Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Thursday, 17 October 2019
NGUZO ZA MAAMUZI SAHIHI,JIFUNZE.
Na Mwanasayansi Saul Kalivubha.
Habari ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako hii pendwa na karibu tena katika safu hii ambayo tunajifunza mambo chanya kwa ajili ya kuitafuta hatua mpya zaidi ,karibu tujifunze.
Maamuzi sio neno geni hata kidogo na kila siku lazima kila mtu afanye maamuzi mara nyingi sana japo idadi ya maamuzi haziwezi kuwa sawa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, maamuzi ni machaguzi hivyo huwezi kuamua ukiwa na jambo moja mkononi lazima uwe na mambo mawili au zaidi mkononi ndipo ufanye maamuzi ya kubaki na jambo moja kati ya mengi,je una uhakika gani kama maamuzi unayoenda kuyafanya ni sahihi? Kuna nini nyuma ya maamuzi yako? .
Tumesikia watu wengi sana wakijilaumu kwa maamuzi yao ya jana na kujutia kana kwamba wangalijua mapema wasingefanya maamuzi yale hii ni wazi kuwa maamuzi yao sio sahihi japo kwa muda ule wanaamua walijiona kuwa wapo sahihi.
Tuangazie kidogo juu ya nini kinafanya watu wafanye maamuzi na kwa nini majuto yanafuata baada ya maamuzi.
Kwa nini tunafanya maamuzi? Tunafanya maamuzi kwa sababu mambo tunayokutana nayo hatuwezi kwenda nayo yote hivyo lazima tuamue ili kuchagua machache yanayotufaa na kuacha yasiyo tufaa, maamuzi yoyote yale lazima kuna chaguo moja ulilipenda ndio maana ukaamua kulichagua chaguo hilo.
Kwa nini ulizwe na chaguo lako mwenyewe?.Nyuma ya maamuzi yoyote yale kuna ufahamu,hisia,msukumo wa watu na muda.Hivi vitu vinne ndio hasa vinaoongoza maamuzi yetu hivyo unapoona unajutia maamuzi yako lazima kuna moja kati ya ufahamu wako,msukumo wa watu,hisia au muda lilikuvuruga.
MUDA, tunapokuja suala la muda tunaangazia sana kuchelewa yaani mtu anapoingiwa na hofu ya kuchelewa huwa anajikuta akifanya maamuzi bila kuyafikiria maamuzi yake kwa utulivu kwani lengo lake kubwa inakuwa ni kutaka tu awahi hivyo atatumia vigezo vichache katika kufanya machaguzi.
Mara nyingi maamuzi ambayo yanafanywa kwa kukimbizana na muda huwa ni sahihi kwa muda ule mtu anapoyafanya lakini baadaye anakuja kuyajutia maamuzi yake.Usikubali kufanya maamuzi na hisia za kuchelewa utakosea hivyo ni vizuri utafute utulivu ndio kisha ufanye maamuzi.
Msukumo wa watu, hizi tunaziita kelele za nje zinazokusukuma ufanye jambo fulani , sio kwamba hutapswi kutosikiliza kelele za nje la hasha ila unachopaswa ni kutofanya maamuzi kwa sababu umepigiwa kelele,kelele za nje ni kama upepo uvumao ambapo ukikukuta huna msimamo utayumba na kujikuta unaenda hata usipopotaka , kwenye mahusiano na biashara suala la kupigiwa kelele huwa lipo huu sana na wengi waliofanya maamuzi kwa kusukumwa na kelele walipotea, jitafute wewe ni nani na unataka nini ndipo ufanye maamuzi.
HISIA ,Kila mtu ana msukumo wa hisia ndani yake kwani hisia ni sehemu ya ulinzi pale tu zinapotumiwa vizuri, zipo hisia za aina nyingi kama vile hisia za hasira,hisia za kupenda,hisia za huzuni,hisia za hofu nakadhalika, sasa hisia zikiwa juu huwa zinaficha negative side effects (madhara hasi) na kukuaminisha kuwa utafurahia matokeo ya maamuzi unayotumwa kufanya na hisia, mtu mwenye hasira akifanya maamuzi huwa anajiona mwenye furaha kwa muda kisha hasira ikimuachia tu anabaki na majuto , hivyo unatakiwa kufanya maamuzi bila kusukumwa na hisia.
UFAHAMU, ufahamu wa mtu kuhusu jambo fulani ndio unamuongoza kufanya maamuzi yanayohusu jambo hilo ,kwa mfano wanafunzi wanaochagua kozi za kusoma kwa kutumia ufahamu wa haraka na baadaye wanakuja kuona kuwa wamekosea baada ya ufahamu wao kuongezeka, vivyo hata katika mahusiano,biashara na mengineyo watu wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kutumia ufahamu mdogo ,hivyo inashauriwa kutafuta maarifa ya kutosha kabla ya maamuzi fulani .
Sunday, 14 July 2019
MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.
Habari ndugu na mfuatiliaji wa makala zetu za blogu yako pendwa ya FIKIA NDOTO ZAKO,ikiwa imepita muda wa kutosha bila kukuandikia makala katika blogu yetu hii ni kwa sababu tu ya uboreshaji ambao ulikuwa ukiendelea kwa lengo la kukupatia wewe msomaji na mwanafunzi maarifa yaliyo bora,karibu .
Somo letu la leo ni rahisi kama utalipa muda wa kutosha kalitafakari na ni somo gumu kama utapita juu juu, hivyo inahitaji utulivu wa hali ya juu sana.
Ufahamu ni moja ya eneo muhimu sana ambalo ndio linakutofautisha wewe na mimi ,wewe na rafiki yako ,wewe na mnyama kama vile sungura n.k,kumbe ufahamu ndio muongozo wa kwanza wa maamuzi yetu na ndio gereza limelofunga hatua zetu.
Ufahamu unaanzia mbali sana pindi mtoto anapozaliwa hadipale ambapo mazingira yatamuhitaji atafute mwenyewe (kujitegemea) ,hadi kufikia umri wa miaka 9 mpaka 10 ufahamu wa mtoto unakuwa ukiamini kwa 100% muongozo wa mzazi /mlezi wake ndio maana mtoto wa umri huo anakuwa haamini kama kuna mtu zaidi ya baba /mama yake ,hata akutane na kitu cha kutisha namna gani ambapo hata kina nguvu zaidi ya mzazi wake bado atakitishia kitu hicho kwa kumtaja baba yake au mama yake akiamini hicho kitu kitaogopa na kumuacha,yote hiyo ni kwa sababu ufahamu wake ndio unamtuma hivyo ,je ufahamu wake ni sahihi?
Inawezekana ukawa ;
1.Unaabudu katika dini/dhehebu fulani kwa sababu unaamini uliowakuta wakifanya hivyo hawawezi kukosea kuwa katika sehemu hiyo wanayoabudu.
2.Ulichagua kozi fulani kwa sababu waliokushauri uliwapa thamani ya juu kuwa hawawezi kukosea katika machaguzi.
3.Kwa sababu unaona watu wanafanya ndio maana ufahamu wako unakutuma kuwa hilo jambo ni sahihi n.k
Je unawezaje kuhakikisha kuwa ufahamu wako ni sahihi?
Tukiachana na kupima ufahamu ulinao kuhusu dini/imani/kanisa/msikiti ambapo ni somo ndefu na linalohitaji utulivu wa juu zaidi, tuje katika mbinu za pamoja za kupima ufahamu ulionao kwa ujumla ,kwanza kabla ya mbinu hizo tutambue ya kwamba ufahamu kwa asilimia nyingi unatokana na mazingira yanayokuzunguruka kama vile marafiki na wazazi/walezi n.k, pia ufahamu unategemea na umri.
Kadri mazingira yanavyobadilika na umri unavyosogea ndipo unazidi kuona kuwa kuna mambo zaidi ya vile ulivyokuwa ukifahamu na utagundua kuwa ulikuwa unafanya makosa pasipo kufahamu kwa sababu ufahamu wako ndipo ulipoishia pale,kwani maamuzi yetu ni ,matokeo ya ufahamu wetu ulivyo.
MBINU ZA KUPIMA UFAHAMU WAKO.
1.Kwanza jitambue wewe ninani,sio jina lako wala wapi unaishi ,jitambue kwa nini ulizaliwa? utapata sababu ambayo ndio kusudi la wewe kuzaliwa,sababu ya kuzaliwa kwako unaweza pia kuangalia kipi unaona hakiendi sawa yaani kuna namna unasukumwa kutaka kuweka mfumo sawa,hapo kuna kusudi lako na kipaji chako ,ukishajifahamu wewe ni nani tayari utaanza kutafuta ufahamu wa kutosha kujihusu wewe na safari yako.
2.Makosa yetu,kupitia makosa yetu ni njia nzuri sana ya kupima ufahamu wetu,mfano umetumia ufahamu wako kufungua simu ukashindwa ni wazi kuwa ufahamu wako bado, kuna zaidi ya unavyofahamu,unapoingia kwenye makosa kaa chini ujitafakari ni lazima tu kuna jambo hulijui ndio maana ukakosea hivyo litafute .
3.Kaa chini uchunguze kwa nini unaamini hivyo? ni kwa sababu uliambiwa hivyo na watu au ni kwa sababu umezaliwa na kukuta watu wakifanya hivyo,kwa mfano wengi tumekuwa tukiwa na ufahamu kuwa shule ndio chanzo cha utajiri kwa sababu tuliambiwa hivyo ,kila siku tunatafuta ajira tukiamini kuwa tukipata tu tutaaga umaskini,lakini ambao tayari wamevipata hivyo ndio wengi wao wanakuja kufahamu ya kuwa kuna zaidi ya shule na ajira ili mtu kuwa tajiri.Hapa tunarudi kwenye namba moja ya kuwa ukishajifahamu wewe ni nani utaanza kutafuta mazingira ya kukupeleka kwako na hapo ndipo utaanza kuachana na ufahamu ambao chanzo chake ni kuaminishwa na watu,watu walikuaminisha vile kwa sababu ya ufahamu wao wa muda ule.
Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha,mwanasayansi na mwalimu na mmiliki wa fikia ndoto zako label.
0652 134707.

Tuesday, 9 April 2019
HILI NDIO GEREZA LA HATUA ZAKO
Karibu tena kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako.Ni tumaini langu kuwa wewe ni mzima wa afya na unaendelea kupambana katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ili zikupe ushindi wa kuliishi kusudi lako,karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Somo hili linakusudia kuwasaidia vijana ambao wana tatizo la kutopiga hatua ilihali kila siku wapo kazini na wanapata chochote lakini hawapigi hatua mbele.Katika somo hili ,vijana lengwa ni wale ambao wana maono ya kuifikia hatua fulani lakini siku zasogea na hata dalili za kufika huko hazipo.Wewe pia una tatizo hilo? kama ndivyo ,endelea hadi mwisho utajua gereza lako ni lipi.
KWANINI UNAFANYA HICHO UNACHOKIFANYA LEO?
Hili swali linahitaji sababu ,je umewahi kujiuliza swali kama hilo? na ulipata sababu zipi? .Inawezekana ukawa na majibu yako mengi sana ya kwanini upo unafanya hiyo kazi,wengine watasema ni kwa sababu ndio walichokisomea,wengine watasema ni kwa sababu hawakwenda shule ndo mana wanafanya shughuli hiyo ,n.k.Majibu yatakuwa mengi sana.Mimi kama ningeulizwa swali kama hilo ,jibu langu lingekuwa rahisi sana tu,ningesema sababu inayofanya nifanye hiki nikifanyacho leo ni kwasabu kinanipeleka kwenye kusudi la kuumbwa kwangu. Hivi unafahamu gereza limelofunga hatua zako ni sababu zilipo nyuma ya hicho unachokifanya?
GEREZA LA HATUA YAKO MPYA NI HIYO SABABU YAKO.
Ni ngumu kupiga hatua mpya kama huna sababu zinazokusuma ufanye hivyo ,na sababu ambazo zitakufanya upige hatua mpya zinategemea sana na wewe unajitambua vipi,hapa ninamaamisha kwamba ni vizuri kwanza ujitambue wewe ni nani na wapi unatakiwa kwenda kulingana na kusudi lililowekwa ndani yako,kisha sasa ndio uangalie hicho unachokifanya ,je kinahusiana vipi na uelekeo wako?
Kama kila siku sababu zako ni kutaka ufanye kazi kwa bidii na kwa weledi,sawa ni sababu nzuri lakini je hicho unachotaka kukifanya kwa juhudi na weledi kinahusiana vipi na kusudi la kuumbwa kwako? kama hakuna mahusiano ndipo pale ambapo utaendelea kuwa na juhudi kwa kufanya jambo fulani lakini hufiki kule kwako ,mfano kama wewe uliumbwa uwe mchoraji ,na sasa upo katika kitengo cha afya kama Daktari,je unaunganisha vipi huo udakitari na kipaji chako cha uchoraji? Hapo unaweza kuiwa na sababu nyingi za kukufanya huo udakitari wako vizuri lakini ukawa huna sababu hata moja ya kutaka ufanye huo udakitari wako uendeleze kiapaji chako ,kwa namna hiyo utajikuta unaendelea kuwa gerezani tu .
UNATOKAJE KWENYE GEREZA HILO?
Kama nilivyotangulia kusema mwanzo ,kwanza lazima ujitambue wewe ni nani,kisha uangalie unafanya nini kwa sasa,na je ufanyacho kina mahusiano na wewe ni nani? kama hakuna mahusiano sio ukiache ghafla lakini tengeneza mahusiano ,yaani kitumie hicho unachokifanya kusaidia kusudi la kuumbwa kwako,mfano mimi naelekea kuibadili dunia kwa kupitia maandishi na kuongea lakini kwa sasa natumika hospitalini ,je niache kipi? jibu la haraka ni kwamba navyovipata hospitalini navitumia katika kusukuma kusudi la kuumbwa kwangu ,hivyo nyuma ya haya niyafanyayo kuna sababu zinazoniambia nielekee kwenye ulimwengu wa maandishi na kuzungumza.
Jitahidi utengeneze sababu zinazokusuma kwenda kwenye kusudi lako ,kukosa sababu hizo kunapelekea hali ya kuridhika na hatua hiyo uliyopo ,na hapo ndipo panakuwa mwanzo wa kufanya kazi kwa bidii lakini mbele husogei ,unaishia pale ambapo sababu zako zilikutuma.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
0652 134707

Saturday, 15 December 2018
MBINU ZA KUTOKA NJE YA DUARA LA UMASKINI.
Karibu sana kwenye blog hii ambayo inatoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu ,ni tumaini langu kuwa u mzima wa afya na unaendelea vyema na harakati za kukuwezesha kufikia ndoto zako....Leo nataka tujifunze mbinu kuu tatu za kutoka nje ya duara la umaskini.Somo hili limekuja maalumu kwa sababu ni wazi kwamba ,wengi wetu tunazaliwa na kulelewa katika familia zenye kipato kidogo,sasa tunapoanza kupiga hatua,tunajikuta tuna mzigo mkubwa nyuma yetu,mzigo ambao tuna wajibu wa kuubeba lakini usiathiri hatua zetu za mafanikio....Karibu tujifunze.
DUARA la umaskini ni mzunguko amabao unaanzia kwa maskini na kuishia kwa maskini ,DUARA hili mara nyingi hutokea kwa watu ambao wamezaliwa katika familia za kimaskini,mimi pia ni mmoja wapo,....inakuwa hivi;
Wazazi/ndugu(MASKINI) >MTOTO(ambaye analelewa katika hali ya kimaskini,ya wazazi wake).
Katika hali hiyo,matatizo ya waliokutangulia yataendelea kukufuata mpaka pale utakapo amua kutengeneza mfumo ambao utawafanya wawe na utegemezi wao binafsi(wajitegemee),kinyume na hivyo,kidogo chako kitakuwa kinategemewa na wengi ambao sio wazalishaji.......Hebu tuangalie hizo mbinu tatu ambazo mimi pia ninazitumia,wewe pia zinaweza kukusaidia.
1.Tambua kuwa wewe ndio daraja la kupitisha wengine,hivyo lazima uwe imara zaidi ya hao unaotaka kuwavusha ,uimara ninao uzungumzia hapa ni wa kiuchumi na mawazo,kiuchumi simaanishi uwe na milioni za pesa,la hasha,namaanisha uwe na mfumo unaoeleweka.
2.Tengeneza mfumo ambao chanzo kitakuwa ni wewe lakini waendelezaji watakuwa ni hao umeokusudia kuwasaidia(maana huwezi kusaidia kila mtu),hapa nimaanisha kwamba wewe yafaa uwe mtaji wa mawazo na pesa kwa huyo uliyekusudia kumsaidia kwa lengo la kumfanya awe na mfumo wa kujitegemea.
3. Kumbuka, kutoa pesa kila wanapohitaji sio msaada wa ukombozi,ni bora uwe bahili kwa muda ili kile kiasi ambacho ungekuwa unawapa ukitunze kisha uje ukitumie kutengeneza mfumo ambao utakuwa unajiendesha wenyewe kwa lengo tu la kuwasaidia wao(hapa nazungumzia wale ambao wanategemewa na watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kusimamia wala kufanya biashara zao,....tengeneza wewe biashara alafu faida ndo itumike kuwasaidia pale wanapohitaji na sehemu nyingine ya faida itumike kuendeshea hiyo biashara)
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mmiliki wa FIKIA NDOTO ZAKO.

Saturday, 11 August 2018
FUNGU LA PESA,UNALOPOTEZA.
Karibu tena ndugu msomaji wa makala zetu za FIKIA NDOTO ZAKO ,ni tumaini langu kuwa afya yako ni njema na unaendelea vyema na mapambano ya kila siku ya ushindi,maana kushindwa ni hatua ya kushinda......karibu tuendelee.
FUNGU LA PESA,UNAYOPOTEZA.
Leo nataka kukushirikisha somo hili juu ya pesa inayopotea, pesa ambayo unaitumia kufanyia manunuzi lakini unaitoa kwenye fungo lisilo stahili,je ni pesa gani unaitumia kufanyia manunuzi? na ni aina gani ya manunuzi unayafanya?.........Hapa nataka tuzungumzie manunuzi ya vitu ambavyo havizalishi pesa,mfano radio,tv,kabati ya nguo nk.....je huwa unanua vitu hivyo kwa kutumia pesa ya aina gani?
AKIBA ,hii ni pesa ambayo inatakiwa itumike kununulia vitu ambayo vinazalisha pesa nyingine,ukitumia pesa ya akiba kununulia kitu kisicho ingiza pesa ,unakuwa umeipoteza pesa hiyo.....Kwa nini unakuwa umeipoteza hiyo pesa?........kwa sababu ulitumia muda mwingi kuiweka hiyo pesa kidogokidogo,alafu unakuja kununua kitu ambacho badala kikuingizie pesa ,kinahitaji uendelee kutoa pesa ili ukihudumie,mfano ,unaweka pesa kama akiba ,alafu unakuja kununua radio,ambalo litahitaji uendelee kulihudumia kama vile kununulia CD nk, .....pesa umeyolimbikiza kwa muda mrefu,unaipoteza kwa siku moja,kimahesabu,hapo unakuwa unarudi nyuma,huendi mbele.........Unatakiwa ufa
nye nini? ....iwekeze akiba yako,ikuzalishie faida kwanza.
FAIDA,Hii ndio pesa inayotakiwa itumike katika matumizi ya aina mbili,ambayo ni ;

- Kununulia vitu visivyoingiza,mfano ,kama radio linauzwa Tsh 100000,ni bra uiwekeze hiyo pesa ikuletee faida ambapo hiyo faida ndio uitumie kununulia radio........hapo utakuwa hujapoteza.
- Faida inatumika kupanulia uwekezaji wako....... Kabla ya manunuzi ,hakikisha unatambua hicho unachataka kukinunua kina ongezeko la aina gani kwenye uhuru wako wa kifedha, hiin itakusaidia kufahamu aina ipi ya pesa itumike katikamanunuzi.
- Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha.
- 0652 134707
Wednesday, 4 April 2018
PANDE MBILI MUHIMU ZA UWEKEZAJI.
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani upo mzima kiafya,pia nikupe pole kwa wewe ambaye afya yako haipo sawa,Mungu akuponye.....karibu.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze pande mbili za uwekezaji,ambazo ni muhimu sana,nimejifunza kwangu ,pia nimejifunza kutoka kwa wawekezaji mbali mbali..............pande hizo ni zipi?,karibu tujifunze.
PANDE MBILI ZA UWEKEZAJI.
