Saturday 15 December 2018

MBINU ZA KUTOKA NJE YA DUARA LA UMASKINI.

Karibu sana kwenye blog hii ambayo inatoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu ,ni tumaini langu kuwa u mzima wa afya na unaendelea vyema na harakati za kukuwezesha kufikia ndoto zako....Leo nataka tujifunze mbinu kuu tatu za kutoka nje ya duara la umaskini.Somo hili limekuja maalumu kwa sababu ni wazi kwamba ,wengi wetu tunazaliwa na kulelewa katika familia zenye kipato kidogo,sasa tunapoanza kupiga hatua,tunajikuta tuna mzigo mkubwa nyuma yetu,mzigo ambao tuna wajibu wa kuubeba lakini usiathiri hatua zetu za mafanikio....Karibu tujifunze.

DUARA la umaskini ni mzunguko amabao unaanzia kwa maskini na kuishia kwa maskini ,DUARA hili mara nyingi hutokea kwa watu ambao wamezaliwa katika familia za kimaskini,mimi pia ni mmoja wapo,....inakuwa hivi;

Wazazi/ndugu(MASKINI)  >MTOTO(ambaye analelewa katika hali ya kimaskini,ya wazazi wake).

Katika hali hiyo,matatizo ya  waliokutangulia yataendelea kukufuata mpaka pale utakapo amua kutengeneza  mfumo ambao utawafanya wawe na utegemezi wao binafsi(wajitegemee),kinyume na hivyo,kidogo chako kitakuwa kinategemewa na wengi ambao sio wazalishaji.......Hebu tuangalie hizo mbinu tatu ambazo mimi pia ninazitumia,wewe pia zinaweza kukusaidia.

1.Tambua kuwa wewe ndio daraja la kupitisha wengine,hivyo lazima uwe imara zaidi ya hao unaotaka kuwavusha ,uimara ninao uzungumzia hapa ni wa kiuchumi na mawazo,kiuchumi simaanishi uwe na milioni za pesa,la hasha,namaanisha uwe na mfumo unaoeleweka.

2.Tengeneza mfumo ambao chanzo kitakuwa ni wewe lakini waendelezaji watakuwa ni hao umeokusudia kuwasaidia(maana huwezi kusaidia kila mtu),hapa nimaanisha kwamba wewe yafaa uwe mtaji wa mawazo na pesa kwa huyo uliyekusudia kumsaidia kwa lengo la kumfanya awe na mfumo wa kujitegemea.

3. Kumbuka, kutoa pesa kila wanapohitaji sio msaada wa ukombozi,ni bora uwe bahili kwa muda ili kile kiasi ambacho ungekuwa unawapa ukitunze kisha uje ukitumie kutengeneza mfumo ambao utakuwa unajiendesha wenyewe kwa lengo tu la kuwasaidia wao(hapa nazungumzia wale ambao wanategemewa na watu  ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kusimamia wala kufanya biashara zao,....tengeneza wewe biashara alafu faida ndo itumike kuwasaidia pale wanapohitaji na sehemu nyingine ya faida itumike kuendeshea hiyo biashara) 

Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa FIKIA NDOTO ZAKO.