Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni siku nyingine Mungu amefanya tukutane kwa lengo la kufundishana jinsi ya kufikia ndoto zetu
.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu hatua ya awali katika safari ya maisha yenye ushindi, bado kuna watu ambao wamejaribu kila namna ya kupiga hatua ili kufikia malengo yao ila badala ya kusogea mbele wao wanarudi nyuma. ........Kibaya zaidi watu hao wameshindwa kufanya tasmini ya matokeo yao ambayo hayaridhishi. ..
Tatizo nini? .....zinaweza kuwa zipo sababu nyingi ila sababu kubwa inaweza kuwa ni kosa la awali. ...ni lipi hilo? .....karibu tujifunze.
HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.
Unapoweka malengo ya safari yako lazima ujue mambo muhimu ya kukufanya upige hatua, bila hivyo unaweza kuwa na malengo mazuri yasiyo tembea, zipo njia nyingi ambazo watu tofauti tofauti wanaweza kuzieleza, ila kwa upande wangu taeleza njia tatu za kufanya uweze kupiga hatua, njia ambazo hutengeneza hatua ya awali na muhimu kwenye mafanikio yako. .....njia hizo ni hizi ;
1.Kuwa na marafiki sahihi.ni usemi wa kila siku kuwa mafanikio yako yapo kwa rafiki yako, ila wengi huwa hatujui hilo, bora utumie muda mrefu kuishi bila rafiki kuliko kuwa na rafiki asiyetambua umuhimu wa kusudi lako,Watu wengi wameshindwa kufika waendapo kwa kuwa karibu na marafiki hasi, ....lazima uwe na rafiki sahihi ili uweze kupiga hatua
.
2.Matumizi ya muda. Kwenye matumizi ya muda ndipo kuna mafanikio yote (tembelea Google search uandike muda wa ziada kalivubha blog ujifunze matumizi sahihi ya muda).Ni ngumu kupiga hatua yoyote ya mafanikio ikiwa bado una matumizi mabovu ya muda, kuna mambo ambayo lazima uyafanye ili yakupe kibali cha kuendelea, mambo hayo yanahitaji uwe na matumizi mazuri ya muda wako, hatua ya awali ni pamoja na kuwa na ratiba zinazofata muda wako vizuri.
3.Kutambua madhaifu yako. ..wanafalsafa wamewahi kuzungumza kuwa, .."mtu anaekushinda mafanikio kuna mambo anayofanya ambayo wewe hufanyi "..nini maana yake?.ni muhimu kufanya tasmini ya madhaifu ambayo yanaweza kuwa sababu ya kuzuia hatua zako, hiyo itakusaidia kujifunza namna ya kupiga hatua kwa kutumia njia tofauti tofauti zenye kuziba madhaifu yako, ..kujifunza kwa kupitia watu waliofanikiwa sio vibaya, lazima ujue nini ambacho wao wanakushinda .
Ni hatua chache sana za kukufanya upige hatua kwenye malengo yako, ila ni watu wachache sana wamekamilika katika hatua zote hizo tatu, ...fanya tasmini ya maisha yako.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652134707 )
Enter your comment...nimeipata hiii
ReplyDeletekeep on learning
ReplyDelete