Saturday 30 April 2022

MAISHA HAYA HAPA

UNATAFUTA MAISHA? HAYA HAPA.

Kumekuwa na semi nyingi kuhusu maisha na karibia kila siku watu hutoa majibu kuwa wametingwa na harakati za kutafuta maisha  lakini swali ni je unajua unachokitafuta?  Unayajua maisha?  
Maisha ni uhai hivyo kama wewe sio mfu basi tayari una maisha kwa sababu ungekuwa huna maisha ungekuwa kaburini leo ila kwa kuwa unapumua tayari maisha unayo yafaa ushukuru Mungu kwanza kwa hilo la wewe kuwa na uhai mpaka sasa ni nafasi ya upendeleo kwako.
Unatafuta nini? Unachotafuta ni vitu ambavyo vitafanya maisha yako yaendelee kuwepo ambapo vitu hivyo vipo kwenye makundi makubwa mawili  ambayo ni vitu vya msingi kwa uhai na vitu vya zaidi ya uhai .
Vitu vya msingi kwa uhai ndivyo huitwa mahitaji ya lazima ili kuulinda uhai wako  na ukifanikiwa vitu hivyo tayari hiyo ni hatua ya awali ya mafanikio kwa sababu ukiwa na hivyo akili itaacha kuwa na msongo wa mawazo juu ya vitu hivyo na sasa itaanza kuwazia hatua ya pili ambayo ni mafanikio zaidi ya kuwa hai .
Mahitaji ya msingi kulinda uhai wako ni kama vile  Chakula, malazi na mavazi . Bila chakula huwezi kuwa na uhai kwa sababu mwili unahitaji chakula ili usipoteze uhai  , bila malazi pia unakuwa kwenye hatari kubwa ya kuupoteza uhai kwa sababu ni rahisi kushambuliwa na wanyama wakali na endapo utalala nje na hatimaye kuupoteza uhai na bila ya mavazi pia ni hatari kwa sababu ni hatari kushambuliwa na vimelea vya magonjwa na hata kupoteza kujiamini kwa sababu tu unatembea utupu ilihali wengine wamevaa. 
Unaweza kumudu Chakula?
 Unaweza kujimudu sehemu ya kuishi?
 Unaweza kujimudu mavazi?  
Kama maswali yote matatu kwako majibu ni ndiyo basi hongera sana hiyo ni hatua kubwa sana kimafanikio inayolinda uhai na kama majibu yako kwa maswali yote matatu ni hapana basi bado kwa namna moja utakuwa bado ni tegemezi na kama umri wako kisheria ushavuka utegemezi basi mapambano yaendelee kutafuta kwanza vitu hivyo vitatu ili uweze kujimudu kwanza na kisha uanze kuwazia hatua ya pili ya mafanikio. 
Hatua ya pili ya mafanikio inategemea na hiyo ya kwanza, ukishakuwa una uwezo wa kujimudu tayari  sasa hatua ya pili itakuwa kutafuta zaidi ya uhai na hiyo ndio hatua ya kuacha alama kwenye maisha yako , hatua hiyo ya pili ni kuliishi kusudi la kuumbwa kwako hivyo kama uliumbwa kuwa mchezaji wa mpira basi simamia vizuri eneo lako , kama uliumbiwa kuwa mwimbaji basi simamia vizuri eneo hilo kwa ufupi tu tuseme kuwa hatua ya pili ni kuishi ulichoumbiwa  .

Mafanikio mazuri ni muungano wa hatua zote mbili ambazo  ni uwezo wa kujimudu na uwezo wa kuishi kusudi la kuumbwa. Hatua ya kwanza ya kujimudu kwenye chakula, malazi na mavazi inahitaji ubunifu wa hali ya juu sana la sivyo utashindwa kuivuka hatua hiyo na muda wote utakuwa unapambana kwa ajili  ya mwili wako tu na sio kwa mapendeleo zaidi, unahitaji ujenge mfumo utakaofanya uwe unapata mahitaji yako bila wewe kujishughurisha moja kwa moja kwa mfano unaweza kuwa na biashara ambayo itakuwa inajiendesha ili kukupatia pesa ya chakula, malazi na mavazi  lli kipindi biashara hiyo inaendelea wewe unakuwa busy na kupambania hatua ya pili ya mafanikio. 
Karibia kila siku inatakiwa uwe unajitathmini kujiona ni hatua gani upo? na mipango ipi umeweka ili kuvuka  hatua ya kwanza.

