Tuesday 9 April 2019

HILI NDIO GEREZA LA HATUA ZAKO

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako.Ni tumaini langu kuwa wewe ni mzima wa afya na unaendelea kupambana katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ili zikupe ushindi wa kuliishi kusudi lako,karibu tujifunze.


KUSUDI LA SOMO.
Somo hili linakusudia kuwasaidia vijana ambao wana tatizo la kutopiga hatua ilihali kila siku wapo kazini na wanapata chochote lakini hawapigi hatua mbele.Katika somo hili ,vijana lengwa ni wale ambao wana maono ya kuifikia hatua fulani lakini siku zasogea na hata dalili za kufika huko hazipo.Wewe pia una tatizo hilo? kama ndivyo ,endelea hadi mwisho utajua gereza lako ni lipi.


KWANINI UNAFANYA HICHO UNACHOKIFANYA LEO?
Hili swali linahitaji sababu ,je umewahi kujiuliza swali kama hilo? na ulipata sababu zipi? .Inawezekana ukawa na majibu yako mengi sana ya kwanini upo unafanya hiyo kazi,wengine watasema ni kwa sababu ndio walichokisomea,wengine watasema ni kwa sababu hawakwenda shule ndo mana wanafanya shughuli hiyo ,n.k.Majibu yatakuwa mengi sana.Mimi kama ningeulizwa swali kama hilo ,jibu langu lingekuwa rahisi sana tu,ningesema sababu inayofanya nifanye hiki nikifanyacho leo ni kwasabu kinanipeleka kwenye kusudi la kuumbwa kwangu. Hivi unafahamu gereza limelofunga hatua zako ni sababu zilipo nyuma ya hicho unachokifanya?

GEREZA LA HATUA YAKO MPYA NI HIYO SABABU YAKO.
 Ni ngumu kupiga hatua mpya kama huna sababu zinazokusuma ufanye hivyo ,na sababu ambazo zitakufanya upige hatua mpya zinategemea sana na wewe unajitambua vipi,hapa ninamaamisha kwamba ni vizuri kwanza ujitambue wewe ni nani na wapi unatakiwa kwenda kulingana na kusudi lililowekwa ndani yako,kisha sasa ndio uangalie hicho unachokifanya ,je kinahusiana vipi na uelekeo wako?

Kama kila siku sababu zako ni kutaka ufanye kazi kwa bidii na kwa weledi,sawa ni sababu nzuri lakini je hicho unachotaka kukifanya kwa juhudi na weledi kinahusiana vipi na kusudi la kuumbwa kwako? kama hakuna mahusiano ndipo pale ambapo utaendelea kuwa na juhudi kwa kufanya jambo fulani lakini hufiki kule kwako ,mfano kama wewe uliumbwa uwe mchoraji ,na sasa upo katika kitengo cha afya kama Daktari,je unaunganisha vipi huo udakitari na kipaji chako cha uchoraji? Hapo unaweza kuiwa na sababu nyingi za kukufanya huo udakitari wako vizuri lakini ukawa huna sababu hata moja ya kutaka ufanye huo udakitari wako uendeleze kiapaji chako ,kwa namna hiyo  utajikuta unaendelea kuwa gerezani tu .

UNATOKAJE KWENYE GEREZA HILO?
Kama nilivyotangulia kusema mwanzo ,kwanza lazima ujitambue wewe ni nani,kisha uangalie unafanya nini kwa sasa,na je ufanyacho kina mahusiano na wewe ni nani? kama hakuna mahusiano sio ukiache ghafla lakini tengeneza mahusiano ,yaani kitumie hicho unachokifanya kusaidia kusudi la kuumbwa kwako,mfano mimi naelekea kuibadili dunia kwa kupitia maandishi na kuongea lakini kwa sasa natumika hospitalini ,je niache kipi?  jibu la haraka ni kwamba navyovipata hospitalini navitumia katika kusukuma kusudi la kuumbwa kwangu ,hivyo nyuma ya haya niyafanyayo kuna sababu zinazoniambia nielekee kwenye ulimwengu wa maandishi na kuzungumza.
Jitahidi utengeneze sababu zinazokusuma kwenda kwenye kusudi lako ,kukosa sababu hizo kunapelekea hali ya kuridhika na hatua hiyo uliyopo ,na hapo ndipo panakuwa mwanzo wa kufanya kazi kwa bidii lakini mbele husogei ,unaishia pale ambapo sababu zako zilikutuma.

Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
            0652 134707



5 comments: