Sunday, 8 January 2023

JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI

 JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI KWENYE MAHUSIANO 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Wivu kwa maana rahisi ni kutojiamini , unahisi kuna watu wenye sifa zaidi yako watakuibia mpenzi wako 😔 Wivu hukoleza mapenzi 😊 

Kutojiamini ni wivu uliopitiliza kiasi , muda wote unahisi umpendaye ana njama mbaya dhidi yako kiasi cha kila siku kuwa na migogoro isiyoisha 

Kutojiamini ni sumu ya mahusiano.Wafikiri sababu zake ni nini? Na utajijuaje ikiwa una tatizo hili ?  Karibu darasani 

DALLI ZA KUTOJIAMINI 

Asipojibu meseji kwa wakati tayari unahisi kafanya makusudi 😔 

Asipoitikia simu yako wewe unajua yupo anafanya kitu kibaya 😔 

Ukimpigia simu akiwa anaongea na mtu mwingine tayari unahisi yupo anakusaliti 😢

Siku haiishi bila kumuwazia mabaya yaani unahisi kama vile hakupendi au anakudharau 😔 

Muda wote unahisi kama anakudanganya tu hakuna siku unamuamini 😔 

Unakuwa mwepesi kukasirika kwa vitu vidogo vidogo tu

Hujui bahati mbaya kila kitu kwako unaona ni njama mbaya aliyoipanga kukufanyia 😔 

Akiwa na marafiki zake tayari unahisi anakusaliti au wanamshaurii mabaya kukuhusu wewe 😔


Weka alama ya tick kwenye dalili inayokusumbua ikiwa kila migogoro ya mahusiano yako chanzo ni dalili zaidi ya nusu kati ya hizo kuna uwezekano mkubwa kati yenu kuna tatizo la Kutojiamini .Kutojiamini kuna leta migogoro na ni ngumu kuwa na mahusiano yenye afya nzuri ikiwa kati yenu kuna migogoro ambayo chanzo chake  kikubwa ni Kutojiamini .

Mbona hata dalili za wivu ni kama zinafanana na za Kutojiamini?  Swali zuri sana hilo ni kweli kabisa dalili pia za wivu ni kama hizo hizo sema kama nilivyokwiaha kusema juu kwenye utangulizi kuwa wivu ni Kutojiamini kuliko na kiasi na huwa hakuna migogoro kwenye wivu wa mapenzi bali hukuza mahusiano yenu ya mapenzi , bila wivu wa kiasi mahusiano huwa hayana raha. 


Kwenye wivu kuna upendo lakini kwenye kutojiamini  kuna upendo wa mashaka ndio maana kutojiamini ni chanzo kingine cha kuvunja mahusiano au kufanya watu wakuogope kwa sababu tu ya migogoro kila siku, hakuna anayependa migogoro ya kila siku .

Kutojiamini chanzo chake ni nini?  Kuna vyanzo vingi vya tatizo hilo yawezekana ikawa ni sababu za kimazingira au za kuzaliwa nazo( kurithi). Tuone sababu chache zifuatazo:

Kuwa na historia ya kusalitiwa : Mara nyingi tatizo la Kutojiamini linaonekana kwa watu ambao wana historia ya kusalitiwa na wenzi waliowapenda sana hivyo wanakuwa hawana imani tena watu , na mara nyingi tatizo linakuwa kubwa kama muhusika ataamua kuingia kwenye mahusiano mapya bila kupona kwa jeraha lake la kwanza hivyo matokeo yake anakuwa anaishi na mtu wa pili kama vile ni mtu yule wa kwanza.Tiba ya  tatizo hilo ikiwa chanzo ni hiki basi tiba yake ni kujiponya majeraha kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya. 

Chanzo kingine ni tabia yako ya kutafuta ukamilifu wa 100%; Tatizo hili ndio chanzo cha kutoamini kuwa kuna bahati mbaya ndio maana mwenzio akifanya vitu bahati mbaya tayari unajua ni makusudi kakufanyia na tayari ni mgogoro huo , hutaki kumuona kama na yeye ni binadamu bali unamuona kama ni malaika ambaye hakosei hata kidogo.  Tiba yake hapa  ni kujifunza kupuuzia baadhi ya vitu vinavyotokea kwenye mahusiano yako muhimu tu visiwe vina madhara makubwa kwenye safari yenu , kuna mambo unaweza kuyapuuzia na yasilete madhara kwenye mahusiano yenu lakini ukikata kufuatilia kila kitu lazima mtakuwa na migogoro mingi sana kwenye mahusiano yenu .

Chanzo kingine ni kuathiriwa na huyo umpendaye yaani unayempenda anakuwa na historia ya kukusaliti hivyo tayari kumuamini tena inakuwa ngumu hivyo anakujengea tabia ya Kutojiamini tena na matokeo yake ni kuwa na mashaka dhidi ya matendo yake. Tiba ya hapa inachukua muda wa kutosha na lazima yeye ndiye akutibu kwa kukuaminisha kuwa kaacha tabia zake za awali .

Chanzo kingine ni urithi; Tayari umezaliwa upo hivyo tu yaani una tatizo la Kutojiamini la kuzaliwa nalo , hapa kuna tiba kutoka pande mbili ambazo ni kutoka kwako na anayekupenda. Lazima ujikubali kuwa una tatizo na kujidhibiti pale uwezapo  na huyo akupendaye inabidi ajue kuwa una kasoro hiyo Hivyo lazima ajifunze kuishi na wewe. 

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

Mafunzo yetu yapo mitandaoni kote kwa jina la fikiandotozako 

Pia kitabu cha siri za urafiki kinapatikana soft copy ( nakala tete) kwa Tsh4000 tu , ukilipa utatumiwa muda huo huo 


+255652 134707

2 comments: