Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani wewe hapo ni mzima wa afya,kama ni mgonjwa usijali,Mungu yupo kwa ajili yetu wote.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya kumi ya urafiki ambayo ni UKWELI ,ila kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukapitia na kujifunza kwanza siri ya tisa ya urafiki(SIRI YA TISA YA URAFIKI).
SIRI YA KUMI YA URAFIKI (UKWELI).
Kwenye urafiki kuna kuwekana wazi mambo,ila kabla ya kuweka wazi mambo yako kwa rafiki yako lazima kwanza uwe umejihakikishia uaminifu wa kutosha ,ila wakati mwingine kuna watu wapo kwenye urafiki kwa kuficha ukweli,wanatumia uongo kutengeneza ukaribu wao....je hii ni sahihi?
Wanasaikolojia wa mambo ya mahusiano wanazungumza kwamba ...Watu wanatafuta wasiyoyafahamu,hawana shida na wanayoyafahamu,,,hii tafasiri yake ni kwamba rafiki yako anatafuta mambo ambayo hayafahamu kutoka kwako,inaweza kuwa umemdanganya jambo fulani,siku akilifahamu lazima sura ya urafiki wenu ubadilike,...jifunze kuwa mkweli.
Ni bora kumficha mtu jambo kuliko kumdanganya,sababu za kumficha mtu jambo zinaweza kuwa zina maana kubwa kuliko sababu za kumdanganya mtu,,,,,kumdanganya maana yake umemwambia ukweli wenye hila ndani yake,umetafuta kuaminiwa kwa njia isiyosahihi.
Ukiona rafiki yako amekukwepa kwa sababu umemwambia ukweli,jua huyo sio mtu mzuri kwako,maana ukweli una thamani kubwa sana kwenye urafiki wa kweli,urafiki ambao una lengo la kufikia mafanikio makubwa.
Tatuzo ukisha anza na uongo tu kwenye urafiki wako,itakufanya kila siku uendelee kutengeneza uongo wa kudumisha uomgo wa mwanzo....urafiki wa aina hiyo una umuhimu gani?, ukijiona mjanja wa kudanganya ,tambua thamani yako inashuka,pia unapoteza muda wako kudanganya na kuendeleza uongo wako.
Kitabu cha SIRI ZA URAFIKI kinaelekea kuwa tayari,utakipata kwa mawakala wa fikia ndoto zako....
See you at the top.
Scientist Saul kalivubha.
0652 134707
Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Sunday, 16 July 2017
Monday, 10 July 2017
SIRI YA TISA YA URAFIKI
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa uzimab wake kwangu ,pia ni imani yangu kuwa wewe ni mzima........karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Tunaendelea na somo letu la siri za urafiki,leo ni siri ya tisa ambayo ni mipaka ya ufahamu,...kabla yakuendelea na somo letu hili,ni vyema ukajifunza kwanza siri ya nane ya urafiki(SIRI YA NANE).,karibu tuendelee.
SIRI YA TISA YA URAFIKI(MIPAKA YA UFAHAMU).
Katika urafiki ni jambo la kawaida sana kufahamu habari za rafiki yako,swala hili ni zuri sana ikiwa unataka kufahamu habari hizo kwa lengo la kudumisha urafiki,ila kuna habari zingine za rafiki yako zinaumiza,kama hauna ujasiri,badala ya urafiki kuimarika,utavunjika......kabla ya kuanza kuzifatilia habari za rafiki yako jitahidi kufahamu haya.
- Weka mipaka,hakikisha unafahamu mambo yenye fada tu katika ujenzi wa urafiki.
- Kuwa makini na chanzo cha habari, sio kila chanzo cha taarifa za rafiki yako ni chanzo sahihi.
- usifatilie habari za rafiki kama kumpeleleza,akijua urafiki wenu utapoteza uaminifu,kuwa mpole na taratibu tu utafahamu mengi kuhusu yeye.
