Thursday 26 January 2017

NDOTO YA MSIMU -1

Nakukaribisha tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha,binafsi namshukuru Mungu kwa makuu yake kwangu, nina imani na wewe ni mzima.
Bado tupo mwanzo wa safari, kila anaye jitambua najua yupo makini na aendapo.

.
   KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze somo la,NDOTO YA MSIMU,   katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu.
1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
2.CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU.
3. MADHARA YA NDOTO YA MSIMU.

    1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
Ndoto, ni jumla ya picha mtu anayokuwa nayo kuhusu kesho yake, watu wengi huchanganya kati ya "ndoto"  na "malengo "
Malengo ni sehemu  ndogo ndogo ambazo mtu anapaswa kuziunganisha ili kuifikia ndoto yake.

Ndoto ya msimu ni picha ya maisha ambayo mtu huichora kwa kuchochewa na mabadiliko ya mazingira(msimu ).
NB. ....Ndoto ya msimu inaweza kubadilika na kuwa ndoto ya kudumu ila ni watu wachache sana ambao wanafurahia maisha yameyojengwa na badiliko hilo. ...wengi hujuta.

Kwa upana wa kulielewa vizuri somo hili, pitia mifano hii michache.

#  Wanafunzi wengi katika levels zote za elimu huwa wanajikuta wanatengeza ndoto zao kulingana matukio yanayofanyika shuleni,  ila baada ya siku chache kupita baada ya tukio kuisha, wanafunzi hao husahau kabisa kuwa waliweka ndoto flani. ..siku mazingira ya tukio yakijirudia ndipo wanafunzi hao hupata kumbukumbu (ndoto ya msimu hiyo ).

#Watu wengi mwishoni mwa mwaka huwa wanatengeza ndoto nyingi ili mwaka mpya waweze kuzikamilsha. ....ila mambo huwa tofauti, mwaka Ukianza mpya wanasahau kuwa kuna mambo walijiwekea kuyafanya.
Hali hiyo kuna uwezekano ikawa inasababishwa na mada kuu inayo zungumzwa mwishoni mwa mwaka. .....mwishoni mwa mwaka neno MALENGO huwa kwa wingi masikioni kwa watu, hivyo mazingira hayo humfanya mtu kutengeneza ndoto nje ya uhalisia.

#MAHUSIANO, kuna mtu humpenda mtu kulingana na mazingira, mtu huyu hujikuta moyoni mwake  anatengeneza picha juu ya mtu yule kuhusu kesho yake. ....hatari zaidi mtu huyo kulingana na uchochezi wa mazingira hujikuta anafanya AGANO la kudumu kwenye Upendo wa msimu. .....siku mazingira yale yakipotea mtu huyu ndipo anagundua yupo sehemu isiyo sahihi(ndoto ya msimu )

Nina imani kwa mifano hiyo somo limeeleweka kwa kiasi flanI.
Jiulize ,ndoto uliyonayo ni ya msimu? Kama ndio, umewahi kufikiria ni hali gani utakuwa nayo siku mazingira yameyotengeneza ndoto yako yakitoweka?
NB. ..
Kabla ya kuchukua maamuzi hakikisha umefahamu madhara ya ndoto ya msimu.



                                       See you at the top.
                                       Scientist Saul Kalivubha.
                                              0652 134707.. 

Friday 20 January 2017

JITAMBUE 2

Nimshukuru  Mungu kwa siku nyingine hii, pia niseme asante kwake kwa uzima wako, Karibu tena kwenye blog hii kwa series ya somo letu la KUJITAMBUA.
Week iliyopita tulijifunza SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA. ......kama hukupitia somo hilo ni vyema ukalipitia kabla ya kuendelea na hili la leo  (http://kalivubha.blogspot.com/2017/01/jitambue.html?m=1).

Leo nataka tujifunze sehemu zilizobaki kwenye somo letu hili. .....nazo ni MADHARA YA KUTOJITAMBUA NA JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA. ..


        2.MADHARA YA KUTOJITAMBUA.
Kutojitambua ni tatizo ambalo  limefanya wahusika wawe sehemu zisizo sahihi  (kwenye mahusiano, biashara, mafanikio n.k).
Madhara ya kutojitambua ni matokeo ya kuwa sehemu isiyo ya kwako. ......

 Madhara makubwa ambayo yanaweza beba yote kwa mtu asiye jitambua ni kutofanikiwa kwa jambo lolote, huwezi fanikiwa ikiwa hujui wapi umetoka, wapi ulipo na wapi uendapo, ili mtu afanikiwe kwa jambo lolote lazima ajue vizuri sehemu anayoenda, ikiwa haitoshi lazima mtu atambue vizuri mazingira ya kumfikisha aendapo.

Mtu asiye jitambua mara nyingi hushangiliwa na watu wavivu(watu wanaopenda sehemu rahisi )  hii humfanya mtu huyo kuendelea kufanya mambo ambayo yapo kinyume na jamii inayojitambua, hivyo mtu huyu hupoteza uaminifu. ....

  3. JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA.  
Kutojitambua huwa nasema ni ugonjwa kwa sababu kila mtu anaweza ambukizwa tabia ya kutojitambua kutoka kwenye mazingira.
Huwa ni rahisi kuzuia ugonjwa huu, ila ni Kazi kubwa sana kuutibu endapo mtu akiupata. ...hii hutokana na wagonjwa wa tabia hii kuwa wagumu kukubali kuwa ni victims.

 Ili mtu apone ugonjwa huu inabidi kwanza yeye mwenyewe atambue kuwa ni mgonjwa, kisha hatua inayofata ni zoezi la kubadili MARAFIKI. .....maana mtu asiye jitambua kuna uwezekano mkubwa hata rafiki zake hawajitambui pia.
Zoezi la kubadili rafiki huwa ni ngumu kidogo  (lina hitaji ujasiri ) Ila ndio tiba pekee ya kuaminika kwa mgonjwa wa aina hii.


Let's meet on the next week , we will be having  a new lesson termed as NDOTO YA MSIMU.



                    see you at the top
                    Scientist Saul kalivubha.

Thursday 12 January 2017

JITAMBUE 1

 Nashukuru Mungu kwa uzima wangu, bila shaka wewe pia ni mzima wa afya. Ni utamaduni mzuri sana kuwa na ibada ya kumshukuru Mungu kwa makuu yake.

KUSUDI LASOMO
.Tukiwa bado tupo kwenye safari ya maisha nimeona vyema tujifunze somo la KUJITAMBUA. Somo hili litakuwa na sehemu tatu.

   1.SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA.

  2.MADHARA YA KUTOJITAMBUA.
                        3.JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA.


Kujitambua kwa maana (definition) rahisi ni kufahamu vizuri mazingira yako, ..kufahamu mazingira yako tu haitoshi, kufahamu kwa nini upo kwenye mazingira hayo ndo Kujitambua kamili.
Kuna uwezekano kuwa watu wengi wapo maeneo yasiyo sahihi kwa sababu tu hawajitambui, na wataendelea kuwa maeneo hayo sababu  ya tatizo la kutofanya TASMINI.


                         SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA

Kutojitambua
ni tatizo ambalo wengi wetu tunalo,ila ukiwa hujakutana na mazingira ya kulichochea tatizo hilo ni vigumu kuona dalili zake. ......na mara nyingi mtu mwenye tatizo hilo huwa hakubali kama analo. ....

zifatazo ni baadhi ya sifa za mtu aliye na tatizo la KUTOJITAMBUA.

KUTOKUWA NA MALENGO : hii inaweza kuwa ni sifa kuu ya mtu asiye jitambua,  neno malengo kwake anakuwa analisika tu. Kumbuka tu usipokuwa na malengo huwezi kujua usahihi wa eneo ulilopo, kila jambo kwako utaona sahihi ila mazingira yakibadilika kidogo utaona sio eneo sahihi kwako.

 KUTOKUWA NA RATIBA; mtu asiye jitambua huishi kwa ratiba za watu wengine,  kama huna ratiba ya kuongoza maisha yako ni ngumu  kuwa na mipaka ya kulinda muda wako. .....kila ratiba ya nje itakuwa inafanya mabadiliko kwako...kumbuka tu watu hupenda sehemu rahisi, kila wakiwa na free time hutafuta sehemu rahisi ya kupumzikia. ...mtu asiye jitambua huwa busy kwenye free za watu wengine.


KUWA TAYARI KUACHIA ALICHO NACHO; ..Ni jambo jema mtu kufanya tasmini na kubadili mazingira  (endapo akigundua hayupo sehemu sahihi ,ila hii ni tofauti kwa mtu asiye jitambua, ..mtu huyu yupo tayari kuacha sehemu salama na kuelekea pasipo salama,  hii mara nyingi hutokana na tabia kutojiamini (tabia ya mtu asiye jitambua ).....ni vigumu kuamini kitu ulicho nacho na wakati hujui sahihi ni kipi, na ukikosa imani na ulicho nacho just muda wote utakuwa na mawazo ya kukiacha.


