Nakukaribisha tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, mimi ni mzima wa afya, nina imani wewe pia ni mzima.
Tupo kwenye sehemu ya somo letu la NDOTO YA MSIMU , na leo tunamalizia somo letu hili.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza MADHARA YA NDOTO YA MSIMU. Nikukumbushe tu, somo letu lilikuwa na sehemu tatu.
1. MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
2.CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU.
3.MADHARA YA NDOTO YA MSIMU.
Kabla ya somo la leo ni vyema ukapitia masomo yaliyo pita ya NDOTO YA MSIMU,Ingia Google kisha andika NDOTO YA MSIMU Kalivubha blog, utaletewa masomo hayo.
3.MADHARA YA NDOTO YA MSIMU.
Leo tuangalie ni madhara gani yanaweza kumkuta mtu ambaye hutegemea mabadiliko ya mazingira katika kutengeneza ndotoya yake (ndoto ya msimu )...........
Tumuangalie mtu huyo kwa kumlinganisha na sehemu tatu, biashara, mahusiano na mafanikio yake.
#BIASHARA; katika biashara huwa ni ngumu mtu mwenye ndoto ya msimu kuendelea, maana mtu huyu hufanya biashara kwa kutegemea maneno ya watu, leo akisikia Ufugaji wa kuku unalipa, hukurupukia Ufugaji huo bila kufanya tasmini kabla, kesho akisikia kilimo kinalipa, anaweka ndoto zake kwenye kilimo na huku bado swala la Ufugaji ajalifanyia uhakiki.
Mwisho wa siku mtu huyu hujikuta ana malengo mengi yasiyo hai. .........ikiwa huna jambo la kusimama, utajikuta kila wazo kutoka nje kwako ni sahihi, ila huwezi fanikiwa kwa mwendo huo.
#MAHUSIANO, Katika mahusiano, mtu mwenye ndoto ya msimu hutegemea mazingira yaongoze mahusiano yake, hawezi kutulia sehemu moja na mtu mmoja.
Leo akisikia flani yupo kwenye mahusiano na yeye atahitaji kuingia kwenye mahusiano, kesho akisikia mahusiano yana changamoto mtu huyo atahitaji kuachana na mahusiano.
Madhara ya mwendo huo ni mtu wa namna hiyo atakuwa na orodha ya watu wengi kwenye mahusiano yake, hali hiyo itampa madhara ya kisaikolojia na mwisho wa siku ataishia sehemu isiyo sahihi.
#MAFANIKIO, mafanikio kwa ujumla kwa mtu mwenye ndoto ya muda mfupi (msimu ) huwa sio mazuri, maana juhudi za mtu mwenye ndoto ya msimu huwa ni za msimu pia.
Leo akifanya vibaya kwenye masomo, atawekeza juhudi nzito, muda ukipita kidogo husahau na kurudi kwenye hali iliyomfanya apate ufaulu usio mzuri, hata kwenye mambo mengine pia anakuwa na juhudi za muda mfupi.
Hali hii humfanya mtu huyo kuendelea kupata matokeo yale yale kwenye mambo anayofanya. .......
MUHIMU; Dawa pekee ya kuachana na ndoto za muda mfupi ni kuhakikisha unafahamu vizuri kitu unachokitafuta
Ukiwa na lengo la kupata Chungwa na huku hulifahamu vizuri, ni rahisi wewe kupokea Embe(hali ambayo ni hatari sana kwenye maisha )
SWALI ZURI KUJIULIZA; hali uliyokuwa nayo mwishoni mwa mwaka (ki malengo ) ndiyo unayo hadi sasa? .....au mazingira ya mwisho wa mwaka kwa kuwa yameisha, umesahau malengo yako yote.... ikifika tena mwisho mwaka utaanza kuwa busy na kuweka malengo. .........JITASMINI.
Tukutane week ijayo kwa somo mpya.
Jiandae pia kupata kitabu chenye siri za URAFIKI katika mafanikio yako.
See you at the top.
Scientist Saul kalivubha.
( 0652 134 707 )
No comments:
Post a Comment