Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Thursday, 17 October 2019
NGUZO ZA MAAMUZI SAHIHI,JIFUNZE.
Na Mwanasayansi Saul Kalivubha.
Habari ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako hii pendwa na karibu tena katika safu hii ambayo tunajifunza mambo chanya kwa ajili ya kuitafuta hatua mpya zaidi ,karibu tujifunze.
Maamuzi sio neno geni hata kidogo na kila siku lazima kila mtu afanye maamuzi mara nyingi sana japo idadi ya maamuzi haziwezi kuwa sawa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, maamuzi ni machaguzi hivyo huwezi kuamua ukiwa na jambo moja mkononi lazima uwe na mambo mawili au zaidi mkononi ndipo ufanye maamuzi ya kubaki na jambo moja kati ya mengi,je una uhakika gani kama maamuzi unayoenda kuyafanya ni sahihi? Kuna nini nyuma ya maamuzi yako? .
Tumesikia watu wengi sana wakijilaumu kwa maamuzi yao ya jana na kujutia kana kwamba wangalijua mapema wasingefanya maamuzi yale hii ni wazi kuwa maamuzi yao sio sahihi japo kwa muda ule wanaamua walijiona kuwa wapo sahihi.
Tuangazie kidogo juu ya nini kinafanya watu wafanye maamuzi na kwa nini majuto yanafuata baada ya maamuzi.
Kwa nini tunafanya maamuzi? Tunafanya maamuzi kwa sababu mambo tunayokutana nayo hatuwezi kwenda nayo yote hivyo lazima tuamue ili kuchagua machache yanayotufaa na kuacha yasiyo tufaa, maamuzi yoyote yale lazima kuna chaguo moja ulilipenda ndio maana ukaamua kulichagua chaguo hilo.
Kwa nini ulizwe na chaguo lako mwenyewe?.Nyuma ya maamuzi yoyote yale kuna ufahamu,hisia,msukumo wa watu na muda.Hivi vitu vinne ndio hasa vinaoongoza maamuzi yetu hivyo unapoona unajutia maamuzi yako lazima kuna moja kati ya ufahamu wako,msukumo wa watu,hisia au muda lilikuvuruga.
MUDA, tunapokuja suala la muda tunaangazia sana kuchelewa yaani mtu anapoingiwa na hofu ya kuchelewa huwa anajikuta akifanya maamuzi bila kuyafikiria maamuzi yake kwa utulivu kwani lengo lake kubwa inakuwa ni kutaka tu awahi hivyo atatumia vigezo vichache katika kufanya machaguzi.
Mara nyingi maamuzi ambayo yanafanywa kwa kukimbizana na muda huwa ni sahihi kwa muda ule mtu anapoyafanya lakini baadaye anakuja kuyajutia maamuzi yake.Usikubali kufanya maamuzi na hisia za kuchelewa utakosea hivyo ni vizuri utafute utulivu ndio kisha ufanye maamuzi.
Msukumo wa watu, hizi tunaziita kelele za nje zinazokusukuma ufanye jambo fulani , sio kwamba hutapswi kutosikiliza kelele za nje la hasha ila unachopaswa ni kutofanya maamuzi kwa sababu umepigiwa kelele,kelele za nje ni kama upepo uvumao ambapo ukikukuta huna msimamo utayumba na kujikuta unaenda hata usipopotaka , kwenye mahusiano na biashara suala la kupigiwa kelele huwa lipo huu sana na wengi waliofanya maamuzi kwa kusukumwa na kelele walipotea, jitafute wewe ni nani na unataka nini ndipo ufanye maamuzi.
HISIA ,Kila mtu ana msukumo wa hisia ndani yake kwani hisia ni sehemu ya ulinzi pale tu zinapotumiwa vizuri, zipo hisia za aina nyingi kama vile hisia za hasira,hisia za kupenda,hisia za huzuni,hisia za hofu nakadhalika, sasa hisia zikiwa juu huwa zinaficha negative side effects (madhara hasi) na kukuaminisha kuwa utafurahia matokeo ya maamuzi unayotumwa kufanya na hisia, mtu mwenye hasira akifanya maamuzi huwa anajiona mwenye furaha kwa muda kisha hasira ikimuachia tu anabaki na majuto , hivyo unatakiwa kufanya maamuzi bila kusukumwa na hisia.
UFAHAMU, ufahamu wa mtu kuhusu jambo fulani ndio unamuongoza kufanya maamuzi yanayohusu jambo hilo ,kwa mfano wanafunzi wanaochagua kozi za kusoma kwa kutumia ufahamu wa haraka na baadaye wanakuja kuona kuwa wamekosea baada ya ufahamu wao kuongezeka, vivyo hata katika mahusiano,biashara na mengineyo watu wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kutumia ufahamu mdogo ,hivyo inashauriwa kutafuta maarifa ya kutosha kabla ya maamuzi fulani .
Subscribe to:
Posts (Atom)