- Fanyia kazi mambo utayo yafahamu kwa rafiki yako kwa lengo la ujenzi na sio kwa leng la kumuhukumu rafiki yako.
Mwamdishi mmoja wa mambo ya saikolojia aliwahi kuandika kanuni moja muhimu sana ,kanuni hiyo ni hii "Msongo wa mawazo(Stress) unaongezeka,kila ufahamu unapoongezeka"
Kanuni hii inasaidia kupunguza kufahamu mambo yasiyokuhusu,watu wengi kwenye urafiki wanaishi kwa mawazo kwa sababu tu walifatilia mambo yasiyo wahusu ya rafiki zao.
Kuna mambo sio lazima uyafahamu kutoka kwa rafiki yako,utaumiza kichwa bure tu,tena kibaya zaidi hakuna uwezo wa kuyabadilisha mambo hayo,tena kuyafahamu kwako hakuna faida yoyote kwenye uraki wako .....
See you at the top.
Saul kalivubha
0652 134707.
Sunday, 2 July 2017
SIRI YA NANE YA URAFIKI.
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. ......Karibu sana kwenye muendelezo wa somo letu la urafiki, nina imani kuna kitu unajifunza. ..karibu.
LENGO LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nane ya urafiki kulingana na mpangilio wangu, siri hiyo ni Jichunguze tabia yako. ... .Unaweza pitia kwanza SIRI YA SABA, kisha uje tuwe wote. .....karibu tuendelee.
SIRI YA NANE (JICHUNGUZE TABIA YAKO ).
Urafiki unapitia mazingira mengi sana, kila mazingira huwa yanahitaji style (mfumo ) wa kuishi ili kuhakikisha urafiki unaendelea na thamani yake.Ila kuna kipindi mtu anaona rafiki yake kabadilika tabia, amekuwa na tabia mpya ambayo hapo nyuma hakuwa nayo.
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.
Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134 707.
0

- Je umewahi kukutwa na hali hiyo?
- Urafiki wako ulikuwa na sura gani baada ya hali hiyo?
- Unafikiri chanzo chake ni nini?
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.
Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134 707.
0
Sunday, 25 June 2017
SIRI YA SABA YA URAFIKI
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania hadi sasa ,hongera sana kwa kuwa na afya njema,kwa wale wagonjwa poleni sana ila Mungu niwetu sote.
KUSUDI LA SOMO.Leo nataka tuendelee na somo letu la urafiki,kabla ya kuendelea na siri ya saba, jifunze kwanza ( SIRI YA SITA),Kisha tuendelee na siri ya saba ya urafiki ambayo ni tasmini ya uchaguzi wa rafiki,.....karibu tujifunze.
SIRI YA SABA YA URAFIKI(TASMINI YA UCHAGUZI).
Kuwa na rafiki flani ni ni matokeo ya uchaguzi uliofanya,hakuna kulazimisha kwenye mambo ya urafiki,huwa ni hiari ya muhusika,je uchaguzi wako una matokeo gani?
Kila uchaguzi lazima uwe na matokeo,matokeo ya uchaguzi ndio sehemu ambayo tunaitumia kupima kufanya evaluation(tasmini) ya usahihi wa mtu katika uchaguzi wake,....hii ni sehemu ambayo kila mtu anapaswa kuifanya yeye binafsi, je nini kinafata baada ya tasmini ya matokeo?
Matokeo ya uchaguzi wa rafiki yana sehemu ya kuvumilikika ambayo ni moja ya madhaifu ya binadamu, ila matokeo yanaweza kuwa pia hayaruhusu urafiki uendelee,hapa lazima uchukue maamuzi magumu,bila hivyo itakuwa ngumu kwako kufikia ndoto zako......
Zoezi la tasmini ya matokeo ya urafiki huwa ni ngumu kidogo, maana kuna watu wanachukua maamuzzi magumu kwa kukwepa changamoto za urafiki tu ,kwa hiyo inahitaji umakini sana katika zoezi hili,,,,,,
Jiulize swali hili,....matokeo ya uchaguzi wa rafiki uliyrnaye yana endana na ndoto zako?,kama sio ,unafanya nini kwemye urafiki huo?
Habari ya kusikitisha kwenye urafiki ni kwamba,watu wengi wanaweza kugundua hawapo kwenye njia sahihi,ila wakwa wanajifariji ,mwisho wa siku wanafanya maamuzi magumu tayari walisha poteza thamani yao,,,,,,,fanya tasmini,chukua maamuzi sahihi.....
See you at the top
Scientist Saul kalivubha.
0652 134707
Sunday, 18 June 2017
SIRI YA SITA YA URAFIKI
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,maana nina imani kuwa na wewe ni mzima,.....karibu tujifunze.
Kusudi la somo.
Leo ni muendelezo wa siri za urafiki,tunaendelea na siri ya sita ya urafiki ambayo ni utatuzi wa migogoro,kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukajifunza kwanza SIRI YA TANO ,Karibu tujifunze.
UTATUZI WA MIGOGORO YA URAFIKI.
Jambo la kufahamu kwenye urafiki ni kwamba ,unakutana na mtu ambaye hujazaliwa naye,ana madhaifu yake na pengine ana historia yake ya maisha tofauti na yako.......lazima kuna migogoro itatokea tu ndani ya urafiki,,,,,jaribu kujibu maswali haya kabla ya kuendelea mbele......je umewahi kuingia kwenye mgogoro na rafiki zako?,ulifanya maamuzi gani ?.baada ya maamuzi hayo urafiki wenu ulipata sura gani?
Migogoro kwenye urafiki ni muhimu sana kwani ni dalili ya kuonyeha hali ya kutokuwa sawa sehemu flani,ila inaweza kuwa na madhara ya kudumu kwa wahusika endapo watashindwa kutambua sababu za utokeaji wa migogo hiyo,
Uwezo wa utatuzi wa migogoro ya urafiki bila kuharibu thamani ya muhusika ndio kipimo kizuri cha uwezo wa uendeshaji wa urafiki.
Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye utatuzi wa migogoro.
- Kabla ya maamuzi yoyote hakikisha unajua chanzo cha tatizo .
- Usipende kuonekana mshindi,ili kumudu hili hakikisha unatawala hisia zako za hasira ili usifanye maamuzi yenye msingi wa hasira.
- Kama kosa lipo kwa rafiki yako,vaa uhusika ili upime yeye angefanya maamuzi gani juu yako.
- Usipende kutumia ushauri wa watu wengine katika kutatua mgogoro unaokuhusu wewe.
- Hakikisha unajua tafasiri ya kila changamoto kwenye urafiki wako,ili ufanye maamuzi ambayo hayana majuto.
Kumbuka tu ili uweze kufikia ndoto zako ni muhimu uwe kwenye system ya marafiki waliobeba kusudi lako,ila kuwa na rafiki ambaye kabeba kusudi lako sio tafasiri ya kutokuwa na migogoro.
See you at the top.
scientist SAUL KALIVUBHA.
0652 134 707.
Sunday, 11 June 2017
SIRI YA TANO YA URAFIKI
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa afya yangu pamoja na wewe. ....karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo la leo ni kuendelea na sehemu ya tano ya siri ya Urafiki. ..ni vyema ukajifunza sehemu ya nne SIRI YA NNE kisha uendelee na siri ya tano( SIRI YA NNE)..... lengo la kufundisha urafiki ni kutaka tufahamu jinsi ya kuishi na marafiki kwa lengo la kufikia ndoto zetu ...maana mafanikio yako yapo kwa rafiki yako. ...karibu.
SIRI YA TANO YA URAFIKI.
