Ni tumaini langu kuwa wote ni wazima wa afya, tukiwa mwishoni mwa mwaka huu najua kila mmoja mwenye Upendo na kesho yake yupo busy na tasmini ya safari yake ya maisha. Kumbuka kumshukutu Mungu kwa viwango umevyofikia, haijalishi ni kwa hatua gani umefikia malengo yako
Leo kuna vitu vitatu vitatu nahitaji tujifunze kuhusu mahusiano ya mafanikio na maamuzi yetu tuyafanyao tukiwa kileleni mwa safari,
Hapa ndipo wengi tunakosea na kuharibu uzuri wa hatua zetu za nyuma, yafatayo ni mambo ambayo wengi wetu huyafanya tukiwa kweny kilele cha safari
KULEWA NA MAFANIKIO : ili kuhamia upande wa pili ni vyema ufanye tasmini ya upande wa kwanza ili ujue jinsi ya kuanza upande wa pili. .tasmini ikionyesha mafanikio huwa kuna changamoto kwa anayepokea mafanikio hayo, usipokuwa kuwa makini utajikuta unaishi maisha ambayo yamebebwa na ziada uliyoipata na sio uhalisia wako, Hapa ndipo wengi tunajikuta tunanua mambo yenye kupunguza tamaa za miili yetu na kusahau kuwa kufanikiwa sio mwisho wa kutafuta.
KUKATA TAMAA :tasmini yako ikionyesha kushindwa huwa ni changamoto kwa mtu muhusika, wengi hapa hujikuta hufanya maamuzi ya kudumu kwa hali ya muda mfupi, mfano mtu ambaye alikuwa na lengo la kufunga ndoa mwanzoni mwa 2017 lakin mwishoni mwa mwaka 2016 anaachana na mchumba wake. ..kweny mfano huu wengi huwa wanafanya maamuzi ya kudumu na kujikuta anapteza imani ya watu wote wa aina ya aliyeachana nae. Yapo maamuzi meng ya kudumu tunayafanya mwishoni mwa tasmini na kuishi maisha yenye matendo ya maamuzi hayo huku tukisahau kuwa hali ya muda mfupi huwa ni changamoto na sio tatizo.
KUFANYA AGANO :kuna philosophy inasema " epuka kufanya AGANO na mtu ukiwa ktk furaha au huzuni"......tasmini yako ya mwaka ina matokeo ya aina mbili , mafanikio au kuwa chini ya mafanikio, je hali hiyo imekufanya uweke AGANO na mtu? hakikisha umejipa muda wa kutosha baada ya tasmini yako kisha uwe huru kufanya AGANO na watu (rafiki ).
Nikutakie maandaliz mema ya Christmas.
Scientific Saul kalivubha, see you next session!
Welcome
ReplyDelete