Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu....nikupongeze kwa maamuzi yako ya kuamua kuwa mtembeleaji wa blog hii,nina amini hutobaki kama ulivyo....lazima mafunzo haya yatasogeza hatua zako mbele ....karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza sababu zinazopunguza uwezo wa kufikiri,.....na hili somo limekuja maalumu kwa sababu huwezi kufanikiwa nje ya fikra zako,pale ulipo ni matokeo ya kile unachokifikria....mambo gani yanapunguza uwezo wa kufikiria?...jifunze kwa nini rafiki yako hakuamini(urafiki)......
MAMBO YANAYOPUNGUZA UWEZO WA KUFIKIRI.
1.Mahusiano mabovu,..Hapa nazungumzia mahusiano ambayo yamekufanya kuwa mtumwa,haya ni yale mahusiano ambayo yanakufanya muda wote uyafikirie,...kufikiria mahusiano sio vibaya ,ila ubaya huja pale ambapo uliye naye kwenye urafiki amekutengenezea mazingira ya kutojiamini,..muda mwingi utakuwa unafikiria ufanye nini ili asiondoke na matokeo yake utajikuta unakwamisha mipamgo yako mizuri kwa sababu hutoipa nafasi kuifikiria mipango hiyo.
2.Marafiki,Jaribu kuchunguza kile unachokiwaza sana,kisha jiulize ,kwa nini unakiwaza sana?......fatilia marafiki zako wa karibu,wana mtizamo gani kwa kile unachokiwaza sana?.....kama unazungukwa na marafiki wenye uwezo mdogo wa kufikiri,usitegemee kuwa na fikra zaidi yao,.....
3.Ukosefu wa maarifa,Watu wasio na malengo hawpati shida katika kufikria kwa sababu hakuna wanachokitafuta,na mara nyingi watu ambao hawana malengo hupungukiwa pia na maarifa,....ukipata maarifa,lazima utaongeza uwezo wako wa fikra ili uyahamishe malengo hayo kuwa vitu kamili......kwa hiyo kadri unavyokosa maarifa ya kutosha kuhusu jambo flani ndivyo uwezo wako wa kurifikria jambo hilo unapungua.
4.Historia ya maisha yako,Changamoto ni kinu cha mafunzo ila kwa wasiofahamu hilo mara nyingi hujikuta kwenye falsafa hasi...watu hawa mara nyingi huamini kuwa waliyoptia yaliwapunguzia vigezo vya mafanikio,hivyo hawaoni sababu ya kufikiria mambo makubwa zaidi,muda mwingi hufikria waliyopitia.....
Hapo ulipo ni matokeo ya uwezo wako wa kufikiri,je upo sehemu sahihi?,kama sio hakikisha unapunguza mambo unayoyapokea kutoka kwenye mazingira yanayokuzunguka,.......jitengenezee uwezo mkubwa wa kufikri ili ubadilishe hivyo ulivyo.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha ,mmiliki wa label ya FIKIA NDOTO zako,
0652 134707.
No comments:
Post a Comment