FUNGU LA PESA,UNAYOPOTEZA.
Leo nataka kukushirikisha somo hili juu ya pesa inayopotea, pesa ambayo unaitumia kufanyia manunuzi lakini unaitoa kwenye fungo lisilo stahili,je ni pesa gani unaitumia kufanyia manunuzi? na ni aina gani ya manunuzi unayafanya?.........Hapa nataka tuzungumzie manunuzi ya vitu ambavyo havizalishi pesa,mfano radio,tv,kabati ya nguo nk.....je huwa unanua vitu hivyo kwa kutumia pesa ya aina gani?
AKIBA ,hii ni pesa ambayo inatakiwa itumike kununulia vitu ambayo vinazalisha pesa nyingine,ukitumia pesa ya akiba kununulia kitu kisicho ingiza pesa ,unakuwa umeipoteza pesa hiyo.....Kwa nini unakuwa umeipoteza hiyo pesa?........kwa sababu ulitumia muda mwingi kuiweka hiyo pesa kidogokidogo,alafu unakuja kununua kitu ambacho badala kikuingizie pesa ,kinahitaji uendelee kutoa pesa ili ukihudumie,mfano ,unaweka pesa kama akiba ,alafu unakuja kununua radio,ambalo litahitaji uendelee kulihudumia kama vile kununulia CD nk, .....pesa umeyolimbikiza kwa muda mrefu,unaipoteza kwa siku moja,kimahesabu,hapo unakuwa unarudi nyuma,huendi mbele.........Unatakiwa ufa
nye nini? ....iwekeze akiba yako,ikuzalishie faida kwanza.
FAIDA,Hii ndio pesa inayotakiwa itumike katika matumizi ya aina mbili,ambayo ni ;
- Kununulia vitu visivyoingiza,mfano ,kama radio linauzwa Tsh 100000,ni bra uiwekeze hiyo pesa ikuletee faida ambapo hiyo faida ndio uitumie kununulia radio........hapo utakuwa hujapoteza.
- Faida inatumika kupanulia uwekezaji wako....... Kabla ya manunuzi ,hakikisha unatambua hicho unachataka kukinunua kina ongezeko la aina gani kwenye uhuru wako wa kifedha, hiin itakusaidia kufahamu aina ipi ya pesa itumike katikamanunuzi.
- Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha.
- 0652 134707
No comments:
Post a Comment