Saturday 19 June 2021

ELIMU YA DARASANI HAITOSHI JIFUNZE NA HIZI

 WANAFUNZI TUJIONGEZE ZAIDI YA ELIMU YA DARASANI 

Tupo katika zama ambazo ajira ni changamoto kubwa sana sio katika nchi yetu tu bali Duniani kote kilio ni kimoja kwa wasomi wengi  lakini tukiachana na tatizo la ajira bado kuna maisha mengine nje ya shule yamekuwa changamoto sana kiasi cha wahitimu kupachukia uraiani  kwa mfano maisha ya mahusiano, maisha ya kujitegemea, elimu ya pesa n.k

Jamii mara zote humuandaa mtoto aende shule kwa lengo kuu aje kuwa na maisha bora baadaye na hata mwanafunzi mwenyewe kadri anavyozidi kuvuka viunzi vya kielimu kuelekea elimu ya juu ndivyo anakuwa na imani kuwa shule itampa maisha mazuri lakini baadaye anapohitimu  hukutana na maisha tofauti kabisa mtaani hata kama atapata ajira lakini utakuta elimu ya pesa inamsumbua au alimu ya namna ya kuishi na watu inamsumbua.

Kitu ambacho ni kigeni kwa wanafunzi wengi huwa wanasahau kuwa shuleni tunaenda kusomea taaluma kwa sehemu kubwa mfano Dakitari wa binadamu miaka mitano yote huandaliwa kumtibu binadamu, Mwanasheria miaka yake minnne huandaliwa kuja kuitafasiri sheria kwa vitendo, mwalimu miaka yake mitatu huandaliwa kuja kumfundisha mwanafunzi mbinu mbali mbali za kufaulu mitihani na kujua kuandika na kuhesabu n.k , ukitazama mifano hiyo utagundua kuwa  shuleni tunaenda kujifunza namna ya kuitumikia taaluma katika mazingira husika na sio namna ya kukabiliana na mazingira ili maisha yawe mazuri. 

Maisha ni zaidi ya taaluma kwa sababu ukihitimu maisha yako yatakuwa sio kutibu tu au kufundisha tu bado utahitaji uwe na familia, utalipwa mshahara na utatakiwa uutumie vizuri, utatakiwa ujitegemee kimaamuzi sasa swali ni je elimu hizo utafundishwa darasani? ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kujifunza zaidi mambo nje ya taaluma yako na njia pekee na rahisi kujifunza mambo nje ya taaluma ni kusoma vitabu vya stadi za maisha vilivyoandikwa na wabobezi katika maeneo mbalimbali ya maisha, kuna maeneo muhimu ya kujifunza ambapo unaweza kuwa unafanya kwenye muda wako wa ziada  ukawa unajisomea vitabu

Elimu ya pesa ni elimu ambayo ni muhimu sana kwa sababu matokeo ya kuitumikia taaluma yako ni kulipwa pesa lakini una elimu ya kuitumia pesa yako? tafuta vitabu vya pesa vilivyoandikwa na wabobezi katika eneo hilo jifunze mbinu mbali mbali za namna ya kuzalisha pesa kwa kutumia mshahara wako au mkopo wako, vitabu vitakupa mbinu za kuweka akiba na kutumia pesa uliyonayo kutafutia pesa usiyokuwa nayo. 

Elimu ya  mahusiano pia ni elimu ambayo ni muhimu sana katika maisha kwa sababu utahitaji uwe na familia na wewe utakuwa baba au mama katika familia sasa utawaongazaje wana familia?  vitabu vimeeleza mengi na wabobezi hivyo vitakufunza Ujasiri katika kuyakabili mazingira ya kimahusiano, mbali na mahusiano ya kimapenzi bado kuna mahusiano ya wafanyakazi hivyo utatakiwa uwasiliane nao vyema la sivyo utachukiwa kazini kila siku na watu kwa tahitaji zako

Elimu ya kujitegemea hii ni elimu muhimu sana kwani uwezo wako utapimwa kwenye namna unavyoweza kujitegemea kwa kufanya mambo hata siku utakayokuwa peke yako, elimu hii pia ipo vitabu muhimu tu uchukue vitabu ambavyo vimeandikwa na wabobezi katika eneo hilo.

Elimu ya biashara pia ni elimu muhimu sana kwa sababu maisha ni biashara unaweza usiifanye moja kwa moja lakini usisahau kuwa hata ukienda sokoni kufanya manunuzi tayari hiyo ni biashara au ile namna ya kuitumia mshahara wako ili ukifikishe mwezi ujao hiyo ni biashara tayari kwani utatakiwa utoe vipaumbele vya kimanunuzi ili ubaki na salio , elimu hii ipo vitabu imeandikwa na wabobezi katika eneo hilo la  biashara hivyo kazi ni kwako tu kujipangia ratiba rafiki.

Elimu zaidi ya taaluma kitakufanya uwe na mbinu nyingi za kuyakabili maisha mbali na kuitumikia taaluma yako bado utaweza kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha 


Saul Kalivubha ni Mwanasayansi tiba na mwandishi 

0652 134707