Walioachwa kwenye mahusiano wakakurupukia mengine haraka wakiwa kwenye hali ya kuvurugwa wengi wao walijikuta wakikosea tena vibaya zaidi ya mwanzo.
Waliofumania wenzi wao au kusikia taarifa mbaya dhidi ya wenzi wao na wakafanya maamuzi wakiwa kwenye hali ya kuvurugwa wengi walijikuta kwenye maamuzi mabaya na yenye majuto kama vile kuua au kujiua.
Waliojibizana wakiwa kwenye hali ya kuvurugwa wengi walijikuta wakiongea maneno ya hovyo na yaliyokosa hekima kiasi cha kujipotezea heshima.
Furaha na huzuni vyote vinaweza kupoteza utulivu wako na utulivu ukipotea basi tarajia maamuzi ya hovyo kwa asilimia kubwa.
Adui wabobevu wanalijua hilo ndio maana wakitaka kukushambulia kirahisi basi watatafuta namna ya kukuvuruga na kukushinikiza ufanye maamuzi ukiwa kwenye huo mvurogo wakiamini ni lazima utakosea tu.
Utulivu ndio silaha pekee kwenye nyakati kama hizo na hapo utapata jicho la tatu la kuona hali halisi na maamuzi gani uchukue .
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
#Mitandaoni @Fikia Ndoto Zako