Sunday, 16 July 2017

SIRI YA KUMI YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani wewe hapo ni mzima wa afya,kama ni mgonjwa usijali,Mungu yupo kwa ajili yetu wote.


  KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya kumi ya urafiki ambayo ni UKWELI ,ila kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukapitia na kujifunza kwanza siri ya tisa ya urafiki(SIRI YA TISA YA URAFIKI).


           SIRI YA KUMI  YA URAFIKI   (UKWELI).
Kwenye urafiki kuna kuwekana wazi mambo,ila kabla ya kuweka wazi mambo yako kwa rafiki yako lazima kwanza uwe umejihakikishia uaminifu wa kutosha ,ila wakati mwingine kuna watu wapo kwenye urafiki kwa kuficha ukweli,wanatumia uongo kutengeneza ukaribu wao....je hii ni sahihi?


Wanasaikolojia wa mambo ya mahusiano wanazungumza kwamba ...Watu wanatafuta wasiyoyafahamu,hawana shida na wanayoyafahamu,,,hii tafasiri yake ni kwamba rafiki yako anatafuta mambo ambayo hayafahamu kutoka kwako,inaweza kuwa umemdanganya jambo fulani,siku akilifahamu lazima sura ya urafiki wenu ubadilike,...jifunze kuwa mkweli.


Ni bora kumficha mtu jambo kuliko kumdanganya,sababu za kumficha mtu jambo zinaweza kuwa zina maana kubwa kuliko sababu za kumdanganya mtu,,,,,kumdanganya maana yake umemwambia ukweli wenye hila ndani yake,umetafuta kuaminiwa kwa njia isiyosahihi.



Ukiona rafiki yako amekukwepa kwa sababu umemwambia ukweli,jua huyo sio mtu mzuri kwako,maana ukweli una thamani kubwa sana kwenye urafiki wa kweli,urafiki ambao una lengo la kufikia mafanikio makubwa.


Tatuzo ukisha anza na uongo tu kwenye urafiki wako,itakufanya kila siku uendelee kutengeneza uongo wa kudumisha uomgo wa mwanzo....urafiki wa aina hiyo una umuhimu gani?, ukijiona mjanja wa kudanganya ,tambua thamani yako inashuka,pia unapoteza muda wako kudanganya na kuendeleza uongo wako.



Kitabu cha SIRI ZA URAFIKI kinaelekea kuwa tayari,utakipata kwa mawakala wa fikia ndoto zako....


                           See you at the top.
                    Scientist Saul kalivubha.
                              0652 134707

No comments:

Post a Comment