Sunday 10 December 2017

DAFTARI LA MALENGO

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya,kwa wale wagonjwa,Mungu yupo kwa ajili yetu,atatuponya,tusichoke kuzungumza naye.......Karibu tujifunze.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze kuhusu daftari la malengo,somo letu litakuwa katika sehemu kubwa mbili,maana ya daftari la malengo na umuhimu wa daftari la malengo.......karibu tuendelee.

MAANA YA DAFTARI LA MALENGO.
Daftari la malengo nafikiri ni neno maarufu ila lenye kutumika mara chache sana kwa watu,daftari la malengo ni daftari ambalo linatumika kuandikia malengo na jinsi ya kuyafanikisha hasa kwa kuzingatia mipango inayoonyesha namna ya kukamilisha malengo hayo..................kabla ya kuhamia sehemu ya pili,tujifunze sehemu muhimu zinazotakiwa uwe nazo kwenye daftari lako la malengo.

  • Anza na kurasa chache kwa kuandika malengo yako na kikomo cha malengo hayo(deadline)
  • Kurasa zinazofata andika mipango ambayo unatakiwa kuifanya ili uweze kufikia malengo yako,mipamgo ni sehemu ambazo zinatakiwa kukamilishwa ili zisaidie kutimiza malengo hayo....mfano,una lengo la kununua gari,lazima uwe na mipango ya kufanya ili uweze kupata pesa inayotakiwa.
  • Kurasa baada ya mipango,andika bajeti ,,,,,bajeti itakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa na yenye uhusiano mzuri wa malengo yako.....

UMUHIMU WA KUWA NA DAFTARI LA MALENGO.
Zipo faida nyingi za kuwa na daftari la malengo,ila faida kubwa sana ni kutimiza malengo yako.....daftari la malengo linasaidia kukupa kifungo ,kifungo ambacho muda mwingi kitakufanya uwazie malengo yako,na kitakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa,maana utakuwa na hofu ya kutumia pesa iliyo nje ya bajeti yako.

       Makala hii imeandikwa na mkurugenzi wa label ya fikia ndoto zako.....Saul Kalivubha.
             0652 134707.

Tuesday 24 October 2017

JITENGENEZEE KESHO YENYE MATUNDA.

Habari za kwako rafiki ambaye tumekuwa pamoja kwenye darasa hili la maisha ,kwa lengo la kusaidia kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,karibu tujifunze.

Kusudi la somo.
Leo nataka tujifunze namna tunavyoweza kutengeneza kesho yetu iliyo ndani ya ndoto zetu,somo hili kwa bahati mbaya wengi wanalipata wakiwa tayari wamekosea sana kiasi kwamba kuanza safari upya inakuwa ngumu ,hivyo wanaamua kuendelea na safari isiyo ya aina yao,...tatizo kubwa ni kwamba mazingira yapo kinyume na kesho za watu wengi,hivyo kulipata somo hili na kuliishi,inahitaji ujasiri wa kutosha ,karibu tuendelee(tengeneza soko lako kabla ya safari)

ITAMBUE KESHO YAKO.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kuandaa kesho yako,bahati mbaya kwa upande wa Afrika ni watu wachache sana ambao wanafanikiwa kutambua kesho yao mapema,na wanaofanikwa kufanya hivyo ,wanashindwa kuifikia kwa kukusa maandalizi,kwa wenzetu wazungu ,hali ipo tofauti,wao hutambua kesho yao wakiwa na umri mdogo na wanaanza kutengeza mazingira mapema ya kuja kuiishi kesho yao..........Unafikiri kwa nini wao wanaweza?

Bill Gate akiwa na umri mdogo sana,aligundua kuwa anapenda sana kuchezea Computer,alichofanya alitafuta rafiki wa aina yake ambapo walitenga muda wa kuwa wanajifunza zaidi kuhusu computer kwenye Library ya shule,....akiwa na ndoto ya kumiliki company,alitumia muda mwingi kuwa kwenye mazingira yaliyomfanya awe mpya kila siku kwenye kile akipendacho,Je wewe hadi sasa hujagundua unapenda nini?,Je unakuwa mpya kila siku kwenye eneo lako?......Unafikiri tatizo ni  nini?


HALI YA KUSHANGAZA.

  • Watu wengi wanaifahamu mapema sana kesho yao,na wanajua kabisa jinsi ya kufanya ili waje kuishi kesho hiyo,ila tatizo ni uwezo wa kuthubutu unakuwa mdogo,...kama wewe unataka kesho umiliki kampuni,una maandalizi gani sasa?.....jaribu kutengeneza uhusiano wa kile unachokifanya sasa kiwe msaada wa kusaidia ndoto zako za kesho....kuna gharama,ila lazime uzilipe ili kuweza kuifikia kesho yako.

  • Watu wengi wa wengi tunakwepa maumivu kwa kuyahamishia kesho,....kuliko mtu kuanza maandalizi mapema ya kuandaa kesho ya malengo yake,anaona afanye maandalizi hayo kesho,unachokwepa leo nini?......kila siku ifanye iwe ya maandalizi ya kesho yako.

  • Watu wengi tunataka tuifikie kesho iliyo kamilika.....Hapa nakumbuka mwanafunzi mmoja aliwahi kuniambia,safari yake ya maisha itaanza baada ya kumaliza chuo,swali la haraka likanijia,....Atamaliza na umri gani?,kisha nikajiuliza,ina maana huyu mwanafunzi leo yupo anapoteza muda?,maana bado hajaanza safari ya maisha.
Kesho yako inaanza pale ambapo tayari umejitambua upo kwenye safari ya aina gani,kama safari yako inaenda kwenye kumiliki nyumba za kifahari,anza kuzitengeza leo,,,,,huwezi kuzipa ta nyumba hizo kwa siku moja,ujenzi wake unaanza leo,kila siku jitaahidi unapata maarifa ya kutosha kuhusu hizo myumba unazo zihitaji.



Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO zako.

                    See You At The Top.
                        0652 134707

Friday 13 October 2017

TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa pumzi ambayo amekuwa akitupatia bure,karibu tujifunze.

KUSUDI LA SOMO.
Somo letu la leo linahusu umuhimu wa kutengeza soko kabla ya kuanza safari yoyote ya maisha,....Nafikiri wazo la haraka unaposikia neno soko ni biashara,lakini hapa nina maana zaidi ya soko la biashara,,,kabla ya kuendelea na somo jifunze kwanza somo hili (kwa nini hupigi hatua?).....karibu tuendelee.

MAANA YA NENO SOKO.
Kwa haraka ,soko ni sehemu ya kufanyia mauzo ya bidhaa/kitu flani,soko ni kipimo kizuri cha ubora wa kitu flani,mfano,soko la bidhaa flani likishuka,ni wazi kuwa ubora wa bidhaa hiyo unakuwa umeshuka.........Kwa maana pana zaidi na ambayo nataka ndio iwe sehemu kubwa ya somo letu ni hii,SOKO pia ni kipimo kizuri cha huduma yako,huduma yako inapimwa thamani sokoni,ubora wa huduma yako ndio unafanya soko lako liwe juu au chini.


KWANINI UTENGENEZE SOKO KABLA YA SAFARI?
Nafikiri umewahi kuona au kusikia majina ambayo yalifanya vizuri,ila hadi sasa hivi huyasikii tena,...tatizo ni nini?
Pia utakuwa umewahi kushuhudia mtu flani akianza kwa kasi kubwa na kwa ubora wa juu,ila baadae anapotea,tatizo ni nini?

Pamoja na sababu myingi zinazochangia hali hiyo,ila sababu nyingine kubwa ni watu wengi wanaanza safari bila ya kuandaa aina gani ya watu ambao watawafikia na changamoto zake,unapofahamu huduma yako itafikia watu wa aina gani (soko),itakusaidia uanze maandalizi ya kutosha kuhusu ubora wa huduma yako itayokidhi mahitaji ya watu hao kwenye vipindi tofauti tofauti .

Mazingira yanabadilika,mahitaji pia yana badilika,je umejipanga kuibadilisha huduma yako ili iweze kuendana na mabadiliko hayo?

Kabla ya safari ,hakikisha unatambua vizuri soko lako,tena utengeneze na soko mpya litalopatikana kulingana na mabadiliko yatayotokea,ukiendelea kutoa huduma ya aina moja muda wote,ubora wake utashuka kama ikitokea jamii imebadilika ila wewe hujabadilisha aina ya huduma yako.....TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.


Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
     mkurugenzi wa fikia ndoto zako label
       0652 134707.

Wednesday 27 September 2017

KWA NINI HUPIGI HATUA?

Karibu tena kwenye blog hii  inayotoa elimu ya maisha na  jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa afya yangu ,ni matumaini yangu kuwa na wewe nimzima wa afya(sababu unapumua)..karibu tujifunze............

KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza sababu ambazo zinazuia hatua za watu wengi,mimi pia ni moja ya wahanga wa sababu hizo,kwa muda mrefu nilikuwa nina mawazo makubwa ila sipigi hatua,na mwisho wa siku nayapoteza mawazo yale.....kwa nini hupigi hatua?


Kupiga hatua ni hali ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine,kutoka sehemu yenye viwango vidogo,kwenda kwenye sehemu  sehemu yemye viwango vikubwa zaidi,inaaweza kuwa kwenye biashara ,shule,urafiki ,uwekezaji n.k( jifunze elimu ya pesa)......Kuna watu wana mawazo mazuri,juhudi na wanajitahidi kujifunza kila siku ,ila bado hawapigi hatua mbele,bado matokeo wapatayo hayaendani na jinsi wanavyojituma........Tujifunze kupitia baadhi ya vikwazo vinavyozuia kupiga hatua kwetu.

 SABABU ZINAZO FANYA USIPIGE HATUA.