Upo hatua gani wewe? 

#Mwanasayansi Saul Kalivubha. 
#Fikiandotozako.
+255652134707

Saturday 9 April 2022

NAMNA YA KUTIBU MAJERAHA YA KIHISIA

 TIBA YA HISIA ZILIZOJERUHIWA. 

HISIA ni msukumo ambao unahitaji kutimilizwa , mfano  mtu ukiwa na hisia za kupenda utafurahi ukipendwa, ukiwa na hisia za hasira utataka ufanye jambo fulani kuimaliza hasira n.k, sasa tunapata picha kuwa kila kwenye hisia kuna jambo litatakiwa kufanywa ili kutimiliza lengo la hisia.Tuangalie kisa  hiki ambapo najua kwa namna moja au nyingine utakuwa umewahi kuwa muhanga, mmepanga kukutana na rafiki yako mnayependana kweli   mara ghafla siku moja kabla anakutumia ujumbe kuwa hatoweza kuja tena siku hiyo kapatwa na dharura  hivyo mpaka siku nyingine kama wewe utajisikiaje? Kwa jibu la haraka utajisikia vibaya na sababu kubwa sio kuwa kakupotezea muda kama wengi wanavyodai la hasha ni kwa sababu ujio wake kwako ulikuwa ni tiba ya hisia fulani ambazo tayari zilikupanda pale tu mlipokubaliana  kukutana  tena kibaya zaidi mkiwa mna mahusiano ya kimapenzi ndio utatumia zaidi  kwa sababu kajeruhi hisia zako. 

Tumeona kuwa kila kwenye hisia kuna jambo linatakiwa hivyo lisipofanyika basi hisia zako zitakuwa zimejeruhiwa. Jeraha la kihisia ( psychological trauma)   linatofautiana ukubwa kutokana na aina ya hisia iliyojeruhiwa  mfano hasira uliyonayo dhidi ya mtu unayemdai na unataka uonane naye umwambie bayana endapo hutaonana naye utaumia lakini muda sio mrefu jeraha lake litapona utaendelea na maisha lakini hisia za kupenda ikitokea umempenda mtu  lakini mwenzako akawa msaliti na mwisho mkavunja uhusiano hilo jeraha lake  kupona sio rahisi na litakuathiri sana kama utakosa mbinu za kujitibu.

Bila shaka umewahi kuona watu wakiwa na tabia mpya punde tu baada ya kukutwa na maswaibu fulani, ulevi, wizi, uhuni , kuchelewa kuoa/kuolewa kwa kutoamini tena mahusiano  n.k, hayo ni moja ya matokeo ya kushindwa kujitibu majeraha ya hisia zilizojeruhiwa au  kujitibu kwa mbinu zisizo sahihi  kwa sababu baada ya hisia kujeruhiwa  kinachofuata  ni muhusika kutafuta tabia mpya itakayomsaidia kusahau maumivu  sasa hapo ndipo kuna tatizo  wengi huchagua tabia ambayo ndio badala ya kuwatibu ndio inawakandamiza zaidi mfano baada ya mtu kuachwa kwenye mahusiano anaamua kutokuwa tena muaminifu au kutowaamini tena watu tabia ambayo inamfanya aendelee kuteseka kwa sababu ataachwa tena kwa kukosa uaminifu. 

Hisia zinapojeruhiwa jitahidi ukubali kwanza hali  na pia katika machaguzi ya tabia mpya itayokufanya ujione sawa usichague vilevi  na wala usichague kulipiza kisasi bali chagua kujiboresha zaidi ili hata ikitokea tena basi sababu nyingi zisilalie kwako , fuata hatua hizi :

1.ikubali hali. 

2.Usianzishe tabia za kujisaulisha kwa muda  mfano kuanza ulevi n.k,bali tafuta tabia itayokuboresha zaidi 

3. Jipe muda mrefu wa kujiboresha ukiwa bora itakujengea kujiamini. 

4.Ukiridhika kuwa umejiboresha sasa unaweza kuendelea na maisha mengine na ukiweza epuka vichocheo vitavyokufanya ukumbuke namna ulivyojeruhiwa kihisia.

Saul Kalivubha ,Mwanasayansi tiba  

            +255652 134707