Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo na jinsi ya kufikia ndoto zetu....nina imani kwa namna yoyote ile ,unaendelea vyema.....mshukuru Mungu kwa hali hiyo uliyonayo.ipo sababu ya wewe kuwa kwenye hali hiyo.......karibu sana.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu mapato na matumizi...hili ni somo pana sana na karibia kila mtu ana nidhamu yake kwenye elimu hii....ila nina kitu pia cha kukuongezea kwenye ufahamu wako.......ila hapa nataka wale wenye mawazo ya kutaka kutumia kidogo walichonacho ili waje wawekeze.....karibu sana.
MAPATO.
Mapato ni kile kiasi unachoingiza,unaweza kukigawa kwa mwezi au kwa siku ...au hata kwa mwaka,je unaingiza shilling ngapi?...hapa ndipo kuna shida sasa.
Usidharau kiasi unachoingiza,hata kiwe kidogo namna gani,kiandike kwenye daftari,na kwa ushauri wangu ni vizuri ugawe kipato chako kwa sikiu.....mfano kama unaingiza elfu 30 kwa mwezi ,basi kwa siku utakuwa unaingiza 1000 kwa siku....nini umuhimu wake?.....tutajifunza kwenye matumizi.
Kama unaingiza chochote ,lazima uwe na uwezo wa kutoa chochote pia,hivyo heshimu sana unachokiingiza,na hakikisha unakuwa mbunifu kwa kidogo hicho unachokipata ili ukitumie kuongeza vyanzo vya mapato.
Ili uwe na uwezo wa kuongeza chanzo cha mapato ,lazima uwe vizuri kwenye kutambua unachoingiza ili ujibane kwenye matumizi kwa lengo la kubaki na kidogo utakachozalisha.
MATUMIZI
Hapa ndipo kuna matatizo sasa,.....nilisema ugawe mapato yako kwa siku ili ujipime matumizi yako kwa siku yapo juu/chini ya unachoingiza kwa siku?.......je kiasi kinachozidi unakipeleka wapi?....
- Tengeneza bajeti ya siku moja,kisha tafuta jumla kwa mwezi unatumia kiasi gani,,,,ila jitahidi unachotumia kwa siku kisizidi kile unachoingiza .
- Kwenye maisha kuna dharura ,kutenga kiasi cha dharura sio vibaya,ila lazima uangalizie na dharura ambazo unaweza kuleta matokeo,nyingine ziache zipite.
- Namba moja nafikiri inakufundisha kutumia kwa nidhamu,usitumie kilicho nje ya uwezo wako.....je bajeti yako inaruhusu ubaki na chochote?
- Tunashariwa kuweka akiba kabla ya matumizi ,ila ni vizuri ukafahamu kwanza mapato yako yakoje kisha ndio uanze kuweka akiba.
- Akiba ipe thamani ya kipato kingine,akiba ndio mtaji wako sasa,kama unatafuta mtaji kila siku na huna nidhamu ya kuweka akiba utasumbuka sana.....kama una akiba basi tayari una mtaji mmojawapo.....
NB. Kuwekeza au biashara ni elimu nyingine tofauti na elimu ya kuweka akiba,ingawa unatakiwa uweke akiba ukiwa unafahamu nini unatakiwa kufanya kesho......!!!
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa label ya FIKIA NDOTO ZAKO.
0652 134707
No comments:
Post a Comment