Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa hali yako ki afya ni nzuri, ila kwa wale ambao hawapo vizuri ki afya, Mungu asimamie harakati zote za kuirudisha afya yenu. Tupo kwenye kumalizia robo ya kwanza ya mwaka huu, nakusihi rejea kwenye daftari lako la malengo ujitasmini umefikia wapi.
Karibu kwenye somo letu la HOFU YA KUSHINDWA, nikukumbushe tu kuwa somo letu lina sehemu tatu ambazo ni. 1.CHANZO CHA HOFU. 2 . MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA. 3 . JINSI YA KUSHINDA HOFU YA KUSHINDWA.
KUSUDI LA SOMO.
Leo tunaangalia sehemu ya pili , MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA, nakusihi upitie somo la kwanza, unaweza fata link hii (http://kalivubha.blogspot.com/2017/02/hofu-ya-kushindwa-1.html?m=1) au ingia Google search,andika kalivubha blog hofu ya kushindwa, utapata somo hilo.
NB.Lengo la somo hili ni kujifunza jinsi HOFU inavyoweza kuzuia mafanikio yako, hapa ninazungumza hofu iliyo zidi kawaida.
2.MADHARA YA HOFU YA KUSHINDWA.
Hofu ina madhara mengi sana katika kufikia ndoto zetu, tuangalie jinsi HOFU inavyoweza kuathiri sehemu hizi tatu muhimu; MAAMUZI, UVUMILIVU NA KUJIAMIN I. .........ukiweza kufahamu madhara ya hofu katika sehemu hizo tatu, nafikiri utakuwa na uwezo wa kujipima ili ujitambue upo kundi lipi .
MAAMUZI, hii ni sehemu muhimu sana kwenye maisha, ili uweze kuchagua machache kati ya mengi lazima ufanye maamuzi.........ipo vipi kwa mtu mwenye hofu? ...Mtu mwenye hofu anakuwa hajakamilika, tayari akilini mwake anakuwa na jibu la kushindwa hata kabla ya kufanya maamuzi.....Hivyo mtu huyo anakuwa yupo tayari kuchagua jambo lolote lile ambalo ana amini litapunguza hofu yake.
Kumbuka tu ni watu wachache sana ambao wamewahi kufanya maamuzi sahihi wakiwa kwenye hali ya HOFU ya kushindwa.
KUJIAMINI...Nakumbuka mwalimu mmoja aliwahi kuniambia usemi huu. ."Ukitaka kumshinda adui yako, hakikisha unamfanya apunguze KUJIAMINI "
ipo vipi kwa mtu mwenye hofu ya kushindwa? .....Mtu akiwa na tatizo la HOFU YA KUSHINDWA, anakuwa hajiamini, maana tayari anakuwa ameshindwa AKILINI mwake hata kabla ya kujaribu. ...madhara ya kutojiamini ni kufanya mambo hayaendani na thamani yako. .....
Watu wasio jiamini siku zote huwa hawapati wanayostahili, ila hupata yale wanayo amini yanaweza punguza hofu yao.
UVUMILIVU,mtu mvumilivu mara nyingi lazima awe ana jiamini kwa kiasi kinachostahili na pia lazima awe mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yasiyo bebwa na Imani ya HOFU. ........
Mtu mwenye hofu ya kushindwa ni vigumu kuwa mvumilivu, huwezi kuwa mvumilivu kwenye jambo ambalo kwa imani yako tayari unajua utashindwa......je una weza kufanikiwa kwa hali hiyo? ......hapana, maana kwenye maisha kuna malengo ambayo yanahitaji muda mrefu ili yaweze kukamilika, yanahitaji uvumilivu wa kutosha.
Hofu ya kushindwa ni hatari sana, hakikisha unajua tiba yake mapema.....Watu wengi wameacha njia zao ndefu ila zenye mafanikio kwa kufata njia fupi zisizo na mafanikio, wamefanya hivyo kwa kuwa WANA HOFU YA KUSHINDWA. .....wamejiona hawawezi .
Kitabu cha RAFIKI kipo kwenye maandalizi, kitakusaidia kujua kujua siri za mafanikio kupitia rafiki.
Let's meet on the next week , on the same day.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652 134 707 )
No comments:
Post a Comment