Kabla hujaanza uwekezaji ,kuna sehemu mbili muhimu ambazo lazima ujipange,kuingia kwenye uwekezaji bila kuwa vizuri kwenye sehemu hizi,nakuhakikishia,uwekezaji wako utakuwa wa mashaka sana.......tuziangalie sehemu hizo;
1.PESA ZA KUENDESHA MRADI...Kitu amacho wengi tunakosea ni kwenye kupanga bajeti za kuendesha uwekezaji,wengi tunadhani ukisha fungua uwekezaji wako tu basi inatosha......hapana,kuna pesa ya kufungulia mradi na kuna pesa ya kuendeshea mradi wako,ni vitu viwili tofauti,wengi huwa tunaazisha biashara /uwekezaji tukiwa na pesa ya kufungulia mradi.......je mradi wako utajiendeshaje?.Bora uanze na mradi wa gharama ndogo ili ubakize kiasi cha kuendesha mradi wako,na sio uanzishe mradi wenye gharama kubwa ,halafu ukose fungu la kuendeshea mradi wako,hutofika popote,utaishia njiani.
2.USIMAMIZI....Kabla ya kuanzisha mradi wako,jifanyie tathimini,una muda wa kutosha wa kusimamia mradi wako?....kama asilimia za kusimamia mradi wako ni chini ya 60,bora usianzishe huo mradi wako.Mafanikio ya uwekezaji hayapo kwenye kuanzisha uwekezaji huo tu,yapo kwenye jinsi ya kusimamia aina ya uwekezaji huo.Usimamizi mzuri una faida nyingi sana,ila kubwa na muhumu ni kuzalisha matunda bora,ukisimamia vizuri,mazao yatakuwa mazuri pia,maana usitegemee kuwa kuna watu watajituma kwa juhudi kusimamia mradi wako zaidi ya juhudi zako,wewe ndio unapaswa uwe na usimamizi mzuri ili wafanyakazi wako wafate ubora wako.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
0652 134 707.
Monday, 12 March 2018
JINSI YA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIDHAA YAKO.
Karibu sana kwenye blog hii inayotoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zako,hongera kwa hali uliyo nayo,ipo sababu ya wewe kuwa ivyo.
KUSUDI LA SOMO.
Somo hili ni majibu ya watu ambao kila siku wanaogopa kufanya biashara au kuwekeza kwenye kitu ambacho tayari kinafanywa na wengine,kwa hofu ya kupata soko la kutosha.....karibu upate majibu. Kabla hujaendelea mbele,jifunze( JINSI YA KUTENGENEZA SOKO)........Karibu tuendelee.
JINSI YA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIDHAA YAKO.
Mwaka 2016 nilifanya utafiti wenye lengo la kugundua sababu zinazofanya wanakijiji wengi waendelee kulima bila kupata mafanikio ya kutosha,utafiti huu niliufanya kwenye kijiji kimoja mkoani Morogoro,,,,,pamoja na mengi niliyoyapata,yapo mambo mambo muhimu matatu ambayo wengi wetu tunakosea hadi kufanya soko liwe changamoto kubwa.
Jitahidi uongeze thamani ya pili kwenye bidhaa yako.mfano,kama una unaona kila mtu ana duka la mbolea,wewe fanya kinyume toa ushauri wa jinsi ya kutumia hiyo mbolea......watu watakuja kupata ushauri huo,wakiridhika ,ni ngumu wakanunue mbolea sehemu nyingine tofauti na kwako.
Usiingize bidhaa yako sokoni ukiwa na shida inayohitaji utatuzi wa haraka.....utajikuta unatumia mbinu ya kuishusha thamani ya bidhaa yako kwa kuiuza kwa bei ya chini,....wanakijiji wengi huingia kwenye kilimo ili watatue matatizo yao kwa haraka,mwisho wa siku wanajikuta wanauza mazoa yao kwa bei yoyote ile,tena wanauza haraka baada tu ya kuvuna......!
Ifanye bidhaa yako kuwa adimu,unaifanya vipi?......hapa unafanya bidhaa yako iwe inapatikana kwa utaratibu ambao wengi hawaufanyi,fatilia wateja wnapata usumbufu gani hadi kuja kuipata bidhaa yako......wapunguzie usumbufu huo....mfano badala ya kuwauzia sabuni kwenye gazeti,wauzie kwenye mfuko mweusi.
Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya fikia ndoto zako.

Subscribe to:
Posts (Atom)