KILA MTU ANA MTU WA HADHI YAKE 😊 MATESO YAPO PALE UTAPOWANG'ANG'ANIA WASIO WA HADHI YAKO 😢
Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍
Bila shaka kichwa cha andiko kimekusisimua 😄 kama ni kweli basi nawe tayari upo kwenye kundi la watu ambao wanasumbuliwa na watu 😔 Mwanasayansi kakuvuruga? 😔 haya twende darasani ✍
Kuna watu hata kwa nini hamuwezi kukaa kiti kimoja mkaelewana kwa sababu tu mna hadhi tofauti mpaka mmoja apande/ashuke kwenye hadhi ya mwingine ndio mtakaa pamoja na kuelewana, wewe una hadhi gani? watu gani unawakumbatia? Ndugu yangu ukitaka mahusiano yakutese wakumbatie watu mnaopishana hadhi 😔
Kwa mfano wewe kwa sasa hadhi yako ni kuhudumia shilingi elfu kumi kwa mwezi wafikiri utaweza kukaa na mtu mwenye hadhi ya kuhudumiwa milioni moja kwa mwezi? kwa namna yoyote hapo haiwezekani tu kabisa mpaka ajishushe kwenye hadhi yako au wewe upande kwenye hadhi yake tofauti na hivyo utatumia nguvu kubwa mpaka kukopa au kuuza rasilimali zako ili tu uendane naye lakini ukweli ni kuwa unaweza kufanikiwa mwanzoni tu lakini baadaye utashindwa na utabaki hovyo sana
Huo ni mfano tu mmoja lakini ipo mifano mingi kwenye maisha ya kila siku ambapo watu hujikuta kwenye mateso kwa sababu tu ya kuwakumbatia watu wenye hadhi tofauti. Ukiona hudumu sana na watu kwenye mahusiano yoyote yale kaa chini jitafakari sio ukimbilie kusema wewe una mkosi la hasha yawezekana una kasoro hii ya kuwakumbatia watu mnaopishana hadhi na mwisho wa siku unakuwa mtu wa kulaumu tu na wakati mchawi ni tabia yako hiyo.
Utajuaje hadhi yako? Swali nzuri sana hili , ni kweli ni lazima kwanza ujitambue hadhi yako kwa sasa ni ipi na sio kazi ngumu hata muhimu ni kujiangalia kwenye maeneo haya matatu WEWE NI NANI, UNATAKA NINI NA UNA MUDU KIPI. Kama unajitambua kwenye hayo na bado matokeo ni yale yale basi yawezekana pia wewe ni mbishi hutaki kujikubali kuwa wewe ni nani ndio maana unalazimisha wasio na hadhi yako.
Siku utakokubali kuwa kuna watu tu sio hadhi yako ndipo utayaona mahusiano ni mazuri kwa sehemu 😊 na utaona ukipendwa na kuheshimiwa 😊 lakini huyaoni hayo kwa sababu upo na watu ambao sio hadhi yako unaumia tu kila siku na kucheleweshwa na usipokuwa makini utakumbuka shuka tayari ni asubuhi 😔 Fanya tu maamuzi magumu ya kuwaacha watu wa ambao sio hadhi yako ili upatane na wenye hadhi yako au tulia kwanza ukuze hadhi yako ndio upate wenye hadhi sawa.
Kuna watu huwapati na hutowapata kwa sababu tu sio hadhi yako na unapoteza muda kwenye hilo. Kuna msemo unasema kuwa embe halianguki mbali na mti wake , huu ni msemo wenye hekima na wahenga waliifikiria mbali kwenye hilo maana sio kazi rahisi ukute embe chini kusiko na mti wake labda tu liwe limetupwa 😄 na kwa nini litupwe ? Ila ukiona embe chini kikawaida kuna mti wake pembeni ndio sawa na maisha yetu ukiona wawili wanaendana kuna uwezekano mkubwa wakawa na hadhi moja tofauti na hivyo basi kuna mmoja amekubali kuwa mtumwa wa mwingine 😔 Sasa kwa nini ukubali kuwa mtumwa? na wakati wa hadhi yako yupo tu na mngefurahia maisha tu
Tafuta mtu wa hadhi yako ndio sasa taratibu muanze kupanda hadhi pamoja na kama utapata mtu asio wa hadhi yako mkaendana basi pia shukuru Mungu na hii huwa inatokea lakini ni mara chache sana
Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha
+255652134707
Madarasa yetu yapo Instagram kwa jina la fikiandotozako
No comments:
Post a Comment