UNATAFUTA MAISHA? HAYA HAPA.
Kumekuwa na semi nyingi kuhusu maisha na karibia kila siku watu hutoa majibu kuwa wametingwa na harakati za kutafuta maisha lakini swali ni je unajua unachokitafuta? Unayajua maisha?
Maisha ni uhai hivyo kama wewe sio mfu basi tayari una maisha kwa sababu ungekuwa huna maisha ungekuwa kaburini leo ila kwa kuwa unapumua tayari maisha unayo yafaa ushukuru Mungu kwanza kwa hilo la wewe kuwa na uhai mpaka sasa ni nafasi ya upendeleo kwako.
Unatafuta nini? Unachotafuta ni vitu ambavyo vitafanya maisha yako yaendelee kuwepo ambapo vitu hivyo vipo kwenye makundi makubwa mawili ambayo ni vitu vya msingi kwa uhai na vitu vya zaidi ya uhai .
Vitu vya msingi kwa uhai ndivyo huitwa mahitaji ya lazima ili kuulinda uhai wako na ukifanikiwa vitu hivyo tayari hiyo ni hatua ya awali ya mafanikio kwa sababu ukiwa na hivyo akili itaacha kuwa na msongo wa mawazo juu ya vitu hivyo na sasa itaanza kuwazia hatua ya pili ambayo ni mafanikio zaidi ya kuwa hai .
Mahitaji ya msingi kulinda uhai wako ni kama vile Chakula, malazi na mavazi . Bila chakula huwezi kuwa na uhai kwa sababu mwili unahitaji chakula ili usipoteze uhai , bila malazi pia unakuwa kwenye hatari kubwa ya kuupoteza uhai kwa sababu ni rahisi kushambuliwa na wanyama wakali na endapo utalala nje na hatimaye kuupoteza uhai na bila ya mavazi pia ni hatari kwa sababu ni hatari kushambuliwa na vimelea vya magonjwa na hata kupoteza kujiamini kwa sababu tu unatembea utupu ilihali wengine wamevaa.
Unaweza kumudu Chakula?
Unaweza kujimudu sehemu ya kuishi?
Unaweza kujimudu mavazi?
Kama maswali yote matatu kwako majibu ni ndiyo basi hongera sana hiyo ni hatua kubwa sana kimafanikio inayolinda uhai na kama majibu yako kwa maswali yote matatu ni hapana basi bado kwa namna moja utakuwa bado ni tegemezi na kama umri wako kisheria ushavuka utegemezi basi mapambano yaendelee kutafuta kwanza vitu hivyo vitatu ili uweze kujimudu kwanza na kisha uanze kuwazia hatua ya pili ya mafanikio.
Hatua ya pili ya mafanikio inategemea na hiyo ya kwanza, ukishakuwa una uwezo wa kujimudu tayari sasa hatua ya pili itakuwa kutafuta zaidi ya uhai na hiyo ndio hatua ya kuacha alama kwenye maisha yako , hatua hiyo ya pili ni kuliishi kusudi la kuumbwa kwako hivyo kama uliumbwa kuwa mchezaji wa mpira basi simamia vizuri eneo lako , kama uliumbiwa kuwa mwimbaji basi simamia vizuri eneo hilo kwa ufupi tu tuseme kuwa hatua ya pili ni kuishi ulichoumbiwa .
Mafanikio mazuri ni muungano wa hatua zote mbili ambazo ni uwezo wa kujimudu na uwezo wa kuishi kusudi la kuumbwa. Hatua ya kwanza ya kujimudu kwenye chakula, malazi na mavazi inahitaji ubunifu wa hali ya juu sana la sivyo utashindwa kuivuka hatua hiyo na muda wote utakuwa unapambana kwa ajili ya mwili wako tu na sio kwa mapendeleo zaidi, unahitaji ujenge mfumo utakaofanya uwe unapata mahitaji yako bila wewe kujishughurisha moja kwa moja kwa mfano unaweza kuwa na biashara ambayo itakuwa inajiendesha ili kukupatia pesa ya chakula, malazi na mavazi lli kipindi biashara hiyo inaendelea wewe unakuwa busy na kupambania hatua ya pili ya mafanikio.
Karibia kila siku inatakiwa uwe unajitathmini kujiona ni hatua gani upo? na mipango ipi umeweka ili kuvuka hatua ya kwanza.
Upo hatua gani wewe?
#Mwanasayansi Saul Kalivubha.
#Fikiandotozako.
+255652134707
No comments:
Post a Comment