Sunday 14 July 2019

MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.

Habari ndugu na mfuatiliaji wa makala zetu za blogu yako pendwa ya FIKIA NDOTO ZAKO,ikiwa imepita muda wa kutosha bila kukuandikia makala katika blogu yetu hii ni kwa sababu tu ya uboreshaji ambao ulikuwa ukiendelea kwa lengo la kukupatia wewe msomaji na mwanafunzi maarifa yaliyo bora,karibu .

Somo letu la leo ni rahisi kama utalipa muda wa kutosha kalitafakari na ni somo gumu kama utapita juu juu,  hivyo inahitaji utulivu wa hali ya juu sana.
Ufahamu  ni moja ya eneo muhimu sana ambalo ndio linakutofautisha wewe na mimi ,wewe na rafiki yako ,wewe na mnyama kama vile sungura n.k,kumbe ufahamu ndio muongozo wa kwanza wa maamuzi yetu na ndio gereza limelofunga hatua zetu.

Ufahamu unaanzia mbali sana pindi mtoto anapozaliwa hadipale ambapo mazingira yatamuhitaji atafute mwenyewe (kujitegemea)  ,hadi kufikia umri wa miaka 9 mpaka 10 ufahamu wa mtoto unakuwa ukiamini kwa 100% muongozo wa mzazi /mlezi wake ndio maana mtoto wa umri huo anakuwa haamini kama kuna mtu zaidi ya baba /mama yake ,hata akutane na kitu cha kutisha namna gani ambapo hata kina nguvu zaidi ya mzazi wake bado atakitishia kitu hicho kwa kumtaja baba yake au mama yake akiamini hicho kitu kitaogopa na kumuacha,yote hiyo ni kwa sababu ufahamu  wake ndio unamtuma hivyo ,je ufahamu wake ni sahihi?

Inawezekana  ukawa ;

1.Unaabudu katika dini/dhehebu  fulani kwa sababu unaamini uliowakuta wakifanya hivyo hawawezi kukosea kuwa katika sehemu hiyo wanayoabudu.
2.Ulichagua kozi fulani kwa sababu waliokushauri uliwapa thamani ya juu kuwa hawawezi kukosea katika machaguzi.
3.Kwa sababu unaona watu wanafanya  ndio maana ufahamu wako unakutuma kuwa hilo jambo ni sahihi n.k

Je unawezaje kuhakikisha kuwa ufahamu wako ni sahihi?
Tukiachana na kupima ufahamu  ulinao kuhusu dini/imani/kanisa/msikiti  ambapo ni somo ndefu na linalohitaji utulivu wa juu zaidi, tuje katika mbinu za pamoja za kupima ufahamu ulionao kwa ujumla ,kwanza  kabla ya mbinu hizo tutambue ya kwamba ufahamu  kwa asilimia nyingi unatokana na mazingira yanayokuzunguruka kama vile marafiki na wazazi/walezi  n.k, pia ufahamu unategemea na umri.

Kadri mazingira yanavyobadilika na umri unavyosogea ndipo unazidi kuona kuwa kuna mambo zaidi ya vile ulivyokuwa ukifahamu na utagundua kuwa ulikuwa unafanya makosa pasipo kufahamu kwa sababu ufahamu wako ndipo ulipoishia pale,kwani maamuzi yetu ni ,matokeo ya ufahamu wetu ulivyo.

MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.

1.Kwanza jitambue wewe ninani,sio jina lako wala wapi unaishi ,jitambue kwa nini ulizaliwa? utapata sababu ambayo ndio kusudi la wewe kuzaliwa,sababu ya kuzaliwa kwako unaweza pia kuangalia kipi unaona hakiendi sawa yaani kuna namna unasukumwa kutaka kuweka mfumo sawa,hapo kuna kusudi lako na kipaji chako ,ukishajifahamu wewe ni nani tayari utaanza kutafuta ufahamu wa kutosha kujihusu wewe na safari yako.

2.Makosa yetu,kupitia makosa yetu ni njia nzuri sana ya kupima ufahamu wetu,mfano umetumia ufahamu wako kufungua simu ukashindwa ni wazi kuwa ufahamu wako bado, kuna zaidi ya unavyofahamu,unapoingia kwenye makosa kaa chini ujitafakari  ni lazima tu kuna jambo hulijui ndio maana ukakosea hivyo litafute .

3.Kaa chini uchunguze kwa nini unaamini hivyo?  ni kwa sababu uliambiwa hivyo na watu au ni kwa sababu umezaliwa na kukuta watu wakifanya hivyo,kwa mfano wengi tumekuwa tukiwa na ufahamu kuwa shule ndio chanzo cha utajiri kwa sababu tuliambiwa hivyo ,kila siku tunatafuta ajira tukiamini kuwa tukipata tu tutaaga umaskini,lakini ambao tayari wamevipata hivyo ndio wengi wao wanakuja kufahamu ya kuwa kuna zaidi ya shule na ajira ili mtu kuwa tajiri.Hapa tunarudi kwenye namba moja ya kuwa ukishajifahamu wewe ni nani utaanza kutafuta mazingira ya kukupeleka kwako na hapo ndipo utaanza kuachana na ufahamu ambao chanzo chake ni kuaminishwa na watu,watu walikuaminisha vile kwa sababu ya ufahamu wao wa muda ule.


Makala hii imeandikwa na  Saul kalivubha,mwanasayansi na  mwalimu  na mmiliki wa fikia ndoto zako label.

0652 134707.

3 comments: