Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha kwa lengo la kufikia ndoto zetu. ...Leo tuna somo mpya la madhara ya kutojiamini katika kufikia ndoto zetu. ..karibu.
kusudi la somo.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza jinsi gani hali ya kutojiamini inaweza kuzuia ndoto zako za mafanikio. .... Somo letu limelenga hasa sehemu ya .Maana ya kutojiamini. Ukielewa vizuri maana ya kutojiamini,utajitambua upo upande upi,na mafanikio kwako yapo kwa asilimia ngapi,nimejitahidi kufafanua maana ya kutojiamini na uhusiano wake kwenye mafanikio.....karibu.
MAANA YA KUTOJIAMINI.
Kunarafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa ukoo wao sio wa biashara hivyo hata akianzisha biashara hatafanikiwa. .je ni sahihi?
Mtu mwingine alisema .." Hata asome vipi hawezi kufaulu kwa ufaulu wa kiwango cha daraja A (grade A)"...umewahi kujiona ukiwa kwenye hali ya kushindwa? .....Nini maana ya KUTOJIAMINI..?
Kutojiamini ni hali ya mtu kujiona mwenye mapungufu, hali hiyo humfanya mtu huyo kuona watu wengine wana uwezo wa juu kuliko yeye. ........Nini maana yake? Tujaribu kuangalia ufafanuzi wa hali ya kutojiamini kupitia maelezohaya hapa chinI. ..
1.Wanasikolojia wana zungumzia hali ya kutojiamini kama vita anayokuwa nayo mtu dhidi ya watu wengine ambaoanaamini kuwa wana uwezo dhidi ya kile anachofanya /anachotaka kukifanya. ...Upo katika hali hiyo?
Kuwa katika vita na watu wasiotambua kama unapambana nao ndio chanzo cha mtu kupunguza kujiaminI. ..maana hali hiyo humfanya mtu ajione yupo upande wa kushindwa muda wote.
2. kutojiamini inaweza kuwa pia hali ambayo mtu anajiona mwenye kuhitaji sifa flani ili akubalike kwenye jamii. ....Hali hii humfanya mtu huyo kujiongezea sifa ya ziada ili akidhi hisia zake, ...hapa ndipo watu wasiojamini huanza kutumia nguvu kubwa kupamba sifa kivuli ili tu aondokane na hali ya kujiona mwenye mapungufu. ..je unaweza kuitunza sifa uliyojiongezea muda wote wa maisha?
3.Kutojiamini inaweza pia kuwa hali ya mtu kuamini zaidi matokeo ambayo yametokana na Kazi za watu wengine....kwa hiyo muda wote mtu asiyejiamini...anakuwa anaishi maisha ya watu wengine ambao mtu huyo anakuwa amewapa uwezo wa ushindi. .. hali hii humfanya mtu asiyejiamini asijaribu jambo lolote lile kwa kutumia mawazo yako. ....je unaweza kufikia ndoto zako kwa kuishi maisha yakutegemea juhudi za watu wengine?
.
Kutojiamini ni tatizo ambalo linatajwa kama chanzo kikubwa cha wivu ambao umepelekea mahusiano mengi ya mapenzi kufa,kama sio mapenzi kufa basi itamfanya mtu asiye jiamini kuwa mtumwa wa mapenzi.
Kutojiamini kwa ujumla ni hali ambayo ukiwa inayo itakufanya uwe unaishi maisha ya watu wengine,maana utakuwa unajiona mwenye mapungufu muda wote,.......unajua tatizo la kujiona mwenye mapungufu muda wote?..Tatizo lake kubwa ni kushindwa kujaribu,mana kulingana na mapungufu unayohisi ni mengi kwako ,utajenga imani ya kukosea kwa kila jambo linalokuhitaji kujaribu,na kumbuka tu ni ngumu kufanikiwa kama una hofu ya kujaribu.
....
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134707.
Enter your comment...asante kwa somo zuri barikiwa
ReplyDelete