Thursday 17 October 2019

NGUZO ZA MAAMUZI SAHIHI,JIFUNZE.


Na Mwanasayansi Saul Kalivubha.

Habari ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako hii pendwa na karibu tena katika safu hii ambayo tunajifunza  mambo chanya kwa ajili ya kuitafuta hatua mpya  zaidi  ,karibu tujifunze.
Maamuzi sio neno geni hata kidogo na  kila siku lazima kila mtu afanye maamuzi mara nyingi sana  japo idadi ya maamuzi haziwezi kuwa sawa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, maamuzi ni machaguzi hivyo huwezi kuamua ukiwa na jambo moja mkononi  lazima uwe na mambo mawili au zaidi  mkononi ndipo ufanye maamuzi ya kubaki na jambo moja kati ya mengi,je una uhakika gani kama maamuzi unayoenda kuyafanya ni sahihi? Kuna nini nyuma ya maamuzi yako? .

Tumesikia watu wengi sana wakijilaumu kwa maamuzi yao ya jana na kujutia kana kwamba wangalijua mapema wasingefanya maamuzi yale hii ni wazi kuwa maamuzi yao sio sahihi japo kwa muda ule wanaamua walijiona kuwa wapo sahihi.

Tuangazie kidogo juu ya nini kinafanya watu wafanye maamuzi na kwa nini majuto yanafuata baada ya maamuzi.
Kwa nini tunafanya maamuzi? Tunafanya maamuzi kwa sababu mambo tunayokutana nayo hatuwezi kwenda nayo yote hivyo lazima tuamue ili kuchagua machache yanayotufaa na kuacha yasiyo tufaa, maamuzi yoyote yale lazima kuna  chaguo moja ulilipenda ndio maana ukaamua kulichagua chaguo hilo.

Kwa nini ulizwe na chaguo lako mwenyewe?.Nyuma ya maamuzi yoyote yale kuna ufahamu,hisia,msukumo wa watu  na muda.Hivi vitu vinne ndio hasa  vinaoongoza maamuzi yetu hivyo unapoona unajutia maamuzi yako lazima kuna moja kati ya ufahamu wako,msukumo wa watu,hisia  au muda lilikuvuruga.
MUDA, tunapokuja suala la muda tunaangazia sana kuchelewa yaani mtu anapoingiwa na hofu ya kuchelewa huwa anajikuta akifanya maamuzi bila kuyafikiria maamuzi yake kwa utulivu kwani lengo lake kubwa inakuwa ni kutaka tu awahi  hivyo atatumia vigezo vichache katika kufanya machaguzi.

Mara nyingi maamuzi ambayo yanafanywa  kwa kukimbizana na muda huwa ni sahihi kwa muda ule mtu anapoyafanya lakini baadaye anakuja kuyajutia maamuzi yake.Usikubali kufanya maamuzi na hisia za kuchelewa utakosea hivyo ni vizuri utafute utulivu ndio kisha ufanye maamuzi.
Msukumo wa watu, hizi tunaziita kelele za nje zinazokusukuma ufanye jambo  fulani  , sio kwamba hutapswi kutosikiliza kelele za nje la hasha  ila unachopaswa ni kutofanya maamuzi kwa sababu umepigiwa kelele,kelele za nje ni kama upepo uvumao ambapo ukikukuta huna msimamo utayumba na kujikuta unaenda hata usipopotaka  , kwenye mahusiano na biashara suala la kupigiwa kelele huwa lipo huu sana  na wengi waliofanya maamuzi kwa kusukumwa na kelele walipotea, jitafute wewe ni nani na unataka nini ndipo ufanye maamuzi.

HISIA  ,Kila mtu ana msukumo wa hisia ndani yake  kwani hisia ni sehemu ya ulinzi pale tu zinapotumiwa vizuri, zipo hisia za aina nyingi   kama vile  hisia za hasira,hisia za kupenda,hisia za huzuni,hisia za hofu  nakadhalika, sasa  hisia zikiwa juu huwa zinaficha negative side effects (madhara hasi)  na kukuaminisha kuwa  utafurahia matokeo ya maamuzi unayotumwa kufanya na hisia, mtu mwenye hasira akifanya  maamuzi huwa anajiona mwenye furaha kwa muda kisha hasira ikimuachia tu anabaki na majuto  , hivyo unatakiwa kufanya maamuzi bila kusukumwa na hisia.

UFAHAMU, ufahamu wa mtu kuhusu jambo fulani  ndio unamuongoza kufanya maamuzi yanayohusu jambo hilo  ,kwa mfano  wanafunzi wanaochagua kozi za kusoma kwa kutumia ufahamu wa haraka na baadaye wanakuja kuona kuwa wamekosea baada ya ufahamu wao kuongezeka, vivyo hata katika mahusiano,biashara na mengineyo watu wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kutumia ufahamu mdogo ,hivyo inashauriwa kutafuta maarifa ya kutosha kabla ya maamuzi fulani .



2 comments: