Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu....nikupongeze kwa maamuzi yako ya kuamua kuwa mtembeleaji wa blog hii,nina amini hutobaki kama ulivyo....lazima mafunzo haya yatasogeza hatua zako mbele ....karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza sababu zinazopunguza uwezo wa kufikiri,.....na hili somo limekuja maalumu kwa sababu huwezi kufanikiwa nje ya fikra zako,pale ulipo ni matokeo ya kile unachokifikria....mambo gani yanapunguza uwezo wa kufikiria?...jifunze kwa nini rafiki yako hakuamini(urafiki)......
MAMBO YANAYOPUNGUZA UWEZO WA KUFIKIRI.
1.Mahusiano mabovu,..Hapa nazungumzia mahusiano ambayo yamekufanya kuwa mtumwa,haya ni yale mahusiano ambayo yanakufanya muda wote uyafikirie,...kufikiria mahusiano sio vibaya ,ila ubaya huja pale ambapo uliye naye kwenye urafiki amekutengenezea mazingira ya kutojiamini,..muda mwingi utakuwa unafikiria ufanye nini ili asiondoke na matokeo yake utajikuta unakwamisha mipamgo yako mizuri kwa sababu hutoipa nafasi kuifikiria mipango hiyo.
2.Marafiki,Jaribu kuchunguza kile unachokiwaza sana,kisha jiulize ,kwa nini unakiwaza sana?......fatilia marafiki zako wa karibu,wana mtizamo gani kwa kile unachokiwaza sana?.....kama unazungukwa na marafiki wenye uwezo mdogo wa kufikiri,usitegemee kuwa na fikra zaidi yao,.....
3.Ukosefu wa maarifa,Watu wasio na malengo hawpati shida katika kufikria kwa sababu hakuna wanachokitafuta,na mara nyingi watu ambao hawana malengo hupungukiwa pia na maarifa,....ukipata maarifa,lazima utaongeza uwezo wako wa fikra ili uyahamishe malengo hayo kuwa vitu kamili......kwa hiyo kadri unavyokosa maarifa ya kutosha kuhusu jambo flani ndivyo uwezo wako wa kurifikria jambo hilo unapungua.
4.Historia ya maisha yako,Changamoto ni kinu cha mafunzo ila kwa wasiofahamu hilo mara nyingi hujikuta kwenye falsafa hasi...watu hawa mara nyingi huamini kuwa waliyoptia yaliwapunguzia vigezo vya mafanikio,hivyo hawaoni sababu ya kufikiria mambo makubwa zaidi,muda mwingi hufikria waliyopitia.....
Hapo ulipo ni matokeo ya uwezo wako wa kufikiri,je upo sehemu sahihi?,kama sio hakikisha unapunguza mambo unayoyapokea kutoka kwenye mazingira yanayokuzunguka,.......jitengenezee uwezo mkubwa wa kufikri ili ubadilishe hivyo ulivyo.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha ,mmiliki wa label ya FIKIA NDOTO zako,
0652 134707.
Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Wednesday, 28 February 2018
Friday, 16 February 2018
KWA NINI RAFIKI YAKO HAKUAMINI?
Tarehe 22 FEBRUARY ni siku ambayo nasherehekea siku ya kuzaliwa kwangu......pamoja na furaha yote ya siku hiyo,huwa ni siku pia ambayo nimejiwekea utaratibu wa kukumbuka mambo ambayo yalitokea kwenye safari yangu ya maisha......kiufupi safari yangu kwa asilimia kubwa ilikuwa ya maumivu......hapo ndipo nakumbuka nafasi ya rafiki katika maisha yangu........karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo hili ni kutaka kutoa majibu ya kwa nini huna imani na rafiki yako?.....au kwa nini yeye hakuamini?.....hii ni vita kubwa sana ambayo inayumbisha urafiki wa watu wengi na kusababisha kifo cha urafiki..........karibu.
KWA NINI HUNA IMANI NARAFIKI YAKO?.......Sabubu za kwa nini humuanini rafiki yako zipo sawa na kwa nini yeye hakuamini.........hivyo ngoja nielezee sababu zinazo fanya ukose imani na rafikiyako.....kisha utazigeuzia upande wa pili.
1.HISTORIA YAKE.......kufahamu historia ya rafiki yako sio vibaya.na inaweza isiwe hatari kabisa kwa yeye kuptia historia hiyo...tatizo liko wapi?.........hadi wewe kukubali kuwa na urafiki na mtu unayejua historia yake,ni wazi uliamini kuwa kabadilika....lakini kubadilika kwake haina maana kuwa attaishi bila madhaifu yoyote yale........kosa lipo pale ambapo utaanza kuunganisha madhaifu yake ya kawaida na maisha aliyopitia.....ukiruhusu hali hiyo,nakuhakakishia,hutomuamini hata kidogo,utakuwa mtu wa wasiwasi tu muda wote......ukiona huna busara ya kubeba historia ya nyuma ya rafiki yako,au umejiaminisha kuwa bado hajabadilika......kuwa mbali.
2.HISTORIA YAKO,.....Usipokuwa mwenye hekima na busara,kile unachokitenda au umechotendewa au kuona wengine wakitendewa,kitakufanya uamini watu wote duniani wapo hivyo.....hali hii ukiiruhusu,itakufanya ujihami.....unajua madhara ya kujihami?.......KWANZA wewe mwenyewe utakuwa sio muaminifu,pili, rafiki yako utampa uhusika wako ....hutomuamini pia........kuna kipindi inabidi uishi bila hamasa za nje,hamasa ambazo ni za mawazo hasi.,,,zitakufanya uingiwe na ugonjwa wa kutoamini watu wasio na hatia............
Hapa nakumbuka utafiti wangu ambao niliufanya ili kugundua ni kwa namna gani watu hawana imani na marafiki zao sababu zilizosababisha hivyo........nilitumia marafiki wa jinsia tofauti,,,,wavulana kumi ambao nilwaulizwa wanajisikiaje ikitokea simu ya rafiki wake wa kike haitapokelewa au itakuwa busy(kutumika) pindi wakiwatafuta.......maatokeo yalikuwa hivi:
SITA walisema ,wakikuta hali hiyo,watahisi kusalitiwa,wawili walisema watajisikia vibaya tu.....wengine wawili wa mwisho walisema hiyo ni hali ya kawaida tu......kwa ufupi utafiti huo unaonyesha ni namna gani uaminifu umepungua ......nilivyofatilia zaidi kwa marafiki hao sita ndipo nikapata somo hili la leo......ndani ya sababu hizo mbili kuna sababu ndogo ndogo nyingi.....
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.....Mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO ZAKO.
06552 134707.
Friday, 9 February 2018
MAMBO MATANO MUHIMU KABLA YA BIASHARA.
Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,nikupe pongezi tu kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutembelea blog hi,hutobaki kama ulivyo....karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo hili nataka tujifunze mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukusaidia katika kuanzisha biashara yako.........mambo haya nimejifunza kupitia uzoefu wangu niliojifunza kwenye biashara ambayo nimeahi kuifanya na kwenye uwekezaji ambao tayari nipo naufanyasasa, ,pia mengine nimefanya utafiti kutoka kwa watu wengine........Karibu tujifunze.
Nafikiri kama wewe sio mfanya biashara ,basi utakuwa umewahi kuwaza kuwa mfanya biashara......na kwa sababu umeamua kusoma makala hii,kuna mambo mawili....moja,utakuwa umewahi kufanya biashara lakini haikukulipa,pili utakuwa una shauku kubwa ya kuanzisha biashara ......ni mahali sahihi,.......karibu tujifunze mambo hayo matano.
1.Kuwa makini na biashara zinazofika mtaani kuwa zinaingiza pesa haraka,......inaweza kuwa ni kweli ndio,ila mvuto huo usiwe ndio hamasa namba moja ya kukufanya uifanye bishara hiyo.....biashara inayosifika sana huwa haikawii kuchoka kwa sababu hufanywa na wengi,......kwa hiyo ifatilie kwa kina upate taarifa kamili za wakati huo kuhusu soko lake.....mfano wa biashara zilizosifika ni kilimo cha matikiti,mpunga,bodaboda na bajaji.......bodaboda na matikiti soko lake sio lile ambalo lilisifika miaka michache iliyopita,..limeshuka.....usiingie kwenye biashara bila kuwa na taarifa za wakati huo.
2.Jitahidi uiandike biashara kwenye daftari kabla ya kuanza kuifanya,........andika kuanzia mtaji ,soko lake na malengo ya wewe kuamua kuifanya biashara hiyo.....jipe kikomo cha kukamilisha malengo hayo........weka mikakati itayokufanya uyafikie malengo hayo kwa kupitia biashara hiyo......mfano mimi ni mkulima ambapo malengo yangu ni kumiliki ekari zaidi kumi hadi mwaka kesho kutoka kwenye chache nilizonazo.
3.Weka fungu la pesa,au anzakutafuta pesa ili ukamilishe biashara hiyo sasa uliyoiandika kwenye daftari,...jitahidi tu usitumie pesa yako yote kuanzia biashara,.....tumia akiba kuanzishia biashara.
4.Fanya maamuzi magumu,ishinde hofu ya kushindwa....ukimaliza maandalizi ,mara moja anza biashara.......ila hakikisha umetengeneza soko kabla ya biashara.....tambua ni watu wa aina gani umekusudia waipate bidhaa yako.
5.Fanya biashara kwa juhudi zako zote,kwa ubunifu ,hakikisha unafanya ambayo wengine hawayafanyi kwenye biashara iliyo sawa na wewe.....kuwa mvumilivu na mwenye subira,...biashara mara nyingi hainzi sawa na ulivyotarajia ...utasumbuka kidogo mwanzoni hadi kuja kufikia matarjio.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa label ya fikia ndoto zako.
See you at the top.
0652 134707

Friday, 12 January 2018
WAZO LA UJASIRIAMALI.
Karibu sana kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,....kwanza nikupongeze kwa kuanza mwaka mpya vizuri,nafahamu kuna mapito mengi,mengine yalikuumiza,mengine yalikupa raha,ila yote na yote kila ulipopita,kuna kitu ulijifunza.........kwa kuanza na mwaka huu ,nimeona vyema nikushirikishe somo letu zuri ambalo kwa sehemu nina amini litakufanya uwe wa tofauti.
KUSUDI LA SOMO.
Somo letu la leo ni wazo la ujasiriamali,somo hili litatupa hatua za kufanya wazo letu lizae matunda,inawezekana kwa muda mrefu umekuwa ukiweka mawazo kuhusu biashara /uwekezaji flani.ila mwisho wa siku unaishia kuwaza tu,wazo lisilotekelezeka ,huwa ni wazo sisilo la kijasiriamali,.....wazo la kijasriamali ni nini?.....karibu tujifunze.
WAZO LA KIJASIRIAMALI.
Hili ni wazo ambalo mwisho wa siku ,linatekelezwa,...wazo la kijasriamali huwa lina hatua zake ili liwe na sifa ya kutekelezeka,..wazo linapotekelezwa ,lazima lilete matokeo,matokeo sio lazima yawe na faida tu,yanaweza kuwa na hasara pia......ila faida ya kuwa na wazo la kijasiriamali ni mafunzo tunayoyapata(iwe ni faida au hasara).............jiulize wazo lako ni lipi?, umelipa hatua zipi?
HATUA ZA WAZO LA KIJASIRIAMALI.
Wazo la kijasriamali,lina lina hatua zake tatu,ambazo ni kama zifatazo;
1.WAZO,hii ni hatua ya kwanza,lazima uwe na wazo,wazo una amini litakufikisha uendapo,wazo hilo inatakiwa litanguliwe na kujitambua........ukijitambue wapi unataka kwenda,temgeneza wazo la kuongoza safari yako,.....mfano wazo la kilimo,ufugaji ,biashra flani,elimu nk.....wazo lipi litakufikisha uendapo?......hapa namaanisha nini ufanye ili ufikie unapotaka kwenda?
2,MAANDALIZI: Ukisha kuwa na wazo tayari,anza maandalizi.....maandalizi ni pamoja na kuweka mikakati itayosaidia kuliwezesha wazo lako,.....fanya tafiti za kutosha,jitahidi utambue uhusiano uliopo kati ya wazo lako na mazingira,,,,hii itakusaidia kutambua kama wazo lako hilo litasaidia kutatua chngamoto za watu?...... wazo lako hilo litakupa uhuru wa kujitegemea kuliko kutegemea?
3.UTEKELEZAJI.
Huu ni muda ambao ni wa utekelezaji tu,.....kosa ambalo wengi tunafanya ni kuchangamya vipindi,....kipindi cha utekelezaji ndio tunafanya maandalizi......mara nyingi watu wanao changanya vipindi,huwa wanaishia kupanga tu...........MUHIMU TU....kumbuka kila hatua lazma utakutana na hofu ,jitahidi tu kupunguza mazingira yenye kukupa hofu,.....hofu ndio chanzo kinachofanya watu waishie kwenye hatua ya kwanza.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa fikia ndoto zako label.
mawasiliano: 0652 134707.

Sunday, 10 December 2017
DAFTARI LA MALENGO
Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya,kwa wale wagonjwa,Mungu yupo kwa ajili yetu,atatuponya,tusichoke kuzungumza naye.......Karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze kuhusu daftari la malengo,somo letu litakuwa katika sehemu kubwa mbili,maana ya daftari la malengo na umuhimu wa daftari la malengo.......karibu tuendelee.
MAANA YA DAFTARI LA MALENGO.
Daftari la malengo nafikiri ni neno maarufu ila lenye kutumika mara chache sana kwa watu,daftari la malengo ni daftari ambalo linatumika kuandikia malengo na jinsi ya kuyafanikisha hasa kwa kuzingatia mipango inayoonyesha namna ya kukamilisha malengo hayo..................kabla ya kuhamia sehemu ya pili,tujifunze sehemu muhimu zinazotakiwa uwe nazo kwenye daftari lako la malengo.

- Anza na kurasa chache kwa kuandika malengo yako na kikomo cha malengo hayo(deadline)
- Kurasa zinazofata andika mipango ambayo unatakiwa kuifanya ili uweze kufikia malengo yako,mipamgo ni sehemu ambazo zinatakiwa kukamilishwa ili zisaidie kutimiza malengo hayo....mfano,una lengo la kununua gari,lazima uwe na mipango ya kufanya ili uweze kupata pesa inayotakiwa.
- Kurasa baada ya mipango,andika bajeti ,,,,,bajeti itakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa na yenye uhusiano mzuri wa malengo yako.....
UMUHIMU WA KUWA NA DAFTARI LA MALENGO.
Zipo faida nyingi za kuwa na daftari la malengo,ila faida kubwa sana ni kutimiza malengo yako.....daftari la malengo linasaidia kukupa kifungo ,kifungo ambacho muda mwingi kitakufanya uwazie malengo yako,na kitakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa,maana utakuwa na hofu ya kutumia pesa iliyo nje ya bajeti yako.
Makala hii imeandikwa na mkurugenzi wa label ya fikia ndoto zako.....Saul Kalivubha.
0652 134707.
Tuesday, 24 October 2017
JITENGENEZEE KESHO YENYE MATUNDA.
Habari za kwako rafiki ambaye tumekuwa pamoja kwenye darasa hili la maisha ,kwa lengo la kusaidia kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,karibu tujifunze.
Kusudi la somo.
Leo nataka tujifunze namna tunavyoweza kutengeneza kesho yetu iliyo ndani ya ndoto zetu,somo hili kwa bahati mbaya wengi wanalipata wakiwa tayari wamekosea sana kiasi kwamba kuanza safari upya inakuwa ngumu ,hivyo wanaamua kuendelea na safari isiyo ya aina yao,...tatizo kubwa ni kwamba mazingira yapo kinyume na kesho za watu wengi,hivyo kulipata somo hili na kuliishi,inahitaji ujasiri wa kutosha ,karibu tuendelee(tengeneza soko lako kabla ya safari)
ITAMBUE KESHO YAKO.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kuandaa kesho yako,bahati mbaya kwa upande wa Afrika ni watu wachache sana ambao wanafanikiwa kutambua kesho yao mapema,na wanaofanikwa kufanya hivyo ,wanashindwa kuifikia kwa kukusa maandalizi,kwa wenzetu wazungu ,hali ipo tofauti,wao hutambua kesho yao wakiwa na umri mdogo na wanaanza kutengeza mazingira mapema ya kuja kuiishi kesho yao..........Unafikiri kwa nini wao wanaweza?
Bill Gate akiwa na umri mdogo sana,aligundua kuwa anapenda sana kuchezea Computer,alichofanya alitafuta rafiki wa aina yake ambapo walitenga muda wa kuwa wanajifunza zaidi kuhusu computer kwenye Library ya shule,....akiwa na ndoto ya kumiliki company,alitumia muda mwingi kuwa kwenye mazingira yaliyomfanya awe mpya kila siku kwenye kile akipendacho,Je wewe hadi sasa hujagundua unapenda nini?,Je unakuwa mpya kila siku kwenye eneo lako?......Unafikiri tatizo ni nini?
HALI YA KUSHANGAZA.

- Watu wengi wanaifahamu mapema sana kesho yao,na wanajua kabisa jinsi ya kufanya ili waje kuishi kesho hiyo,ila tatizo ni uwezo wa kuthubutu unakuwa mdogo,...kama wewe unataka kesho umiliki kampuni,una maandalizi gani sasa?.....jaribu kutengeneza uhusiano wa kile unachokifanya sasa kiwe msaada wa kusaidia ndoto zako za kesho....kuna gharama,ila lazime uzilipe ili kuweza kuifikia kesho yako.
- Watu wengi wa wengi tunakwepa maumivu kwa kuyahamishia kesho,....kuliko mtu kuanza maandalizi mapema ya kuandaa kesho ya malengo yake,anaona afanye maandalizi hayo kesho,unachokwepa leo nini?......kila siku ifanye iwe ya maandalizi ya kesho yako.
- Watu wengi tunataka tuifikie kesho iliyo kamilika.....Hapa nakumbuka mwanafunzi mmoja aliwahi kuniambia,safari yake ya maisha itaanza baada ya kumaliza chuo,swali la haraka likanijia,....Atamaliza na umri gani?,kisha nikajiuliza,ina maana huyu mwanafunzi leo yupo anapoteza muda?,maana bado hajaanza safari ya maisha.
Kesho yako inaanza pale ambapo tayari umejitambua upo kwenye safari ya aina gani,kama safari yako inaenda kwenye kumiliki nyumba za kifahari,anza kuzitengeza leo,,,,,huwezi kuzipa ta nyumba hizo kwa siku moja,ujenzi wake unaanza leo,kila siku jitaahidi unapata maarifa ya kutosha kuhusu hizo myumba unazo zihitaji.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO zako.
See You At The Top.
0652 134707
Friday, 13 October 2017
TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.
Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa pumzi ambayo amekuwa akitupatia bure,karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Somo letu la leo linahusu umuhimu wa kutengeza soko kabla ya kuanza safari yoyote ya maisha,....Nafikiri wazo la haraka unaposikia neno soko ni biashara,lakini hapa nina maana zaidi ya soko la biashara,,,kabla ya kuendelea na somo jifunze kwanza somo hili (kwa nini hupigi hatua?).....karibu tuendelee.
MAANA YA NENO SOKO.
Kwa haraka ,soko ni sehemu ya kufanyia mauzo ya bidhaa/kitu flani,soko ni kipimo kizuri cha ubora wa kitu flani,mfano,soko la bidhaa flani likishuka,ni wazi kuwa ubora wa bidhaa hiyo unakuwa umeshuka.........Kwa maana pana zaidi na ambayo nataka ndio iwe sehemu kubwa ya somo letu ni hii,SOKO pia ni kipimo kizuri cha huduma yako,huduma yako inapimwa thamani sokoni,ubora wa huduma yako ndio unafanya soko lako liwe juu au chini.
KWANINI UTENGENEZE SOKO KABLA YA SAFARI?
Nafikiri umewahi kuona au kusikia majina ambayo yalifanya vizuri,ila hadi sasa hivi huyasikii tena,...tatizo ni nini?
Pia utakuwa umewahi kushuhudia mtu flani akianza kwa kasi kubwa na kwa ubora wa juu,ila baadae anapotea,tatizo ni nini?
Pamoja na sababu myingi zinazochangia hali hiyo,ila sababu nyingine kubwa ni watu wengi wanaanza safari bila ya kuandaa aina gani ya watu ambao watawafikia na changamoto zake,unapofahamu huduma yako itafikia watu wa aina gani (soko),itakusaidia uanze maandalizi ya kutosha kuhusu ubora wa huduma yako itayokidhi mahitaji ya watu hao kwenye vipindi tofauti tofauti .
Mazingira yanabadilika,mahitaji pia yana badilika,je umejipanga kuibadilisha huduma yako ili iweze kuendana na mabadiliko hayo?
Kabla ya safari ,hakikisha unatambua vizuri soko lako,tena utengeneze na soko mpya litalopatikana kulingana na mabadiliko yatayotokea,ukiendelea kutoa huduma ya aina moja muda wote,ubora wake utashuka kama ikitokea jamii imebadilika ila wewe hujabadilisha aina ya huduma yako.....TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
mkurugenzi wa fikia ndoto zako label

Subscribe to:
Posts (Atom)