UNATAFUTA MAISHA ? HAYA HAPA.
Karibu ndugu msomaji kwenye blogu yako hii pendwa ya FIKIA NDOTO ZAKO ambapo tunajifunza mengi sana kuhusu maisha ya kila siku.Tupo kwenye hali ya taharuki nakusihi sana ufaute ushauri wa watalaamu na kwa ushauri wangu wa nyongeza katika uchumi kwa sasa kutunza pesa iwe lengo la kwanza kwa sababu mfumo umeyumba kwa janga hili la Corona hivyo inahitaji utulivu sana kabla ya kuwekeza pesa yako vinginevyo utaisaidia Corona badala ya kujisaidia wewe, tuwe watulivu na hali hii itapita.
Tuachane na stori twende moja kwa moja kwenye somo letu maalumu kwa leo kabla ya vyote nikuulize na wewe upo kundi la watu wasemao " NINATAFUTA MAISHA" umewahi kuyapata? .
Kwa mujibu wa kamusi mbali mbali MAISHA ni hali ya wewe kuwa mzima tayari hayo ni maisha hivyo mtu ambaye ni mfu huyo hana maisha Duniani pengine huko aendako ( kuna imani nyingi kuhusu maisha baada ya kifo sitaki twende huko) .Tayari maisha unayo hivyo jivunie kuwa na maisha.
UHAI ni kitu ambacho kinafanya wewe uwe na maisha mfano chakula ni uhai, maji ni uhai nk kwa sababu ukivikosa unaweza kupoteza maisha ( kufa).
KUISHI ni namna ya kutetea maisha yako hapa ndipo kiini cha somo, maisha unayo lakini unafanya nini ili UISHI?
Ili uishi kuna mahitaji muhimu ya kwanza ambayo ni CHAKULA na MALAZI ( ule upate na pakulala) kwa sababu ukikosa chakula utakufa, ukilala nje uanaweza shambuliwa na wanyama wakali ukafa .
Mtu akiwa na Nyumba nzuri, gari zuri na kula vyakula vizuri ki kawaida hiyo ni hali ya kawaida na sio mafanikio ya kujitamba kwa sababu ni kawaida ule na upate pakulala ili kutetea uhai wako mambo ya gari ni ziada tu lakini gari halitetei uhai wako. Hatua hii ya kula na kuishi ni hatua ambayo kama umeifikia kujipatia mahitaji hayo tayari unatetea uhai wako ( magonjwa , ajari nk ni changamoto tu katika kuwinda uhai wako).
HATUA YA PILI NA KUBWA. Kujitofautisha kutoka kwenye kutetea uhai wako tu mpaka kutetea maisha ya wengine hii ni hatua kubwa zaidi ambayo tunaiweka kwenye SAIKOLOJIA na FALSAFA yaani kujitambua kuwa kuna zaidi ya kula na kulala na starehe. Hapa ni kutafuta wewe halisi ni nani, je ni mwimbaji? Mchezaji mpira nk.
WEWE HALISI NI NANI? Watu wanaofanikiwa kujitambua hivyo huwa wanaonekana wa tofauti sana kwenye jamii na kile wanachokifanya hakitetei uhai wao tu bali kuna wengine wanafaidika pia mfano tuseme msanii Diamond kuimba kwake kuna mfanya atetee uhai wake lakini pia kuna ambao wameajiriwa naye lakini pia kuna watu ambao hisia zao zinapona kwa kusikia tu nyimbo zake.
UNATAFUTA MAISHA? Maisha unayo ila unatafuta namna ya kutetea uhai wako lakini namna nzuri usiishie kwenye kula, kulala na starehe ila tafuta wewe halisi ni nani? Tafuta kipaji chako na ukiishi. Kuishi kipaji chako ni nyongeza kubwa sana ya KUTETEA UHAI WAKO NA WENGINE. Kipaji sio kuimba tu na kucheza mpira au kuandika hapana hata ubunifu nao ni kipaji,kuchora, kushona nk yaani ni vile tu unaishi kile ulichoombwa kufanya na njia rahisi ya kukijua ni msukumo wako wa ndani unajihisi furaha yako ipo ukiwa unafanya nini?
Makala hii imeandikwa na
Mwanasayansi Saul Kalivubha.
fikiandotozako.
Bila kusahau vitabu vya siri za urafiki na thamani ya changamoto vinapatikana kwa bei ya ofa kwa Tsh 6000 tu vyote, ni soft copy ( nakala tete).
0652134707/ 0756388688.
Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Thursday, 30 April 2020
Friday, 21 February 2020
USIYOJUA KUMUHUSU SAUL KALIVUBHA
USIYOJUA KUMUHUSU SAUL KALIVUBHA.
Karibu sana ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako pendwa hii ya fikiandotozako ambayo inakupa mafunzo mbali mbali ya maisha na bila kusahau kutufuatilia katika majukwaa yetu ya Facebook, you tube na Instagram kwa jina moja tu la FIKIANDOTOZAKO, Karibu sana.
Leo ni somo la tofauti sana kama zawadi kwako ikiwa ni sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwangu nikiwa natimiza umri wa miaka 28 , ulifikiri nina umri gani kabla?.Nawashukuru sana wazazi wangu na nyinyi wapenzi wasomaji kwa kuwa nami karibu katika kujifunza mambo mbali mbali ya maisha.
SAUL KALIVUBHA ni nani? na itakusaidia nini kumfahamu? twende sambamba mpaka mwisho wa darasa kuna kitu utajifunza.
1.Ni mzawa wa Kigoma katika familia yenye uchumi wa kawaida sana (uchumi wa daraja la tatu) yaani uchumi wa mwisho kutokea uchumi wa juu, uchumi wa kati na uchumi wa mwisho, hivyo Saul Kalivubha katokea familia yenye uchumi wa mwisho.
2.Ni mtu wa kundi la watu wasiowaongeaji sana na wenye usiri mkubwa sana (melancholic) , hili ni kundi la watu ambao muda mwingi hupenda kukaa peke yao kuliko kuwa na makundi, faida ya kundi hilo mojawapo ni kuwa wabunifu na wenye kufikiria sana lakini pia hasara moja wapo ya watu wa kundi hilo ni kuumia sana kwa sababu hukaa na mambo mengi moyoni bila kushirikisha wengine (marafiki).
3.Kasoma katika mazingira magumu kuanzia shule ya msingi mpaka shule ya upili, mazingira magumu yalimfanya atoke shule ya vipaji maalumu ya Musoma wavulana sekondari ya ufundi na kurudi shule ya kata ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne, hilo halikumkatisha tamaa zaidi ya kujitoa zaidi akiwa shule hiyo ya kata na kupata matokea mazuri ya kuendelea kidato cha tano na sita .
4.Maisha ya kidato cha tano na sita katika shule ya bwiru wavulana pia hayakuwa rahisi ki uchumi kwani ilimlazimu awe anasoma huku akitafuta pesa za kulipia michango midogo midogo ya shuleni.
5.Ugumu wa maisha ya shule hamkufanya akate tamaa hivyo alipambana na vikwazo na hatimaye akapata ufaulu wa kumfanya aendelee na masomo ya chuo kikuu japo hakuweza kwenda mwaka huo aliomaliza shule (2014) na akaenda chuo mwaka uliofata (2015).
5.Mwaka 2015 aliweza kujiunga na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi (Muhimbili) kwa kozi ya Mwanasayansi tiba wa maabara za binadamu (Medical laboratory science) .Maisha ya chuo hayakuwa magumu sana ki uchumi kulinganisha na hatua za nyuma hivyo kidogo unafuu ulionekaa wa maisha.
6.Maisha ya chuo yana changamoto nyingi sana lakini pia ni jukwaa zuri sana la kujifunza maisha kwa upana zaidi kwani unakutana na watu wengi mnaopishana mitizamo hivyo kupitia kupishana huko mtu unajifunza mambo mengi sana.
7.Safari ya uandishi ulianza rasmi akiwa chuoni mwaka wa pili ni safari isiyo rahisi lakini ilikuwa ndio mahala pake kwani kukutana na watu wengi wenye upeo tofauti ilimfanya ajifunze zaidi na kuanzisha jukwaa la FIKIANDOTOZAKO ambalo hadi sasa linafikia watu wengi nchini na nje ya nje katika kuwafungua vijana namna na kuwapa moyo wa kuendelea mbele.
8.Saul Kalivubha sasa sio mwanafunzi tena tayari ni muhimu haijalishi changamoto zipi zilijitokeza lakini safari iliisha salama.Vikwazo vya maisha ni vingi sana lakini hupaswi kusema nimeshindwa kwa sababu hakuna safari rahisi japo ugumu unatofautiana kulingana na aina ya safari uliyonayo.
9.kuna muda unahisi wewe utabaki hapo hapo ulipo kulingana na vikwazo vinavyofanya usione njia mbele, safari inakuwa na giza na Dunia hata siku moja haitambui shida zako hivyo haiwezi kukuonea huruma. Muhimu ni kutoa imani ya kubaki ulipo kwa sababu maisha ya leo yatakufunza funzo la kuishi kesho hivyo kesho utakuwa mtu mpya kabisa ni uvumilivu tu.
10.Uvumilivu sio kazi rahisi hata kidogo ni kazi ngumu sana kwa sababu silaha pekee ya uvumilivu ni IMANI , unavumilia ukiwa na tumaini kuwa hali hiyo itapita na kweli itapita kwa sababu njia unazohisi zitakupa mafanikio ya haraka zina gharama iliyo nje ya uwezo wako zitakufanya ufilisike na bado hayo mafanikio usiyaone , tembea mwendo wako kwa kufuata nchi yako (Mungu aliyokuandalia).
Makala hii imeandikwa na.
#Mwanasayansi Saul Kalivubha
#0652 134707

Thursday, 19 December 2019
RAFIKI YAKO NI NANI?
Habari za kwako ndugu mpenzi msomaji wa blogu yetu pendwa ya FIKIANDOTOZAKO na hongera sana kwa majukumu ya kila siku na pole kwa changamoto za kila siku pia, karibu kwenye somo maalumu la kufunga na kufungua mwaka liitwalo RAFIKI YAKO NI NANI?.
Ni kawaida yangu kila mwaka kufanya tathmini ya malengo yango na kisha kutafuta sababu za kwa nini nimeshindwa au nimefanikiwa na hapo huwa nakuta sababu nyingi sana nyuma yake lakini sababu moja tu huwa ninaipa uzito nayo ni RAFIKI ALIYE NYUMA YANGU NI YUPI? napenda sana kukupa changamoto ya kujitafakari na wewe uchunguze nyuma ya kushindwa/kufanikiwa kwako yupo RAFIKI WA AINA GANI?
Ni kawaida ya watu wengi kujiwekea malengo kila mwanzo wa mwaka mimi pia ni mmoja wao na malengo hayo yanakuwa na uhusiano na maono(vision)yako mfano una maono ya kuwa na kampuni kubwa ya kusaidia vijana baada ya miaka kumi ijayo hivyo ni jukumu lako la kuishi maandalizi kila siku kila mwaka ujione kusogea kwenye hayo maono yako , sasa angalia maono yako umeyasogelea au umesogea nyuma kabisa? Kwa nini?
