Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa Mungu katimiza mapenzi yake kwetu sote. ......
KUSUDI LA SOMO
.
Lengo la somo letu la leo ni kuendelea na sehemu ya pili ya siri za uvumilivu,Kumbuka tu somo letu lina sehemu tatu. 1.maana ya uvumilivu. 2.faida za uvumilivu. 3.hasara za kukosa uvumilivu.
Ni vizuri kama utafatilia sehemu ya kwanza kwa kuingia Google search na kuandika kalivubha blog siri za uvumilivu utaletewa sehemu hiyo. ....karibu tuendelee.
2.FAIDA ZA UVUMILIVU.
Kwenye maisha tunayoishi kuna hali kuu mbili zinazochanganya watu wengi sana katika kufanya maamuzi, hali hizo ni kupata kitu kwa wakati na kupata kitu nje ya wakati .Ili kuweza kuzitawala hali zote hizo mbili bila kufanya maamuzi hatarishi inahitaji uvumilivu. Nmejaribu kuelezea faida za uvumilivu kupitia hali zifatazo.
1.Kukwepa hasara, katika mazingira tunayopitia kuelekea ndoto zetu kuna faida na hasara tuzipatazo kama matokeo ya yale tufanyayo. .....zipo hasara zinakuja kama changamoto, ila zipo hasara huja kama matokeo ya kupoteza uvumilivu, .......mara nyingi mtu akishindwa kutawala hisia zake kwenye mazingira yasiyo ya kawaida hujikuta amefanya maamuzi yasiyo ya kawaida ambayo ni HASARA.
2.Kujiongezea thamani ; Wanasikolojia tuna amini kuwa mtu mwenye uvumilivu huwa ana tabia ya kunyamaza pia kwenye mazingira yenye kuhitaji uvumilivu, hii huongeza thamani ya mtu huyo kwenye jamii, maana anakuwa amefanikisha kuzitawala hisia zako ambazo zingepelekea matokeo mabovu kulingana na maamuzi yenye kukosa uvumilivu. ....
3.Kutimiza ndoto; kila mtu mwenye kujitambua lazima awe na ndoto za maisha, ....ila taarifa isiyo pendeza masikioni kwa wengi ni kwamba. ili kufanikisha ndoto zako huwa inahitaji muda mrefu kidogo. ....taarifa hiyo sio nzuri kwa wengi maana watu wengi hupenda njia za mkato ktk kuelekea ndoto zao, ila kwa kuwa swala la kufikia ndoto zetu linahitajI muda wale wavumilivu tu ndo wamekuwa wakifikia ndoto zao.
Kumbuka kuwa uvumilivu sio Kazi rahisi, lazima uumie, ila ukiweza kubeba maumivu ya UVUMILIVU , kuna uwezekano ukaziishi ndoto zako.
karibu tena katika sehemu ya tatu na ya mwisho wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652 134 707 )
No comments:
Post a Comment