  •  Kuwa na imani kwamba kuna watu wanahitajika kukusaidia ili ufikie hatua flani,hii ni imani ambayo inasababisha watu wemgi wasipige hatua mbele kwa kusubiri aina flani ya watu waje watoe msaada,kwa lugha ya haraka tunasema connection au channels....sawa mafanikio yanahitaji watu,ila hata wewe unaweza kuwa channel kwa watu wengine kwa kujaribu kwako.Bahati ina nguvu kwa mtu mwenye juhudi,....jaribu hadi kwenye sehemu inayohitaji mtu wa kukusaidia,ili akitokea akute upo vizuri ki maandalizi

  • Usiogope makosa,....hapa ndipo kuna watu wenye mawazo mazuri sana na elimu ya kutosha kuhusu jambo flani,ila hawapigi hatua,..kwa nini? Watu wenye ujuzi mwingi mara nyingi hawtaki kuonekana wakikosea,bora waendelee kuwa na ujuzi wao kwenye fikra kuliko kujaribu kwa vitendo,hali hii ndio inafanya mara nyingi walimu kushindwa na wanafunzi wao...Hata uwe na elimu ya viwango vya juu kuhusu jambo flani,bila kuihamisha kwenye vitendo ni sawa na kazi bure,kubali kukosea ili upige hatua mbele kwa kufanya sahihi ,

  • Fanya maamuzi ,hata kama matokeo yake yanaumiza au yanapingwa na rafiki zako wa karibu,kuna watu tayari wanatambua ili kupiga hatua lazima wafanye jambo flani,ila kwa sababu tu jambo hilo linapingwa na marafiki ,wanaamua kuvumilia tu ili kuendeleza mahusiano mazuri ,Maisha ni ya kwako,rafiki wataokukimbia kwa maamuzi yako ya mafanikio ,achana nao,ukifanikwa watatafuta njia ya kutudi tena kwako

  • ,
  • Mafanikio ni haki ya kila mtu,hakuna aliyepangiwa viwango flani,hata wewe unawezakufika,ondo ile imani ya kwamba biashara flani inafanywa na watu flani tu,au ufaulu flani una watu wa aina flani tu,hata wewe umo kwenye watu hao ,,,,hivyo usiache malemgo flani kwa kuwa hakuna mtu wa familia yenu amewahi kufanya hivyo,,,,,,hutopiga hatua'

Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha,kwa label ya fikia ndoto zako

Friday 15 September 2017

SAIKOLOJIA YA PESA.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha ,nashukuru Mungu kwa kunipigania kwake kila siku, furaha yangu kubwa ni sababu  na wewe ni mzima.,kama ni mgonjwa pia ondoa hofu,yupo mponyaji mkuu kwa  ajili yako ambaye ni Mungu.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze saikolojia ya pesa katika sehemu kuu tatu ;BAJETI,AKIBA NA UWEKEZAJI....Kabla ya kuanza somo letu hili ni vizuri ukaelewa kwanza  maana ya Saikolojia kwa ufupi.
SAIKOLOJIA sio neno geni sana,ila kwa ufupi lina maana ya elimu ya tabia ,sababu zinazofanya utokeaji wa tabia na madhara ya tabia......kwa leo tujifunze tabia ambazo pesa inahitaji ili iweze kukaa mikononi kwako.......karibu tujifunze.



 BAJETI.
Bajeti ni muongozo ambao unahusisha mapato na matumizi ya pesa,ni watu wachache sana ambao wanatumia pesa kwa kufata bajeti,maana rahisi ni kwamba watu wengi hawana malemgo kwenye maisha yao ya kesho,haijalishi kipato chako ni cha ukubwa gani,lazima utengeneze bajeti ya kuonyesha pesa unayoingiza,matumizi unayotumia na akiba unayoweka.......Mambo muhimu sana ya kuzingatia kabla ya kupanga bajeti ni haya; Ukubwa wa pesa unayoingiza,  malengo yako yanayohitaji pesa ,  mazimgira yako(familia yako) na ufahamu matumizi ya lazima na yale yasiyo ya lazima....Mambo hayo machache yatakusaidia uishi maisha yanayo endana na bajeti yako ila yenye mchango mkubwa kwenye malengo yako ya kesho.



AKIBA.
Akiba ni pesa ambayo unahifdhi kabla ya kuanza matumizi yoyote ya pesa na kwa lengo maalumu,lazima uwe na malengo kisha ndio uanze kuweka akiba,Ukiona unashindwa kuweka akiba jitahidi upitie bajeti yako vizuri na kisha uanze kupunguza matumizi yasiyo ya lazima au kununua  vitu vyenye bei ya kawaida .....kiufupi lazima uishi maisha ya kawaida kwa sasa ili kesho uishi maisha ya tofauti,.....Kuna watu wanajidanganya kwmba kuweka akiba lazima uwe na kpato kikubwa,jibu ni hapana.....nakumbuka kuna kipindi nilikuwa naingiza laki moja kwa mwezi ila nilifanikiwa kupanga bajeti hadi kuweka akiba ya laki sita kwa mwaka,hivyo nikawa na jeuri ya kufanya kitu bora zaidiya kile cha kuingiza laki moja kwa mwezi.



UWEKEZAJI.
Ukiwa na bajeti nzuri utakuwa na uwezo wa kuweka akiba,usiweke akiba kama huna kitu cha kufanya kesho,utaitumia pesa yako ovyo,weka akiba kwa lengo flani,ili ile akiba ianze kukuzalishia pesa,......njia nzuri ya kutumia akiba ni kuwekeza au kufanyia biashara.....kwa hiyo ni vizuri kuwa na elimu ya pesa,elimu ya kile unachotaka kuwekeza na ukubali kuishi maisha ya kawida kwa muda flani.


            See you at the top
               Saul kalivubha
                  0652 134707

Sunday 16 July 2017

SIRI YA KUMI YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani wewe hapo ni mzima wa afya,kama ni mgonjwa usijali,Mungu yupo kwa ajili yetu wote.


  KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya kumi ya urafiki ambayo ni UKWELI ,ila kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukapitia na kujifunza kwanza siri ya tisa ya urafiki(SIRI YA TISA YA URAFIKI).


           SIRI YA KUMI  YA URAFIKI   (UKWELI).
Kwenye urafiki kuna kuwekana wazi mambo,ila kabla ya kuweka wazi mambo yako kwa rafiki yako lazima kwanza uwe umejihakikishia uaminifu wa kutosha ,ila wakati mwingine kuna watu wapo kwenye urafiki kwa kuficha ukweli,wanatumia uongo kutengeneza ukaribu wao....je hii ni sahihi?


Wanasaikolojia wa mambo ya mahusiano wanazungumza kwamba ...Watu wanatafuta wasiyoyafahamu,hawana shida na wanayoyafahamu,,,hii tafasiri yake ni kwamba rafiki yako anatafuta mambo ambayo hayafahamu kutoka kwako,inaweza kuwa umemdanganya jambo fulani,siku akilifahamu lazima sura ya urafiki wenu ubadilike,...jifunze kuwa mkweli.


Ni bora kumficha mtu jambo kuliko kumdanganya,sababu za kumficha mtu jambo zinaweza kuwa zina maana kubwa kuliko sababu za kumdanganya mtu,,,,,kumdanganya maana yake umemwambia ukweli wenye hila ndani yake,umetafuta kuaminiwa kwa njia isiyosahihi.



Ukiona rafiki yako amekukwepa kwa sababu umemwambia ukweli,jua huyo sio mtu mzuri kwako,maana ukweli una thamani kubwa sana kwenye urafiki wa kweli,urafiki ambao una lengo la kufikia mafanikio makubwa.


Tatuzo ukisha anza na uongo tu kwenye urafiki wako,itakufanya kila siku uendelee kutengeneza uongo wa kudumisha uomgo wa mwanzo....urafiki wa aina hiyo una umuhimu gani?, ukijiona mjanja wa kudanganya ,tambua thamani yako inashuka,pia unapoteza muda wako kudanganya na kuendeleza uongo wako.



Kitabu cha SIRI ZA URAFIKI kinaelekea kuwa tayari,utakipata kwa mawakala wa fikia ndoto zako....


                           See you at the top.
                    Scientist Saul kalivubha.
                              0652 134707

Monday 10 July 2017

SIRI YA TISA YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa uzimab wake kwangu ,pia ni imani yangu kuwa wewe ni mzima........karibu.



   KUSUDI LA SOMO.

Tunaendelea na somo letu la siri za urafiki,leo ni siri ya tisa ambayo ni mipaka ya ufahamu,...kabla yakuendelea na somo letu hili,ni vyema ukajifunza kwanza siri ya nane ya urafiki(SIRI YA NANE).,karibu tuendelee.



SIRI YA TISA YA URAFIKI(MIPAKA YA UFAHAMU).

Katika urafiki ni jambo la kawaida sana kufahamu habari za rafiki yako,swala hili ni zuri sana ikiwa unataka kufahamu habari hizo kwa lengo la kudumisha urafiki,ila kuna habari zingine za rafiki yako zinaumiza,kama hauna ujasiri,badala ya urafiki kuimarika,utavunjika......kabla ya kuanza kuzifatilia habari za rafiki yako jitahidi kufahamu haya.

  • Weka mipaka,hakikisha unafahamu mambo yenye fada tu katika ujenzi wa urafiki.
  • Kuwa makini na chanzo cha habari, sio kila chanzo cha taarifa za rafiki yako ni chanzo sahihi.
  • usifatilie habari za rafiki kama kumpeleleza,akijua urafiki wenu utapoteza uaminifu,kuwa mpole na taratibu tu utafahamu mengi kuhusu yeye.
  • Fanyia kazi mambo utayo yafahamu kwa rafiki yako kwa lengo la ujenzi na sio kwa leng la kumuhukumu rafiki yako.


