Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Thursday, 18 May 2017
SIRI YA PILI YA URAFIKI
karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha. ...nashukuru Mungu kwa neema yake kwangu. .........karibu tujifunze.
Kusudi la somo.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza siri ya pili ya urafiki. ....Nimeona vyema kufundisha somo hili kwa sababu najua urafiki una sehemu kubwa sana kwenye mafanikio yetu. ....karibu.
SIRI YA PILI YA URAFIKI.
Tuangalie siri ya pili ya urafiki. ..unaweza kujifunza siri ya kwanza ya urafiki kwa kuandika kalivubha blog siri ya kwanza ya urafiki. ....kisha ndio uendelee na mimi kwenye somo hili.
(siri yakwanzayaurafiki )...
Siri ya pili ya urafiki ni hii USIFANYE URAFIKI KWA MAJARABIO...........
Moja ya sababu inayofanya urafiki upungue thamani ni kubadilika kwa mazingira ambayo yalitumika kutengeneza urafiki. ...kwa nini mazingira yabadilike? ......kuna watu ambao wana tabia ya kufanya majarabio ya urafiki. ...wengi wao hufanya hivyo ili kuangalia kama urafiki huo una weza kutimiza mahitaji yake. .....
Urafiki wa aina yoyote ile una changamoto zake. ...hivyo mtu anayeingia kwenye urafiki kwa majarabio hawezi kuvumilia changamoto. .....mara nyingi watu wanaingia kwenye urafiki kwa majarabio wana sifa kuu tatu.
1.Sio wavumilivu wa changamoto.
2.muda wote wanawaza kubadili marafiki.
3.Wanatumia nguvu kubwa kuanzisha urafiki. ....hufanya hivi kwa sababu wanakuwa wanataka waone kama watatimiza malengo yao ..kama hapana basi wabadili marafiki ...........
Jiandae kupata kitabu cha SIRI ZA URAFIKI .
See You At The Top.
Saul kalivubha.
(065123707 )
Labels:
URAFIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment