UKIZALIWA FAMILIA MASKINI JUA TAYARI UMEKUWA JESHI LA MTU MMOJA MSITUNI, ACHA KUDEKA.
Maisha hayako sawa hilo lazima tukubali na usipolikubali basi utashindwa kupambana kulingana na mwanzo wako ulivyo , Kwa mfano kuna kuna ambao wanarithishwa mali waendeleze na kuna wanaorithishwa matatizo wayatatue.
Kuna ambaye akipata kazi tu hupongezwa kwa kupewa kiwanja cha nyumba ama fungu la pesa na kuna wewe ambaye ukipata kazi tu matatizo yanaongezeka yaani utatakiwa ujengee wazazi, usomeshe watoto wa ndugu zako na kisha ndio uanze kujiimarisha .
Wewe ambaye simu zote unazopigiwa ni za matatizo usijilinganishe na ambaye hupigiwa simu kwa kukumbukwa, Wewe ni jeshi la mtu mmoja tayari hivyo usitegemee msaada wowote wa kivita kutoka nyuma wala mbele hivyo ni kupambana tu mpaka kieleweke .
Mambo ya kudeka waachie wenyewe ila wewe tambua ukifeli ndugu zako wataumia zaidi kuliko hata wewe muhusika kwa sababu umebeba matumaini ya wengine .
Kila siku historia ya ulipotoka iwe inakukumbusha kuwa WEWE NI JESHI LA MTU MMOJA MSITUNI.
#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#Fikia Ndoto zako
+255652 134707