Mwamdishi mmoja wa mambo ya saikolojia aliwahi kuandika kanuni moja muhimu sana ,kanuni hiyo ni hii   "Msongo wa mawazo(Stress) unaongezeka,kila ufahamu unapoongezeka"
Kanuni hii inasaidia kupunguza kufahamu mambo yasiyokuhusu,watu wengi kwenye urafiki wanaishi kwa mawazo kwa sababu tu walifatilia mambo yasiyo wahusu ya rafiki zao.


Kuna mambo sio lazima uyafahamu kutoka kwa rafiki yako,utaumiza kichwa bure tu,tena kibaya zaidi hakuna uwezo wa kuyabadilisha mambo hayo,tena kuyafahamu kwako hakuna faida yoyote kwenye uraki wako .....


                        See you at the top.
                            Saul kalivubha
                               0652 134707.

Sunday 2 July 2017

SIRI YA NANE YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. ......Karibu sana kwenye muendelezo wa somo letu la urafiki, nina imani kuna kitu unajifunza. ..karibu.

LENGO LA SOMO. 
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nane ya urafiki kulingana na mpangilio wangu, siri hiyo ni  Jichunguze tabia yako. ... .Unaweza pitia kwanza SIRI YA SABA, kisha uje tuwe wote. .....karibu tuendelee.

SIRI YA NANE  (JICHUNGUZE TABIA YAKO ).

Urafiki unapitia mazingira mengi sana, kila mazingira huwa yanahitaji style  (mfumo ) wa kuishi ili kuhakikisha urafiki unaendelea na thamani yake.Ila kuna kipindi mtu anaona rafiki yake kabadilika tabia, amekuwa na tabia mpya ambayo hapo nyuma hakuwa nayo.

  • Je umewahi kukutwa na hali hiyo? 
  • Urafiki wako ulikuwa na sura gani baada ya hali hiyo? 
  • Unafikiri chanzo chake ni nini? 
Ni hali ya kawaida sana kusikia mtu akilaumu kuhusu kubadilika kwa tabia ya rafiki yake, tena kwa sababu nyingi za kujiona yeye mshindi na kumfanya rafiki yake kuwa mwenye hatia. ..
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.

Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.

            See you at the top.
           scientist Saul kalivubha.
               0652 134 707.
0

Sunday 25 June 2017

SIRI YA SABA YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania hadi sasa ,hongera sana kwa kuwa na afya njema,kwa wale wagonjwa poleni sana ila Mungu niwetu sote.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tuendelee na somo letu la urafiki,kabla ya kuendelea na siri ya saba, jifunze kwanza     ( SIRI YA SITA),Kisha tuendelee na siri ya saba ya urafiki ambayo ni tasmini ya uchaguzi wa rafiki,.....karibu tujifunze.

SIRI YA SABA YA URAFIKI(TASMINI YA UCHAGUZI).

Kuwa na rafiki flani ni ni matokeo ya uchaguzi uliofanya,hakuna kulazimisha kwenye mambo ya urafiki,huwa ni hiari ya muhusika,je uchaguzi wako una matokeo gani?

Kila uchaguzi lazima uwe na matokeo,matokeo ya uchaguzi ndio sehemu ambayo tunaitumia kupima kufanya evaluation(tasmini) ya usahihi wa mtu katika uchaguzi wake,....hii ni sehemu ambayo kila mtu anapaswa kuifanya yeye binafsi, je nini kinafata baada ya tasmini ya matokeo?

Matokeo ya uchaguzi wa rafiki yana sehemu ya kuvumilikika ambayo ni moja ya madhaifu ya binadamu, ila matokeo yanaweza kuwa pia hayaruhusu urafiki uendelee,hapa lazima uchukue maamuzi magumu,bila hivyo itakuwa ngumu kwako kufikia ndoto zako......


Zoezi la tasmini ya matokeo ya urafiki huwa ni ngumu kidogo, maana kuna watu wanachukua maamuzzi magumu kwa kukwepa changamoto za urafiki tu ,kwa hiyo inahitaji umakini sana katika zoezi hili,,,,,,
Jiulize swali hili,....matokeo ya uchaguzi wa rafiki uliyrnaye yana endana na ndoto zako?,kama sio ,unafanya nini kwemye urafiki huo?

Habari ya kusikitisha kwenye urafiki ni kwamba,watu wengi wanaweza kugundua hawapo kwenye njia sahihi,ila wakwa wanajifariji ,mwisho wa siku wanafanya maamuzi magumu tayari walisha poteza thamani yao,,,,,,,fanya tasmini,chukua maamuzi sahihi.....

                          See you at the top
                        Scientist Saul kalivubha.
                               0652 134707

Sunday 18 June 2017

SIRI YA SITA YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,maana nina imani kuwa na wewe ni mzima,.....karibu tujifunze.

Kusudi la somo.

Leo ni muendelezo wa siri za urafiki,tunaendelea na siri ya sita ya urafiki ambayo ni utatuzi wa migogoro,kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukajifunza kwanza  SIRI YA TANO ,Karibu tujifunze.

UTATUZI WA MIGOGORO YA URAFIKI.

Jambo la kufahamu kwenye urafiki ni kwamba ,unakutana na mtu ambaye hujazaliwa naye,ana madhaifu yake na pengine ana historia yake ya maisha tofauti na yako.......lazima kuna migogoro itatokea tu ndani ya urafiki,,,,,jaribu kujibu maswali haya kabla ya kuendelea mbele......je umewahi kuingia kwenye mgogoro na rafiki zako?,ulifanya maamuzi gani ?.baada ya maamuzi hayo urafiki wenu ulipata sura gani?

Migogoro kwenye urafiki ni muhimu sana kwani ni dalili ya kuonyeha hali ya kutokuwa sawa sehemu flani,ila inaweza kuwa na madhara ya kudumu kwa wahusika endapo watashindwa kutambua sababu za utokeaji wa migogo hiyo,

Uwezo wa utatuzi wa migogoro ya urafiki bila kuharibu thamani ya muhusika ndio kipimo kizuri cha uwezo wa uendeshaji wa urafiki.


Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye utatuzi wa migogoro.
  1. Kabla ya maamuzi yoyote hakikisha unajua chanzo cha tatizo .
  2. Usipende kuonekana mshindi,ili kumudu hili hakikisha unatawala hisia zako za hasira ili usifanye maamuzi yenye msingi wa hasira.
  3. Kama kosa lipo kwa rafiki yako,vaa uhusika ili upime yeye angefanya maamuzi gani juu yako.
  4. Usipende kutumia ushauri wa watu wengine katika kutatua mgogoro unaokuhusu wewe.
  5. Hakikisha unajua tafasiri ya kila changamoto kwenye urafiki wako,ili ufanye maamuzi ambayo hayana majuto.


Kumbuka tu ili uweze kufikia ndoto zako ni muhimu uwe kwenye system ya marafiki waliobeba kusudi lako,ila kuwa na rafiki ambaye kabeba kusudi lako sio tafasiri ya kutokuwa na migogoro.

                   See you at the top.
     scientist SAUL KALIVUBHA.
                   0652 134 707.

Sunday 11 June 2017

SIRI YA TANO YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa afya yangu pamoja na wewe. ....karibu.

  KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo la leo ni kuendelea na sehemu ya tano ya siri ya Urafiki. ..ni vyema ukajifunza sehemu ya nne SIRI YA NNE  kisha uendelee na siri ya tano( SIRI YA NNE)..... lengo la kufundisha urafiki ni kutaka tufahamu jinsi ya kuishi na marafiki kwa lengo la kufikia ndoto zetu ...maana mafanikio yako yapo kwa rafiki yako. ...karibu.

SIRI YA TANO YA URAFIKI.
Siri ya tano ya urafiki ni  mawasiliano .Kwenye mawasiliano tuangalie kwenye upande mmoja tu. jinsi mawasiliano yanavyoweza kuvunja urafiki. ....nafikiri utakuwa tayari umeshuhudia urafiki ukivunjika kwa sababu ya mawasiliano. ....au inaweza kuwa umekutwa na tatizo hili la kupoteza marafiki kwa kigezo cha mawasiliano. ....
Mawasiliano yanaweza kavunja urafiki kupitia sehemu hizi.

  • Mawasiliano mabovu, ..hapa nina maanisha kiwango cha chini cha mawasiliano au mawasiliano ambayo hayana hisia za Upendo. ....kila mazingira yana aina yake ya mawasiliano na kiwango chake, ukiwa kwenye mazingira yenye kuhitaji mawasiliano kwa wingi ila wewe ukafanya chini ya kiwango , urafiki utakuwa unaelekea kwenye hatari ya kuvunjika. ....jitahidiutambue aina ya urafiki uliyonayo, mazingira mliyopo. .ili ufanye mawasiliano yanayostahili. 
  • Mawasiliano hupoteza thamani ya habari, ...utafiti wa kisaikolojia unaonyesha kwamba habari inavyozidi kupita mikononi kwa watu wengi ndio inavyozidi kupungua uhalisia wake, ila kuna watu bila kufanya utafiti wa kina wamekuwa wakifanya maamuzi ya kudumu kwa kupitia taarifa imeyopitia mikononi kwa watu wengi. ..hali hii imefanya watu wengi kupoteza marafiki .....fanya tasmini kabla ya maamuzi, unavyozidi kuwa mbali na chanzo cha habari ndivyo ukweli wa taarifa unavyozidi kupungua. .....
             Seeyou at the top. 
        scientist Saul kalivubha. 
          (0652 134 707)






Wednesday 31 May 2017

SIRI YA NNE YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya elimu ya maisha kwa lengo la kufikia ndoto zetu,nashukuru mungu kwa kuendelea kunipigania mimi pamoja na wewe...........karibu.


KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nne ya urafiki ambayo ni uvumilivu,ili tuwe pamoja jifunze kwanza SIRI YA TATU kwa kubofya hapa.SIRI YA TATU,..........ikumbukwe tu rafiki ana sehemu kubwa sana kwenye ndoto zetu,hii ndio sababu ya mimi kufundisha somo hili.