KUISHI KWA MAZOEA;  mtu asiye jitambua huishi kwa mazoea, muda wote yeye anakuwa anaamini kufanya mafanikio mwisho wa safari yake,  kwa kuwa amepoteza kujitambua,mtu huyu
hana sababu za kwanini yupo  pale alipo. ....swali zuri la kujiuliza siku zote ni " upo hapo ulipo kwa sababu wengine wapo or upo kwa sababu lipo kusudi la wewe kuwepo hapo ?"


KUKOSA UVUMILIVU; mtu asiye jitambua hana uvumilivu hata kidogo, hii hutokana na kutojua  umuhimu au hasara wa alicho nacho, ni vigumu kuvumilia na huku hujui kwa nini unavumilia. ......wavumilivu ni wale wanao tambua mazingira yao vizuri.


      KUTOJITAMBUA ni ugonjwa wa kuzuia mafanikio, ugonjwa huu tafasiri yake ni sawa na msafiri ambaye huchukua maamuzi ya kupanda gari bila kujua aendapo.

.......welcome again next session on next week.

                 See you at the top.
             Scientist Saul kalivubha.
                 0652 134707


Thursday 5 January 2017

MAAMUZI

Nimshukuru kwa kunipigania kila siku, hadi sasa nipo salama. .....ni vyema kama na wewe una utaratibu wa kumshukutu Mungu.....

KUSUDI LA SOMO. 

Leo nataka  tujifunze machache kuhusu  Maamuzi......karibu tujifunze,

                  MAAMUZI. .....

 Mwandishi :Saul kalivubha.

Maamuzi kwa mtazamo wangu huwa nasema. ....Maamuzi ni miguu,  usipofanya maamuzi huwezi piga hatua. ..
Mazingira tunayoishi yamebeba mambo mengi,...ili kupiga hatua lazima tuchague machache kati ya mengi. ...maamuzi ni kuchagua pia na ni changamoto kubwa sana kwenye mafanikio yetu. ...

                  MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU MAAMUZI. 
Unapofanya maamuzi, fahamu kuna hatua itafata ambayo ni utekelezaji, kabla ya utekelezaji  ni bora ukatasmini upya maamuzi yako. hii nafaida kubwa, maana mara nyingi mtu hufanya maamuzi kulingana na hali aliyonayo muda huo. .....inawezekana maamuzi yako sio halisi ila ya hali uliyokuwa nayo tu. ....je hali hiyo ikitoweka bado utaona upo kwenye maamuzi sahihi? 

Sifa kubwa ya maamuzi sahihi ni kuwa na matokeo yenye changamoto, Hapa ndipo wengi hujikuta wakibadilisha msimamo. ....Maamuzi sahihi ni chukizo kubwa kwa rafiki zako wanaotamani usitembee, changamoto zitaanzia kwa wao kupinga utekelezaji wa maamuzi yako. Kwa sababu wengi wetu hufanya maamuzi ili kufurahisha watu, tukiona rafiki zetu huchukia maamuzi yetu na sisi hubadili msimamo wetu. ......usiogope kupoteza rafiki walio kinyume na wewe,kumbuka tu bila maamuzi huwezi kupiga hatua. 

Kama una ugonjwa wa kukata tamaa hakikisha unafanya maamuzi ya kutibu ugonjwa huo kabla ya kufanya maamuzi mengine. ....almost watu wote waliokata tamaa huwa maamuzi yao ni sahihi kwao ila huwa hayana mafanikio. ......mtu aliyekata tamaa huwa na imani flani akilini mwake, hivyo imani yake ndio hutwala maamuzi yake.Imani ya mtu aliyekata tamaa ni  ni HOFU. .....ukifanya maamuzi ukiwa na hali ya hofu jiandae kupokea matokeo yenye kukatisha tamaa zaidi ya mwanzo. 


Ukishindwa kufanya maamuzi, mazingira yatafakufanyia maamuzi. ....wapo watu ambao hawajui waendapo wala watokapo. ..ni vigumu kusema jambo hili sio sahihi na huku sahihi hulijui,hivyo ukiwa kwenye hali hiyo tayari umetoa kibali cha mazingira kukufanyia maamuzi. 
Tatizo hili wanalo wengi, ili ujue kama una tatizo hilo jaribu kutasmini maamuzi unayofanya ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu. .....jiulize hayo maamuzi ni yako au ni influence za wanaokuzunguka? ............


Watu ambao mazingira yamewafanyia maamuzi ila bado wanahisi ni maamuzi yao kuna uwezekano kuwa hawapo sehemu sahihi  (iwe  kwenye mahusiano, ndoa, biashara nk).
Jitahidi uwe makini kwenye maamuzi. 


                             See you at the top.
                      scientist Saul kalivubha.
                                  0652 134707.