RAFIKI YAKO NI NANI? Siku nzima ni ngumu kuisha bila kuwasiliana na rafiki yako wa karibu na hiyo ndio kawaida ya URAFIKI yaani kunakuwa na hisia za kutaka ujione karibu na rafiki yako sasa je MNAONGEA nini? mnaongea kwa mazoea tu salamu , kukumbushana ya nyuma na kuambiana move zipi nzuri au viwanja vipi vizuri vya starehe kisha usiku mnatakiana usiku mwema, huyo ndio rafiki yako? rafiki anakutafuta akiwa na shida tu au ili URAFIKI uendelee wewe ndio unatakiwa kila siku kuanzisha mazungumzo wewe na kama hiyo haitoshi URAFIKI umejengwa na vitu yaani mmoja anatumia nguvu ya ziada kuufanya URAFIKI uendelee, nikupe pole sana kama upo kwenye URAFIKI wa aina hii kwa sababu hakuna namna unaweza kufikia malengo yako ukiwa kwenye hali hiyo ya marafiki sana utaishi tu maisha ya kawaida huku ukiamini ndio maisha yalivyo.
CHAGUA MARAFIKI WA KUAMBATANA NAO.
Unataka kwenda wapi?
Marafiki wazuri ni wale ambao ukiwa nao unajiona mpya kwenye malengo yako yaani mkiwa wote wanakupa namna utakavyofika na sio wanakuonyesha namna utakavyoshindwa kwa kila malengo yako , usiwe na marafiki ambao watakufanya mtumwa kwao badala ya wote kwa pamoja kusaidiana jinsi ya kufika wao wanajenga mazingira ya wewe kuwa mtumwa kwao.
Rafiki yako ni nani?
Soft copy ya kitabu cha siri za URAFIKI kinapatikana kwa Tsh 4000 tu .
Saul Kalivubha.
Mwanasayansi.
FIKIANDOTOZAKO.
0652 134707

Thursday, 17 October 2019
NGUZO ZA MAAMUZI SAHIHI,JIFUNZE.
Na Mwanasayansi Saul Kalivubha.
Habari ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako hii pendwa na karibu tena katika safu hii ambayo tunajifunza mambo chanya kwa ajili ya kuitafuta hatua mpya zaidi ,karibu tujifunze.
Maamuzi sio neno geni hata kidogo na kila siku lazima kila mtu afanye maamuzi mara nyingi sana japo idadi ya maamuzi haziwezi kuwa sawa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, maamuzi ni machaguzi hivyo huwezi kuamua ukiwa na jambo moja mkononi lazima uwe na mambo mawili au zaidi mkononi ndipo ufanye maamuzi ya kubaki na jambo moja kati ya mengi,je una uhakika gani kama maamuzi unayoenda kuyafanya ni sahihi? Kuna nini nyuma ya maamuzi yako? .
Tumesikia watu wengi sana wakijilaumu kwa maamuzi yao ya jana na kujutia kana kwamba wangalijua mapema wasingefanya maamuzi yale hii ni wazi kuwa maamuzi yao sio sahihi japo kwa muda ule wanaamua walijiona kuwa wapo sahihi.
Tuangazie kidogo juu ya nini kinafanya watu wafanye maamuzi na kwa nini majuto yanafuata baada ya maamuzi.
Kwa nini tunafanya maamuzi? Tunafanya maamuzi kwa sababu mambo tunayokutana nayo hatuwezi kwenda nayo yote hivyo lazima tuamue ili kuchagua machache yanayotufaa na kuacha yasiyo tufaa, maamuzi yoyote yale lazima kuna chaguo moja ulilipenda ndio maana ukaamua kulichagua chaguo hilo.
Kwa nini ulizwe na chaguo lako mwenyewe?.Nyuma ya maamuzi yoyote yale kuna ufahamu,hisia,msukumo wa watu na muda.Hivi vitu vinne ndio hasa vinaoongoza maamuzi yetu hivyo unapoona unajutia maamuzi yako lazima kuna moja kati ya ufahamu wako,msukumo wa watu,hisia au muda lilikuvuruga.
MUDA, tunapokuja suala la muda tunaangazia sana kuchelewa yaani mtu anapoingiwa na hofu ya kuchelewa huwa anajikuta akifanya maamuzi bila kuyafikiria maamuzi yake kwa utulivu kwani lengo lake kubwa inakuwa ni kutaka tu awahi hivyo atatumia vigezo vichache katika kufanya machaguzi.
Mara nyingi maamuzi ambayo yanafanywa kwa kukimbizana na muda huwa ni sahihi kwa muda ule mtu anapoyafanya lakini baadaye anakuja kuyajutia maamuzi yake.Usikubali kufanya maamuzi na hisia za kuchelewa utakosea hivyo ni vizuri utafute utulivu ndio kisha ufanye maamuzi.
Msukumo wa watu, hizi tunaziita kelele za nje zinazokusukuma ufanye jambo fulani , sio kwamba hutapswi kutosikiliza kelele za nje la hasha ila unachopaswa ni kutofanya maamuzi kwa sababu umepigiwa kelele,kelele za nje ni kama upepo uvumao ambapo ukikukuta huna msimamo utayumba na kujikuta unaenda hata usipopotaka , kwenye mahusiano na biashara suala la kupigiwa kelele huwa lipo huu sana na wengi waliofanya maamuzi kwa kusukumwa na kelele walipotea, jitafute wewe ni nani na unataka nini ndipo ufanye maamuzi.
HISIA ,Kila mtu ana msukumo wa hisia ndani yake kwani hisia ni sehemu ya ulinzi pale tu zinapotumiwa vizuri, zipo hisia za aina nyingi kama vile hisia za hasira,hisia za kupenda,hisia za huzuni,hisia za hofu nakadhalika, sasa hisia zikiwa juu huwa zinaficha negative side effects (madhara hasi) na kukuaminisha kuwa utafurahia matokeo ya maamuzi unayotumwa kufanya na hisia, mtu mwenye hasira akifanya maamuzi huwa anajiona mwenye furaha kwa muda kisha hasira ikimuachia tu anabaki na majuto , hivyo unatakiwa kufanya maamuzi bila kusukumwa na hisia.
UFAHAMU, ufahamu wa mtu kuhusu jambo fulani ndio unamuongoza kufanya maamuzi yanayohusu jambo hilo ,kwa mfano wanafunzi wanaochagua kozi za kusoma kwa kutumia ufahamu wa haraka na baadaye wanakuja kuona kuwa wamekosea baada ya ufahamu wao kuongezeka, vivyo hata katika mahusiano,biashara na mengineyo watu wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kutumia ufahamu mdogo ,hivyo inashauriwa kutafuta maarifa ya kutosha kabla ya maamuzi fulani .
Sunday, 14 July 2019
MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.
Habari ndugu na mfuatiliaji wa makala zetu za blogu yako pendwa ya FIKIA NDOTO ZAKO,ikiwa imepita muda wa kutosha bila kukuandikia makala katika blogu yetu hii ni kwa sababu tu ya uboreshaji ambao ulikuwa ukiendelea kwa lengo la kukupatia wewe msomaji na mwanafunzi maarifa yaliyo bora,karibu .
Somo letu la leo ni rahisi kama utalipa muda wa kutosha kalitafakari na ni somo gumu kama utapita juu juu, hivyo inahitaji utulivu wa hali ya juu sana.
Ufahamu ni moja ya eneo muhimu sana ambalo ndio linakutofautisha wewe na mimi ,wewe na rafiki yako ,wewe na mnyama kama vile sungura n.k,kumbe ufahamu ndio muongozo wa kwanza wa maamuzi yetu na ndio gereza limelofunga hatua zetu.