SIRI YA NNE YA URAFIKI(UVUMILIVU).
Uvumilivu ni uwezo wa kuzitawala hisia zitokanazo na mambo yasiyo pendeza,hisia ambazo zikiruhusiwa zinaweza kuwa hanzo cha matokeo hasi(negatives effects).........kwenye urafiki pia kuna mambo ambayo yanahitaji kuvumiliwa,ndani ya urafiki kuna mambo yasiyopendeza yenye lengo la kuimarisha urafiki,mtu usipo kuwa mvumilivu unaweza kuwapotezamarafiki wengi sana wasio na hatia..............

Uvumilivu katika urafiki unahitajika sana hasa kwenye hali kuu mbili zifatazo:



  • MADHAIFU;watu wengi wanaingia kwenye urafiki wakiwa na picha ya madhaifu machache waliyo yaona kabla ya kuanza urafiki,ila kuna madhaifu mengine ya ndani ambayo huwezi kuyaona hadi uingie kwenye urafiki,......usipokuwa mvumilivu ,madhaifu haya ya ndani yana nguvu kubwa ya kuvunja urafiki.

  • CHANGAMOTO:Changamoto ni moja ya sehemu muhimu sana ya urafiki,ni sehemu ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu,pia ni sehemu ambayo inahitaji matumizi ya hekima na busara,maanakila changamoto ina jambo la kufundisha kwenye urafiki wako.....kuna usemi mmoja unasema "Kama upo kwenye urafiki usio na changamoto yoyote ile,kaa chini ufikirie tena mara ya pili"

              See you at the top.
          Scientist Saul kalivubha.
                (0652 134707)

Wednesday 24 May 2017

SIRI YA TATU YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, ....nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania hadi sasa.......karibu.

KUSUDI LA SOMO. 
Lengo la somo letu hili la leo ni kuendelea kujifunza siri za urafiki, na leo tupo kwenye siri ya tatu ambayo ni kujiamini.......karibu tujifunze. ..jifunze siri ya pili kwanza siri ya pili ya urafiki

               SIRI YA TATU YA URAFIKI.
Kujiamini ni hali ya kujiona mkamilifu..kujiona upo kwenye mazingira sahihi ya kufanya jambo flani, ....kinyume chake ni kutojiamini ..kujiona mwenye mapungufu au kujiona huna vigezo vinavyotakiwa......ina madhara gani kwenye urafiki? ......sina tatizo na mtu anayejiamini. ..ila kwa asiye jiamini karibu tujifunze. ........

Mtu asiye jiamini kwenye urafiki anakuwa muda wote anahisi kuachwa au kumpoteza rafiki yake. ...hali hii ina madhara gani? 
Hali ya kutojiamini inasababisha mtu atumie nguvu kubwa kuendesha urafiki, kutumia nguvu kubwa ni pamoja na kutumia sifa ya ziada. ..

Mtu asiye jiamini lazima atafute sifa ya kujiongezea ili aweze kujiona mkamilifu. ....hivyo urafiki wake unakuwa umejengeka ndani ya sifa yake ya ziada na sio uhalisia wake. ...

Wanasikolojia wanashauri kwamba, ukiona una tatizo la kutojiamini ni bora ukalitatatua kwanza kabla ya kuingia kwenye urafiki. .mbali na hivyo utasumbuka sana. ...
         
             See you at the top. 
           scientist Saul kalivubha. 
            (0652 134 707 )




Thursday 18 May 2017

SIRI YA PILI YA URAFIKI


karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha. ...nashukuru Mungu kwa neema yake kwangu. .........karibu tujifunze.

Kusudi la somo.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza siri ya pili ya urafiki. ....Nimeona vyema kufundisha somo hili kwa sababu najua urafiki una sehemu kubwa sana kwenye mafanikio yetu. ....karibu.

SIRI YA PILI YA URAFIKI. 
Tuangalie siri ya pili ya urafiki. ..unaweza kujifunza siri ya kwanza ya urafiki kwa kuandika kalivubha blog siri ya kwanza ya urafiki. ....kisha ndio uendelee na mimi kwenye somo hili.
(siri yakwanzayaurafiki )...

Siri ya pili ya urafiki ni hii USIFANYE URAFIKI KWA MAJARABIO...........

Moja ya sababu inayofanya urafiki upungue thamani ni kubadilika kwa mazingira ambayo yalitumika kutengeneza urafiki. ...kwa nini mazingira yabadilike? ......kuna watu ambao wana tabia ya kufanya majarabio ya urafiki. ...wengi wao hufanya hivyo ili kuangalia kama urafiki huo una weza kutimiza mahitaji yake. .....

Urafiki wa aina yoyote ile una changamoto zake. ...hivyo mtu anayeingia kwenye urafiki kwa majarabio hawezi kuvumilia changamoto. .....mara nyingi watu wanaingia kwenye urafiki kwa majarabio wana sifa kuu tatu.

1.Sio wavumilivu wa changamoto.

2.muda wote wanawaza kubadili marafiki.

3.Wanatumia nguvu kubwa kuanzisha urafiki. ....hufanya hivi kwa sababu wanakuwa wanataka waone kama watatimiza malengo yao ..kama hapana basi wabadili marafiki  ...........
Jiandae kupata kitabu cha SIRI ZA URAFIKI  .
     
                      See You At The Top.
                        Saul kalivubha.
                         (065123707 )



Monday 15 May 2017

SIRI YA KWANZA YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania hadi sasa ......karibu.

Kusudi la somo.
Leo nataka tujifunze siri moja ya urafiki ambayo wengi hawajui, au wanaijua lakini hawaitumii. ....mwalimu wangu aliwahi kuniambia kwamba, ikiwa una ujuzi usio kusaidia, ...huna cha kujivunia. ....karibu tuendelee.

         SIRI YA KWANZA YA URAFIKI(SIFA YA ZIADA ).

Kwa nini urafiki? ..... utafiti unaonyesha mafanikio yetu yapo ndani ya rafiki zetu wa karibu. ...hii ndio sababu ya mimi kuandika somo hili. .....Siri ya kwanza ni ipi?
Siri ya kwanza kwenye urafiki ni ...sifa ya ziada .....

Sifa ya ziada ni ni sifa ambayo mtu anajiongezea kwa lengo la kumvutia rafiki yake. ..  hali hutokea mwanzoni mwa urafiki, .....nini madhara yake?

Kuna watu wapo kwenye urafiki mzuri, ila urafiki huo unaendeshwa na sifa ya ziada ambayo mmoja katika urafiki huo anaitumia. .Mtu ambaye anaitumia sifa ya ziada kuendesha urafiki, anatumia nguvu kubwa sana. ...tena nguvu anayoitumia ina mrudisha sana nyuma kimafanikio na ina mpa madhara ya kisaikolojia. ......!

Je, una uwezo wa kuyaishi maisha yaliyobebwa na sifa ya ziada?

Kila siku tunashuhudia kuvunjika kwa urafiki ambapo sababu kubwa ni mmoja wapo kwenye urafiki kupoteza sifa ya ziada aliyojipatia. ...
Tiba pekee kabla ya kuwa na rafiki, hakikisha unaishi maisha yako. ....be you, be smart. (ishi maisha yako, kuwa nadhifu )....utapata rafiki aina yako.

                See you at the top.
         scientist Saul kalivubha.
            (0652 134 707 )



Friday 5 May 2017

KUTOJIAMINI NI SUMU YA MAFANIKIO

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha kwa lengo la kufikia ndoto zetu. ...Leo tuna somo mpya la madhara ya kutojiamini katika kufikia ndoto zetu. ..karibu.

kusudi  la somo.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza jinsi gani hali ya kutojiamini inaweza kuzuia ndoto zako za mafanikio. .... Somo letu limelenga hasa sehemu ya .Maana ya kutojiamini. Ukielewa vizuri maana ya kutojiamini,utajitambua upo upande upi,na mafanikio kwako yapo kwa asilimia ngapi,nimejitahidi kufafanua maana ya kutojiamini na uhusiano wake kwenye mafanikio.....karibu.

        MAANA YA KUTOJIAMINI.
Kunarafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa ukoo wao sio wa biashara hivyo hata akianzisha biashara hatafanikiwa. .je ni sahihi?
Mtu mwingine alisema .." Hata asome vipi hawezi kufaulu kwa ufaulu wa kiwango cha daraja A (grade A)"...umewahi kujiona ukiwa kwenye hali ya kushindwa? .....Nini maana ya KUTOJIAMINI..?


Kutojiamini ni hali ya mtu kujiona mwenye mapungufu, hali hiyo humfanya mtu huyo kuona watu wengine wana uwezo wa juu kuliko yeye. ........Nini maana yake? Tujaribu kuangalia ufafanuzi wa hali ya kutojiamini kupitia maelezohaya hapa chinI. ..

1.Wanasikolojia wana zungumzia hali ya kutojiamini kama vita anayokuwa nayo mtu dhidi ya watu wengine ambaoanaamini kuwa wana uwezo dhidi ya kile anachofanya /anachotaka kukifanya. ...Upo katika hali hiyo?
Kuwa katika vita na watu wasiotambua kama unapambana nao ndio chanzo cha mtu kupunguza kujiaminI. ..maana hali hiyo humfanya mtu ajione yupo upande wa kushindwa muda wote.

2. kutojiamini inaweza kuwa pia hali ambayo mtu anajiona mwenye kuhitaji sifa flani ili akubalike kwenye jamii. ....Hali hii humfanya mtu huyo kujiongezea sifa ya ziada ili akidhi hisia zake, ...hapa ndipo watu wasiojamini huanza kutumia nguvu kubwa kupamba sifa kivuli ili tu aondokane  na hali ya kujiona mwenye mapungufu. ..je unaweza kuitunza sifa uliyojiongezea muda wote wa maisha?

