia mafanikio yako, hapa ninazungumza hofu iliyo zidi kawaida.

                                   2.MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA.
Hofu ina madhara mengi sana katika kufikia ndoto zetu, tuangalie jinsi HOFU inavyoweza kuathiri sehemu hizi tatu muhimu; MAAMUZI, UVUMILIVU NA KUJIAMIN I. .........ukiweza kufahamu madhara ya hofu katika sehemu hizo tatu, nafikiri utakuwa na uwezo wa kujipima  ili ujitambue upo kundi lipi .

MAAMUZI, hii ni sehemu muhimu sana kwenye maisha, ili uweze kuchagua machache kati ya mengi lazima ufanye maamuzi.........ipo vipi kwa mtu mwenye hofu? ...Mtu mwenye hofu anakuwa hajakamilika, tayari akilini mwake anakuwa na jibu la kushindwa hata kabla ya kufanya maamuzi.....Hivyo mtu huyo anakuwa yupo tayari kuchagua jambo lolote lile ambalo ana amini litapunguza hofu yake.
Kumbuka tu ni watu wachache sana ambao wamewahi kufanya maamuzi sahihi wakiwa kwenye hali ya HOFU ya kushindwa.

KUJIAMINI...Nakumbuka mwalimu mmoja aliwahi kuniambia usemi huu. ."Ukitaka kumshinda adui yako, hakikisha unamfanya apunguze KUJIAMINI "
ipo vipi kwa mtu mwenye hofu ya kushindwa? .....Mtu akiwa na tatizo la HOFU YA KUSHINDWA, anakuwa hajiamini, maana tayari anakuwa ameshindwa AKILINI mwake hata kabla ya kujaribu. ...madhara ya kutojiamini ni kufanya mambo hayaendani na thamani yako. .....
Watu wasio jiamini siku zote huwa hawapati wanayostahili, ila hupata yale wanayo amini yanaweza punguza hofu yao.

UVUMILIVU,mtu mvumilivu mara nyingi lazima awe ana jiamini kwa kiasi kinachostahili na pia lazima awe mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yasiyo bebwa na Imani ya HOFU. ........
Mtu mwenye hofu ya kushindwa ni vigumu kuwa mvumilivu, huwezi kuwa mvumilivu kwenye jambo ambalo kwa imani yako tayari unajua utashindwa......je una weza kufanikiwa kwa hali hiyo?  ......hapana, maana kwenye maisha kuna malengo ambayo yanahitaji muda mrefu ili yaweze kukamilika, yanahitaji uvumilivu wa kutosha.

Hofu ya kushindwa ni hatari sana, hakikisha unajua tiba yake mapema.....Watu wengi wameacha njia zao ndefu ila zenye mafanikio kwa kufata njia fupi zisizo na mafanikio, wamefanya hivyo kwa kuwa WANA HOFU YA KUSHINDWA. .....wamejiona hawawezi .

Kitabu cha RAFIKI kipo kwenye maandalizi, kitakusaidia kujua kujua siri za mafanikio kupitia rafiki.
        Let's meet on the next week , on the same day.
                       
                                 See you at the top.
                                   scientist Saul kalivubha.
                                    (0652 134 707 )