Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha kila jumatano
jumatano ya wiki, nashukuru Mungu
kwa kuendelea kunisamamia....karibu.
tujifunze.
KUSUDILA SOMO.
Kabla ya kuendelea na kusudi la somo letu hili, nikukumbushe kuwa somo letu lina sehemu mbili. 1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.........
ili tuwe sambamba pitia somo la sehemu ya kwanza, tembelea Google search na kuandika kalivubha blog muda wa ziada au Tembelea page ya FIKIA NDOTO ZAKO Facebook.
Leo tunaendelea na sehemu yetu ya pili.
kumbuka kuwa muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja, huu ni ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi. .....karibu tuendelee.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.....
KUWA NA MAMBO MENGI;Kuwa na mambo ambayo yana positive effect (matokeo chanya)kwenye ndoto yako sio tatizo, tatizo ni pale mtu anapokosa utaratibu katika kupanga mambo yanayostahili kwanza yawe mbele. ..ukianza kutumia muda wako wa ziada leo kufanya mambo ya kesho hata kama ni mazuri, utakuwa unapoteza muda, ....lazima uwe na utaratibu katika kufanya mambo yako ili upate muda wa kutosha kufanya yanayostahili kwanza.
STAREHE; hapa ndipo kundi kubwa la watu lipo, maana wengi wanajua starehe lazima itumie pesa .........hata
ukitumia muda wa ziada kwa mambo yaliyo nje ya ndoto zako tunasema upo
kwenye starehe.
Hili tatizo wanalo watu wengi ambao hawana malengo, ambao hawaumii kutumia sentensi hiii. ."NIPO NAPOTEZA MUDA ".....kila muda unaopoteza lazima utaulipa , je utaulipaje? .....utaulipa kwa majuto.
KULIPA NAFASI JAMBO MOJA. ...hapa tuelewane vizuri , kuna watu ambao wapo addicted na jambo flani, muda wote wa ziada anakuwa busy na jambo hilo tu. .....sio tatizo ikiwa ndio maisha yako yapo kwenye jambo hilo, ..ila kama kuna mambo mengine yamebeba maisha yako ,utakuwa unapoteza muda kwa kufanya jambo hilo moja. ....toa nafasi kwa mambo mengine pia. ...
NB....Kila muda unaopoteza, lazima utaulipa kwa majuto yasiyo na tiba,wengi wetu huwa tunapuuzia usemi huo sababu madhara ya kulipa muda huo huwa yanachelewa. .ila
muda ukifika wa kulipa muda huo lazima mtu akumbuke mambo yaliyo poteza muda wake. .....
Tumia muda wako vizuri leo, ndoto zako zipo kwenye matumizi mazuri ya muda wako wa leo. .........
Unatumiaje muda wako wa ziada?
Karibu kwenye somo mpya muda kama huu. ....
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134707.
No comments:
Post a Comment