3.Kutojiamini  inaweza pia  kuwa hali ya mtu kuamini zaidi matokeo ambayo yametokana na Kazi za watu wengine....kwa hiyo muda wote mtu asiyejiamini...anakuwa anaishi maisha ya watu wengine ambao mtu huyo anakuwa amewapa uwezo wa ushindi. .. hali hii humfanya mtu asiyejiamini asijaribu jambo lolote lile kwa kutumia mawazo yako. ....je unaweza kufikia ndoto zako kwa kuishi maisha yakutegemea juhudi za watu wengine?
.

Kutojiamini ni tatizo ambalo linatajwa kama chanzo kikubwa cha wivu ambao umepelekea mahusiano mengi ya mapenzi kufa,kama sio mapenzi kufa basi itamfanya mtu asiye jiamini kuwa mtumwa wa mapenzi.


Kutojiamini kwa ujumla ni hali ambayo ukiwa inayo itakufanya uwe unaishi maisha ya watu wengine,maana utakuwa unajiona mwenye mapungufu muda wote,.......unajua tatizo la kujiona mwenye mapungufu muda wote?..Tatizo lake kubwa ni kushindwa kujaribu,mana kulingana na mapungufu unayohisi ni mengi kwako ,utajenga imani ya kukosea kwa kila jambo linalokuhitaji kujaribu,na kumbuka tu ni ngumu kufanikiwa kama una hofu ya kujaribu.
....
                 
              See you at the top.
            scientist Saul kalivubha.
              0652 134707.
         
                 




Wednesday 26 April 2017

KUANGUKA KWA MTU ALIYEFANIKIWA

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa  Mungu anaendelea kukupigania. ...karibu tujifunze.

 KUSUDI LA SOMO. 
Leo nataka tujifunze somo la kuanguka kwa mtu aliyefanikiwa, unaweza kuhisi tofauti kidogo kwa kuona somo hili kwenye blog hii. ..ila ni hali ambayo wewe pia unaweza kuwa shahidi kwa kuona baadhi ya watu wakipoteza mafanikio yao makubwa....kwa hiyo nataka tuangalie baadhi ya sababu zinazofanya watu wapoteze mafanikio yao, kwa kujua sababu hizo itakuwa msaada kwetu kulinda mafanikio yetu. 
Zipo sababu nyingi ila leo nataka tuangalie sababu kuu tatu......karibu. 

SABABU ZA KUANGUKA KWA MTU ALIYEFANIKIWA.
1.Marafiki wapya;siku zote mtu aliyefanikiwa huwa anakuwa
 tofauti na wengine, mafanikio yake yanavuta watu wengi kuwa karibu yake, watu hao ni pamoja na wale ambao waliona kuwa hawezi kipindi alipoanza safari ya mafanikio. .....hiki ni kipindi kigumu sana kwa mtu aliyefanikiwa, ni kipindi kigumu kwake kwa sababu ya ugumu wa kutambua nani rafiki wa kweli kwake, ....  mafanikio yake hupotea pale atapoanza kushirikiana na rafiki wanaoshangalia mafanikio yake na kusahau rafiki waliomfaraji kwenye shida. ..siku zote rafiki anayeshagalia mafanikio yako huwa sio rafiki mzuri, maana kufata mafanikio yako na sio uhalisia wako
2.Kulewa sifa;  sifa ni sehemu ya lazima kwamafanikio yako. .tatizo sio kusifiwa, tatizo ni kuzitawala hisia za furaha itokanayo na sifa. ....Wanasikolojia tunaamini kuwa tabia nyingi zitokanazo na sifa huwa ni za uharibifu na majivuno. ..mtu aliyefanikiwa akianza kuziishi tabia zitokanazo na kusifiwa anakuwa kwenye wakati mgumu sana wa kusahau alipotoka na kubadili njia ya kumpeleka aendapo. ...hatari yake ni kupoteza mafanikio yake. 

3.Kukosa maandalizi kabla; Kuna watu wanafanikiwa bila kujiandaa kuyaishi maisha ya mafanikio, ..maisha ya mafanikio yana changamoto zake,  mtu aliyefanikiwa kuipitia. .lazima watu wasifie tena kubwa sana. ..ni muhimu mtu ukafahamu wapi unaelekea, na nini utakibeba, kutambua hilo itakusaidia kuwa makini na mambo ambayo yapo nje ya kuendeza mafanikio yako. ..kinyume chake ni kupoteza mafanikio.

Kufikia ndoto zako sio kushinda, ushindi ni kuendeza mafanikio yako. ..
Tukutane wiki ijayo. 
                       
                  See you at the top. 
                  scientist Saul kalivubha. 
                    0652 134707. 
      

Friday 21 April 2017

SIRI ZA UVUMILIVU -3

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ...nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. Karibu kwenye sehemu hii ya tatu na mwisho wa somo letu la siri za uvumilivu....karibu tuendelee.

KUSUDI LA SOMO.
 lengo la somo letu hili ni kujifunza siri zilizopo kwenye uvumilivu, na somo letu lina sehemu tatu. 1.maana ya uvumilivu. 2. faida za uvumilivu. 3.hasara za kukosa uvumilivu. ..Leo nataka tujifunze hasara zipi zinaweza kutokana na ukosefu wa uvumilivu. ...Kabla ya kuendelea ingia Google search na kuandika kalivubha blog siri za uvumilivu. ..hiyo itakusaidia kuendana na sehemu hii ya mwisho.

3.HASARA ZA KUKOSA UVUMILIVU .

Mambo karibia yote yenye matokeo mazuri yanahitaji uvumilivu ili kuweza kufanikiwa kupata matokeo hayo mazuri. .....nataka tujifunze hasara za uvumilivu kwenye sehemu hizi tatu. .mahusiano ,biashara na mafanikio kwa ujumla. .....karibu tuendelee. 

MAHUSIANO; Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa anahisi kuwa anabahati mbaya, kwani huwa hadumu kwenye mahusiano. ..utafiti unadhibitisha kuwa watu wengi wameacha watu sahihi sababu tu ya kukosa uvumilivu, ..Mahusiano yana changamoto zake, na hii hutokana na mahusiano kuhusisha watu wenye asili tofauti....kumbe kuna mazingira yatahitaji uvumilivu dhidi ya madhaifu, uvumilivu dhidi ya mabadiliko ya hisia ambayo yanaweza kuwa chanzo cha maamuzi mabovu.

BIASHARA. Kosa ambalo wengi tunalifanya kwenye biashara ni kutengeneza imani ya kupata mafanikio ya haraka. ...Hili ni kosa kwa sababu biashara karibu zote zinahitaji muda wa kutosha ili kutoa faida kamili, huo muda wa kutosha unahitaji mtu mvumilivu, ...pia kwenye biashara kuna hasara, na mara nyingine kuna kuanza upya, yote hayo yanahitaji uvumilivu wa kutosha. .ukikosa uvumilivu ni ngumu kufanikiwa katika biashara...

MAFANIKIO KWA UJUMLA; kufanikiwa kwa ujumla ni kuwa kwenye hatua ambayo ni matokeo ya kushinda maumivu ya UVUMILIVU. ...Msanii wa filamu maarufu kwa jina la Sylivester Stalone Rambo aliwahi kusema alijaribu zaidi ya mara 70 na kushindwa mara zote, ila kilicho msaidia ni uvumilivu wake, hadi sasa ni muigizaji maarufu dunianI. inahitaji uvumilivu wa hali ya juu katika safari yetu ya KUFIKIA NDOTO ZETU. ...Ukikosa uvumilivu ni ngumu kufanikiwa kwa jambo lolote lile. ....jiulize ni maamuzi gani uliyafanya kwa kukosa uvumilivu? 
 Karibu wiki ijayo.

            See you at the top. 
scientist Saul kalivubha 
                0652 134707.
             

       

Wednesday 12 April 2017

SIRI ZA UVUMILIVU -2

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa Mungu katimiza mapenzi yake kwetu sote. ......

KUSUDI LA SOMO
.
Lengo la somo letu la leo ni kuendelea na sehemu ya pili ya siri za uvumilivu,Kumbuka tu somo letu lina sehemu tatu. 1.maana ya uvumilivu. 2.faida za uvumilivu. 3.hasara za kukosa uvumilivu.
Ni vizuri kama utafatilia sehemu ya kwanza kwa kuingia Google search na kuandika kalivubha blog siri za uvumilivu utaletewa sehemu hiyo. ....karibu tuendelee.

     2.FAIDA ZA UVUMILIVU.

Kwenye maisha tunayoishi kuna hali kuu mbili zinazochanganya watu wengi sana katika kufanya maamuzi, hali hizo ni kupata kitu kwa wakati na kupata kitu nje ya wakati .Ili kuweza kuzitawala hali zote hizo mbili bila kufanya maamuzi hatarishi inahitaji uvumilivu. Nmejaribu kuelezea faida za uvumilivu kupitia hali zifatazo.

1.Kukwepa hasara, katika mazingira tunayopitia kuelekea ndoto zetu kuna faida na hasara tuzipatazo kama matokeo ya yale tufanyayo. .....zipo hasara zinakuja kama changamoto, ila zipo hasara huja kama matokeo ya kupoteza uvumilivu, .......mara nyingi mtu akishindwa kutawala hisia zake kwenye mazingira yasiyo ya kawaida hujikuta amefanya maamuzi yasiyo ya kawaida ambayo ni HASARA.


2.Kujiongezea thamani ; Wanasikolojia tuna amini kuwa mtu mwenye uvumilivu huwa ana tabia ya kunyamaza pia kwenye mazingira yenye kuhitaji uvumilivu, hii huongeza thamani ya mtu huyo kwenye jamii, maana anakuwa amefanikisha kuzitawala hisia zako ambazo zingepelekea matokeo mabovu kulingana na maamuzi yenye kukosa uvumilivu. ....

