KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu sehemu ya pili ya somo letu hili ambayo ni CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU. ...... Nakukumbusha tena, somo letu lina sehemu tatu.
1 .maana ya ndoto ya msimu.
2.chanzo cha mtu kuwa na ndoto ya msimu.
3. Madhara ya ndoto ya msimu.
2.CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU.
Hapa nataka tuangalie baadhi ya sababu zinazo fanya watu wasiwe na ndoto za kudumu za maisha yao, kinyume chake mazingira yanawafanya watengeze ndoto za msimu ambazo hupotea baada ya mazingira kubadilika. Zipo sababu nyingi ila chache kati ya hizo ni hizi hapa;
KUKOSA UBUNIFU. Ubunifu kwa maana ya haraka ni kutengeneza jambo la tofauti , mtu mbunifu huwa maisha yake yana asilimia nyingi ya juhudi zake. ...ila mtu ambaye siyo mbunifu maisha yake yamejengwa na mazingira ya nje.
Mtu asiye mbunifu tabia yake kubwa ni kukosa msimamo na alicho nacho , leo akiwa na ndoto hii kesho akikutana mazingira tofauti anatengeneza ndoto nyingine.
KUTOJITAMBUA. Kutojitambua ni tatizo kubwa sana, mtu asiye jitambua ni vigumu kutoa sababu za kwanini yupo pale alipo. .....kwa hiyo kila sehemu kwake ni sahihi maana sehemu sahihi haijui. mtu huyu hata ndoto ya msimu hana,bora uwe na ndoto ya msimu kuliko kutokuwa na ndoto kabisa.
Mtu asiye jitambua ni sawa na kipofu wa kuzaliwa anaye bishana na mwenye macho kuhusu uzuri wa mwezi.
UVIVU. Hii hali inawakumba wengi sana, mtu anaweza kuwa ana ndoto nzuri na ametengeneza mazingira ya kuifikia ndoto yake. . Ila akawa mvivu.
Mtu mvivu hupenda mambo rahisi, huyu ni mtu anaye tamani kufanya biashara isiyo na changamoto, ni mtu anayetamani awe kwenye mahusiano ya kutimiza kila a nachohitaji.
Mtu mvivu hujikuta ameacha ndoto yake na kuingia kwenye ndoto ya msimu kwa lengo la kutafuta urahisi.
KUKATA TAMAA. Kukata tamaa mara nyingi hutokana na imani ya muhusika , kuna mtu aliye kata tamaa (huyu ni hatari zaidi ) na kuna mtu ambaye yupo karibu na MARAFIKI walio kata tamaa, wote hawa wamejengwa na imani kuwa kufanikiwa ni bahati na sio juhudi. ......
Mtu wa aliye kata tamaa hawezi kuwa na ndoto ambayo ana mifano ya watu walioshindwa kupitia ndoto hiyo. ......hivyo mazingira humtengenezea ndoto ya msimu.
Sentensi inayochosha wengi ila ndiyo uhalisia ni hii ............................
" lazima kuna vitu uvipoteze ili uweze kuifikia ndoto ya kudumu "
let's meet on next session!
See you at the top.
scientist Saul kalivubha
(0652 134 707 )
No comments:
Post a Comment