Sunday, 26 February 2023

HIVI NAWE UNAFANYA MAMBO KWA HASARA? 😔 KAMA JIBU NI NDIO, MAKALA HII  INAKUHUSU 

 HIVI NAWE UNAFANYA MAMBO KWA HASARA? 😔 KAMA JIBU NI NDIO, MAKALA HII  INAKUHUSU .

Japo wataalamu wanasema hakuna kipimo cha muda sahihi wa mafanikio lakini vipo vipimo vya kujipima kuwa unafanya mambo kwa hasara na ukijua hilo itakuwa rahisi kufanya maamuzi magumu ya kutoendelea na shughuli hiyo inayokupa hasara au kujiboresha ili upate uanze kupata faida.  Inaumiza sana kutumia nguvu kubwa halafu matokeo yaje kidogo au yasije kabisa 😔  Bahati mbaya ni kuwa wengi huwa hatujitambui kuwa tupo tunapoteza muda bure bali tunakuwa tunajifariji kuwa tupo tunavumilia na ipo siku tutafanikiwa, sio vibaya kujipa faraja lakini ni vibaya pia kujipa faraja kwenye sehemu isyo yako au kujipa faraja kwa kitu ambacho haiwezekani.Somo hili lipo mahususi kwa watu ambao wanasumbuka na changamoto ya kufanya mambo kwa hasara.

Zipo dalili nyingi za kujipima ili kujifahamu kuwa upo kwenye kundi la watu ambao hufabya mambo yao kwa hasara, dalili hizo ni kama zifuatazo;

1. Unafanya mambo bila kuyamaliza , kwa mfano leo unaanza safari ya kusoma kabla ya hujamaliza miaka yako ya ki elimu unaona kuwa umekosea unaachana na kozi hiyo na kutafuta kozi nyingine 😔 Unafungua biashara fulani na kabla hujaimudu vyema unajiona kuwa umekosea unaifunga na kuanzisha nyingine 😔 Unaanzisha mahusiano ya kimapenzi kwa furaha zote lakini ndani ya muda mfupi unaona umekosea unamuacha na kutafuta mwingine 😔 

2. Unakaa hatua moja kimafanikio kwa muda mrefu bila kuhama,hii hutokea pale ambapo mbele husogei kwa mfano unauza biashara ya nyanya miaka na miaka na kwa mtaji ule ule  .

3.Unafanya jambo bila kuwa na muda wa ukomo kwa mfano  unaamua kufanya biashara ya kutembeza mitumba ya n  lako la nguo na uachane na kutembeza mtaani. 

4. Upo kwenye mahusiano  na unaona kabisa ishara zote kuwa hutakiwi hapo lakini unaendelea kuvumilia kwa sababu unaona utakosa pakwenda  , hii ni dalili ya kuwa unafanya kihasara. 

Je kuna dalili moja wapo unayo hapo juu? Au zifananazo na hapo? Kama jibu ni ndio basi upo unafanya vitu bila mafanikio , je utatokaje? 

Njia rahisi ya kutoka kwenye kufanya mambo yasiyo na mafanikio ni kuwa na muda wa kutosha wa kujitathmini kwenye chochote ufanyacho na kujitengea ukomo wa muda usikubali ukae eneo moja muda wote la sivyo iwe ndio mwisho wa malengo yako  kama sivyo jiwekee muda wa kutoka hapo kama unauza maji ya basi moja uwe na kiwanda cha kutengeneza maji . Jiwekee mbinu za kujifanyia uchunguzi kila muda fulani.


Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

+255652134707

Saturday, 14 January 2023

 HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA UWE MTU WA KUJUTIA MAAMUZI YAKO

 HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA UWE MTU WA KUJUTIA MAAMUZI YAKO 


Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 


Ulijawa na furaha siku hiyo na hata kama angetokea mtu wa kukwambia kuwa unachotaka kufanya ni hatari pengine ungemuona ni adui asiyependa mafanikio yako lakini furaha yako leo haipo tena 😞 Unajutia  maamuzi yale .Kwa nini umekuwa mtu wa kujutia maamuzi yako ? Na ilihali jana ulijiona upo sahihi kwa maamuzi hayo? Twende darasani. 

Maamuzi ni eneo muhimu sana kwenye maisha yetu kwa sababu maamuzi ndio miguu yetu ya kutembelea , upo hapo ulipo leo  kwa sababu kuna maamuzi uliyafanya jana na hata hao unaowashangaa leo wapo hivyo kwa sababu kuna maamuzi waliyafanya jana .

Kujutia sio kitu kigeni kwa sababu karibu kila mtu ana siku moja au zaidi za kujutia maamuzi yake, hakuna ambaye hajawahi kujutia katika maisha yake lakini wapo watu ambao kwao ni zaidi yaani kwenye maamuzi kumi waliyofanya basi   zaidi ya maamuzi matano kwao sio sahihi ni lazima wayajutie.

Kwa nini leo ujione umekosea na wakati jana ulijiona sahihi kwa maamuzi yale yale?  Yapo mambo mengi ambayo yanachangia hali hiyo kutokea  na vizuri uyafahamu mambo hayo ili ujue namna ya kupunguza majuto , na kama unakuwa mwingi wa majuto kuna uwezekano mkubwa ukawa ni mtu ambaye huna furaha kwenye maisha yako kwa sababu unakuwa unafikiria  yaliyopita tu .

Ufahamu wako wakati wa maamuzi ni sababu kubwa sana ya majuto kwa wengi, wajua ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu kinachofanya uamue ni Ufahamu wako wa muda huo hivyo kama ufahahamu wako ni mdogo sana basi hata maamuzi yako kwa asilimia kubwa  yatakuwa sio bora pia na siku ufahahamu wako ukikua ni lazima utaona kuwa ulikosea maamuzi . Tunajutia maamuzi yetu ya jana kwa sababu tuliyafanya tukiwa na ufahahamu mdogo tofauti na leo tulivyo kwa mfano  kama jana ulifanya maamuzi ya kuacha shule kwa ufahahamu kuwa shule inakupotezea muda  ni bora ufanye biashara lakini ulipoanza biashara ukakutana na changamoto zikakumbusha kuwa kuna kiwango cha elimu kinatakiwa ili uweze kuimudu hiyo biashara na hapo ndipo utaaanza kujiona ulikurupuka kwenye maamuzi. 

Matokeo ya maamuzi yetu tuliyoyafanya jana ndio yanasema na sisi leo kutu onyesha ni jinsi gani tulikosea/kupatia  kwenye maamuzi yetu hayo , kuna kanuni moja ya kimaamuzi inasema kuwa kila maamuzi uliofanya ni lazima matokeo yake yaje kusema na wewe siku moja na hapo ndipo utagundua ni jinsi gani ulikuwa sahihi. Matokeo hufanya watu tujifahamu vizuri tukoje na kama utakuwa mtu chanya basi utatumia matokeo hayo kujifunza. 

Mihemko pia ni sababu nyingine inayofanya tukosee maamuzi kwa sababu maamuzi yako yatakuwa ni matokeo ya hisia za muda mfupi tu zisizo na fikra ndani yake ndio maana unashauriwa kuwa na utulivu kabla ya maamuzi japo kuna maamuzi mengine ni lazima tuyafanye kwa haraka kulingana na uhitaji wake lakini hayo ni kama dharura  tu ila maamuzi mengi lazima kuna muda utapata wa kufikiria hivyo kabla hujaamua jitahidi huna mihemko . Mihemko mara nyingi chanzo chake ni kukosa utulivu na muda mwingine kuchochewa na mazingira ya nje ikiwemo kuishi kwa kujilinganisha sana. Ukiishi kwa kujilinganisha utakuwa mtu wa kujiona umechelewa kwenye maisha na mwishowe utaanza kufanya vitu bila utulivu .

Kushindwa kuitawala shauku yako pia ni sababu inayoweza kukufanya ukosee maamuzi kwa sababu utakuwa mtu wa kukurupukia mambo kabla ya wakati wake ili tu ukidhi shauku yako Maamuzi yako Hayawezi kuwa sahihi kama unayafanya kwa shauku ambayo haikudhibitiwa .

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

Mitandaoni tunapatikana kwa jina la fikiandotozako. 

Pia kitabu cha namna ya kudhibiti mwili kinapatikana kwa soft copy Tsh 3000 

+255652134707

Sunday, 8 January 2023

JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI

 JIFUNZE TOFAUTI KATI YA WIVU NA KUTOJIAMINI KWENYE MAHUSIANO 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Wivu kwa maana rahisi ni kutojiamini , unahisi kuna watu wenye sifa zaidi yako watakuibia mpenzi wako 😔 Wivu hukoleza mapenzi 😊 

Kutojiamini ni wivu uliopitiliza kiasi , muda wote unahisi umpendaye ana njama mbaya dhidi yako kiasi cha kila siku kuwa na migogoro isiyoisha 

Kutojiamini ni sumu ya mahusiano.Wafikiri sababu zake ni nini? Na utajijuaje ikiwa una tatizo hili ?  Karibu darasani 

DALLI ZA KUTOJIAMINI 

Asipojibu meseji kwa wakati tayari unahisi kafanya makusudi 😔 

Asipoitikia simu yako wewe unajua yupo anafanya kitu kibaya 😔 

Ukimpigia simu akiwa anaongea na mtu mwingine tayari unahisi yupo anakusaliti 😢

Siku haiishi bila kumuwazia mabaya yaani unahisi kama vile hakupendi au anakudharau 😔 

Muda wote unahisi kama anakudanganya tu hakuna siku unamuamini 😔 

Unakuwa mwepesi kukasirika kwa vitu vidogo vidogo tu

Hujui bahati mbaya kila kitu kwako unaona ni njama mbaya aliyoipanga kukufanyia 😔 

Akiwa na marafiki zake tayari unahisi anakusaliti au wanamshaurii mabaya kukuhusu wewe 😔


Weka alama ya tick kwenye dalili inayokusumbua ikiwa kila migogoro ya mahusiano yako chanzo ni dalili zaidi ya nusu kati ya hizo kuna uwezekano mkubwa kati yenu kuna tatizo la Kutojiamini .Kutojiamini kuna leta migogoro na ni ngumu kuwa na mahusiano yenye afya nzuri ikiwa kati yenu kuna migogoro ambayo chanzo chake  kikubwa ni Kutojiamini .

Mbona hata dalili za wivu ni kama zinafanana na za Kutojiamini?  Swali zuri sana hilo ni kweli kabisa dalili pia za wivu ni kama hizo hizo sema kama nilivyokwiaha kusema juu kwenye utangulizi kuwa wivu ni Kutojiamini kuliko na kiasi na huwa hakuna migogoro kwenye wivu wa mapenzi bali hukuza mahusiano yenu ya mapenzi , bila wivu wa kiasi mahusiano huwa hayana raha. 


Kwenye wivu kuna upendo lakini kwenye kutojiamini  kuna upendo wa mashaka ndio maana kutojiamini ni chanzo kingine cha kuvunja mahusiano au kufanya watu wakuogope kwa sababu tu ya migogoro kila siku, hakuna anayependa migogoro ya kila siku .

Kutojiamini chanzo chake ni nini?  Kuna vyanzo vingi vya tatizo hilo yawezekana ikawa ni sababu za kimazingira au za kuzaliwa nazo( kurithi). Tuone sababu chache zifuatazo:

Kuwa na historia ya kusalitiwa : Mara nyingi tatizo la Kutojiamini linaonekana kwa watu ambao wana historia ya kusalitiwa na wenzi waliowapenda sana hivyo wanakuwa hawana imani tena watu , na mara nyingi tatizo linakuwa kubwa kama muhusika ataamua kuingia kwenye mahusiano mapya bila kupona kwa jeraha lake la kwanza hivyo matokeo yake anakuwa anaishi na mtu wa pili kama vile ni mtu yule wa kwanza.Tiba ya  tatizo hilo ikiwa chanzo ni hiki basi tiba yake ni kujiponya majeraha kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya. 

Chanzo kingine ni tabia yako ya kutafuta ukamilifu wa 100%; Tatizo hili ndio chanzo cha kutoamini kuwa kuna bahati mbaya ndio maana mwenzio akifanya vitu bahati mbaya tayari unajua ni makusudi kakufanyia na tayari ni mgogoro huo , hutaki kumuona kama na yeye ni binadamu bali unamuona kama ni malaika ambaye hakosei hata kidogo.  Tiba yake hapa  ni kujifunza kupuuzia baadhi ya vitu vinavyotokea kwenye mahusiano yako muhimu tu visiwe vina madhara makubwa kwenye safari yenu , kuna mambo unaweza kuyapuuzia na yasilete madhara kwenye mahusiano yenu lakini ukikata kufuatilia kila kitu lazima mtakuwa na migogoro mingi sana kwenye mahusiano yenu .

Chanzo kingine ni kuathiriwa na huyo umpendaye yaani unayempenda anakuwa na historia ya kukusaliti hivyo tayari kumuamini tena inakuwa ngumu hivyo anakujengea tabia ya Kutojiamini tena na matokeo yake ni kuwa na mashaka dhidi ya matendo yake. Tiba ya hapa inachukua muda wa kutosha na lazima yeye ndiye akutibu kwa kukuaminisha kuwa kaacha tabia zake za awali .

Chanzo kingine ni urithi; Tayari umezaliwa upo hivyo tu yaani una tatizo la Kutojiamini la kuzaliwa nalo , hapa kuna tiba kutoka pande mbili ambazo ni kutoka kwako na anayekupenda. Lazima ujikubali kuwa una tatizo na kujidhibiti pale uwezapo  na huyo akupendaye inabidi ajue kuwa una kasoro hiyo Hivyo lazima ajifunze kuishi na wewe. 

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

Mafunzo yetu yapo mitandaoni kote kwa jina la fikiandotozako 

Pia kitabu cha siri za urafiki kinapatikana soft copy ( nakala tete) kwa Tsh4000 tu , ukilipa utatumiwa muda huo huo 


+255652 134707

Friday, 6 January 2023

KILA MTU ANA MTU WA HADHI YAKE  😊 MATESO YAPO PALE UTAPOWANG'ANG'ANIA WASIO WA HADHI YAKO 😢 

 KILA MTU ANA MTU WA HADHI YAKE  😊 MATESO YAPO PALE UTAPOWANG'ANG'ANIA WASIO WA HADHI YAKO 😢 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Bila shaka kichwa cha andiko kimekusisimua 😄 kama ni kweli basi nawe tayari upo kwenye kundi la watu ambao wanasumbuliwa na watu 😔 Mwanasayansi kakuvuruga? 😔  haya twende darasani ✍

Kuna watu hata kwa nini hamuwezi kukaa kiti kimoja mkaelewana kwa sababu tu mna hadhi tofauti  mpaka mmoja apande/ashuke kwenye hadhi ya mwingine ndio mtakaa pamoja na kuelewana, wewe una hadhi gani? watu gani unawakumbatia? Ndugu yangu ukitaka mahusiano yakutese wakumbatie watu mnaopishana hadhi 😔

Kwa mfano wewe kwa sasa hadhi yako ni kuhudumia shilingi elfu kumi kwa mwezi wafikiri utaweza kukaa na mtu mwenye hadhi ya kuhudumiwa milioni moja kwa mwezi?  kwa namna yoyote hapo haiwezekani tu kabisa mpaka ajishushe kwenye hadhi yako au wewe upande kwenye hadhi yake tofauti na hivyo utatumia nguvu kubwa mpaka kukopa au kuuza rasilimali zako ili tu uendane naye lakini ukweli ni kuwa unaweza kufanikiwa mwanzoni tu lakini baadaye utashindwa na utabaki hovyo sana  

Huo ni mfano tu mmoja lakini ipo mifano mingi kwenye maisha ya kila siku ambapo watu hujikuta kwenye mateso kwa sababu tu ya kuwakumbatia watu wenye hadhi tofauti.  Ukiona hudumu sana na watu kwenye mahusiano yoyote yale kaa chini jitafakari sio ukimbilie kusema wewe una mkosi la hasha yawezekana una kasoro hii ya kuwakumbatia watu mnaopishana hadhi na mwisho wa siku unakuwa mtu wa kulaumu tu na wakati mchawi ni tabia yako hiyo.

Utajuaje hadhi yako? Swali nzuri sana hili , ni kweli ni lazima kwanza ujitambue hadhi yako kwa sasa ni ipi na sio kazi ngumu hata muhimu ni kujiangalia kwenye maeneo haya matatu WEWE NI NANI, UNATAKA NINI NA UNA MUDU KIPI.   Kama unajitambua kwenye hayo na bado matokeo ni yale yale basi yawezekana pia wewe ni mbishi hutaki kujikubali kuwa wewe ni nani ndio maana unalazimisha wasio na hadhi yako.

Siku utakokubali kuwa kuna watu tu sio hadhi yako ndipo utayaona mahusiano ni mazuri kwa sehemu 😊 na utaona ukipendwa na kuheshimiwa 😊 lakini huyaoni hayo kwa sababu upo na watu ambao sio hadhi yako unaumia tu kila siku na kucheleweshwa na usipokuwa makini utakumbuka shuka tayari ni asubuhi 😔  Fanya tu maamuzi magumu ya kuwaacha watu wa ambao sio hadhi yako ili upatane na wenye hadhi yako au tulia kwanza ukuze hadhi yako ndio upate wenye hadhi sawa.

Kuna watu huwapati na hutowapata kwa sababu tu sio hadhi yako na unapoteza muda kwenye hilo. Kuna msemo unasema kuwa embe halianguki mbali na mti wake , huu ni msemo wenye hekima na wahenga waliifikiria mbali kwenye hilo maana sio kazi rahisi ukute embe chini kusiko na mti wake labda tu liwe limetupwa 😄  na kwa nini litupwe ? Ila ukiona embe chini kikawaida kuna mti wake pembeni ndio sawa na maisha yetu ukiona wawili wanaendana kuna uwezekano mkubwa wakawa na hadhi moja tofauti na hivyo basi kuna mmoja amekubali kuwa mtumwa wa mwingine 😔 Sasa kwa nini ukubali kuwa mtumwa? na wakati wa hadhi yako yupo tu na mngefurahia maisha tu

Tafuta mtu wa hadhi yako ndio sasa taratibu muanze kupanda hadhi pamoja na kama utapata mtu asio wa hadhi yako mkaendana basi pia shukuru Mungu na hii huwa inatokea lakini ni mara chache sana 


Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul Kalivubha 

+255652134707


Madarasa yetu yapo Instagram  kwa jina la  fikiandotozako 

Sunday, 1 January 2023

KUNA TOFAUTI KATI YA MTU MASKINI NA MTU AMBAYE HANA PESA 

 KUNA TOFAUTI KATI YA MTU MASKINI NA MTU AMBAYE HANA PESA 

Na Mwanasayansi Saul Kalivubha ✍ 

Mtu anaweza kuwa hana kabisa pesa hata shilingi mia lakini asiwe MASKINI na mtu anaweza kuwa anakula tu vizuri na kila kitu cha ndani lakini akawa MASKINI 😔  Mwanasayansi kakuchanganya? 😄 🤣 

Hapana nipo sahihi ✍ 

Umaskini ni IMANI lakini kukosa pesa ni MAPITO , Unaweza pitia kipindi cha kukosa pesa lakini imani yako ni ya KITAJIRI 

Umaskini ni imani kama zilivyo imani nyingine tu za kiroho mfano uislam na Ukristo ulivyo na waumini ndivyo ilivyo hata kwenye Umaskini kuna waumini wake wamo humo ndio maana sio kazi rahisi kuaga Umaskini, narudia tena sio kazi rahisi kuaga Umaskini kama ilivyo ngumu kumbadilisha muislamu kuwa mkristo  au kinyume chake, unajua sababu? Ni kwa sababu tu kila muumini ameshika mizizi ya dini yake hivyo sio rahisi kuiachia kirahisi. 

Umaskini huanzia kwenye akili ya mtu ndio maana watu maskini huwa wana viashiria vya kufanana kwa sababu tu wapo imani moja, je wajua viashiria? ( Dalili za umaskini)


#Ni watu wa visingizio

#Ni watu wa kuridhika na maisha ya kujaza tumbo tu

#Huamini kuwa wanaoshindwa wametoa rushwa au ni wenye imani za kishirikina 

#Kila jambo wanasema ni mpango wa Mungu hata ambalo  ni matokeo ya uzembe wao

Hizo ni dalili chache kati ya nyingi za muumini wa UMASKINI yawezekana unazo chache au zote kati ya hizo basi jijue wewe ni muumini wa UMASKINI tayari 😔 

Unaweza kutoka humo? Ndio inawezekana kutoka humo japo sio rahisi kama nilivyokwisha kusema kuwa sio rahisi kubadili imani 😔 nguvu kubwa inatakiwa 

Lazima kwanza ukubali kuwa wewe ni maskini upo kwenye imani hiyo sasa unatakiwa kuanza taratibu kuzikana imani hizo za kimaskini ili uhame kutoka imani hiyo uende kwenye imani ya UTAJIRI 

UTAJIRI ni imani pia yenye waumini wachache lakini na misingi ya imani yao ipo kinyume na misingi ya umaskini hivyo ni rahisi tu kuwa humo kama tu utaikana misingi ya umaskini 


Nikutakie mwaka mpya mwema ndugu yangu 


+255652 134707

Monday, 3 October 2022

 USISUBIRI PESA IPUNGUE NDIO UWEKE NIDHAMU YA MATUMIZI

Matumizi ya pesa bado ni changamoto kwa watu wengi na matokeo yake hujikuta katika ukosefu wa pesa wa mara kwa mara na hii sio kwa waajiwa tu hata waliojiajiri kwenye mambo yao binafsi  bado hujikuta kwenye kipindi kigumu cha ukosefu wa pesa sio kwa sababu haikuwepo la hasha ni kwa sababu ilikuwepo lakini ikatumiwa bila kuzingatia matumizi sahihi kutokana na kipato. Ukipata muda tulivu ukajitafakari utagundua kuwa pindi upatapo pesa matumizi yako yanakuwa juu na hupungua kadri pesa inavyopungua yaani kwa lugha rahisi  ni kuwa nidhamu yako ya matumizi ya pesa inaongezeka kadri unavyoishiwa pesa. 

Pesa ni nguvu ya kihisia ambapo usipoitawala itakutawala yenyewe kwa kukupa maamuzi mengi na hapo utakosa utulivu hali ambayo itafanya upoteze nidhamu ya matumizi ndio maana mshahara ukiingia unaweza jikuta unafanya manunuzi bila kuangalia ukubwa wa gharama kwa sababu unajua pesa ipo lakini ukianza kusikia mfuko umepwaya ndio utarudisha makini wa matumizi kwa mfano mwanzo ulilipwa laki tano na ilipofikia mfukoni umebaki na laki moja ndio utaanza kuipigia mahesabu hiyo laki moja kuangalia kama itakufikisha mwezi mwingine, je kwa nini hukufikiria hivyo tangu ukiwa na laki tano? 

Nidhamu ya pesa ni kuheshimu pato lako kwanza na pili ni kuheshimu matumizi sahihi yaliyo ndani ya kipato chako kama ulipanga kununua kitu cha shilingi mia ndio itakuwa sawa kulingana na kipato chako basi fanya hivyo lakini ulinunua kwa shilingi Mia mbili ujue umekula na pesa ya siku fulani hivyo jiandaye siku hiyo kukosa pesa la sivyo iwe ni dharura ndio tumia lakini kama si dharura yatakiwa ujidhibiti dhidi ya matumizi ya pesa pale tu unapoipata, changamoto ya pesa ni kuwa ukitumia pesa ndogo unaona kawaida tu lakini mwisho wa siku ukijumlisha unakuta kama ungehifadhi ungekuwa mbali sana kifedha hivyo nidhamu ukianza na kuheshimu matumizi yako yaliyo ndani ya kipato chako utakuwa kwenye kiwango kizuri cha kuweka akiba. 