3.Kutimiza ndoto;   kila mtu mwenye kujitambua lazima awe na ndoto za maisha, ....ila taarifa isiyo pendeza masikioni kwa wengi ni kwamba.  ili kufanikisha ndoto zako huwa inahitaji muda mrefu kidogo. ....taarifa hiyo sio nzuri kwa wengi maana watu wengi hupenda njia za mkato ktk kuelekea ndoto zao,  ila kwa kuwa swala la kufikia ndoto zetu linahitajI muda wale wavumilivu tu ndo wamekuwa wakifikia ndoto zao.

Kumbuka kuwa uvumilivu sio Kazi rahisi, lazima uumie, ila ukiweza kubeba maumivu ya UVUMILIVU , kuna uwezekano ukaziishi ndoto zako.

     karibu tena katika sehemu ya tatu na ya mwisho wiki ijayo.

                   
                    See you at the top.
               scientist Saul kalivubha.
                         (0652 134 707 )

Friday 7 April 2017

SIRI ZA UVUMILIVU -1.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania, ...karibu.
Leo nataka tujifunze somo la uvumilivu kwenye harakati zetu za kuelekea ndoto zetu.


KUSUDI LA SOMO.

somo letu la siri za uvumilivu limelenga kufundisha sehemu zifatazo. 1.maana ya uvumilivu. 2. faida za uvumilivu. 2.Hasara za kukosa uvumilivu. ..karibu kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili.


1.MAANA YA UVUMILIVU.

Kuna watu ambao wana tumia neno uvumilivu ila hawajui maana yake, kuna watu wengine wanajua maana yake ila wanashindwa kuliishi neno uvumilivu hasa pale wanapokutana na mazingira yenye kuhitaji uvumilivu. nimetumia mifano kulifafanua neno uvumilivu, karibu tujifunze.



  • Uvumilivuni ni uwezo wa kutawala hisia zako kipindi unapopata matokeo tofauti na makusudio yako, Wanasikolojia wanazunguwa kuwa moja ya zoezi gumu ni kutawala hisia zako kipindi unapopata matokeo tofauti na makusudio yako. .....hii inasababishwa na tabia ya binadam kupenda kila kitu kifanyike ndani ya uhitaji wake. ....ila kuna mazingira ambayo lazima uweke uvumilivu , ....sio kila kitu utakipata ndani ya muda unaohitaji wewe,  ukiweza kutawala hisia zako kipindi hicho utakuwa umeliishi neno uvumilivu.



  • .Uvumilivu ni uwezo wa kutawala hisia zako kipindi watu  (rafiki zetu ) wanaposhindwa kutufanyia kama tunavyohitaji. ....maamuzi ambayo wengi tumefanya hasa pale rafiki zetu wanapofanya tofauti na tutakavyo huwa ni maamuzi yaliyokosa uvumilivu, ni maamuzi ya kubadili  (badala ya maamuzi ya kusubiri wakati mwingine )......uwezo wa kutawala hisia zako ndani ya mazingira hayo ni tafasiri ya kuliishi neno uvumilivu. .



  • .Uvumilivu ni UPENDO, kipimo cha Upendo kipo kwenye uvumilivu, ukiona umeshindwa kufanya uvumilivu wajambo flani kuna uwezekano mkubwa kuwa huna Upendo wa dhati na jambo hilo linalohitaji kuvumiliwa...



Kuliishi neno uvumilivu ni zoezi ngumu, ila matokeo ya kutoliishi neno hilo ni wengi wetu kupoteza ndoto zao. .lazima tuwe wavumilivu ili tuweze KUFIKIA NDOTO ZETU. ......jiulize swali hilI, Utabadilisha maamuzi mangapi? ..maana matokeo ya kukosa uvumilivu ni kubadili mawazo.
Tukutane wiki ijayo katika sehemu ya pili.    

                     See you at the top.
                    scientist Saul kalivubha.
                       0652 134 707.


Thursday 30 March 2017

HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni siku nyingine Mungu amefanya tukutane kwa lengo la kufundishana jinsi ya kufikia ndoto zetu
.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu hatua ya awali katika safari ya maisha yenye ushindi, bado kuna watu ambao wamejaribu kila namna ya kupiga hatua ili kufikia malengo yao ila badala ya kusogea mbele wao wanarudi nyuma. ........Kibaya zaidi watu hao wameshindwa kufanya tasmini ya matokeo yao ambayo hayaridhishi. ..
Tatizo nini? .....zinaweza kuwa zipo sababu nyingi ila sababu kubwa inaweza kuwa ni kosa la awali. ...ni lipi hilo? .....karibu tujifunze.

 HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.
Unapoweka malengo ya safari yako lazima ujue mambo muhimu ya kukufanya upige hatua, bila hivyo unaweza kuwa na malengo mazuri yasiyo tembea, zipo njia nyingi ambazo watu tofauti tofauti wanaweza kuzieleza, ila kwa upande wangu taeleza njia tatu za kufanya uweze kupiga hatua, njia ambazo hutengeneza hatua ya awali na muhimu kwenye mafanikio yako. .....njia hizo ni hizi ;

1.Kuwa na marafiki sahihi.ni usemi wa kila siku kuwa mafanikio yako yapo kwa rafiki yako, ila wengi huwa hatujui hilo, bora utumie muda mrefu kuishi bila rafiki kuliko kuwa na rafiki asiyetambua umuhimu wa kusudi lako,Watu wengi wameshindwa kufika waendapo kwa kuwa karibu na marafiki hasi, ....lazima uwe na rafiki sahihi ili uweze kupiga hatua
.
2.Matumizi ya muda. Kwenye matumizi ya muda ndipo kuna mafanikio yote  (tembelea Google search uandike muda wa ziada kalivubha blog ujifunze matumizi sahihi ya muda).Ni ngumu kupiga hatua yoyote ya mafanikio ikiwa bado una matumizi mabovu ya muda,  kuna mambo ambayo lazima uyafanye ili yakupe kibali cha kuendelea, mambo hayo yanahitaji uwe na matumizi mazuri ya muda wako, hatua ya awali ni pamoja na kuwa na ratiba zinazofata muda wako vizuri.

3.Kutambua madhaifu yako. ..wanafalsafa wamewahi kuzungumza kuwa, .."mtu anaekushinda mafanikio kuna mambo anayofanya ambayo wewe hufanyi "..nini maana yake?.ni muhimu kufanya tasmini ya madhaifu ambayo yanaweza kuwa sababu ya kuzuia hatua zako, hiyo itakusaidia kujifunza namna ya kupiga hatua kwa kutumia njia tofauti tofauti zenye kuziba madhaifu yako, ..kujifunza kwa kupitia watu waliofanikiwa sio vibaya, lazima ujue nini ambacho wao wanakushinda .

Ni hatua chache sana za kukufanya upige hatua kwenye malengo yako, ila ni watu wachache sana wamekamilika katika hatua zote hizo tatu, ...fanya tasmini ya maisha yako.

          See you at the top.
          scientist Saul kalivubha.
              (0652134707 )

Wednesday 22 March 2017

MUDA WA ZIADA -2

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha kila jumatano
jumatano ya wiki, nashukuru Mungu
kwa kuendelea kunisamamia....karibu.
tujifunze.

KUSUDILA SOMO.

Kabla ya kuendelea na kusudi la somo letu hili, nikukumbushe kuwa somo letu lina sehemu mbili. 1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.........

ili tuwe sambamba pitia somo la sehemu ya kwanza, tembelea Google search na kuandika kalivubha blog muda wa ziada au Tembelea page ya FIKIA NDOTO ZAKO Facebook.
Leo tunaendelea na sehemu yetu ya pili.
kumbuka kuwa muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja, huu ni ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi. .....karibu tuendelee.

2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.....

KUWA NA MAMBO MENGI;Kuwa na mambo ambayo yana positive effect (matokeo chanya)kwenye ndoto yako sio tatizo, tatizo ni pale mtu anapokosa utaratibu katika kupanga mambo yanayostahili kwanza yawe mbele. ..ukianza kutumia muda wako wa ziada leo  kufanya mambo ya kesho hata kama ni mazuri, utakuwa unapoteza muda, ....lazima uwe na utaratibu katika kufanya mambo yako ili upate muda wa kutosha kufanya yanayostahili kwanza.

STAREHE; hapa ndipo kundi kubwa la watu lipo, maana wengi wanajua starehe lazima itumie pesa  .........hata
ukitumia muda wa ziada kwa mambo yaliyo nje ya ndoto zako tunasema upo
kwenye starehe.
Hili tatizo wanalo watu wengi ambao hawana malengo, ambao hawaumii kutumia sentensi hiii. ."NIPO NAPOTEZA MUDA ".....kila muda unaopoteza lazima utaulipa , je utaulipaje? .....utaulipa kwa majuto.

KULIPA NAFASI JAMBO MOJA. ...hapa tuelewane vizuri , kuna watu ambao wapo addicted na jambo flani, muda wote wa ziada anakuwa busy na jambo hilo tu. .....sio tatizo ikiwa ndio maisha yako yapo kwenye jambo hilo, ..ila kama kuna mambo mengine yamebeba maisha yako ,utakuwa unapoteza muda kwa kufanya jambo hilo moja. ....toa nafasi kwa mambo mengine pia. ...

NB....Kila muda unaopoteza, lazima utaulipa kwa majuto yasiyo na tiba,wengi wetu huwa tunapuuzia usemi huo sababu madhara ya kulipa muda huo huwa yanachelewa. .ila
muda ukifika wa kulipa muda huo lazima mtu akumbuke mambo yaliyo poteza muda wake. .....
Tumia muda wako vizuri leo, ndoto zako zipo kwenye matumizi mazuri ya muda wako wa leo. .........
Unatumiaje muda wako wa ziada?

Karibu kwenye somo mpya muda kama huu. ....

                   See you at the top.
            scientist Saul kalivubha.
                    0652 134707.


