Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,nikupe pongezi tu kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutembelea blog hi,hutobaki kama ulivyo....karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo hili nataka tujifunze mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukusaidia katika kuanzisha biashara yako.........mambo haya nimejifunza kupitia uzoefu wangu niliojifunza kwenye biashara ambayo nimeahi kuifanya na kwenye uwekezaji ambao tayari nipo naufanyasasa, ,pia mengine nimefanya utafiti kutoka kwa watu wengine........Karibu tujifunze.
Nafikiri kama wewe sio mfanya biashara ,basi utakuwa umewahi kuwaza kuwa mfanya biashara......na kwa sababu umeamua kusoma makala hii,kuna mambo mawili....moja,utakuwa umewahi kufanya biashara lakini haikukulipa,pili utakuwa una shauku kubwa ya kuanzisha biashara ......ni mahali sahihi,.......karibu tujifunze mambo hayo matano.
1.Kuwa makini na biashara zinazofika mtaani kuwa zinaingiza pesa haraka,......inaweza kuwa ni kweli ndio,ila mvuto huo usiwe ndio hamasa namba moja ya kukufanya uifanye bishara hiyo.....biashara inayosifika sana huwa haikawii kuchoka kwa sababu hufanywa na wengi,......kwa hiyo ifatilie kwa kina upate taarifa kamili za wakati huo kuhusu soko lake.....mfano wa biashara zilizosifika ni kilimo cha matikiti,mpunga,bodaboda na bajaji.......bodaboda na matikiti soko lake sio lile ambalo lilisifika miaka michache iliyopita,..limeshuka.....usiingie kwenye biashara bila kuwa na taarifa za wakati huo.
2.Jitahidi uiandike biashara kwenye daftari kabla ya kuanza kuifanya,........andika kuanzia mtaji ,soko lake na malengo ya wewe kuamua kuifanya biashara hiyo.....jipe kikomo cha kukamilisha malengo hayo........weka mikakati itayokufanya uyafikie malengo hayo kwa kupitia biashara hiyo......mfano mimi ni mkulima ambapo malengo yangu ni kumiliki ekari zaidi kumi hadi mwaka kesho kutoka kwenye chache nilizonazo.
3.Weka fungu la pesa,au anzakutafuta pesa ili ukamilishe biashara hiyo sasa uliyoiandika kwenye daftari,...jitahidi tu usitumie pesa yako yote kuanzia biashara,.....tumia akiba kuanzishia biashara.
4.Fanya maamuzi magumu,ishinde hofu ya kushindwa....ukimaliza maandalizi ,mara moja anza biashara.......ila hakikisha umetengeneza soko kabla ya biashara.....tambua ni watu wa aina gani umekusudia waipate bidhaa yako.
5.Fanya biashara kwa juhudi zako zote,kwa ubunifu ,hakikisha unafanya ambayo wengine hawayafanyi kwenye biashara iliyo sawa na wewe.....kuwa mvumilivu na mwenye subira,...biashara mara nyingi hainzi sawa na ulivyotarajia ...utasumbuka kidogo mwanzoni hadi kuja kufikia matarjio.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa label ya fikia ndoto zako.
See you at the top.
0652 134707
No comments:
Post a Comment