Tuesday, 24 October 2017

JITENGENEZEE KESHO YENYE MATUNDA.

Habari za kwako rafiki ambaye tumekuwa pamoja kwenye darasa hili la maisha ,kwa lengo la kusaidia kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,karibu tujifunze.

Kusudi la somo.
Leo nataka tujifunze namna tunavyoweza kutengeneza kesho yetu iliyo ndani ya ndoto zetu,somo hili kwa bahati mbaya wengi wanalipata wakiwa tayari wamekosea sana kiasi kwamba kuanza safari upya inakuwa ngumu ,hivyo wanaamua kuendelea na safari isiyo ya aina yao,...tatizo kubwa ni kwamba mazingira yapo kinyume na kesho za watu wengi,hivyo kulipata somo hili na kuliishi,inahitaji ujasiri wa kutosha ,karibu tuendelee(tengeneza soko lako kabla ya safari)

ITAMBUE KESHO YAKO.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kuandaa kesho yako,bahati mbaya kwa upande wa Afrika ni watu wachache sana ambao wanafanikiwa kutambua kesho yao mapema,na wanaofanikwa kufanya hivyo ,wanashindwa kuifikia kwa kukusa maandalizi,kwa wenzetu wazungu ,hali ipo tofauti,wao hutambua kesho yao wakiwa na umri mdogo na wanaanza kutengeza mazingira mapema ya kuja kuiishi kesho yao..........Unafikiri kwa nini wao wanaweza?

Bill Gate akiwa na umri mdogo sana,aligundua kuwa anapenda sana kuchezea Computer,alichofanya alitafuta rafiki wa aina yake ambapo walitenga muda wa kuwa wanajifunza zaidi kuhusu computer kwenye Library ya shule,....akiwa na ndoto ya kumiliki company,alitumia muda mwingi kuwa kwenye mazingira yaliyomfanya awe mpya kila siku kwenye kile akipendacho,Je wewe hadi sasa hujagundua unapenda nini?,Je unakuwa mpya kila siku kwenye eneo lako?......Unafikiri tatizo ni  nini?


HALI YA KUSHANGAZA.

  • Watu wengi wanaifahamu mapema sana kesho yao,na wanajua kabisa jinsi ya kufanya ili waje kuishi kesho hiyo,ila tatizo ni uwezo wa kuthubutu unakuwa mdogo,...kama wewe unataka kesho umiliki kampuni,una maandalizi gani sasa?.....jaribu kutengeneza uhusiano wa kile unachokifanya sasa kiwe msaada wa kusaidia ndoto zako za kesho....kuna gharama,ila lazime uzilipe ili kuweza kuifikia kesho yako.

  • Watu wengi wa wengi tunakwepa maumivu kwa kuyahamishia kesho,....kuliko mtu kuanza maandalizi mapema ya kuandaa kesho ya malengo yake,anaona afanye maandalizi hayo kesho,unachokwepa leo nini?......kila siku ifanye iwe ya maandalizi ya kesho yako.

  • Watu wengi tunataka tuifikie kesho iliyo kamilika.....Hapa nakumbuka mwanafunzi mmoja aliwahi kuniambia,safari yake ya maisha itaanza baada ya kumaliza chuo,swali la haraka likanijia,....Atamaliza na umri gani?,kisha nikajiuliza,ina maana huyu mwanafunzi leo yupo anapoteza muda?,maana bado hajaanza safari ya maisha.
Kesho yako inaanza pale ambapo tayari umejitambua upo kwenye safari ya aina gani,kama safari yako inaenda kwenye kumiliki nyumba za kifahari,anza kuzitengeza leo,,,,,huwezi kuzipa ta nyumba hizo kwa siku moja,ujenzi wake unaanza leo,kila siku jitaahidi unapata maarifa ya kutosha kuhusu hizo myumba unazo zihitaji.



Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO zako.

                    See You At The Top.
                        0652 134707

No comments:

Post a Comment