Wednesday 15 March 2017

MUDA WA ZIADA -1

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa wema wake kwangu, ni jambo jema kama na wewe una utaratibu wa kumshukuru Mungu kwa makuu yake kwako.
Leo ni siku nyingine tena ambayo nimeona vyema tujifunze jinsi ya kutumia muda wetu vizuri ili tufikie malengo yetu.

KUSUDI LA SOMO .
Lengo la somo letu hili ni kujifunza mambo makubwa mawili ambayo ni.
1. SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA. 2.MATUMIZI MABOVU YA MUDA
WA ZIADA.

Kabla ya kuanza na sehemu ya kwanza ya somo letu, tuangalie maana ya muda wa ziada.
Muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja , huu ni ule ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi.

      1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.

Utofauti uliopo kati ya watu wenye majukumu sawa ila mafanikio tofauti upo kwenye jinsi ya kutumia muda wao wa ziada, zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha utofauti huo,
ila matumizi ya muda wa ziada yana nafasi kubwa kwenye kufanya utofauti huo. siri zilizopo kwenye muda wa ziada ni hizi hapa.


Kwenye muda wa ziada ndio sehemu pekee ambayo mtu unaweza tulia na kufanya tasmini ya safari yako, umefikia wapi, na nini ufanye ili kufika uendapo.
Watu wengi huendelea kuishi maisha yasiyo badilika sababu hawafanyi tasmini ya maisha yao.....huwezi kufanya maamuzi ya kubadilisha aina ya maisha unayoishi ikiwa kwenye muda wako wa ziada unautumia kuboresha mazingira ya maisha yenye matokeo hasi.


Kwenye maisha tunapitia mazingira mengi sana hadi kufikia ndoto zetu, kila mazingira yamebeba mchango mkubwa wa ndoto zetu......kuna uwezekano wa kutofikia uendapo ikiwa  utafanya uzembe katika mazingira yako unayopitia.......ili uweze kujua mazingira uliyopo yamebeba nini kwa ajili yako, lazima uwe na muda mzuri wa kuchambua mazingira hayo. .....!

Wana falsafa huwa wanasema kwamba. ....   "usipo charge akili yako huwezi kuwa na uelewa
Nini maana yake?   walimaanisha ili  tuweze kuwa watu wapya lazima tuwe na muda wa
wa kuingiza mambo mapya na yenye  kubeba malengo yetu.....lazima upate muda wa
kuongeza maarifa,utaongeza vipi?  ...fatilia somo la njia za kuongeza maarifa, litafata baada
ya somo hili.

Kuna watu ambao ni wazee sasa, ila hawajui utofauti wao ni upi, kila mtu ana kitu cha
tofauti ambacho ni zawadi kutoka kwa Mungu, ila kuigundua inahitaji muda wa ziada.
utofauti wako ndio umebeba mafanikio yako, kama una matumizi mabovu ya muda wako,
unaweza usijue utofauti ulionao  (labda ije neema ya Mungu tu ).....

Jiulize, unatumia vipi muda wako wa ziada? ...zipo gharama za kulipa kila muda unaopoteza,
unazifahamu? .......................Tukutane wiki ijayo.


                           see you at the top.
                             scientist Saul kalivubha.
                              (0652 134 707 )









Wednesday 8 March 2017

HOFU YA KUSHINDWA -3

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, upande wangu nashukuru Mungu anazidi kuonekana katika maisha yangu,ni jambo la kushukuru Mungu ikiwa na wewe ni mzima wa afya.
Karibu tena katika sehemu ya tatu na ya mwisho wa somo letu la HOFU YA KUSHINDWA.
NB. unaweza fatilia sehemu ya 1 na 2 ya somo hili kwa kuingia Google na kuandika. ...hofu ya kushindwa kalivubha blog  , ni vyema ufanye ivyo ili twende sambamba na sehemu yetu hii ya tatu. 

KUSUDI LA SOMO. 
Leo tuna jifunza sehemu ya tatu ya somo letu,kumbuka somo letu lina sehemu tatu ambazo ni  1.CHANZO CHA HOFU YA KUSHINDWA 2.MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA NA 3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA. 
NB. Kumbuka tu huwezi kufanikiwa kufanya maamuzi sahihi ikiwa upo kwenye hali ya hofu. 


                3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA .
Leo tuangalie njia za kuishinda hofu ya kushindwa ambayo ni ugonjwa hatari sana katika mafanikio yetu, na mbaya zaidi, watu wengi ni wagonjwa wa ugonjwa wa HOFU. ......
Kuna sehemu nyingi ambazo mafanikio yake yanahitaji uishinde kwanza hofu, siwezi kuelezea kila sehemu ,ila nimechagua sehemu tatu ambazo taeleza jinsi ya kukabiliana na hofu kwenye sehemu hizo, ukiweza vizuri itakusaidia kwenye sehemu zingine. 
Sehemu hizo ni BIASHARA, MAHUSIANO NA MAFANIKIO KWA UJUMLA. 
NB. Kumbuka hofu ni tatizo ambalo linahitaji muda ili kulimaliza, na lazima muhusika mwenyewe ajitambue kwanza. 

BIASHARA; watu wengi tumeishia kuwa na malengo ya bila vitendo katika kuanzisha biashara kulingana na HOFU YA KUSHINDWA, nini kifanyike? .....kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unatambua kuwa changamoto zipo, usianze ukitegemea faida tu, kwa kutambua hilo itakusaidia kupunguza hofu ya kushindwa, maana tayari umetambua changamoto kabla ya kutokea. ........ila utaendelea kuwa imara kupitia changamoto hizo 
Wanasikolojia wanasema.." Changamoto ambayo umesha itambua kabla haiumizi sana "

MAHUSIANO; Vijana wengi huwa na hofu ya kuambiwa wamechelewa kuingia kwenye mahusiano hadi ndoa, hii imefanya vijana hao kuchukua maamuzi ya haraka na yenye kuipendezesha jamii bila kuwa na manufaa kwao. ....ipo pia hofu inayozuka pale mtu anapoachana na mchumba wake  (hofu ya kutopta tena ).....nini kifanyike? ..hakuna kanuni
ya moja kwa moja ila zipo njia ambazo kwa aslimia nyingi zinaweza punguza HOFU. 
(i).KUJIAMINI, lazima mtu ujiamini kuwa una thamani kwa mwenye kuijua thamani yako, kutambua hilo litakusaidia kufanya mambo yako binafsi huku ukisubiria mtu sahihi kwenye wakati sahihi. 
(ii) kuhakikisha unafahamu uendapo , ni ngumu kupoteza muda na mtu asiye wa kwako. ...ikiwa wako unamjua. ...kwanin usiwe mvumilivu kumsubiri? ....huwezi kuwa na hofu ya kuchelewa ikiwa  unamjua wako yupo njiani. .......yapo mengi ila hayo ni machache ambayo ukiyafahamu unaweza punguza hofu ya kushindwa. 
MAISHA KWA UJUMLA; maisha hayataki haraka  (kama wasemavyo waswahili),yanahitaji 
uvumilivu wa kutosha, ila mtu mwenye hofu sio mvumilivu. ......wataalam wa saikolojia wanasema mtu mwenye hofu hutamani kujisaidia kwa kukimbia  (haraka ) hivyo mambo yake huwa ya haraka haraka. .......nini kifanyike? lazima utambue kuwa mambo unaweza kufikia ndoto zako endapo tu ukiwa na subira, ila iwe subira yenye juhudi. 
Hivyo hata upitie changamoto nyingi sio njia ya wewe kutengeneza hofu. ..ila jifunze na ukiweza badilli mfumo wa utafutaji ili kuendelea na safari ya kuelekea mafanikio yako. 

Nina imani kuna kitu umejifunza kuhusu jinsi ya kuipunguza hofu kwa njia sahihi, somo la hofu ni pana sana, na hofu ndio adui mkubwa wa mafanikio yetu,Shetani pia hupenda mazingira yenye hofu. 
Kwa wale wanao amini, njia nzuri ni kuweka imani na Mungu, ukiweka hofu maana yake huna imani na Mungu. 
ulicho jifunza kitumie katika sehemu zote za maisha, ....ishinde HOFU YA KUSHINDWA. 

Karibu tena kwenye somo mpya muda kama huu, somo hilo ni MUDA WA ZIADA.......
ukitumia muda wa ziada vibaya utajuta milele. ...unatumiaje muda wako wa ziada? 

                                    see you at the top. 
                          scientist Saul kalivubha. 
                           ( 0652 134 707 )

Wednesday 1 March 2017

HOFU YA KUSHINDWA -2

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa hali yako ki afya ni nzuri, ila kwa wale ambao hawapo vizuri ki afya, Mungu asimamie harakati zote za kuirudisha afya yenu. Tupo kwenye kumalizia robo ya kwanza ya mwaka huu, nakusihi rejea kwenye daftari lako la malengo ujitasmini umefikia wapi.

Karibu kwenye somo letu la HOFU YA KUSHINDWA, nikukumbushe tu kuwa somo letu lina sehemu tatu ambazo ni. 1.CHANZO CHA HOFU. 2 . MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA. 3 . JINSI YA KUSHINDA HOFU YA KUSHINDWA.

KUSUDI LA SOMO.
Leo tunaangalia sehemu ya pili , MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA, nakusihi upitie somo la kwanza, unaweza fata link hii  (http://kalivubha.blogspot.com/2017/02/hofu-ya-kushindwa-1.html?m=1) au ingia Google search,andika kalivubha blog hofu ya kushindwa, utapata somo hilo.
NB.Lengo la somo hili ni kujifunza jinsi HOFU inavyoweza kuzuia mafanikio yako, hapa ninazungumza hofu iliyo zidi kawaida.

                                   2.MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA.
Hofu ina madhara mengi sana katika kufikia ndoto zetu, tuangalie jinsi HOFU inavyoweza kuathiri sehemu hizi tatu muhimu; MAAMUZI, UVUMILIVU NA KUJIAMIN I. .........ukiweza kufahamu madhara ya hofu katika sehemu hizo tatu, nafikiri utakuwa na uwezo wa kujipima  ili ujitambue upo kundi lipi .

