Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nina imani hali yako ya afya ni njema, shukuru Mungu kwa hilo.
Leo nimeona tujifunze swala zima la HOFU.....maana hakuna mafanikio unaweza fikia ikiwa hofu yako imezidi hali ya kawaida.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza HOFU YA KUSHINDWA, Somo hili lina sehemu tatu ambazo ni.
1. CHANZO CHA HOFU
2. MADHARA YA HOFU.
3.JINSI YA KUISHINDA HOFU YA KUSHINDWA.
NB. zipo hofu za aina nyingi sana Mfn hofu ya kujaribu, hofu ya kukoselewa n.k,ila hofu zote hizo matokeo yake ni KUSHINDWA kwa jambo ambalo mtu anakusudia kufanya.
.......Hofu kwa maana halisi ni hali ya kuogopa anayokuwa mtu juu ya matokeo ya jambo flani.
1.CHANZO CHA HOFU YA KUSHINDWA.
Zipo sababu nyingi sana zinazopelekea watu wengi kuwa na hofu ya kushindwa katika mambo yao wanayokusudia kuyafanya, chache kati ya hizo ni;
HISTORIA YA MTU...,katika maisha yapo mambo mengi mtu anapitia ambayo hayakuwa na matokeo mazuri kwake, inaweza kuwa ni mahusiano, biashara , hata katika masomo. Kupitia matokeo mabaya hayo, watu wengi hutengeneza imani ya kukosa uaminifu wa kurudia tena mambo hayo,hivyo mtu huyu anakuwa na hofu ya kushindwa kila anapokutana na mazingira yaliyo mfanya ashindwe.
KUTOJITAMBUA...,mtu asiye tambua mazingira anayostahili kupitia ili kufikia ndoto yake huwa anakuwa na hofu ya kushindwa, kwa nini? kwa sababu hana uhakika na alicho shika,kwa hiyo muda wote anakuwa anawaza kushindwa tu katika harakati zake.
MARAFIKI, marafiki wana nafasi kubwa ya kutengeneza hofu ya kushindwa kwa mtu, ukiwa na rafiki wengi ambao walijaribu na kushindwa. .....kibaya zaidi wakakata tamaa, ni rahisi wewe kutengeneza hofu ya kushindwa katika mambo ambayo rafiki zako walijaribu na kushindwa hadi kukata tamaa.
kuna uwezekano kuwa walio fanikiwa wengi waliacha rafiki zao wenye mtizamo wa kushindwa. ....hiyo iliwasaidia kupunguza hofu ya kushindwa kwenye mambo yao.
KUKOSA JUHUDI, hii ni sababu nyingine kubwa katika kutengeneza hofu ya kushindwa kwa mtu, kabla ya kufanya jambo flani, kuna hali inakuja ya kukukumbusha juu ya maandalizi uliyo fanya kuhusu jambo hilo, hapo ndipo HOFU huanzia kutokana na majibu utayojipa.
mfano, kabla ya kufanya mtihani lazima juhudi yako ikupe hali ya hofu au ushujaa wa kufanya mtihani huo.
NB. Huwezi kufanya maamuzi sahihi ukiwa katika hali ya hofu, maana watu wenye hofu mara nyingi hutafuta njia za ziada za kupunguza hofu zao. .......swali, Hizo njia za ziada zina matokeo gani kwenye kesho yako?
.Hofu ina tiba,fatilia somo hili hadi mwisho utajua tiba yake.
See you at the top
Scientist Saul kalivubha
(0652 134 707 )
Jifunze na uchukue hatua
ReplyDeleteThanks bro. Nimejifunza. Sina hofu tena.
ReplyDelete