Nidhamu binafsi katika matumizi ya pesa inajengwa na lengo kuu ulilonalo la kesho hapo ndio utakuwa unatumia pesa ukikumbuka kesho hivyo utakuwa ukijikumbusha kila kabla ya matumizi ambayo si salama kulingana na kipato chako na utakuwa na nidhamu muda wote, lazima uwe na nidhamu au ukose nidhamu lakini ukubali kupoteza lengo kuu la kesho na njia nzuri nyingine ni kuigawa pesa yako kwa siku utagundua unaingiza shilingi ngapi kila siku na kisha angalia matumizi yako kila siku yanaendana na pato lako la siku? Kwa kuanzia na hapo utajirekebisha kimatumizi na utaheshimu matumizi sahihi ya pesa. 

Pesa ikiwa nyingi itakupa upofu wa kuamini kuwa huwezi kuishiwa hivyo kila matumizi yakujiayo kichwani utayafanya na hapo ndio mwanzo wa kutumia hovyo pesa  mpaka baadaye ikipungua ndio itakutoa upofu uone kuwa kuna hatari itokanayo na ukosefu wa pesa kwa sababu pesa uliyonayo haitoshi kukufikisha msimu mwingine wa pesa kumbe kuna kuna nguvu kubwa inatakiwa uwe nayo awali ili kudhibiti hisia za pesa zisikutawale. 

Kujua unataka nini pia ni moja wapo wa ujenzi mzuri wa nidhamu ya pesa kwa sababu utajizuia dhidi ya matumizi ambayo sio ya msingi kwako na hayapo ndani ya bajeti yako kwa kipato chako na aina yako ya safari uliyonayo, kutojua nini unataka itakuingiza kwenye matumizi yasiyo sahihi kwa sababu kila utakachokiona kinavutia utahitaji kukinunua. Pesa isikuendeshe bali unatakiwa wewe ndio uipangie majukumu  na ukiona unalemewa basi jitahidi usiwe unatembea na pesa nyingi mfukoni hii ni njia nzuri pia ya kuitawala pesa kwa sababu huwezi kufanya manunuzi yasiyo na mpangilio, tunafanya manunuzi yasiyo na mpangilio kwa sababu tunakuwa na pesa au urahisi wa kuipata pesa. Usikumbushwe na matatizo bali jikumbushe mwenyewe kuwa kuna siku changamoto zitatokea na uhitaji wa pesa utatakiwa na sio usubiri matatizo yakufikie ndio uone umuhimu wa kutunza akiba kabla. 

Njia nyingine nzuri itakayokifanya uwe na nidhamu ya pesa wakati wote ni kupunguza matumizi yasiyo na lazima na kujenga utaratibu wa kununua vitu vya jumla kuliko vya reja reja  na pia kusimamia lengo kuu kwa msimu kwa mfano kila mwaka uwe na lengo kuu la kufanya hivyo kwa namna yoyote utajibana ubaki na pesa ya kufanikisha lengo hilo  maana ukitumia hovyo pesa basi uwe tayari pia kulipoteza lengo hilo 


Mwanasayansi Saul Kalivubha 

0652 134707

Thursday, 28 July 2022

NAMNA YA KUWEKA NIDHAMU YA PESA

NIDHAMU YA MATUMIZI SAHIHI YA PESA 

Matumizi ya pesa bado ni changamoto kwa watu wengi na matokeo yake ni hujikuta katika ukosefu wa pesa mara kwa mara na hii sio kwa waajiwa tu hata waliojiajiri kwenye mambo binafsi  bado hujikuta kwenye kipindi kigumu cha ukosefu wa pesa sio kwa sababu haikuwepo la hasha ni kwa sababu ilikuwepo lakini ikatumiwa bila kuzingatia matumizi sahihi kutokana na kipato. Ukipata muda tulivu ukajitafakari utagundua kuwa pindi upatapo pesa matumizi yako yanakuwa juu na hupungua kadri pesa inavyopungua yaani kwa lugha rahisi  ni kuwa nidhamu yako ya matumizi ya pesa inaongezeka kadri unavyoishiwa pesa. 