Siri ya tano ya urafiki ni mawasiliano .Kwenye mawasiliano tuangalie kwenye upande mmoja tu. jinsi mawasiliano yanavyoweza kuvunja urafiki. ....nafikiri utakuwa tayari umeshuhudia urafiki ukivunjika kwa sababu ya mawasiliano. ....au inaweza kuwa umekutwa na tatizo hili la kupoteza marafiki kwa kigezo cha mawasiliano. ....
Mawasiliano yanaweza kavunja urafiki kupitia sehemu hizi.

- Mawasiliano mabovu, ..hapa nina maanisha kiwango cha chini cha mawasiliano au mawasiliano ambayo hayana hisia za Upendo. ....kila mazingira yana aina yake ya mawasiliano na kiwango chake, ukiwa kwenye mazingira yenye kuhitaji mawasiliano kwa wingi ila wewe ukafanya chini ya kiwango , urafiki utakuwa unaelekea kwenye hatari ya kuvunjika. ....jitahidiutambue aina ya urafiki uliyonayo, mazingira mliyopo. .ili ufanye mawasiliano yanayostahili.
- Mawasiliano hupoteza thamani ya habari, ...utafiti wa kisaikolojia unaonyesha kwamba habari inavyozidi kupita mikononi kwa watu wengi ndio inavyozidi kupungua uhalisia wake, ila kuna watu bila kufanya utafiti wa kina wamekuwa wakifanya maamuzi ya kudumu kwa kupitia taarifa imeyopitia mikononi kwa watu wengi. ..hali hii imefanya watu wengi kupoteza marafiki .....fanya tasmini kabla ya maamuzi, unavyozidi kuwa mbali na chanzo cha habari ndivyo ukweli wa taarifa unavyozidi kupungua. .....
Seeyou at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652 134 707)
Wednesday, 31 May 2017
SIRI YA NNE YA URAFIKI
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya elimu ya maisha kwa lengo la kufikia ndoto zetu,nashukuru mungu kwa kuendelea kunipigania mimi pamoja na wewe...........karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nne ya urafiki ambayo ni uvumilivu,ili tuwe pamoja jifunze kwanza SIRI YA TATU kwa kubofya hapa.SIRI YA TATU,..........ikumbukwe tu rafiki ana sehemu kubwa sana kwenye ndoto zetu,hii ndio sababu ya mimi kufundisha somo hili.
SIRI YA NNE YA URAFIKI(UVUMILIVU).
Uvumilivu ni uwezo wa kuzitawala hisia zitokanazo na mambo yasiyo pendeza,hisia ambazo zikiruhusiwa zinaweza kuwa hanzo cha matokeo hasi(negatives effects).........kwenye urafiki pia kuna mambo ambayo yanahitaji kuvumiliwa,ndani ya urafiki kuna mambo yasiyopendeza yenye lengo la kuimarisha urafiki,mtu usipo kuwa mvumilivu unaweza kuwapotezamarafiki wengi sana wasio na hatia..............
Uvumilivu katika urafiki unahitajika sana hasa kwenye hali kuu mbili zifatazo:

- MADHAIFU;watu wengi wanaingia kwenye urafiki wakiwa na picha ya madhaifu machache waliyo yaona kabla ya kuanza urafiki,ila kuna madhaifu mengine ya ndani ambayo huwezi kuyaona hadi uingie kwenye urafiki,......usipokuwa mvumilivu ,madhaifu haya ya ndani yana nguvu kubwa ya kuvunja urafiki.
- CHANGAMOTO:Changamoto ni moja ya sehemu muhimu sana ya urafiki,ni sehemu ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu,pia ni sehemu ambayo inahitaji matumizi ya hekima na busara,maanakila changamoto ina jambo la kufundisha kwenye urafiki wako.....kuna usemi mmoja unasema "Kama upo kwenye urafiki usio na changamoto yoyote ile,kaa chini ufikirie tena mara ya pili"
See you at the top.
Scientist Saul kalivubha.
(0652 134707)
Subscribe to:
Posts (Atom)