Ufahamu unaanzia mbali sana pindi mtoto anapozaliwa hadipale ambapo mazingira yatamuhitaji atafute mwenyewe (kujitegemea) ,hadi kufikia umri wa miaka 9 mpaka 10 ufahamu wa mtoto unakuwa ukiamini kwa 100% muongozo wa mzazi /mlezi wake ndio maana mtoto wa umri huo anakuwa haamini kama kuna mtu zaidi ya baba /mama yake ,hata akutane na kitu cha kutisha namna gani ambapo hata kina nguvu zaidi ya mzazi wake bado atakitishia kitu hicho kwa kumtaja baba yake au mama yake akiamini hicho kitu kitaogopa na kumuacha,yote hiyo ni kwa sababu ufahamu wake ndio unamtuma hivyo ,je ufahamu wake ni sahihi?
Inawezekana ukawa ;
1.Unaabudu katika dini/dhehebu fulani kwa sababu unaamini uliowakuta wakifanya hivyo hawawezi kukosea kuwa katika sehemu hiyo wanayoabudu.
2.Ulichagua kozi fulani kwa sababu waliokushauri uliwapa thamani ya juu kuwa hawawezi kukosea katika machaguzi.
3.Kwa sababu unaona watu wanafanya ndio maana ufahamu wako unakutuma kuwa hilo jambo ni sahihi n.k
Je unawezaje kuhakikisha kuwa ufahamu wako ni sahihi?
Tukiachana na kupima ufahamu ulinao kuhusu dini/imani/kanisa/msikiti ambapo ni somo ndefu na linalohitaji utulivu wa juu zaidi, tuje katika mbinu za pamoja za kupima ufahamu ulionao kwa ujumla ,kwanza kabla ya mbinu hizo tutambue ya kwamba ufahamu kwa asilimia nyingi unatokana na mazingira yanayokuzunguruka kama vile marafiki na wazazi/walezi n.k, pia ufahamu unategemea na umri.
Kadri mazingira yanavyobadilika na umri unavyosogea ndipo unazidi kuona kuwa kuna mambo zaidi ya vile ulivyokuwa ukifahamu na utagundua kuwa ulikuwa unafanya makosa pasipo kufahamu kwa sababu ufahamu wako ndipo ulipoishia pale,kwani maamuzi yetu ni ,matokeo ya ufahamu wetu ulivyo.
MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.
1.Kwanza jitambue wewe ninani,sio jina lako wala wapi unaishi ,jitambue kwa nini ulizaliwa? utapata sababu ambayo ndio kusudi la wewe kuzaliwa,sababu ya kuzaliwa kwako unaweza pia kuangalia kipi unaona hakiendi sawa yaani kuna namna unasukumwa kutaka kuweka mfumo sawa,hapo kuna kusudi lako na kipaji chako ,ukishajifahamu wewe ni nani tayari utaanza kutafuta ufahamu wa kutosha kujihusu wewe na safari yako.
2.Makosa yetu,kupitia makosa yetu ni njia nzuri sana ya kupima ufahamu wetu,mfano umetumia ufahamu wako kufungua simu ukashindwa ni wazi kuwa ufahamu wako bado, kuna zaidi ya unavyofahamu,unapoingia kwenye makosa kaa chini ujitafakari ni lazima tu kuna jambo hulijui ndio maana ukakosea hivyo litafute .
3.Kaa chini uchunguze kwa nini unaamini hivyo? ni kwa sababu uliambiwa hivyo na watu au ni kwa sababu umezaliwa na kukuta watu wakifanya hivyo,kwa mfano wengi tumekuwa tukiwa na ufahamu kuwa shule ndio chanzo cha utajiri kwa sababu tuliambiwa hivyo ,kila siku tunatafuta ajira tukiamini kuwa tukipata tu tutaaga umaskini,lakini ambao tayari wamevipata hivyo ndio wengi wao wanakuja kufahamu ya kuwa kuna zaidi ya shule na ajira ili mtu kuwa tajiri.Hapa tunarudi kwenye namba moja ya kuwa ukishajifahamu wewe ni nani utaanza kutafuta mazingira ya kukupeleka kwako na hapo ndipo utaanza kuachana na ufahamu ambao chanzo chake ni kuaminishwa na watu,watu walikuaminisha vile kwa sababu ya ufahamu wao wa muda ule.
Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha,mwanasayansi na mwalimu na mmiliki wa fikia ndoto zako label.
0652 134707.

Tuesday, 9 April 2019
HILI NDIO GEREZA LA HATUA ZAKO
Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako.Ni tumaini langu kuwa wewe ni mzima wa afya na unaendelea kupambana katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ili zikupe ushindi wa kuliishi kusudi lako,karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Somo hili linakusudia kuwasaidia vijana ambao wana tatizo la kutopiga hatua ilihali kila siku wapo kazini na wanapata chochote lakini hawapigi hatua mbele.Katika somo hili ,vijana lengwa ni wale ambao wana maono ya kuifikia hatua fulani lakini siku zasogea na hata dalili za kufika huko hazipo.Wewe pia una tatizo hilo? kama ndivyo ,endelea hadi mwisho utajua gereza lako ni lipi.
KWANINI UNAFANYA HICHO UNACHOKIFANYA LEO?
Hili swali linahitaji sababu ,je umewahi kujiuliza swali kama hilo? na ulipata sababu zipi? .Inawezekana ukawa na majibu yako mengi sana ya kwanini upo unafanya hiyo kazi,wengine watasema ni kwa sababu ndio walichokisomea,wengine watasema ni kwa sababu hawakwenda shule ndo mana wanafanya shughuli hiyo ,n.k.Majibu yatakuwa mengi sana.Mimi kama ningeulizwa swali kama hilo ,jibu langu lingekuwa rahisi sana tu,ningesema sababu inayofanya nifanye hiki nikifanyacho leo ni kwasabu kinanipeleka kwenye kusudi la kuumbwa kwangu. Hivi unafahamu gereza limelofunga hatua zako ni sababu zilipo nyuma ya hicho unachokifanya?
GEREZA LA HATUA YAKO MPYA NI HIYO SABABU YAKO.
Ni ngumu kupiga hatua mpya kama huna sababu zinazokusuma ufanye hivyo ,na sababu ambazo zitakufanya upige hatua mpya zinategemea sana na wewe unajitambua vipi,hapa ninamaamisha kwamba ni vizuri kwanza ujitambue wewe ni nani na wapi unatakiwa kwenda kulingana na kusudi lililowekwa ndani yako,kisha sasa ndio uangalie hicho unachokifanya ,je kinahusiana vipi na uelekeo wako?
Kama kila siku sababu zako ni kutaka ufanye kazi kwa bidii na kwa weledi,sawa ni sababu nzuri lakini je hicho unachotaka kukifanya kwa juhudi na weledi kinahusiana vipi na kusudi la kuumbwa kwako? kama hakuna mahusiano ndipo pale ambapo utaendelea kuwa na juhudi kwa kufanya jambo fulani lakini hufiki kule kwako ,mfano kama wewe uliumbwa uwe mchoraji ,na sasa upo katika kitengo cha afya kama Daktari,je unaunganisha vipi huo udakitari na kipaji chako cha uchoraji? Hapo unaweza kuiwa na sababu nyingi za kukufanya huo udakitari wako vizuri lakini ukawa huna sababu hata moja ya kutaka ufanye huo udakitari wako uendeleze kiapaji chako ,kwa namna hiyo utajikuta unaendelea kuwa gerezani tu .
UNATOKAJE KWENYE GEREZA HILO?
Kama nilivyotangulia kusema mwanzo ,kwanza lazima ujitambue wewe ni nani,kisha uangalie unafanya nini kwa sasa,na je ufanyacho kina mahusiano na wewe ni nani? kama hakuna mahusiano sio ukiache ghafla lakini tengeneza mahusiano ,yaani kitumie hicho unachokifanya kusaidia kusudi la kuumbwa kwako,mfano mimi naelekea kuibadili dunia kwa kupitia maandishi na kuongea lakini kwa sasa natumika hospitalini ,je niache kipi? jibu la haraka ni kwamba navyovipata hospitalini navitumia katika kusukuma kusudi la kuumbwa kwangu ,hivyo nyuma ya haya niyafanyayo kuna sababu zinazoniambia nielekee kwenye ulimwengu wa maandishi na kuzungumza.
