Saturday, 9 April 2022

NAMNA YA KUTIBU MAJERAHA YA KIHISIA

 TIBA YA HISIA ZILIZOJERUHIWA. 

HISIA ni msukumo ambao unahitaji kutimilizwa , mfano  mtu ukiwa na hisia za kupenda utafurahi ukipendwa, ukiwa na hisia za hasira utataka ufanye jambo fulani kuimaliza hasira n.k, sasa tunapata picha kuwa kila kwenye hisia kuna jambo litatakiwa kufanywa ili kutimiliza lengo la hisia.Tuangalie kisa  hiki ambapo najua kwa namna moja au nyingine utakuwa umewahi kuwa muhanga, mmepanga kukutana na rafiki yako mnayependana kweli   mara ghafla siku moja kabla anakutumia ujumbe kuwa hatoweza kuja tena siku hiyo kapatwa na dharura  hivyo mpaka siku nyingine kama wewe utajisikiaje? Kwa jibu la haraka utajisikia vibaya na sababu kubwa sio kuwa kakupotezea muda kama wengi wanavyodai la hasha ni kwa sababu ujio wake kwako ulikuwa ni tiba ya hisia fulani ambazo tayari zilikupanda pale tu mlipokubaliana  kukutana  tena kibaya zaidi mkiwa mna mahusiano ya kimapenzi ndio utatumia zaidi  kwa sababu kajeruhi hisia zako. 

Tumeona kuwa kila kwenye hisia kuna jambo linatakiwa hivyo lisipofanyika basi hisia zako zitakuwa zimejeruhiwa. Jeraha la kihisia ( psychological trauma)   linatofautiana ukubwa kutokana na aina ya hisia iliyojeruhiwa  mfano hasira uliyonayo dhidi ya mtu unayemdai na unataka uonane naye umwambie bayana endapo hutaonana naye utaumia lakini muda sio mrefu jeraha lake litapona utaendelea na maisha lakini hisia za kupenda ikitokea umempenda mtu  lakini mwenzako akawa msaliti na mwisho mkavunja uhusiano hilo jeraha lake  kupona sio rahisi na litakuathiri sana kama utakosa mbinu za kujitibu.

Bila shaka umewahi kuona watu wakiwa na tabia mpya punde tu baada ya kukutwa na maswaibu fulani, ulevi, wizi, uhuni , kuchelewa kuoa/kuolewa kwa kutoamini tena mahusiano  n.k, hayo ni moja ya matokeo ya kushindwa kujitibu majeraha ya hisia zilizojeruhiwa au  kujitibu kwa mbinu zisizo sahihi  kwa sababu baada ya hisia kujeruhiwa  kinachofuata  ni muhusika kutafuta tabia mpya itakayomsaidia kusahau maumivu  sasa hapo ndipo kuna tatizo  wengi huchagua tabia ambayo ndio badala ya kuwatibu ndio inawakandamiza zaidi mfano baada ya mtu kuachwa kwenye mahusiano anaamua kutokuwa tena muaminifu au kutowaamini tena watu tabia ambayo inamfanya aendelee kuteseka kwa sababu ataachwa tena kwa kukosa uaminifu. 

Hisia zinapojeruhiwa jitahidi ukubali kwanza hali  na pia katika machaguzi ya tabia mpya itayokufanya ujione sawa usichague vilevi  na wala usichague kulipiza kisasi bali chagua kujiboresha zaidi ili hata ikitokea tena basi sababu nyingi zisilalie kwako , fuata hatua hizi :

1.ikubali hali. 

2.Usianzishe tabia za kujisaulisha kwa muda  mfano kuanza ulevi n.k,bali tafuta tabia itayokuboresha zaidi 

3. Jipe muda mrefu wa kujiboresha ukiwa bora itakujengea kujiamini. 

4.Ukiridhika kuwa umejiboresha sasa unaweza kuendelea na maisha mengine na ukiweza epuka vichocheo vitavyokufanya ukumbuke namna ulivyojeruhiwa kihisia.

Saul Kalivubha ,Mwanasayansi tiba  

            +255652 134707


No comments:

Post a Comment