MAAMUZI, hii ni sehemu muhimu sana kwenye maisha, ili uweze kuchagua machache kati ya mengi lazima ufanye maamuzi.........ipo vipi kwa mtu mwenye hofu? ...Mtu mwenye hofu anakuwa hajakamilika, tayari akilini mwake anakuwa na jibu la kushindwa hata kabla ya kufanya maamuzi.....Hivyo mtu huyo anakuwa yupo tayari kuchagua jambo lolote lile ambalo ana amini litapunguza hofu yake.
Kumbuka tu ni watu wachache sana ambao wamewahi kufanya maamuzi sahihi wakiwa kwenye hali ya HOFU ya kushindwa.

KUJIAMINI...Nakumbuka mwalimu mmoja aliwahi kuniambia usemi huu. ."Ukitaka kumshinda adui yako, hakikisha unamfanya apunguze KUJIAMINI "
ipo vipi kwa mtu mwenye hofu ya kushindwa? .....Mtu akiwa na tatizo la HOFU YA KUSHINDWA, anakuwa hajiamini, maana tayari anakuwa ameshindwa AKILINI mwake hata kabla ya kujaribu. ...madhara ya kutojiamini ni kufanya mambo hayaendani na thamani yako. .....
Watu wasio jiamini siku zote huwa hawapati wanayostahili, ila hupata yale wanayo amini yanaweza punguza hofu yao.

UVUMILIVU,mtu mvumilivu mara nyingi lazima awe ana jiamini kwa kiasi kinachostahili na pia lazima awe mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yasiyo bebwa na Imani ya HOFU. ........
Mtu mwenye hofu ya kushindwa ni vigumu kuwa mvumilivu, huwezi kuwa mvumilivu kwenye jambo ambalo kwa imani yako tayari unajua utashindwa......je una weza kufanikiwa kwa hali hiyo?  ......hapana, maana kwenye maisha kuna malengo ambayo yanahitaji muda mrefu ili yaweze kukamilika, yanahitaji uvumilivu wa kutosha.

Hofu ya kushindwa ni hatari sana, hakikisha unajua tiba yake mapema.....Watu wengi wameacha njia zao ndefu ila zenye mafanikio kwa kufata njia fupi zisizo na mafanikio, wamefanya hivyo kwa kuwa WANA HOFU YA KUSHINDWA. .....wamejiona hawawezi .

Kitabu cha RAFIKI kipo kwenye maandalizi, kitakusaidia kujua kujua siri za mafanikio kupitia rafiki.
        Let's meet on the next week , on the same day.
                       
                                 See you at the top.
                                   scientist Saul kalivubha.
                                    (0652 134 707 )

Friday 24 February 2017

HOFU YA KUSHINDWA-1

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nina imani hali yako ya afya ni njema, shukuru Mungu kwa hilo.
Leo nimeona tujifunze swala zima la HOFU.....maana hakuna mafanikio unaweza fikia ikiwa hofu yako imezidi hali ya kawaida.

KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza HOFU YA KUSHINDWA, Somo hili lina sehemu tatu ambazo ni.
                   1. CHANZO CHA HOFU
                     2. MADHARA YA HOFU.
                      3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA.

NB. zipo hofu za aina nyingi sana Mfn  hofu ya kujaribu, hofu ya kukoselewa  n.k,ila hofu zote hizo matokeo yake ni KUSHINDWA kwa jambo ambalo mtu anakusudia kufanya.
.......Hofu kwa maana halisi ni hali ya kuogopa anayokuwa mtu juu ya matokeo ya jambo flani.
               
               1.CHANZO CHA HOFU YA KUSHINDWA.

Zipo sababu nyingi sana zinazopelekea watu wengi kuwa na hofu ya kushindwa katika mambo yao wanayokusudia kuyafanya, chache kati ya hizo ni;

HISTORIA YA MTU...,katika maisha yapo mambo mengi mtu anapitia ambayo hayakuwa na matokeo mazuri kwake, inaweza kuwa ni mahusiano, biashara , hata katika masomo. Kupitia matokeo mabaya hayo, watu wengi hutengeneza imani ya kukosa uaminifu wa kurudia tena mambo hayo,hivyo mtu huyu anakuwa na hofu ya kushindwa kila anapokutana na mazingira yaliyo mfanya ashindwe.

KUTOJITAMBUA...,mtu asiye tambua mazingira anayostahili kupitia ili kufikia ndoto yake huwa anakuwa na hofu ya kushindwa, kwa nini? kwa sababu hana uhakika na alicho shika,kwa hiyo muda wote anakuwa anawaza kushindwa tu katika harakati zake.

MARAFIKI, marafiki wana nafasi kubwa ya kutengeneza hofu ya kushindwa kwa mtu, ukiwa na rafiki wengi ambao walijaribu na kushindwa. .....kibaya zaidi wakakata tamaa, ni rahisi wewe kutengeneza hofu ya kushindwa katika mambo ambayo rafiki zako walijaribu na kushindwa hadi kukata tamaa.
kuna uwezekano kuwa walio fanikiwa wengi waliacha rafiki zao wenye mtizamo wa kushindwa. ....hiyo iliwasaidia kupunguza hofu ya kushindwa kwenye mambo yao.

KUKOSA JUHUDI, hii ni sababu nyingine kubwa katika kutengeneza hofu ya kushindwa kwa mtu, kabla ya kufanya jambo flani,  kuna hali inakuja ya kukukumbusha juu ya maandalizi uliyo fanya kuhusu jambo hilo, hapo ndipo HOFU huanzia kutokana na majibu utayojipa.
mfano, kabla ya kufanya mtihani lazima juhudi yako ikupe hali ya hofu au ushujaa wa kufanya mtihani huo.

NB. Huwezi kufanya maamuzi sahihi ukiwa katika hali ya hofu, maana watu wenye  hofu mara nyingi hutafuta njia za ziada za kupunguza hofu zao. .......swali, Hizo njia za ziada zina matokeo gani kwenye kesho yako?
       .Hofu ina tiba,fatilia somo hili hadi mwisho utajua tiba yake.


                            See you at the top
                          Scientist Saul kalivubha
                           (0652 134 707 )

Thursday 16 February 2017

KOSA LA 1 KWENYE MAFANIKIO

Karibu tena kwenye blog hii ya maisha, upande wangu mimi ni mzima, natarijia hivyo kwako pia. Usisahau kumshukuru Mungu kwa kila hatua unayopitia.
Siku ya leo nimeona vyema tujifunze kosa ambalo wengi tunalifanya na kujikuta tunapoteza ndoto zetu.

                       KUSUDI LA SOMO.

Lengo la somo letu hili ni kutafuta kosa la kwanza ambalo limefanya wengi wetu tuwe sehemu tofauti na kusudi.
Kosa la kwanza ambalo wengi tunafanya ni MAAMUZI YA KUCHAGUA RAFIKI. Ili kulielewa somo hili nmejaribu kugawa vipindi vya umri na uhusiano wa kufanya maamuzi ya RAFIKI.
Fatilia kama ifatavyo;

#MAISHA KATI YA MWAKA 1 HADI 17.
Katika umri huu hakuna tatizo sana, maana  wengi katika umri huu huongozwa na malezi ya walezi wao, pia katika umri huu wengi huwa hawajui nini maana ya rafiki katika mafanikio yao, ingawa kulingana na mabadiliko ya mwili vijana wengi hujaribu mengi na wanao jaribu mabaya huwa karibu na rafiki wa aina hiyo.
Ila huwa ni rahisi kurekebisha makosa ya uchaguzi wa rafiki katika umri huu.

#MAISHA KATI YA  UMRI WA MIAKA 18 -28 (KOSA LA 1)
Hapa ndipo kosa la kwanza huwa na asilimia nyingi za kugeuza njia yako, katika umri huu ukikosea kuchagua rafiki kuna uwezekano usijue utofauti wako, Umri huu ni hatari sana maana vijana wengi huwa kwenye mkusanyiko ya watu wenye malengo tofauti, kibaya zaidi ni kwamba. ......kuna uwezekano kati ya watu kumi, watu watatu tu ndo wana uwezo wa kuishi maisha yao halisi ikiwa watajichanganya na watu wenye malengo tofauti na wao. .....
Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu ambao hawapo sehemu sahihi katika uzee wao, ndoa zao na mafanikio yao walifanya kosa hilo katika umri huu.
Makosa yapo mengi, ila ukipatia kuchagua RAFIKI kuna uwezekano mkubwa wa kuijua njia yako na kupunguza idadi ya makosa.

#MAISHA KUANZIA UMRI WA MIAKA 30 NA KUENDELEA.
Kama upo kwenye umri huu na ulifanikiwa kuwa na uchaguzi mzuri wa MARAFIKI sio tatizo sana, ila kwa walio kosea huwa hali sio nzuri kwao..............Tatizo moja kwa walio kosea na wapo kwenye kundi hili ni IMANI walizojijengea. .....hili ni tatizo kwa sababu kwa imani hizo inakuwa ni ngumu kurudi kwenye njia zao sahihi  (ingawa kwa umri huu huwa ni Kazi kidogo kurudi kwenye ndoto uliyopoteza ingawa kurudi inawezekana ).

RAFIKI sio jambo la kawaida kama wengi wanavyolichukulia, ni jambo la tofauti katika kukufikisha kwenye kusudi sahihi.
Swali la kujiuliza. ..."unafahamu utofauti ulionao? Rafiki yako anatambua kwa nini yupo hapo alipo? "
Kabla ya kufikia umri wa kutumia nguvu kurudi kwenye njia yako sahihi hakikisha unafanya tasmini ya maamuzi yako ya kuwa na rafiki wa aina hiyo. ....

             Tuonane wiki ijayo


                     See you at the top
                Scientist Saul kalivubha
                         (0652 134 707 )