Jitahidi utengeneze sababu zinazokusuma kwenda kwenye kusudi lako ,kukosa sababu hizo kunapelekea hali ya kuridhika na hatua hiyo uliyopo ,na hapo ndipo panakuwa mwanzo wa kufanya kazi kwa bidii lakini mbele husogei ,unaishia pale ambapo sababu zako zilikutuma.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.

Saturday, 15 December 2018
MBINU ZA KUTOKA NJE YA DUARA LA UMASKINI.
Karibu sana kwenye blog hii ambayo inatoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu ,ni tumaini langu kuwa u mzima wa afya na unaendelea vyema na harakati za kukuwezesha kufikia ndoto zako....Leo nataka tujifunze mbinu kuu tatu za kutoka nje ya duara la umaskini.Somo hili limekuja maalumu kwa sababu ni wazi kwamba ,wengi wetu tunazaliwa na kulelewa katika familia zenye kipato kidogo,sasa tunapoanza kupiga hatua,tunajikuta tuna mzigo mkubwa nyuma yetu,mzigo ambao tuna wajibu wa kuubeba lakini usiathiri hatua zetu za mafanikio....Karibu tujifunze.
DUARA la umaskini ni mzunguko amabao unaanzia kwa maskini na kuishia kwa maskini ,DUARA hili mara nyingi hutokea kwa watu ambao wamezaliwa katika familia za kimaskini,mimi pia ni mmoja wapo,....inakuwa hivi;
Wazazi/ndugu(MASKINI) >MTOTO(ambaye analelewa katika hali ya kimaskini,ya wazazi wake).
Katika hali hiyo,matatizo ya waliokutangulia yataendelea kukufuata mpaka pale utakapo amua kutengeneza mfumo ambao utawafanya wawe na utegemezi wao binafsi(wajitegemee),kinyume na hivyo,kidogo chako kitakuwa kinategemewa na wengi ambao sio wazalishaji.......Hebu tuangalie hizo mbinu tatu ambazo mimi pia ninazitumia,wewe pia zinaweza kukusaidia.
1.Tambua kuwa wewe ndio daraja la kupitisha wengine,hivyo lazima uwe imara zaidi ya hao unaotaka kuwavusha ,uimara ninao uzungumzia hapa ni wa kiuchumi na mawazo,kiuchumi simaanishi uwe na milioni za pesa,la hasha,namaanisha uwe na mfumo unaoeleweka.
2.Tengeneza mfumo ambao chanzo kitakuwa ni wewe lakini waendelezaji watakuwa ni hao umeokusudia kuwasaidia(maana huwezi kusaidia kila mtu),hapa nimaanisha kwamba wewe yafaa uwe mtaji wa mawazo na pesa kwa huyo uliyekusudia kumsaidia kwa lengo la kumfanya awe na mfumo wa kujitegemea.
3. Kumbuka, kutoa pesa kila wanapohitaji sio msaada wa ukombozi,ni bora uwe bahili kwa muda ili kile kiasi ambacho ungekuwa unawapa ukitunze kisha uje ukitumie kutengeneza mfumo ambao utakuwa unajiendesha wenyewe kwa lengo tu la kuwasaidia wao(hapa nazungumzia wale ambao wanategemewa na watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kusimamia wala kufanya biashara zao,....tengeneza wewe biashara alafu faida ndo itumike kuwasaidia pale wanapohitaji na sehemu nyingine ya faida itumike kuendeshea hiyo biashara)
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa FIKIA NDOTO ZAKO.

Subscribe to:
Posts (Atom)