Pesa ni nguvu ya kihisia ambapo usipoitawala itakutawala yenyewe kwa kukupa maamuzi mengi na hapo utakosa utulivu hali ambayo itafanya upoteze nidhamu ya matumizi ndio maana mshahara ukiingia unaweza jikuta unafanya manunuzi bila kuangalia ukubwa wa gharama kwa sababu unajua pesa ipo lakini ukianza kusikia mfuko umepwaya ndio utarudisha makini wa matumizi kwa mfano mwanzo ulilipwa laki tano na ilipofikia mfukoni umebaki na laki moja ndio utaanza kuipogia mahesabu hiyo laki moja kuangalia kama itakufikisha mwezi mwingine, je kwa nini hukufikiria hivyo tangu ukiwa na laki tano? 

Nidhamu ya pesa ni kuheshimu pato lako kwanza na pili ni kuheshimu matumizi sahihi yaliyo ndani ya kipato chako kama ulipanga kununua kitu cha shilingi mia ndio itakuwa sawa kulingana na kipato chako basi fanya hivyo lakini ulinunua kwa shilingi Mia mbili ujue umekula na pesa ya siku fulani hivyo jiandaye siku hiyo kukosa pesa la sivyo iwe ni dharura ndio tumia lakini kama si dharura yatakiwa ujidhibiti dhidi ya matumizi ya pesa pale tu unapoipata, changamoto ya pesa ni kuwa ukitumia pesa ndogo unaona kawaida tu lakini mwisho wa siku ukijumlisha unakuta kama ungehifadhi ungekuwa mbali sana kifedha hivyo nidhamu ukianza na kuheshimu matumizi yako yaliyo ndani ya kipato chako utakuwa kwenye kiwango kizuri cha kuweka akiba. 

Nidhamu binafsi katika matumizi ya pesa inajengwa na lengo kuu ulilonalo la kesho hapo ndio utakuwa unatumia pesa ukikumbuka kesho hivyo utakuwa ukijikumbusha kila kabla ya matumizi ambayo si salama kulingana na kipato chako na utakuwa na nidhamu muda wote, lazima uwe na nidhamu au ukose nidhamu lakini ukubali kupoteza lengo kuu la kesho na njia nzuri nyingine ni kuigawa pesa yako kwa siku utagundua unaingiza shilingi ngapi kila siku na kisha angalia matumizi yako kila siku yanaendana na pato lako la siku? Kwa kuanzia na hapo utajirekebisha kimatumizi na utaheshimu matumizi sahihi ya pesa. 

Pesa ikiwa nyingi itakupa upofu uuamini kuwa huwezi kuishiwa hivyo kila matumizi yakujiayo kichwani utayafanya na hapo ndio mwanzo wa kutumia hovyo pesa  mpaka baadaye ikipungua ndio itakutoa upofu uone kuwa kuna hatari itokanayo na ukosefu wa pesa kwa sababu pesa uliyonayo haitoshi kukufikisha msimu mwingine wa pesa kumbe kuna kuna nguvu kubwa inatakiwa uwe nayo awali ili kudhibiti hisia za pesa zisikutawale. 

Kujua unataka nini pia ni moja wapo wa ujenzi mzuri wa nidhamu ya pesa kwa sababu utajizuia dhidi ya matumizi ambayo sio ya msingi kwako na hayapo ndani ya bajeti yako kwa kipato chako na aina yako ya safari uliyonayo, kutojua nini unataka itakuingiza kwenye matumizi yasiyo sahihi kwa sababu kila utakachokiona kinavutia utahitaji kukinunua. 


Mwanasayansi Saul Kalivubha 

0652 134707