Thursday, 26 January 2017

NDOTO YA MSIMU -1

Nakukaribisha tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha,binafsi namshukuru Mungu kwa makuu yake kwangu, nina imani na wewe ni mzima.
Bado tupo mwanzo wa safari, kila anaye jitambua najua yupo makini na aendapo.

.
   KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze somo la,NDOTO YA MSIMU,   katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu.
1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
2.CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU.
3. MADHARA YA NDOTO YA MSIMU.

    1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
Ndoto, ni jumla ya picha mtu anayokuwa nayo kuhusu kesho yake, watu wengi huchanganya kati ya "ndoto"  na "malengo "
Malengo ni sehemu  ndogo ndogo ambazo mtu anapaswa kuziunganisha ili kuifikia ndoto yake.

Ndoto ya msimu ni picha ya maisha ambayo mtu huichora kwa kuchochewa na mabadiliko ya mazingira(msimu ).
NB. ....Ndoto ya msimu inaweza kubadilika na kuwa ndoto ya kudumu ila ni watu wachache sana ambao wanafurahia maisha yameyojengwa na badiliko hilo. ...wengi hujuta.

Kwa upana wa kulielewa vizuri somo hili, pitia mifano hii michache.

#  Wanafunzi wengi katika levels zote za elimu huwa wanajikuta wanatengeza ndoto zao kulingana matukio yanayofanyika shuleni,  ila baada ya siku chache kupita baada ya tukio kuisha, wanafunzi hao husahau kabisa kuwa waliweka ndoto flani. ..siku mazingira ya tukio yakijirudia ndipo wanafunzi hao hupata kumbukumbu (ndoto ya msimu hiyo ).

#Watu wengi mwishoni mwa mwaka huwa wanatengeza ndoto nyingi ili mwaka mpya waweze kuzikamilsha. ....ila mambo huwa tofauti, mwaka Ukianza mpya wanasahau kuwa kuna mambo walijiwekea kuyafanya.
Hali hiyo kuna uwezekano ikawa inasababishwa na mada kuu inayo zungumzwa mwishoni mwa mwaka. .....mwishoni mwa mwaka neno MALENGO huwa kwa wingi masikioni kwa watu, hivyo mazingira hayo humfanya mtu kutengeneza ndoto nje ya uhalisia.

#MAHUSIANO, kuna mtu humpenda mtu kulingana na mazingira, mtu huyu hujikuta moyoni mwake  anatengeneza picha juu ya mtu yule kuhusu kesho yake. ....hatari zaidi mtu huyo kulingana na uchochezi wa mazingira hujikuta anafanya AGANO la kudumu kwenye Upendo wa msimu. .....siku mazingira yale yakipotea mtu huyu ndipo anagundua yupo sehemu isiyo sahihi(ndoto ya msimu )

Nina imani kwa mifano hiyo somo limeeleweka kwa kiasi flanI.
Jiulize ,ndoto uliyonayo ni ya msimu? Kama ndio, umewahi kufikiria ni hali gani utakuwa nayo siku mazingira yameyotengeneza ndoto yako yakitoweka?
NB. ..
Kabla ya kuchukua maamuzi hakikisha umefahamu madhara ya ndoto ya msimu.



                                       See you at the top.
                                       Scientist Saul Kalivubha.
                                              0652 134707.. 

2 comments: