Thursday 19 December 2019

RAFIKI YAKO NI NANI?

Habari za kwako ndugu mpenzi msomaji wa blogu yetu pendwa ya FIKIANDOTOZAKO  na hongera sana kwa majukumu ya kila siku na pole kwa changamoto za kila siku pia, karibu kwenye somo maalumu la kufunga na kufungua mwaka liitwalo  RAFIKI YAKO NI NANI?.

Ni kawaida yangu kila mwaka kufanya tathmini ya malengo yango na kisha kutafuta sababu za kwa nini nimeshindwa au nimefanikiwa  na hapo huwa nakuta sababu nyingi  sana nyuma yake  lakini  sababu moja tu huwa ninaipa uzito nayo ni RAFIKI ALIYE NYUMA YANGU NI YUPI? napenda sana kukupa changamoto ya kujitafakari na wewe uchunguze nyuma ya kushindwa/kufanikiwa kwako yupo RAFIKI WA AINA GANI?

Ni kawaida ya watu wengi kujiwekea malengo kila mwanzo wa mwaka mimi pia ni mmoja wao na malengo hayo yanakuwa na uhusiano na maono(vision)yako mfano una maono ya kuwa na kampuni kubwa ya kusaidia vijana baada ya miaka kumi ijayo hivyo ni jukumu lako la kuishi maandalizi kila siku kila mwaka ujione kusogea kwenye hayo maono yako  , sasa angalia maono yako umeyasogelea au umesogea nyuma kabisa? Kwa nini?

RAFIKI YAKO NI NANI? Siku nzima ni ngumu kuisha bila kuwasiliana na rafiki yako wa karibu  na hiyo ndio kawaida ya URAFIKI yaani kunakuwa na hisia za kutaka  ujione karibu na rafiki yako  sasa je MNAONGEA nini? mnaongea kwa mazoea  tu salamu , kukumbushana ya nyuma na kuambiana move zipi nzuri au viwanja vipi vizuri vya starehe kisha usiku mnatakiana usiku mwema, huyo ndio rafiki yako? rafiki anakutafuta akiwa na shida tu au ili URAFIKI uendelee wewe ndio unatakiwa kila siku kuanzisha mazungumzo wewe na kama hiyo haitoshi URAFIKI umejengwa na vitu yaani mmoja anatumia nguvu ya ziada kuufanya URAFIKI uendelee, nikupe pole sana kama upo kwenye URAFIKI wa aina hii kwa sababu hakuna namna unaweza kufikia malengo yako ukiwa kwenye hali hiyo ya marafiki sana utaishi tu maisha ya kawaida huku ukiamini ndio maisha yalivyo.

CHAGUA MARAFIKI WA KUAMBATANA NAO.

Unataka kwenda wapi?

Marafiki wazuri ni wale ambao ukiwa nao unajiona mpya kwenye malengo yako yaani mkiwa wote wanakupa namna utakavyofika na sio wanakuonyesha namna utakavyoshindwa kwa kila malengo yako  , usiwe na marafiki ambao watakufanya mtumwa kwao badala ya wote kwa pamoja kusaidiana jinsi ya kufika wao wanajenga mazingira ya wewe kuwa mtumwa kwao.

Rafiki yako ni nani?

Soft copy ya kitabu cha siri za URAFIKI kinapatikana kwa Tsh 4000 tu .

 Saul Kalivubha.
  Mwanasayansi.
FIKIANDOTOZAKO.
   0652 134707